CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (7)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
ina maana atakuwa ndani ya gari analoliona la Musa ambalo yeye baba Shua halijui.

“Unaweza kuendesha kwa kasi hadi kulifikia lile gari?” baba Shua alimuuliza dereva ambaye badala ya kujibu aliongeza mafuta kwa kasi. Lakini wakati analikaribia,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
gari hilo likawa limeshaingia barabara kuu. Kwa mbali, ndani aliona watu wawili akiwemo dereva lakini hakuweza kupata mtazamo kamili kama ni wanaume, wanawake au mwanaume na mwanamke kwa vile vioo vya gari vilikuwa ‘tinted’…

“Unajua kuna Bajaj inatufuata kwa kasi sana,” Musa alimwambia mama Shua. Ilibidi mwanamke huyo ageuke kuiangalia lakini akaiona kwa gizagiza sana. Kwa hiyo hakujua ndani ya gari lile mlikuwa na nani na ni nani!

Baba Shua alimwambia suka waishie pale lakini akaisoma namba na kuandika kwenye simu yake kisha akarudi nyumbani akiwa amefura sana. Aliamini moyoni kwamba, mkewe alipanda lile gari…

“Yaani mama Shua sasa amefika pabaya, anafuatwa na magari hadi nyumbani! Hii kwa kweli siwezi kuivumilia hata kidogo,” alisema moyoni huku akituma meseji kwenda kwa mkewe…

“Kwa hiyo sasa umefikia hatua ya kufuatwa na gari hadi nyumbani ili likupeleke kazini. Tutawezana kweli?”

Mama Shua aliposoma meseji hiyo alishtuka sana…

“Mh! Au alikuwa kwenye ile Bajaj nini?”

Alitaka kumfowadia meseji Musa lakini akahisi atakuwa anamtisha kijana wa watu, akaacha…

“Gari gani mume wangu?”

Wakaanza kujibizana sasa…

“Gari gani? Kwani we umepelekwa kazini na gari gani?”

“Nilipanda basi baba Shua.”

“Usinidanganye mimi wewe. Umepanda gari lenye namba za usajili T 349 CAT, unabisha?”

Mama Shua hakuzijua namba za gari lile, lakini akajitutumua na kujibu kwa ufupi…

“Ina maana uliniona nikiingia kwenye gari au?”

“Ndiyo,” baba Shua alifanya kusudi kujibu hivyo ili aone, mkewe atajibu nini.

Mama Shua alihema kwa kasi, akajua kweli alionekana na mumewe, ilibidi asiijibu meseji hiyo.

Baba Shua alipoona nusu saa inapita bila majibu, alituma meseji nyingine…

“Mimi umenichosha na vitabia vyako vya siku hizi, kwa nini usije kuchukua vitu uondoke hapa nyumbani? Maana najua unataka uhuru hapa kwangu umebanwa!”

Ilikuwa meseji nzito sana kwa mama Shua. Alianza kuingiwa na wasiwasi. Aliamini hali ndani ya ndoa yake si nzuri, akaanza kuona hatari ya siku za mbele.

Hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba, mumewe angeweza kumtamkia maneno mazito kama hayo, lakini siku hiyo alitamka bila kutumia lugha ya mafumbo. Hata meseji hiyo hakuijibu.

***

Saa saba juu ya alama, Musa alimpigia simu mama Shua…

“Haloo,” alipokea mama Shua bila maneno ya kuchombezea kama ‘haloo baby’, ‘niambie darling’ na mengineyo…

“Vipi sweet, mbona umepokea simu kama hunifahamu vile?”

“Ah! Siko sawasawa bwana…”

“Kuna nini?”

Mama Shua alijua akisema amwambie yaliyojiri, hata yeye Musa angeshtuka na kuogopa sana, akamdanganya…

“Mwili wangu kama unaumauma kwa mbali halafu moyo kama hauna furaha vile.”

“He! Kuna nini tena? Uko wapi kwani?”

“Nipo job. Wewe..?”

“Mimi nipo hapa hotelini napata mchemsho wa samaki. Kama vipi njoo unywe.”

“Ah! Yaani hata kutoka hapa pia sijisikii kabisa.”

“Basi twende chumbani baby, nikakupetipeti, nikakufinyefinye wee mpaka useme basi. Halafu mambo yetu yawe kama ya siku ile, unasemaje?” alisema Musa na kumfanya mwanamke huyo kusisimka, akajikuta akichangamka mwili…

“Jamani baby, usinifanye nicheke darling…lo! Maneno yako matamu kama asali…”

“Hata mimi mwenyewe nipo kama asali kama ulivyo wewe,” alisema Musa, mama Shua sasa akawa si yule aliyepokea simu, akaachia kicheko cha haja…

“Wapi sasa?”

