SEHEMU YA KUMI
Naam hao walikua ni vijana wa Joel wakiwa wanabishana juu ya nani aanze kumuingilia Suzan ambae kwa muda huo alikuwa amepoteza fahamu na wakati huo Joel alikuwa yupo ndani ya jengo lililoonekana la kisasa katika pori la Bagamoyo mahali ambapo Suzan ndipo alipokua na hata amri ya kubakwa kwa Suzan ni yeye ndiye aliyeitoaSASA ENDELEA...
Wakati huo yeye alikua amejilaza katika sofa lililokuwa sebuleni huku akitazama runinga aina ya flat screen nchi 32, muda wote ambao vijana wake walikua wakibishana juu ya nani aanze kumbaka Suzan yeye alikuwa akiwasikia vyema na alikua akitabasamu huku akiamini kwamba muda mchache ujao atakua amemvurugia Michael maisha yake kwa ujumla. Wakati vijana wale wakiendelea kubishana, ghafla walianza kuona upepo ukivuma kuelekea sehemu ambayo walikuwepo na wakati wakitahamaki kufunga na kufungua vijana nane tayari walikua wapo chini huku miili yao ikiwa haina uhai, hivyo kufanya idadi ya vijana wale kubaki wanne ambao nao ndani ya sekunde kumi, miili yao ilikua haina uhai, naam alikua ni Michael akiwa katika vazi jeusi la kininja huku mkononi akiwa kashika upanga wake wa kininja na vijana wale kumi wote aliwauwa kwa kuwachinja, baada ya kumaliza vijana wote, alirudi mpaka katika kichaka kimoja na kubeba lile box ambalo ndani yake kilikuwepo kichwa cha James ambae alikua ndie mdogo wa pekee wa Joel, alienda kukihifadhi sehemu salama kisha akaenda eneo ambalo mpenzi wake alikuwa amefungwa na alipofika alimpatia huduma ya kwanza na baada ya nusu saa Suzan alirejewa na fahamu.. “We ni nani?” aliuliza Suzan katika hali ya uoga baada ya kumuona mtu akiwa kavaa kininja “Ni mimi mpenzi wako, vipi unaendeleaje?” alijibu Michael huku akitoa kofia ya kininja kichwani mwake na sura yake ikaonekana vyema “Haa!! yani kumbe wewe ni ninja mpenzi, na kwanini ulinificha juu ya jambo hilo?” Suzan alishangaa na kuuliza katika hali ya masikitiko
“Haina haja ya kuwa na hofu, sasa hivi yakupasa urudi nyumbani, mimi kuna jambo bado namalizia huku, tutakuja kuongea nyumbani, sawa mpenzi?” “Sawa mume wangu nimekuelewa, sasa nyumbani narudije?” Suzan alikubali kurudi nyumbani na kumuuliza Michael ni njia gani atatumia kurudi nyumbani “Usijali kuna gari ile pale nimekuja nayo, wewe nenda mimi nitakuja kesho” aliongea Michael huku akimuinua mpenzi wake na kumpeleka sehemu aliyoficha gari lake, na alipohakikisha Suzan ameshakaa katika usukani, alimbusu na kumtaki safari njema na hapo Suzan safari ya kwenda nyumbani Mbezi ilianza na muda huo ilikua yapata saa kumi na moja kasoro alfajiri..
********** ************* **********
Mida ya saa kumi na mbili kamili asubuhi Joel aliamka katika chumba chake lakini alishangazwa na ukimya uliokuwa katika eneo lile, alipochungulia dirishani almanusra azimie, aliwaona vijana wake wote wakiwa wamekufa tena kwa kuchinjwa kama kuku, hakika alipagawa sana, alikurupuka na kuelekea sebuleni na hapo alipiga mueleka na kuinuka na kabla hajatoka nje alikuta kuna box limetengwa katika meza ya chakula, alilisogelea lile box kwa tahadhari akidhani kwamba ni bomu, alipolifungua alijikuta anakaa chini kutokana na miguu kushindwa kuhimili uzito wa kiwiliwili, aliona kichwa cha mdogo wake James huku pembeni pakiwa na kikaratasi ambacho kilionekana kuwa na ujumbe “Siku zote mshahara wa dhambi ni mauti, na hiyo itakua zawadi yako ya mwisho kuiona katika dunia, nipo nje nakusubiri uje nikupe tiketi yako ya kwenda kuzimu, karibu sana” hivyo ndivyo ujumbe ulivyosomeka, Joel alipatwa na hasira kupita kiasi alisimama na kuelekea chumbani kwake ambapo alichukua bunduki yake aina ya SMG(Sub machine gun) ambayo ilikua ina risasi thelathini, aliikoki vyema na kisha kutoka nje, alivyotoka alikutana na mtu akiwa kasimama huku amempa mgongo, alichokifanya ni kuruhusu risasi mfululizo zitoke katika bunduke kuelekea upande aliokua yule mtu, lakini mpaka risasi zimeisha katika bunduki yule mtu alikua bado kasimama vile vile, ilibidi asogee mpaka eneo alilokuwa yule mtu na hapo alipigwa na butwaa baada ya kugundua kua alikua akimimina risasi kwenye kifusi cha majani ambacho kilitengenezwa na kuvalishwa vazi la kininja na huo ni moja ya uchawi ambao maninja hua wanatumia