SEHEMU YA NNE
Nikashika tama katika hali ya sitofahamu nikaingia ndani kuucheki huo mwili amini usiamini ni mimi kabisa cha ajabu nikajalibu kuushika nikawa nautikisa kwa kusemaSASA ENDELEA...
"Wee pacha wangu hamka hamka hujafa wewe nikiwa naendelea kumtikisa nikastuka baada kusikia sauti ikiniambia "kijana acha kujisumbua bure
wewe tayali ushakufa huna jinsi ya kufanya kucheki akaingia nipe nikupe akiwa na kundi la watu kama mia moja hivi wote wapo kama mimi kila ninae mtazama anakenua meno tu kwa kicheko nikashindwa kutambua mimi mwenyewe ni yupi pale nipe nikupe akaupuliza ule mwili pale kitandani na kuondoka nao nikatoka nnje na kuwaona wakitokomea msituni nikataka kupiga kelele kuwaambia jamani ehee nipe nikupe anaondoka na maiti yenu hukuu, ikanibidi nikae kimya baada kutambua ya kwamba haitosaidia kitu usiku ukawa mrefu sana kwangu nazunguka zunguka tu kama vile nimepewa kazi ya ulinzi nifanye dolia nikimtizama mama analia tu mpaka anatia huruma nikatamani pakuche haraka nipate kufahamu hatma ya ule mwili itakuwaje wanasema nimekufa mbona nipo hai, hasubuhi ikafika watu wakazidi kumiminika katika mazishi yangu nikamuona Ankor Mwichande akiinuka na kutoka mbio nikamtizama wapi anapo elekea kumbe kamuona Mwajuma akija msibani analia akawai kumshika na kum bembeleza nikaenda mpaka pale walipokuwa wamesimama nikamsikia Ankor anamuuliza Mwajuma "hivi unaweza kuniambia ni kitu gani kilicho tokea jana baada Hafidhi j ikram kukukimbilia wewe? kwa sauti ya kilio akamjibu "sijui nisemeje yote nimesababisha mimi haya, "usiseme hivyo Mwajuma baba yake akikusikia anaweza hata kukupiga risasi ina maana ulifanya nae mapenzi sio?" ndio hivyo kaning'ang'aniza mpaka nikafanya nae, sasa mbona wewe hujafa wakati watuhumiwa wanakufaga wote?"
binafsi mimi hata sielewi ila kuna kacha alinipa nivae nahisi ndio kinga yenyewe sababu jana usiku nipe nikupe kanijia nikiwa nimelala akaniogopa, "iko wapi hiyo kacha?" hii apa nimeivaa, nikatamani niende kuichukua niivae labda nitapona ndugu jamaa na marafiki kikao kikawekwa nizikwe huku huku kilwa kwa bibi mzaa mama au nisafirishwe kwenda iringa alipo zikwa kaka yangu jibu likatolewa na baba ya kwamba nitazikwa huku huku kilwa vijana wakaandaliwa kwenda kuchimba kaburi huku anae ngojewa kufika ni bibi tu mzaa baba kwa sasa anaishi kibaha kwa Mathias vijana wakaenda makaburini nikaona niwafate kufika kule kila mmoja anaongea lake "hivi Ntonere kaka huyu dogo kifo chake mbona cha gafla hivi?"
mi hata sielewi sijui kavamia shamba la nipe nikupe bila kufahamu kumekatazwa au?
