NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (8)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA NANE ILIPOISHIA... Haraka sana nikaelekea kwenye kijiwe cha bodaboda na kutaka kuchukua moja ya kuniwahisha haraka sana kwani kutoka hapo Veta mpaka Ilala hakukuwa mbali, kazi kwangu kutoka huku Sinza mpaka hapo Ilala. “Oya! Nataka unipeleke Ilala Boma ,” nilimwambia dereva mmoja. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Haina noma! Pakia!” “Unajua kuendesha kwa kasi? Nataka niwahi!” “Wewe tu braza!” “Basi kama vipi, hakikisha hii pikipiki inapaa,” nilimwambia sentensi ambayo ilimaanisha nilikuwa na haraka kupita kawaida. Nilichomwambia ndicho alichokifanya, alikuwa na haraka kupita kawaida. Aliendesha pikipiki mpaka huku nyuma nikahisi kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wangu, na pesa zangu ningeziacha benki. Baada ya dakika tano hivi tukafika Ilala Boma, nikateremka, nikamlipa elfu kumi na kumwambia abaki na chenji wakati mimi nikiingia ndani ya Hoteli …