katika mapambano, wakati akitafakari alisikia sauti kutoka nyuma… “Hello Mr Joel, nafikiri ni muda muafaka wa wewe kwenda kuzimu” alikua ni Michael akiwa katika vazi la kininja huku akiwa amening’iniza upanga wake mgongoni Kwakua Joel alikua anahasira na mtu aliyemuua mdogo wake alijizoa pale chini na kuja kwa kasi sehemu ambayo yule ninja alikua amesimama, lakini kabla hajafika, kwa kasi ya ajabu yule ninja aliruka flight kick iliyotua vyema kwenye kifua cha Joel na kumrusha umbali wa sentimita kadhaa, na hapo joel alikua hawezi tena kusimama kutokana na pigo hilo, na kujikuta akiuliza.. “Wewe ni nani? na kwanini unafanya hivi?” aliuliza Joel huku akiwa katika maumivu makali “Naitwa Michael na huo ndio mshahara wa dhambi zote ulizozifanya” alizungumza Michael sambamba na kufua uso wake Joel alipigwa na butwaa baada ya kumuona Michael “Ni….n..i w..e…we. mwana..ha..r…” kabla Joel hajamalizia kauli yake upanga ulitua katika shingo yake na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, na hapo ndipo ukawa mwisho wa Joel “Watu kama ninyi hamstahili kuishi katika dunia hii ya watu wema” alizungumza Michael na kufunika uso wake kwa kofia ile ya kininja nahapo akaonekana kuwa full ninja, hapo alirudisha jambia sehemu yake na kuanza kutafakari jinsi ya kurudi nyumbani “Jamani muuwajiiiiii!! Muuuwajiiii!! Uwiiiiiii jamani wanakijiji!! muuwajiiiii!!” ni sauti ambayo ilimgutua Michael katika mawazo, walikuwa ni kuna mama watano wakiwa wamebeba majembe wakielekea shambani na hapo walijikuta wakipiga kele hizo baada ya kumuona Ninja akiwa amezungukwa na miili kadhaa ambayo ilikuwa imetenganishwa na vichwa vyao, Michael baada ya kuona hali hiyo akajua tayari lishakua tatizo hivyo alichokifanya ni kutupa bomu la kininja na baada ya sekunde kadhaa alitoweka eneo lile kimuujiza… Dakika nusu saa baada ya Michael kutoweka eneo, wanakijiji walikuwa wamefurika eneo la tukio na hazikupita dakika tano, ambulance tano pamoja na defender nne za polisi ziliwasili eneo la tukio, miili ilipakiwa na kwenda kuzikwa na halmashauri kutokana na ndugu wa marehemu kukosekana licha ya kutangazwa zaidi ya wiki nzima katika vyombo vya habari
************ ************* ***************
Zilikatika siku,wiki na hatimae mwaka kupita huku Michael akiendelea vizuri na kazi zake katika benki ya CRDB tawi la posta, Suzan nae alizidi kunawiri na kunekana mpya mbele ya mboni za Michael kila siku, baada ya miaka miwili kupita Michael alipandishwa cheo na kuwa maneger wa benki hiyo ya CRDB tawi la posta kufutia kustaafu kwa Mr Alex ambae umri ulikua umeenda na aliomba kustaafu, ilifanyika tafrija fupi na hapo ndipo Michael aliamua kumvisha mpenzi wake Suzan pete ya uchumba huku zoezi zima likisimamiwa na Mr Alex ambae alimchukulia Michael kama mwanae. Ilikua imepita miezi miwili tangu Michael amvishe pete ya uchumba mpenzi wake Suzan, katika kanisa moja jijini Dar es salaam, Michael na Suzan walikua katika madhabahu huku mchungaji akiwafungisha ndoa, baada ya zoezi la kufunga ndoa kukamilika ambalo lilikua chini ya Mr Alex, Michael alikabidhiwa kipaza sauti ili aweze kuongea neno la mwisho…
“Ndugu waumini wenzangu, napenda niwashukuru kwa wote mliohudhuria katika sherehe hii na kuhakikisha kijana wenu nakamilisha zoezi hili la kufunga ndoa, shukrani za dhati ziende kwa baba yangu mlezi Mr Alex kwa kuwa na mimi katika kila hatua ya maisha yangu, sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea kwa Mungu kila la heri, shukrani zangu zingine ziende kwa mke wangu mpenzi kwa kuwa nami na kuhakikisha nasimama imara katika misukosuko yote na changamoto zote nilizokumbana nazo katika maisha, hakika “You’re my real SUZAN” Michael alizungumza kwa hisia na kanisa zima likafurika kwa shangwe huku wakisema “YES SHE DESERVES TO BE YOU’RE SUZAN”. Michael alimchukua mke wake na kuelekea nyumbani kwake Mbezi ambapo waliendelea na maisha yao kama kawaida na baada ya mwaka mmoja kupita walibahatika kupata mtoto wa kiume na walikubaliana kumuita “ZAWADI” wakiwa na imani kuwa ni Baraka kutoka kwa Mungu, kwapamoja walipiga magoti na kumshukuru Mungu kwa kuwapigania mpaka hapo walipofikia.
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU