Mtunzi: Latifa
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Basi tuliongea apo adi nikajiisi usingizi nikalala nayeye pia alipanda kitandani kulala tulishtuka Asubuhi kumekucha aliewahi kutoka kitandani Vitalis akaandaa kifungua kinywa mimi bado kuinuka nilikuwa siwezi akaja kunisaidia nakunipeleka bafuni kuoga nilipotoka nikashangaa anatoa mfuko uliokuwa na nguo ndani mpya nakunipa nivae
KAMA UNAISOMA SIMULIZI HII TOFAUTI NA KWENYE APP YA CnZ Media
IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI
IPAKUE ILI KUPATA SIMULIZI KWA WAKATI SAHIHI
👉GUSA INSTALL👈
ENDELEA...
"Nguo za mwanamke wako ndo unanipa mimi?"
"Lisa jamani izi mpya nimenunua jana nilipoenda kukuchukulia dawa"
Alisema basi nikavaa gauni moja akainishika mikono nakunisaidia kutembea adi sebuleni.
Ambapo alikuwa ameshaandaa chai tukajumuika kunywa pamoja, siku iyo iliisha tukiwa tumeshinda wote ilikuwa jumapili
"Kesho ni siku ya kazi Vitalis itakuwaje?"
Nilimuuliza
"Nitaenda mimi kusimamia we nitakuacha apa"
"Kwaiyo nishakuwa mkeo nyumbani kwetu siendi?"
Nilimuuliza
"Lisa jamani subiri ukipona utaenda"
"Sitaki mimi nipeleke sasa"
"Ivi babayako akikuona unatembea ivyo utamwambia umetoka kufanyaje?"
Aliniuliza nikakosa lakujibu ikabidi niwe mpole tu.
Basi siku iyo ikapita adi kesho yake Asubuhi Vitalis akaondoka kazini nakuniacha nyumbani kwake nilikuwa naweza kutembea kidogo nikajaribu kuzunguka nyumba nzima nikikagua isijekuwa anamke anikute nifumaniwe lakini tofauti na mawazo yangu sikukuta kitu chochote cha mwanamke nyumba nzima.
Jioni saa kumi alirudi akaniletea zawadi nakufurahi amenikuta alijua nitaondoka basi tukashinda wote pia wiki nzima nilimaliza nipo kwake hali yangu ikawa nzuri akanirudisha nyumbani.
*****
Nilichukia sana Vitalis kuniingilia mwilini sikupenda sababu sikuona faida yakufanya mapenzi au kuwa na mwanaume wakati kizazi sina nilichoamua ni kuwa pekeyangu bila uhusiano.
sikutaka mawasiliano nae kazini si kwenda tena alipopiga simu nilimkatia mwisho nikamuweka blacklist asinipate.
Wazazi wangu walishangaa kwanini siendi kazi nipo tu nyumbani nikawadanganya nipo likizo mwezi moja ikapita sijaenda kazini nakuwapa hofu wazazi wangu.
"Ivi wewe Lisa kazi umeacha au likizo gani miezi inakatika upo tu nyumbani?"
"Baba jamani likizo nipo"
"Mmh sio bure we kuna kitu umefanya au umegombana na boss wako?"
Aliuliza mama kabla sijajibu tukasikia honi inapigwa nje akatoka baba kwenda kuangalia ni nani, Mara nikasikia sauti ya Vitalis moyo ulishtuka sana na kweli aliingia baba akiwa ameongozana na Vitalis nilipowaona nikainuka nakukimbilia chumbani kwangu.
Wote walishangaa kwanini amekuja Vitalis mimi nikaondoka.
Basi walimkaribisha vizuri akapewa na kinywaji kabisa
"Bora umekuja maana uyu Lisa hatumuelewi anamatatizo gani kazini ataki kuja sasa afadhari umekuja wewe utuambie ameacha kazi au ndo likizo kama anavyosema?"
Baba akaanza maongezi.
"Kiukweli ata mimi nashangaa Lisa haji kazini bila sababu nimempigia simu apokei zaidi kaniweka blacklist simpati kabisa ndo maana nimeamua nije apa kuuliza labda mgonjwa"
Alisema Vitalis
"Ebu ngoja nikamuite kwanza"
Alisema Mama nakuinuka akaja chumbani kwangu.
"Mama sitaki kumuona uyo mtu"
"Kwani amefanyaje si boss wako yule unajua watu wanahangaika kutafuta kazi wanakosa we umepata unaichezea eeh ebu inuka uko"
Mama akanivuta mkono nakunitoa nje uku nimechukia.
"Mtoto mshenzi uyu siku izi kupata kazi ni tabu yeye anafatwa na boss wake adi nyumbani bado anaringa"
Mama aliendelea kufoka
"Basi Mama msamehe bure"
Vitalis akanitetea mi nilikaa kimya tu sikuongea neno.