“Si nimekwambia napata mchemsho…”

“Ina maana huko kunifinyafinya utanifinyia hapohapo hotelini?”

“Aah! Si kule bhana…”

“Saa ngapi?”

“Wewe tu, hata ukisema leo mimi niko tayari.”

“Kweli?”

“Kweli kabisa. Mimi nitaondoka kazini maana leo sina kazi nyingi sana,” alisema Musa na kumfanya mama Shua kuliangalia begi lake lilipo.

Alichofanya, alimtumia meseji mumewe…

“Naumwa, nakwenda hospitali.”

Mumewe hakuijibu meseji hiyo zaidi ya kuachia tabasamu la mshangao huku moyoni akisema…

“Amejua ana msala sasa anatafuta namna ya kuumaliza.”

Mama Shua aliomba ruhusa kazini, akisema anakwenda hospitali hajisikii sawasawa.

Alichukua usafiri huku akimtumia meseji Musa ya kumuuliza kule hotelini aende muda huo au bado!

“We umeshatoka kwani?”

“Niko njiani.”

“Tangulia na mimi natoka hapa nakwenda chukua gari kisha hotelini, hapa nilipo mawazo yangu yote nipo na wewe kitandani.”

Mama Shua alizidi kusisimka mwili, hata maneno ya mumewe akayaweka pembeni kwanza…

“Basi baby usichelewe bwana,” alisema mama Shua huku akihisi kuchelewa kufika kwenye hiyo hoteli.

Alifika, akazama ndani huku mikono ikibonyeza vitufe vya simu kumtaarifu Musa kwamba ameshafika eneo la tukio…

“Baby, nipo eneo la tukio tayari.”

Musa alitoka kama swala, akafika hotelini ndani ya dakika chake…

“Umechukua rum?”

“Kilekile.”

“Oke.”

Mlango ulisukumwa, Musa alizama ndani na kumkuta mama Shua ameshavua kila kitu na yupo na suti ya ngozi tu…

“Du! Baby unanihamasisha siyo?” alisema Musa akimwangalia mama Shua kwa macho yaliyojaa tafsiri ya ‘mahaba niondolee uhai wangu’.

Musa, kwa kasi ya mashine ya cherehani alivua suruali, akatupa huko, akachua shati akatupa kule, akavua boksa akaivurumishia mbali, akachojoa singilendi na kuirushia mbali, akapanda kitandani huku akichekacheka lakini moyoni alipokumbuka kwamba anaweza kuchemsha licha ya mbwembwe nyingi alijikuta akikosa nguvu ghafla…

“Daa! Inawezekana lakini…sijui mganga gani atanisaidia mimi?” alisema moyoni Musa.

Mama Shua kwa kujua kuwa Musa ana ‘ugonjwa’ wa kumaliza haraka, alimdaka, akampa mabusu motomoto huku akimsema kwamba amechelewa…

“Hivi kwa nini umechelewa baby lakini?”

“Mh! Mbona nimewahi darling…”

“Hakuna bwana, yaani mpaka uongee na wanawake wako wee ndiyo uje kwangu.”

“Sikuwa na mwanamke baby, ndiyo maana nilikuita pale. Sasa kama ningekuwa na mwanamke ningesema uje? Acha mawazo yako hayo.”

Muda wote wa mazungumzo, wawili hao walikuwa wakishikana sehemu mbalimbali za mwili huku wamelala. Musa alichaji sana lakini kule kupambana na lawama za mama Shua kulianza kumkatisha tamaa kwa mbali…

“Lakini baby mbona umekuwa mtu wa lawama sana? Huniamini, huniachii nafasi ya kufurahia tukio, vipi kwani?” alilalamika Musa…

“Sikuamini ndiyo, sasa wewe unanisaliti hivihivi naona halafu nikuache kweli?”

Ilifika wakati, mama Shua akiwa anaendelea kumlaumu Musa, mechi ikaanza pamoja na lawama zake juu…

“Nikwambie kitu kimoja baby, mimi sipendi kabisa usaliti. Usaliti utanifanya mimi na wewe tuachane kabisa,” alisema mama Shua huku mechi imeshaanza…

“Mimi sikusaliti mpenzi wangu, hayo mawazo yatupilie kwa mbali. Nakupenda wewe, nakupenda sana.”

Mama Shua hakuacha kumtuhumu Musa kwa usaliti mpaka Musa akajikuta anachukua dakika kumi na tatu hivi akiwa bado uwanjani, ndipo mwanamke huyo akaamua kuachana na lawama na kumsifikia kwa mahaba anayompa, Musa akajikuta anamaliza mchezo, wakamaliza sambamba.

