MAUAJI YA KASISI (11)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Amata aliteremka na kuzunguka lile jingo la ghorofa mbili na alipofika nyuma yake alitikisa kichwa kwa kuugundua upumbavu wa vijana hao waliobaki ndani ya gari wakati nyuma ya jingo kuna ngazi zinazoweza kumtoa mtu yoyote aliye ndani ya jingo hilo, akarudi mpaka mbele na kuwapa taarifa hiyo ambayo iliwafanya wafadahaike sana kwa ujinga walioufanya.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Hakika Bill Van Getgand alikuwa ametokea upande wa pili pamoja na yule mwanadada na kuchukua tax iliyokuwa imeegeshwa huko nyuma na kuondoka zao mpaka uwanja wa ndege ambako walichukua ndege na kuelekea Nairobi.

Baada ya kumsukasuka yule dereva wa tax aliyewabeba Bill na yule mwanadada hakuna jibu la maana walilopata zaidi ya kubaki na lile koba la gitaa ambalo ndani yake kulikuwa na bunduki kubwa iliyotumika kwa mauaji yale lakini hakukuwa na guitar, baada ya uchunguzi wa hali ya juu kufanyika uliohusisha vyombo mbalimbali vya kiintelijensia ilionekana Bill amehusika na mauaji hayo na si sehemu moja tu basil maeneo mbalimbali duniani, nah ii iliifanya nchi yetu kuingia kwenye matatizo ya kimahusiano na nchi husika ya mrehemu yule kwani iligundulika alikuwa ni mtu muhimu serikalini ambaye alikuja kwa shughuli za kiserikali na kufikia hapo hoteli ya Kilimanjaro.


Kamanda Amata aliishusha picha ndogo ya Bill aliyokuwa akitumbulia macho na kuirudisha kwenye kikoba maalum. Mara kengele ya mlango wa chumba chake ikagongwa, akanyanyuka taratibu na kuuendea mlango huo huku bastola yake ndogo ikiwa mkononi mwake, akiwa kaificha kwa nyuma alimruhusu mtu huyo kuufungua mlango. Mwanadada mwembamba, mrefu wa wastani aliupenyeza mwili wake ndani ya chumba cha Amata,

Amata alimeza mate ya uchu hasa alipokutana macho na paja mwororo la mwanadada huyo ambalo lilibaki wazi baada ya sketi yake iliyofungwa kwa vifungo upande wa kulia kulipa nafasi paja hilo kuonekana, kiuno chake kidogo kilibeba kajiumbo ka wastani, si kanene sana, lakini kenye mvuto mahsusi kwa mwanaume yoyote rijali, mikono ya Amata ilipoteza nguvu na kuiruhusu ile bastola yake kurudi mfukoni bila kutarajia, macho yake yalikuwa yakitalii kifua cha mwanadada huyo ambapo blauzi aliyoivaa yenye vifungo vichache mbele iliruhusu nusu ya titi lake ambalo halikuhifadhiwa kwa sidiria kuonekana na kumfanya kamanda kuinuka kutoka pale alipoketi na kumjongelea mwanadada huyu, kabla hajamfikia …

Kabla hajamfikia, yule msichana aliweka magazeti aliyokuwa nayo mkononi juu ya meza ya kioo iliyokuwa hapo ndani.

“Wakati unasubiri kuonana na mwenyeji wako, usome magazeti haya!” sauti tamu ya yule dada iliyapenya masikio ya Kamanda Amata. Baada ya kuyaweka magazeti hayo pale mezani, aligeuka na kutoka nje huku macho ya Amata yakimsindikiza kwa kila hatua aliyoivuta, alitoka na kuurudishia mlango nyuma yake. Amata alibaki kapigwa na bumbuwazi, ‘Mwenyeji, mwenyeji wangu,’ alijiuliaza, kengele za hatari zikalia kichwani mwake, akainama kuchukua yale magazeti lakini kabla hajayachukua kutoka pale mezani, akasita, akatazama saa yake, muda ulikuwa umekwenda sana, akaachana nay ale magazeti na kujiandaa kwenda kuoga.

Dakika chache zilimpita akiwa maliwato na alipomaliza, aakaufungua mlango, akasimama ghafla, akatupa macho yake juu ya kitanda kikubwa kilichopo katika chumba hicho hakuamini anachokiona, akafikicha macho kana kwamba anachokiona ni kiini macho.

