NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (5)

Zephiline F Ezekiel
NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (5)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Kwenye kiti kile wakaniweka na kuanza kuniuliza maswali kuhusu yule mzee niliyekuwa nimemuokoa na almasi. Nilichokigundua ni kwamba hawakujua ni mlinzi gani aliyekuwa amemuokoa yule mzee na mbaya zaidi hawakujua ni nani alikuwa na almasi waliyokuwa wakiitaka. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Kila walichoniuliza, niliwaambia kwamba sifahamu chochote kuhusu almasi lakini nilisikia kuhusu mzee huyo kwamba alitakiwa kuuawa. “Wewe ulikuwa wapi?” aliniuliza. “Nilikuwa Kimanzichana kwa mama! Nilipewa likizo ya siku saba,” niliwajibu kwa sauti ya chini. “Kwa hiyo hujui chochote kuhusu almasi?” “Hapana mkuu! Sijui chochote kile, hata huyo mzee niliambiwa tu,” nilimjibu mwanaume aliyekuwa akiniuliza. Niliwadanganya, walionekana kuniamini lakini hiyo haikuwa sababu ya kuniacha, waliendelea kunitesa mno, soku hiyo ilikuwa ni ya hatari sa…