MAUAJI YA KASISI (9)
Jina: MAUAJI YA KASISI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... mara alivuta kabrasha hili mara lile lakini hakujua anachotaka kufanya kwa muda huo, akiwa katika hali hiyo aligutushwa na hodi iliyogongwa mlangoni mwake kisha mwanamama mmoja aliyevalia kiraia aliingia kwa ukakamavu na kubana miguu yote miwili kuonesha nidhamu ya kijeshi. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Jambo afande?” Inspekta asitoti alisabahi “Jambo!” alijibu yule mwanamke au kana anavyojullkana Sargeant Maria , “Afande natoa taarifa ya kuumia afande Otho’ katika mapano na moja kati ya majambazi tunayoyatafuta” “Oh! Pole sana afande, nieleze kwa kina,” Inspekta Saitoti aliomba aelezwe huku akimpa ishara ya kuketi kitini sergeant Maria. Alipokwishakueleza kinagaubaga kila kilichojiri, alitulia kitini kimya akisubiri amri ya boss wake itasema nini, mara Inspekta Saitoti alikohoa kuashiria kuuvunja ukimya ule. “Ok! Sasa kutokana n…