MAMA MWENYE NYUMBA (21)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA ILIPOISHIA... Japo Suzan moyoni alichukizwa na mzee Mashaka huku akiona uwepo wake pale umesababisha hashindwe kumwita mpenzi wake Edgar, lakini alijitaidi kumwongelesha maneno mazuri mzee Mashaka ili hasigundue kama moyoni anamchukia kwa tabia yake aliyo ionyesha jana pale Full dose SASA ENDELEA... Lakini licha yakutumia muda mrefu sana, wakiongea kuhusu mapenzi yao, ilikuwa tofauti kwa mzee Mashaka ambae alikuwa anavuta muda tu, iliaende kwenye mishe mishe zake, huku pia akiwaza kupata demu wakukata kiu faster, ilisha timia saa sita na nusu “eti baby leo wewe hauendi shamba namama ?” swali hilo lilimtoa mzee Mashaka kwenye mawazo yake ya kutafuta mkata kiu, “hapana , hakuna safari ya shamba week hii labda week hijayo” hapo kengele ya tahadhari ika gonga kichwani kwa Suzan, akajichekesha kidogo, “ok! nilijuwa unaenda, nilitaka nikuagize madafu , kwani mama haendi?” aliuliza swali la mtego Suzan akataka kujuwa lengo la…