“Come to me boy..” sauti ya msichana yule aliyekuja na magazeti ilimfikia tena Amata masikioni, akamtazama kwa makini msichana huyu mrembo aliyejilaza kitandani na kujifunika shuka mpaka maeneo ya kifuani na kuishika kwa mkono mmoja huku mwingine ukifanya ishara ya kumuita Amata kitandani. Lilikuwa ni jicho baya na kali la Amata lililomfanya yule msichana kuurudisha mkono wake chini na kupatwa na sura ya woga. Amata akautazama mlango ambao yeye aliufunga lakini alishangaa huyu msichana kapita vipi mpaka kujitoma ndani ya chumba hicho, kisha akarudisha macho yake pale kitandani, “Toka!” alimuamuru yule msichana, lakini hakuonekana kuitii amri hiyo, “Mmmm boy, kwa nini unanifukuza wakati nimekuja kukuburudisha?”

alianza kutumia silaha ya sauti yake kumlainisha Amata, “Tokaaaa!” Amata aling’aka kwa hasira huku akimfuata yule msichana pale kitandani, yule msichana akanyanyuka haraka na kukiacha kitanda kile, akasimama pembeni akiwa uchi wa mnyama, akachukua nguo zake na kuzivaa kisha akaufungua mlango na kutoka nje. Kamanda Amata akakiendea kioo cha ukutani na kujitazama kisha akaanza kuvaa suti yake nadhifu aliyoichagua kwa siku hiyo. Akiwa pale kiooni alihisi mlango ukifunguliwa kwa mara nyingine, kabla hajageuka aksikia sauti kutoka nyuma yake, “Tulia hivyohivyo, ukijifanya mjuzi, tunaondoka na pumzi yako,” Amata akaona sasa mambo si mambo, akaendelea kujiandaa huku mtutu wa bastola yenye kiwambo cha sauti ikimtazama.

“Ok, umependeza, sasa utaondoka na sisi, bwana Bill anataka kukukona usiku huu kwa maana hana uhakika kama jua la kesho utaliona,” yule jamaa alimwambia Amata huku akimruhusu kutangulia mlangoni ambapo palikuwa na watu wengine wawili, hamna ujanja. Kamanda Amata aliongoza taratibu nje ya chumba kile na kuifikia korido ndefu, mbele yake kulikuwa na mtu mmoja, nyuma yake kulikuwa na mwingine yule mwenye bastola ambayo sasa alikuwa ameifunika kwa koti lake la suti kiasi kwamba kwa mtu mwingine hasingeweza kujua kama mkoni hapo kuna mguu wa kuku. Waliingi ndani ya lifti kwa mtindo huo huo, hakuna aliyeongea kati yao, wakateremka mpaka chini na kuongoza kwenye gari moja la kifahari aina ya Cardilac, gari ya kifahari na gharama ya hali ya juu, Amata alitangulizwa kuingia ndani kiti cha nyuma kisha wawili kati ya wale watatu wakaingia mmoja huku na mwingine kule, yule mwenye bastola akiwa mmoja wao, mwingine wa tatu akaingia siti ya mbele.

“Karibu sana Amata,” ilikuwa sauti ile tamu ya mrembo aliyeongea huku akigeuka nyuma na kumtolea tabasamu pana Kamanda. Taratibu waliyaacha maegesho ya hotele ile na kutokomea mjini, barabara chache na foleni za hapa na pale katika jiji hilo la Nairobi ziliwafanya wachukue muda kidogo kufika wanapopakusudia, mwanadada yule aliyekuwa akiendesha gari hiyo kwa umahiri mkubwa alikatiza kwatika vichochoro mbalimbali na kutimiza kusudio lake.

Mguu wa kulia wa mwanadada yule ulihama kutoka katika pedeli ya mafuta na kukanyaga ile ya breki huku mikono yake ikiuzungusha usukani kwa kidole kimoja kuingia katika maegesho ya hoteli ya Safari Park.

Wote wakashuka na yule mwanadada alitangulia kuelekea ndani ya hotel ile akifuatiwa na wale wengine wakati Kamanda Amata alikuwa katikati ya wote, wakaingia na kupita mapokezi kisha kuingia upande mwingine na kuchukua lifti kushuka ghorofa moja chini, walipotoka walikaribishwa na maandishi makubwa ya kuwakawaka yaliyosomeka, Safari Park Casino, casino ya kisasa iliyojengwa chini ya ardhi katika hotel hiyo, mlangoni walisimama wazaume wawili waliovalia suti nyeusi na kuonekana wameshiba kimazoezi, walikuwa wamesimama mithili ya sanamu ya bismini.

