MAUAJI YA KASISI (7)

Zephiline F Ezekiel
MAUAJI YA KASISI (7)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... “Salama tu Fr, leo tumeonana tena, sina mazungumzo mengi na wewe leo ila ninachohitaji ni ile Monstrance , tuambie ilipo tukaichukue usiku huu kisha tutakuachia huru, mimi sipendi kumwaga damu isiyo na hatia kama yako Reverent Father Frederick Gichuru ” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Bill aliongea kwa pozi huku akiruhusu pumzi zake kumtoka kwa shida. Fr Gichuru alimtazama mtu huyu mnene na kisha kuwatazama wale wengine watano, mara moja akamtambua Gichui , yule jambazi waliyekutana naye kanisani akipekuwa makabati. “Muulizeni huyu kama ameiona” alimueleza Bill huku akimtazama Gichui, “Ile ni mali ya kanisa ninyi mnaitakia nini?” akawauliza. Wote wakatazamana. “Gichuru, kama hutaki kutueleza utataulazimisha kufanya kitu tusichokitaka, haya mi natoka nawaacha vijana wangu utawaelekeza” Bill mtu mnene alizungumza na kutoka katika kile…