Sasa walikuwa wamelala wakiangalia juu huku wote wakihema kwa sana…

“Hivi baby mbona kama lile tatizo halipo, we unatumia dawa gani?”

“Naijua mwenyewe, wala sikwambii ng’o.”

“Niambie kidogo baby jamani.” “Sikwambii ng’o na hiyo dawa naijua mwenyewe. Ukienda kwa mwanamke mwingine utaipata ile hali, dakika moja tu mpira umeisha, aibu kwako,” alisema mama Shua huku akigeuka kumwangalia Musa kwa macho ya utani.

***

Simu ya baba Shua iliita, mama Shua alipoiangalia, akasonya kisha akaacha bila kuipokea…

“Huyu naye,” alisema moyoni mama Shua…

“Mbona hupokei, nani kwani?”

“Mista.”

Musa aliposikia ni mista, damu zikamkimbia mwilini, alihisi baba Shua amesimama mlangoni na kupiga simu ya mkewe…

“Mh! Atakuwa wapi?” aliuliza Musa…

“Mi sijui.” “Siyo kwamba yupo hapo nje kweli!”

“Nje ya mlangoni?”

“Ndiyo.”

“Hawezi. Namjua yule. Ajue mimi nipo ndani humu halafu asimame na kupiga simu! Angeingia na mlango mpaka ndani.”

Mara ikaingia meseji…

“Umekwenda hospitali gani?”

Mama Shua hakuijibu meseji hiyo kwani ilikuwa ngumu kwake kueleza. Angeitaja si ina maana mumewe angemfuata!

***

Baada ya mapumziko ya kama lisaa limoja, mama Shua akataka mechi tena, akamfanyia vilevile Musa na mechi ikaanza kwa uzuri mpaka dakika ya kumi, Musa akamaliza.

Walikaa ndani ya hoteli hiyo mpaka saa kumi na nusu. Musa ndiye aliyeanza kutoka hadi kwenye gari, akafungua mlango na kuzama ndani, akamtumia meseji mama Shua…

“Njoo, kuko shwari.”

Mama Shua naye akachomoka mpaka kwenye gari ambapo alikuta mlango wa upande wa abiria upo wazi.

Musa aliwasha gari, wakaondoka.

“Sasa utashukia wapi?” aliuliza Musa…

“Mh! Jirani na kile kituo, saa hizi najua yeye atakuwa ameshafika nyumbani,” alisema mama Shua.

Musa aliegesha gari pembeni, mama Shua akashuka na kuanza kutembea polepole.

Musa naye alipanda kaukuta na kulipeleka gari anapolilaza. Baba Shua alikuwa akienda dukani, akakutana na mama Shua, lakini pia akaliona gari la Musa na Musa mwenyewe akishuka, akashtuka…

baba shua aliiangalia ile namba ya gari na kukumbuka kuwa ndo ile ile aliyoiona ikiwa mbele yake asubuhi walipokuwa wakiifukuzia na bajaji, pale ndipo hofu yake ikazidi kuongezeka juu ya Musa, alitaka kumuuliza Mama shua lakini akaghairi na kuendelea na shughuli zake,

¤¤¤¤¤¤¤¤

Mama shua aliondoka akiwa na wasiwasi kwamba atakuja kujibu nini kwa baba shua kama ameshtukia ile ishu, aliingia chumbani akabadilisha nguo na kujifunga kanga yake tayari kwa kwenda kuoga,

Upande wa pili Musa yeye alikuwa anasikilizia meseji ya kutoka kwa mama shua kujulishwa kinachoendelea je baba shua atakuwa ameshtukia?, mara meseji ikaingia "baby nakuja sasa hivi tumalizie tena" Musa alistuka "tena?" ndio wangu, "tena sasa hivi?" aliuliza Musa akionesha kuwa na wasiwasi "ndio", alijibu mama shua kiuhakika zaidi,

Kwani baba shua kaenda wapi? Aliuliza Mussa,

Ametoka bhana sijui kaenda wapi atajijua mwenyewe, mi nabeba kanga mbili na maji nayapeleka bafuni alaf kanga moja nitaiacha kanga huko moja ndo nitakuja nitaingia kwako, alimshauri mama shua,

Mmh, "haya njoo" maelezo ya mama shua yalionekana kumuingia Musa,

"Poa usitume meseji tena mi ndo natoka"

Poa.

Mama shua aliiweka simu chaji, akatoka kama alivyopanga akaingia bafuni, akaiweka kanga moja ikiwa inaning'inia akaingia chumbani kwa Musa, haraka haraka wakalianzisha sebene.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni