Mtunzi: Global Publisher
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Pole baby, unaumwa?”
“Hapana… basi tu.”
“Sasa si uje, nimekumisi sana.”
“Da! Musa bwana…unanipa majaribu ujue.”
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
ENDELEA...
“Kwa nini?”
“Si hivyo unavyoniita…mista yupo ujue…”
“Kha! Kwani hata juzi si alikuwepo…mbona ulikuja…njoo bwana…mara moja tu…”
Mama Shua hakumjibu Musa, akavua nguo na kuvaa upande mmoja wa kanga huku moyoni akisema… “Musa naye…yaani kila saa anataka.”
Alitoka sebuleni, akamkuta mumewe amekaza macho kwenye tivii akiangalia taarifa ya habari, akatoka kwenda uani.
Aliweka maji bafuni, akasimama kwa muda akiwaza akaingie chumbani kwa Musa au la!
“Lo! Mbona shughuli…lakini na mimi kama namuhitaji Musa…ngoja nimwambie awe tayaritayari ili nikifika tu chapuchapu ili niwahi kutoka.”
Alirudi chumbani, akamtumia meseji Musa…
“Baby, mlango uwe tayari na wewe pia uwe tayari…nikifika tu chapuchapu ili nitoke.”
“Poa,” alijibu Musa.
Mama Shua alitoka, akajifanya anakwenda uani. Akasimama kwenye mlango wa Musa, akashika kitasa, akafungua, akazama ndani…
“Baby yaani hapa hakuna kupoteza muda, jamaa amekaa sebuleni.”
“Poapoa,” alisema Musa huku akifunga mlango.
Mama Shua alijivua ile kanga na kuitupia kwenye kiti, akajipeleka kitandani mwenyewe huku akiwa anahema kwa kasi.
Hakukuwa na maandalizi wala kupandishana joto, waliingia uwanjani moja kwa moja na kuanza kulisakata kabumbu harakaharaka. Safari hii, mama Shua hakuwa na haja ya kumsemesha Musa ili achelewe matokeo yake akamhamasisha ili amalize mchezo haraka. Kweli ikawa hivyo tena wote kwa pamoja.
Baada ya hapo, mama Shua aliiokota kanga yake haraka, akajifunga kifuani na kutoka kinyemela huku akiurudishia mlango polepole ili usisikike.
Alishtuka kumsikia mumewe anaoga yale maji aliyoyaweka yeye…
“Mh! Ina maana…si atajiuliza mimi niko wapi?” alijiuliza mwenyewe mama Shua huku akitetemeka.
Alikwenda chumbani, akakuta nguo za mumewe ziko chini…
“Ina maana hapa atajua nilikuwa wapi! Chooni ndiyo bafuni kulekule. Jiko liko ndani na limefungwa. Na kama ni jikoni alipokuwa akienda kuoga si angeniona. Da!”
Alishika simu yake, akamtumia meseji Musa…
“Da! Nahisi kama nimeumbuka.”
“Kivipi baby, nikupigie simu?”
“Hapana! Ila kuna ishu kubwa sana.”
“Da! Baby, unanitisha. Jamaa kajua?”
“Atakuwa kajua.”
Mara, baba Shua aliingia akitokea bafuni kuoga. Akajifuta maji kwa taulo, akavaa bukta kisha akatoka kwenda kukaa sebuleni…
“Mh! Ina maana hajajua? Mbona haniulizi?”
Mama Shua naye akatoka kwenda kutenga maji mengine akaoga na kurudi chumbani.
Hakuwa na namna, alipanda kitandani kulala huku moyo ukimwenda kwa kasi ya ajabu…
“Lakini mimi nimeanzisha tabia gani jamani? Mbona zamani sikuwa hivi, sasa itakuaje?” Alipitiwa na usingizi. Alipokuja kuamka, mumewe alikuwa pembeni amelala akiangalia juu na magoti yakiwa juu kwa maana kwamba hakuwa usingizini…
“Baba Shua…”
“Mm…”
“Mbona hujalala?”
“Ungekuwa wewe ungelala?”
“Ningekuwa mimi kivipi sasa?” “Wewe ungekuwa umeniona mimi nikiingia chumbani kwa mwanamke mpangaji mwenzetu na ukasikia kitanda kinalia na mimi natoa sauti za mihemko ya mapenzi ungepata usingizi?”