“Clean!” mmoja wa wale waliomtangulia Amata alitamka neon hilo akimaanisha hakuna shida, mara mlango wa kioo ukafunguka na wote wakaingia ndani. Taa za rangi mbali mbali ziliujaza ukumbi huo ambao ulionekana kuwa na shughuli nyingi, wanaocheza kamali walikuwapo, wacheza uchi nao walilipamba jukwaa wakicheza miziki yao michafu, waliokuwa wakinyonyana ndimi hadharani nao hawakukosa, wale waliokana jinsia zo hawakuwa mbali, ilimradi tu dhambi zote zilihifadhiwa ndani ya casino hilo.

“Huku tafadhali,” Amata alielekezwa ngazi ndefu zilizokuwa zikipanda juu, akazifuata bila ubishi mpaka juu, pale wale wasindikizaji wakamuacha na kupokelewa na wengine kisha akaingizwa ndani ya chumba safi na nadhifu kilichoja samani za gharama ya hali ya juu, mbele yake kulikuwa na mtu mnene amaye alisimama na kuja kumlaki kwa bashasha, “Oooh Kamnda Amata, karibu sana, nisingefurahi kama nisingeonana nawe leo hii, karibu sana,” Bill alimkaribisha Amata na kumuongoza kitini, kisha akampatia glass yenye kinywaji na kuketi katika mtindo wa kutazamana.

˜˜˜

Akiwa kwa mwendo wa miguu huku akipiga mruzi usiku huo, Melchior Ndege alikuwa akipita mbele ya hotel hiyo ya Safari Park, mara akapitwa na gari moja ya kupendeza inayovutia macho, akasimama kuitazama gari ile, Cardillac ya bluu nyeusi, iliyokwenda na kuegeshwa kwa utulivu. Lakini alipata mshtuko baada ya kuwaona wale walioshuka kutoka garini, aliwatazama kwa makini na kuoamua kubadili uelekeo wa safari yake. Melchior aliyaamini macho yake yaliyomwambia kuwa umuonaye ndiye Kamanda Amata, ‘Shiiit, amefika lini?’ alijiuliza na kusukuti kwa sekunde chache kabla kuruhusu miguu yake kuamriwa na ubongo juu ya lile linalopaswa kutendwa kwa wakati huo.

Alipotazama vizuri, kwa macho yake ya kipelelezi akajua wazi kuwa Kamanda alikuwa kwenye hatari, akavuka kijibarabara kidogo na kuelekea mlango mkubwa wa hotel ile kisha akaingia ndani, alipofika mapokezi hakutaka kupoteza muda kwani aliwaona wapi wameingilia, akafuata, wakati wao wakifunga mlango wa lifti kuteremka chini yeye akazifuata ngazi zinazoelekea hukohuko chini. Alizuiliwa mlangoni na kupekuliwa, “Haturuhusu kuingia na silaha, weak pale unapotoka utaichukua.” Melchior alisogea kwenye meza ndogo ambayo ilikaliwa na mwanadada mrembo akaichukua bastola ya Melchior na kumpatia kadi maalum ya kumbukumbu.

Akaelekea kaunta na kuketi juu ya kiti kimoja kirefu mbele ya kaunta hiyo. Akiwa anakunywa kinywaji chake taratibu huku macho yake akiwa kayaongoa kule wlikopelekwa Kamanda Amata, ambapo palitenganishwa na ukumbi mkubwa kwa vioo maalum vinavyoruhusu mtu wa ndani kuweza kuona kinachoendelea ukumbini lakini yule wa ukumbini asiweze kujua nini kinaendendele ndani ya chumba kile. Melchior akatoa miwani yake maalumu na kuipachika usoni, miwani hii ilikuwa na madini ambayo yaliweza kupenya kwenye kioo cha aina yoyote pia yaliweza kukuruhusu kuona mtu kama amebeba silaha au vipi, maana iliruhusu kuona vitu vigumu tu vilivyo mwilini mwa mtu.

Alimuona Kamnda Amata akiwa na Bill wakizungumza, lakini hakuweza kujua wanazungumza nini, aliwatazama walinzi wa mlango wakuingia kule juu aliwaona wakiwa na bastola mbili kila mmoja, kisha akawatazama wafanyakazi wa casino hiyo na kuona kila mmoja alivyoipachika silaha yake, kisha akayarudisha macho yake na kuyatuliza kule aliko Kamanda Amata na kuendelea kuona kinachojiri, huku akiendelea kunywa kinywaji chake. Mara alihisi, akipapaswa kwa nyuma maeneo ya kiunoni, akageuka na kukutana macho na mwanamke mshumami, aliyejiremba akarembeka,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni