MAMA MWENYE NYUMBA (34)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA THELATHINI NA NNE ILIPOISHIA... Wakati huo huo wakasikia hodi, maana kunamtu alikuja kuwa tembelea, mama Edgar akaenda kumtazama huyo mpigaji wa hodi, alikuwa ni mzee Ngonyani SASA ENDELEA... “Karibu shemeji, pita ndani” alikaribisha mama edgar na mzee Ngonyani akaingia ndani, “vipi huyi bwana ameamkaje?” aliuliza mzee ngonyani akitaka kujuwa hali ya mgonjwa, “kwakweli hali ina zidi kubadilika, amevimba vimba mpaka inatisha” alisema mama Edgar akionyesha kwa mfano, “ingia ndani ukamwone” mzee Ngonyani kusiki hivyo akaingia chumbani, kwenda kumtazama rafiki yake, nikweli alimkuta akiwa katika hali mbaya, tofauti na alivyo mwacha jana, “shemeji huyu bwana anaitajika apelekwe hospitali haraka sana, na kwahali yake hatuwezi kutumia baiskeli , wala pikipiki, hapa ni gari tu!” aliongea mzee Ngonyani, nakumfanya mma Edgar apige kelele, “huuuwiiiiiiiiii, mao nene” ela yenyewe nitaitoa wapi mimi” Hapo sasa ika ni kuzungu zungu, maana ni kweli …