MAUAJI YA KASISI (21)

Zephiline F Ezekiel
MAUAJI YA KASISI (21)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... “Wewe unamtaka Bill? Lakini kuna kesi nyingine hapa inaungana nay a Bill. Kiasi kwamba lazima na hiyo uifanyie kazi ili upate picha kamili,” ndege alimwambia Kamanda. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Yeah, ya mauaji ya kasisi?” Kamanda aliuliza kupata uhakika. “Ndiyo hiyo, kwa sababu inaonekana Bill anahusika kwa namna moja au nyingine,” “Nimeshaanza kuifatilia ila nataka nimfahamu mtu anayeitwa sergeant Maria kwa kuwa yeye nasikia ndio kashika hiyo kesi,” Kamanda alimuelezea Ndege . “Usijali, kumpata Maria si kazi ngumu,” Ndege akajibu huku akiizungusha gari kwenye mzunguko wa Dagoreti corner , mtaa wa kwanza, wa pili, nyumba ya tano, Ndege alipita kama hataki kusimama mahali hapo na mbele alikunja kona na kuegesha gari karibu na duka noja kubwa la bidhaa mbalimbali, wakateremka, kwanza Ndege akaingia dukani na kununua …