sema nini dogo alikuwa smart sana juzi tu katupatia heshima kijiji hiki ni mchezaji hatari sana tumelipoteza jembe la ukweli kudadeki kama nipe nikupe ndio katenda hivi hatuna budi kupambana nae tu,' hivi Mudy unavutia bange matakoni au vipi yani wewe kwa akili zako finyu utaweza kupambana na nipe nikupe,? wee boya sana huyo nipe nikupe unamuogopa wewe sio kidume kama mimi kwa kifo cha huyu dogo nasema hapana,'
"Nani boya?" boya si wewe unaemuogopa nipe nikupe, ikazuka vurugu mechi wakitaka kupigana wakagombelezewa kaburi likawa tayari na kurudi nyumbani nikashuhudia mwili wangu ukioshwa na kufanyiwa taratibu zingine nikiwa kama muislamu dahaa tukiwa tumekaa vikombe vya uji vikawa vikipitishwa nikatamani kuchukuwa hata kimoja ninywe yani njaa niliyo nayo mpaka nikahisi utumbo unavuta nikajalibu kukishika kikombe nikakikosa gafla tukasikia sauti ya vilio achana na vya pale msibani ni vya wageni tukageuka kucheki dahaa ni shangazi zangu Dada zake baba wakiwa watatu na bibi mzaa baba akiwa ajiwezi kwa kilio sijui nilijisahau au vipi nikajikuta nimesima na kutoka mbio kwenda kumkumbatia bibi, cha ajabu sijui aliniona akanyamaza kulia akatanua mikono ishara ya kwamba nimkumbatie,
Kitendo cha bibi kunyamaza kulia nakutanua mikono nimkumbatie nikapata matumaini mapya nikaenda mbio cha ajabu yeye akanipita kama upepo akaenda moja kwa moja kulivamia jeneza akawa anataka kulifunua ikabidi watu wamshike na kumzuia asifanye vile akawa anapiga kelele "niacheniiii nasema niacheniii...huyu sio mjukuu wangu Hafidhi bado hajafaa....kauli ambayo iliwafanya wengi wastuke na kuhisi labda bibi kachanganyikiwa tu kutokana na msiba wa mjukuu wake wengine wakasema labda kweli akisemacho "Issa ndugu, "unasemaje bwana? itakuwa yule bibi ana maono ya mbali sana kaona ukweli mtupu,' ahaa embu potezea ujinga huo yule bibi kadata tu, bibi akawa mbishi kukubali huku akionyesha kidole sehemu niliyokuwa nimesimama mimi "Hafidhi mjukuu wangu yule palee sio huyo aliyekuwemo kwenye jeneza ikawa vurugu mshike mshike aking'ang'ania kulifunua jeneza, ikabidi baba aingilie kati kuja kumshika mama yake na kwenda kumfungia ndani jeneza likabebwa safari ya kwenda kaburini ikaanza huku njia nzima nikisomewa dua wakafika makaburini taratibu zikafanyika na kushuhudiwa nazikwa kwa kufukiwa baada apo ikapigwa dua ikasomwa hutuba fupi na shekhe tukarudi nyumbani gumzo kubwa ikawa ni kuhusu bibi yangu watu wakaandaliwa chakula wakala mimi njaa inazidi kunitesa nikaona niende chumba ambacho bibi kafungiwa nikamkuta kajikunyata akiwa analia nikajalibu kumshika begani akastuka na kuinua uso wake, akatabasamu na kufuta machozi, bibi wewe peke yako ndio unaniona wengine wote hawanioni bibi nasikia njaa bibi kwa nini nimekuwa hivi? bibi utanisaidiaje mjukuu wako? ni maswali kedekede nikimuuliza bibi bila kupata jibu mwishoe akaniambia "Hafidhi mjukuu wangu tushachelewa kwa sasa hakuna namna ya wewe kurudi tena utaishi kama mzimu mpaka siku ya kufa kwako,' kwanini bibi iwe tumechelewa? ni kwamba Hafidhi mwenyewe ni yule aliyefukiwa wewe ni kivuli tu, “sasa bibi nitafanyaje mimi ina maana ndio basi