"Aya Lisa tueleze kwanini utaki kwenda kazini?"
Baba akauliza nilitamani kusema ukweli ila niliona ni jambo la aibu kusema nimefanya mapenzi na boss wangu ata chakujitetea sikuwa nacho.
"Kwaiyo huna lakusema basi kesho jiandae urudi kazini sitaki kuona sura yako apa uvivu tu umekujaa"
Alisema Baba nilimsikiliza sikumjibu.
Basi waliendelea na maongezi yao adi alipoaga Vitalis nakuondoka namimi nikarudi chumbani kwangu.
Asubuhi ilifika nikajiandaa tena Baba akanipeleka adi ofisini kabisa, wafanyakazi wezangu waliponiona walinishangaa muda mrefu sikwenda
"Jamani tumekumisi ulikuwa wapi?"
Aliniuliza Irene
"Nilisafiri kijijini nilikuwa na mgonjwa"
"Pole mwaya"
Basi kila alieniona maswali ndo ayo nilikuwa wapi niliwaona wanafki namba yangu wanayo kwanini wasinitafute lakini sikujali nikawapotezea.
Basi nilienda moja kwa moja adi ofisini kwa boss nikakutana na Vitalis ambae alifurahi kuniona akanikabidhi iyo ofisi nibaki nayeye akatoka kuelekea bandarini.
Nilikuwa mchovu sana najisikia kulala tu muda wote mwili umechoka nimekuwa mvivu alafu sura yangu ikaanza kuaribika kutoka mapele mengi usoni.
Wiki moja tu nikaenda kazini baada ya apo nikawa nyumbani hali iyo iliwaogopesha wazazi wangu sana.
"Wewe Lisa unanini kwani?"
"Mama naisi homa tu"
"Yani homa adi vyakula unachagua homa gani iyo au unamimba?"
"Mamaaa mimba nipate wapi mimi mgumba"
"Kesho twende hospital ukapime"
Alisema mama ilikuwa usiku bado basi Asubuhi ilipofika tukaongozana wote adi hospital kwake Muhimbili akamfata Daktari mmoja ofisini kwake anichukue vipimo.
"Nikikupima mimi utasema nakusingizia wote tukae apa tungoje majibu"
Alisema mama tukakaa pamoja.
Baada ya muda mchache akaja yule Daktari alikaa kwenye kiti nakumpa mama karatasi la majibu.
"Hongera sana Dokta Lucy mwanao Lisa ni mjamzito wa mwezi mmoja na wiki mbili"
Alisema uyo Daktari Emmanuel Sanders.
Sikuamini nilichosikia mama akuweza kuongea machozi ya furaha yalimtoka akanisogelea nakunikumbatia uku analia furaha ikawa msiba.
"Siamini mwanangu walikuita mgumba wewe wakakuita tasa leo umebeba mimba kweli Mungu mkubwa"
Alisema Mama akilia adi akanifanya namimi machozi ya uchungu yanitoke sikuamini.
Basi tulimshukuru Daktari tukaondoka kurudi nyumbani.
****
"Lisa ebu nambie hii mimba ya nani?"
Mama akataka kujua sikuona sababu yakuficha nikamueleza ya boss wangu akashtuka
"Sawa ngoja babayako arudi tumueleze ikiwezekana aitwe uyo mwanaume"
Alisema mama nikamuelewa.
Usiku alirudi Baba akaelezwa ata yeye hakuamini kama nina mimba alifurahi sana.
"Basi inabidi aitwe Vitalis"
Alisema Baba nikakubali.
Niliingia ndani nakutoa simu yangu iliyojaa meseji nyingi nikilalamikiwa kazini siendi kwanini, nikaamua nimpigie simu
"Haloo Lisa kwanini hauji kazini jamani?"
"Vitalis bwana mimi naumwa"
"Pole Mama nini tatizo"
"Vitalis nina mimba nimetoka kupima na Mama leo na mwanaume nilielala nae ni wewe tu"
"Uuuu...naaa...semaje?"
Aliuliza kwa mshtuko
"Nina mimba yako"
"Ooh asante mungu hatimae ndoto zangu zakuitwa Baba zimetimia Lisa nakuomba usitoe iyo mimba"
"Siwezi kutoa na wazazi wangu wanakuitaji"
"Nakuja jioni nikimaliza kazi"
Vitalis alikuwa na furaha sana sababu alinipenda lakini mimi sikuwa tayari kuwa nae mimba ndo imefanya tuungane sasa alifurahi sana.
Nikatoka kuwapa taharifa Baba na Mama kuwa Vitalis atakuja jioni wote wakasema sawa.
Basi nilijifungia ndani kulala nilikuwa mvivu sana kulala kila muda.
