MAUAJI YA KASISI (5)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... “Fr, ni nini, nieleze nikusaidie” Fr Joe aliinuka kitini na kulmuendea Fr Gichuru huku akimueleza maneno hayo, alitoa kitambaa chake na kumfuta machozi. Fr Gichuru aliinuka kitini pamoja na Fr Joe wakatoka nje kwenye kabustani kadogo na kutembeatembea wakiwa na rozali zao mikononi. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Fr Joe! Nililala kama kawaida mara baada ya masifu ya jioni, katikati ya usiku huo niliota nipo Roma makao makuu ya kanisa, nipo juu kabisa ya mnara wa jengo hilo, niliangalia chini palikuwa parefu sana, isingekuwa rahisi hata kuruka, sikuwa na msaada, nililia na machozi yangu yalikuwa ni machozi ya damu, yalitirirka na kulowesha kanzu yangu nyeupe lakini hayakufika chini bali yote yalituama kifuani upande wa moyo wangu. Nilimuona Malaika kasimama mbele yangu mkononi kashika kikombe, akanisogelea akanipa kikombe hicho…