Mama Shua alishtuka sana, akaamka na kukaa kitandani. Alitingisha kichwa kama vile alisikia vibaya… “Sijakuelewa baba Shua.” “Hujanielewa nini sasa? Wewe umeingia chumbani kwa yule kijana. Umekula uroda, unabisha? Au ulitaka nisimame mlangoni kwake ndiyo ujue kwamba nimejua umeingia kule?” Mama Shua alikaa kimya. Baba Shua akajipinda na kuangalia upande mwingine kuuchapa usingizi huku akimwacha mkewe bado amekaa akiwaza na kuwazua… “Da! Yaani nilidhani ni siri lakini kumbe nimeonwa? Hivi ni kweli ameniona au anahisi tu? Lakini nawezaje kusema si kweli ila anahisi wakati mimi mwenyewe najijua kweli niliingia chumbani kwa Musa?
“Ila sasa kama baba Shua aliniona kwa nini hakuchukua hatua palepale? Lakini pia kama angeamua kunichukulia hatua je, mimi nilikuwa tayari kwa kuchukuliwa hatua?” Yote hayo aliyawaza mama Shua huku akijisikia aibu mwenyewe. Usingizi ulimkatika, akatoka kwenda chooni. Alipokuwa akipita kwenye mlango wa chumba cha Musa, alihisi kichefuchefu. Akajutia. Lakini wakati anatoka chooni kuingia ndani, akakutana na Musa naye akiwa anatoka kwenda chooni… “Vipi baby?” Musa aliulizia kwa sauti ya chini.
“Poa,” mama Shua alijibu kwa mkato, Musa akamshika mkono kumzuia asiendelee mbele… “Wewe huogopi?” aliuliza mama Shua… “Niogope nini sasa?” “Bwana, mwenzio nina msala chumbani kwa mume wangu.” “Msala gani?” “Nitakwambia.” “Sikia…sikia baby…” “Sema, nakusikiliza…” “Twende chumbani kwangu.” “Ha! We saa hizi wakati nimekwambia kabisa kwamba nina msala…” “Sikiliza baby, ukiamua kula nguruwe kula aliyenona. Kama una msala malizia kula raha ili msala uwe mdogo,” alisema Musa… “Una maanisha nini?” “Namaanisha twende chumbani kwangu tukajirushe, msala utaushughulikia kesho.” Maskini mama Shua, eti maneno hayo tu alijikuta akishawishika na kukubali kuingia chumbani kwa Musa… “Lakini kama saa zile Musa, iwe chapuchapu! Sawa?” alisema mama Shua huku akiwa anaitupa kwenye kochi kanga moja aliyovaa.
Walipanda kitandani na kwa vile walikuwa wanaibia mechi, hakukuwa na maandalizi, palepale wakaingia uwanjani na kuanza kulisakata kabumbu kwenye uwanja wa sita kwa sita.Kweli, safari hii mama Shua alionekana kucharuka sana kitandani kwa sababu alitembea kwenye ile dhana ya Musa kwamba kama kuna msala, ajirushe tu kesho yake atashughulikia msala wake. Ni dakika chache za wizi lakini mama Shua alizitumia vizuri kuliko Musa kwani alipata ushindi wa kwanza, kufumba na kufumbua akapata ushindi wa pili kabla Musa hajapata ushindi wa kwanza kwa mbwembwe. Baada ya kumaliza, mama Shua alisimama, akavaa kanga yake huku akisindikizwa na Musa kutoka.
Lakini kushika mlango hivi, kumbe umefungwa kwa nje… “Haa!” mama Shua alihamaki kwenye masikio ya Musa ili asisikike… “Vipi?” “Mlango umefungwa kwa nje…” “Hamna bwana…nani afunge?” alisema Musa huku akishika kitasa… “Mungu wangu, kweli mama Shua. Unadhani atakuwa nani?” “Nahisi ni mume wangu. Nani mwingine humu ndani anaweza kufunga mlango kwa nje?” alisema mama Shua huku akianza kutetemeka. Mbaya zaidi, simu yake aliiacha chumbani. Moyoni alisema afadhali angekuwa nayo, angempigia msichana wake wa kazi amfungulie. Lakini akili ikakumbuka kwamba, namba za dada wa kazi anazo kichwani hivyo akamwomba simu Musa ili ampigie…
“Sasa kama jamaa amesimama mlangoni si atakusikia?” Musa aliingia wasiwasi… “Nitaongea kwa sauti ya chini sana.” Mama Shua alimtajia namba Musa, akaziandika kwenye simu yake na kumpigia. Simu ilipoita, Musa akampa simu mama Shua… “Haloo…we nani?” dada wa kazi aliuliza kwa sauti ya juu maana hakuwa na namba za Musa… “Sikia dada, mimi mama Shua…” “A…aaa…vipi dada, uko wapi kwani?” “Sikia…toka chumbani, nenda kwenye mlango wa yule kijana mpangaji mgeni, kama mlango wake umefungwa kwa nje mfungulie, sawa?” alisema mama Shua katika mazingira ambayo, dada wa kazi hakujua kama bosi wake huyo alikuwa ndani ya chumba hicho… “Sawa dada.”