Hatimae jioni ilifika akaja Vitalis alipokelewa vizuri nakukaribishwa ndani ambapo maongezi yakaanza aliulizwa kuhusu mimba akakubali yeye ndo muhusika.
Baba akauliza kuhusu ndoa akasema yupo tayari kunioa ila nilikataa angoje adi nitapojifungua sitaki kuolewa na mimba akakubali lakini aliomba anichukue nikaishi nae adi muda wakujifungua ukifika nirudi nyumbani wakamkubalia nikaulizwa na mimi kama nipo tayari sikuweza kukataa nilikubali basi tukaondoka wote sikuchukua kitu changu chochote kilakitu alisema ataninunulia.
Maisha mapya yakaanza tukiwa pamoja kama mke na mume uku tumbo langu likianza kuonekana sasa nakunifanya muda wote nijiisi nafuraha nilisahau machungu yote yakuitwa mgumba.
"Ivi ukizaa mtoto wa kike tumuite nani?"
Aliniuliza Baba kijacho wangu tulipokuwa tumekaa sebuleni.
"Napenda aitwe Happy sababu yeye ndo furaha yangu"
"Ooh jina zuri sana na wakiume je?"
"Aitwe Money"
Nilimwambia nakumfanya acheke sana
"Yani we mwanamke unavituko sana mi nataka wakiume aitwe junior"
Alisema akizidi kucheka
"Sawa Junior jina zuri pia"
Maisha yetu yalijaa furaha na upendo hakika tulipendana sana akuna alietamani kuwa mbali na mwenzake.
Tulikuwa na furaha tukimsubiri mtoto wetu kwa hamu japo mimba ilikuwa bado nina miezi minne.
Siku moja tukiwa tupo hospital clinik alinipeleka Baba kijacho tukiwa tunatoka nje tukakutana na Harvey akiwa na ndugu zake mama, dada na yule mamayake mdogo Neema nilifurahi sana kuwaona nikawafata kuwasalimia wote hawakuamini waliponiona nina mimba
"Haaa Lisa!"
Aliita kwa mshangao Harvey
"Ndo mie mlininyanyasa sana mkanisimanga sizai kumbe we mwanaume ndo kizazi huna na nyie wengine mkajishaua kuniona mi kama takataka leo mungu kaniona sasa mimba ndo hii nimebeba aya nambie we malaya wa field unawatoto wangapi adi sasa?"
Nilimuuliza Harvey
"Lisa unanivunjia heshima unawadharau adi ndugu zangu"
Alisema Harvey akiwa amepandwa na hasira akanisogelea anipige Vitalis akawahi
"Unaona hali ya mke wangu ilivyo aya mguse kama ujakaa gerezani maisha yako yote"
Alisema Vitalis
"Usinitishe wewe kwanza mwanamke mwenyewe tasa uyo ameweka matambala unilushe roho mimi"
Alisema Harvey nakumfanya Vitalis acheke
"Dah pole sana i think huna nguvu za kiume mi maramoja tu mimba ila we umekaa nae miaka bila kitu poleyako alafu siwezi kubishana na mwendaazimu mi pia nitaonekana sina akili Lisa mkewangu tuondoke"
Alimaliza kusema Vitalis akanishika mkono tukawa tunaondoka.
"Nitakukomesha Lisa"
Alisema Neema mamayake mdogo Harvey nikataka nirudi kumjibu lakini Vitalis alinikataza
"Achana nao bwana"
Alisema tukapanda gari nakurudi nyumbani.
"Nambie leo utakula nini mama watoto?"
"Ndizi na nyama mchemsho"
"Yani unavyopenda mchemsho wewe ilo toto litatoka bongee"
Alisema baba kijacho wangu tukacheka wote.
Tuliishi vizuri tukipendana sana zaidi fikra zetu zikiwa kwenye mimba kila mmoja alitamani uyo mtoto azaliwe ata kesho.
***
Siku zilizidi kusonga mimba ikafikisha miezi mitano sasa, Siku moja nikiwa bafuni naoga niliteleza nakuanguka bahati nzuri nilikaa kitako sikuangukia tumbo tatizo likaja sikuweza kusimama pia nilisikia maumivu makali kiunoni mwangu nikajitaidi kusota adi chumbani nilipochukua simu nakumpigia mumewangu.
"Nime..doo..ndokaaaa...bafuni.....njooo naa uu...
Sikuweza kumalizia nilipoteza fahamu sikujua kilichoendelea tena, nilikuja kuamka nakujikuta kitandani.
"Daktari Daktari amefumbua macho"
Nilisikia sauti ya mwanamke ikisema ivyo sikuelewa anamaanisha nini.
Mara nikamuona mwanaume amevaa koti kubwa akaja nakunisogelea.
USIKOSE MWENDELEZO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi