MAMA MWENYE NYUMBA (38)

Zephiline F Ezekiel
MAMA MWENYE NYUMBA (38)
JINA: MAMA MWENYE NYUMBA Mwandishi: Mbogo Edgar SEHEMU YA THELATHINI NA NANE ILIPOISHIA... Mke wa bwana kazole alijikuta akishikwa na hamu ya kuchungulia mle ndani ilikuakikisha kama kweli sauti ile ni ya mume wake.... akasogea karibu na maua, ambayo yalikuwa yame mtenga nisha na kumzuwia asiweze kumwona vizuri, huyo alie zani ni mume wake SASA ENDELEA... Alipo sogea na kuweza kuchungulia vizuri, kweli alimwona mume wake akiwa amekaa kwenye kiti sambamba na mwanamke mmoja kibonge, ambae alikuwa anamchezea chezea kichwani kimahaba, huku mbele yao palionekana chupa za ia zikielekea kuisha, na sahani zilizo jaa mifupa ya kuku zikwa chini ya meza, kwanza kabisa mke wa bwana kazole hakuamini kuwa yule ni mume wake maana alicho juwa yeye hawakuwa na fedha ya kutosha, ila macho yake yali mshawishi kuamini kuwa ni mume wake kwasababu nikweli alikuwa anamwona mbele yake, akiwa ameshikilia noti za elfu kumi kumi tatu, akiziitaji kumkabidhi mhudumu, ambae alikuwa anakuja mbele ya mume wake huyo, aliye…