Msichana wa kazi alitoka, akaenda lakini alishtuka kumkuta baba Shua amesimama mlangoni, akajifanya anakwenda chooni… “Shikamoo baba…” “Unaamkia sana, we pita na hamsini zako.” Msichana wa kazi alipita akitetemeka. Alijilazimisha kujisaidia kisha akarudi ndani. Alichukua simu akatuma tafadhali nipigie kwenye namba ya Musa. Musa akampa simu mama Shua, akapiga… “Dada hujatoka tu?” “Nimetoka mama, baba amesimama katikati ya mlango, akaniambia niendelee na hamsini zangu.” “Ulimwambia unataka kufungua mlango..?”
“Hapana, sijamwambia. Nilimwamkia akasema ninaamkia sana.” Mama Shua akakata simu, akakaa kitandani na kuanza kuporomosha machozi huku akimlaumu Musa... “Nilikwambia nina msala Musa hukutaka kunielewa. Unaona sasa?” “Sasa si wakati wa kulaumiana huu mama Shua, tuangalie itakuaje?” “Sasa unadhani itakuaje na mtu kasimama mlangoni!” Pale nje, baba Shua aliwaza kuwagongea mlango wawili hao ili ijulikane moja.
Aliwaza sana, akaamua kwamba amwambie msichana wake wa kazi ni marufuku kufungua mlango wa chumba cha Musa endapo ataambiwa afanye hivyo…
“Ngo ngo ngo,” aligonga.
Msichana wa kazi akafungua na kusimama mlangoni…
“Dada, mama Shua ameingia kwenye chumba cha yule kijana mgeni…”
“Haa! Kufanya nini?”
“Anajua mwenyewe…sasa sikia, akikupigia simu ukamfungulie mlango usiende maana ni mimi nimefunga kwa nje…”
“Ha! Sasa dada kaenda ndani kwa watu kufanya nini tena jamani? Halafu mbona ni usiku sana?”
“Mama Shua si mwaminifu,” alisema baba Shua huku akiondoka kurudi chumbani kwake.
Alipanda kitandani kulala, akaanza kuwaza kabla ya kuupata usingizi…
“Siwezi kuwa na ndoa tena…na nikisema nimvumilie nitakuwa mwanaume wa ajabu wa kwanza hapa duniani,” alisema moyoni baba Shua. Usingizi ukampitia haraka.
***
Kule chumbani, mama Shua na Musa walikaa tu juu ya kitanda. Muda mwingi mama Shua alikuwa akimwaga machozi. Kuna wakati alimwingiza akilini mama yake mzazi, akajikuta akiogopa zaidi…
“Musa, unadhani itakuwaje sasa?”
“Kuhusu nini?”
“Mimi naachwa mwenzako. Kwani we hujui?”
“Da! Sasa tufanyeje mama Shua?”
“Mi sijui.”
Hakuna aliyelala, muda mwingi walikuwa wakisinzia lakini bila kulala. Mama Shua hakumpigia tena simu msichana wake wa kazi baada ya kujua kuwa, mumewe amesimama mlangoni…
“Yaani najuta mimi najuta! Nilikuwa nakosa nini kwa mume wangu mpaka kujikuta natumbukia kwenye penzi la nje. Nitamwambia nini mama?” alisikitika mama Shua huku machozi yakiufunika uso wake.
Jogoo la kwanza liliwika, mama Shua akashtuka sana…
“Umesikia jogoo hilo?” alimwambia Musa…
“Kumekucha,” alisema Musa huku akiuendea mlango na kujaribu tena kuufungua, akakuta umefungwa vilevile. Akarudi kitandani huku akisikitika sana…
“Da! Mlango bado umefungwa mama Shua…mumeo sijui amenikusudia nini mimi! Mwenyewe najuta sana na hii hali…unadhani nitaendelea kuwa mpangaji kwenye nyumba hii?”
“Uendelee, usiendelee mimi sijui Musa. Kwani sitakuwepo tena.”
Kulikucha kabisa, mlango bado ulifungwa kwa nje. Msichana wa kazi wa mama Shua alishaamka na kuendelea na kazi zake za kila siku huku akijua mama Shua yumo chumbani kwa Musa. Alijiuliza mengi moyoni.
Jua lilichomoza, mama Shua akapata wazo kwamba achukue simu ya Musa, ampigie baba Shua na kumwomba afungue mlango atoke,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi
