CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (4)
Jina: CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA Mtunzi: Global Publisher SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... Kitendo cha kuingia na bodaboda nyumbani kwake, kikamshtua Musa ambaye tayari alikuwa amejiandaa kudumbukia chumbani kwa baba Shua ili kumkabili mama Shua. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alipomuona baba Shua tu, akajifanya anatoka nje moja kwa moja. “Za asubuhi baba Shua,” alisema Musa kwa sauti ya chini. “Salama tu kijana mwenzangu, daah halafu nilisahau kukwambia kuwa nasafiri na hapa nimerudi mara moja kuna kitu nimesahau.” Musa akacheka kimoyomoyo. “Angejua najua kila kitu na hapa nimenusurika kufumwa hata asingeongea yote hayo.” Alimwacha baba Shua akiingia chumbani kwake. Alipofika alimkuta mama Shua akiwa katika kanga moja tu kwenye kochi. “Vipi tena, leo kazini huendi?” “Baba Shua! Hapa nilikuwa natafakari nitawezaje kuvumilia kukaa mbali na wewe hasa huyu mtoto wetu Shua,” alimuongopea na kumuuliza swali. …