RANIA (20)

Zephiline F Ezekiel
RANIA (20)
JINA: RANIA Mtunzi: Teddy Mibaraka SEHEMU YA ISHIRINI ILIPOISHIA... Mama.. Ni kuhusi Rania... Alisema Dom Amekuaje Rania?.. Aliuliza Rai... Wakati huo Rania alikua amekaribia kwao Dom maana hapakua mbali sana.... SASA ENDELEA.. Mama..kwanza kuna mauaji yana.....alisema Dom kisha mama yake akamkatisha. Najua mwanangu... Watu wameshauawa wengi zaidi ya unaowajua...alisema Rai. Rania ameshachukua hatua yoyote?... Aliuliza Rai. Ndo najaribu kumzuia maana hana nguvu ya kutosha kupambana na ufalme... Alisema Dom. Mwache usimzuie...alisema Rai. Mama!!!!...aliita Rai kwa mshtuko. Ndio muda wake...unahisi kama akisubiri nguvu atazipata lini?.. Aliuliza Rai. Dom alikaa kimya kidogo. Mwanangu, Rania alizaliwa kwa ajili ya hili jambo... Kama umeamua kumpenda Rania inabidi ujikane...kubaliana na hatari zote... Alisema Rai. Nakuombea ufanikiwe ili angalau ukamilishe kazi niliyopewa mimi ya kumlinda Rania na imenishinda....alisema Rai. Mama..hivi kwani ni nani aliekupa hiyo kazi?..aliuliza Dom. Ni babu yako mzaa baba …