MAUAJI YA KASISI (23)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU ILIPOISHIA... Ilikuwa ni usiku ambao Madam S alibanwa na kazi nyingi, akikumbuka kikao chake cha machana na watu wengine wa idara ya usalama wa taifa alihisi jambo jipya hasa kutokana na kutoroka kwa Amata hospitali na kwenda kusikojulikana. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Walimtuhumu kuwa ni mtovu wa nidhamu, asiyejali yale anayoambiwa na wakubwa wake, wote kwa sauti moja wakaona Kamanda Amata anyang’anywe cheo chake hasa kutokana na uzembe anaouonesha kwenye kazi za maana kama hizo. Ijapokuwa mvutano ulikuwa mkubwa sana kati ya wana kikao, lakini mtu mmoja alionekana kushikia bango sana kamanda ashushwe cheo, kwa kuwa hafai tena, lakini kabl;a ya yote atafutwe, arudishwe kasha apewe barua ya kushushwa cheo na abadilishiwe idara. Kichwa kilizunguka, Madam S alibaki njia panda, hoja imepitishwa lakini bado moyoni mwake anamhitaji …