tena?" nikawa napiga miyayo tu, akaniuliza “una njaa au?" ndio nina njaa tokea juzi sijala kitu, akaniambia embu twende huku kwanza akanishika mkono kwa kasi ya kimbunga tukapotea eneo lile na kujikuta tupo kwenye mti mkuubwa aina ya mbuyu, nikimtizama bibi hata mavazi aliyo vaa sio yale kashachenji kitambo tu, akaanza kuita “weee nipe nikupeeeee.....haraka kujaaaa...nipe nikupeeee nakuita hapa uje haraka Sana, kufumba na kufumbua kikashuka kitu mbele yetu kwa kishindo hakuwa mwingine ni nipe nikupe akiwa amevimba na kuvimbiana kwa hasira vibaya sana bibi akampa salamu “gonora mwanakurendwa, nipe nikupe hakuitikia zaidi ya kuuliza “wewe nani mpaka unaniita hivyo kama vile mimi ni mtumishi wako?" akamjibu “mimi ni malkia kutoka katika falme ya handeni nimekuja hapa kumchukua mjukuu wangu namuitaji haraka sana nipatie, “hapana siwezi kukupa huyo mjukuu wako kavunja mira na desturi zetu kwahiyo lazima afe, “sikia wewe tambua unaongea na nani mimi ni malkia nakuamlisha muachie kijana wangu haraka iwezekanavyo, “haha!haha! nipe nikupe akaangua kicheko cha dharau na kusema wewe ni malkia huko huko handeni sijui iringa sio huku kilwa kiwawa mimi ndio mfalme wa kijiji hiki fanya uwezavyo mjukuu wako harudi tena, “sawa kama umeamua kutangaza vita kitakacho itokea familia yako utakuja kujuta mi naenda ila kabra sijaondoka nina ombi moja tu, “ombi gani hilo?"
naitaji umpe izini ya kushika chochote akitakacho huu mzimu aweze kula japo hatoonekana, “sawa hiko amepata akanipulizia upepo tu na kusepa zake, bibi akasonya zinga la msonyo “sasa pumbavu zake nilikuwa nataka afanye icho tu kisha mpango mzima nimalize mwenyewe ehee ile kacha niliyokupa kipindi kilee iko wapi?"
kusema kweli bibi yule binti niliyefanya nae mapenzi ndio nilimpa avae, “khaa! yani katika mitoto mijinga wewe jinga kweli akanitia singing na kusema “shauli yako na urofa wako huo ile ndio ilikuwa kinga ya maisha yako sasa basi mimi itabidi nirudi iringa kesho nikaongee na mizimu ila nina wasiwasi marehemu kaka yako ndio atakaye pewa nafasi ya kurudi kuja kupambana na nipe nikupe, “kwahiyo bibi kama kaka Hafidhi j ikram atarudi mimi je itakuwa?"
wewe itabidi ukachukuwe nafasi yake kule kuzimu ili yeye aje kuifanya kazi hii baada kazi kuisha wewe utarudi na kuwa mzima kama zamani, dahaa bibi akanishika mkono kama tulivyo kuja ndivyo tulivyo ondoka
tukafika home na kuwa vile vile kama tulivyokuwa kabra ya kuondoka nikatoka mpaka jikoni kushika mfuniko wa sufulia si nikashika usintanie kuna ubwabwa ndondo nikaufakamia mpaka kitumbo kikawa ndii hasubuhi na mapema kikasomwa kisomo cha taha timu watu wakanywa chai kwa maandazi nikataka kwenda kuchukua kikombe cha chai bibi akanikataza kwa ishara kisha akaingia ndani nikamfata kufika tu akaniambia “usisubutu hata siku moja kuwatisha watu, “nawatisha kivipi kwani?" kwanza tambua wewe ni mzimu ukishika kitu chochote kile kinaonekana kikielea wewe hauto onekana kwahiyo unatakiwa ule kwa kificho, “sawa bibi nimekusikia, “sasa mimi najiandaa kuondoka ndani ya siku tatu au nne nitarudi na dawa kuja kukufufua,
wengi walishangaa na kujiuliza inakuwaje bibi aondoke gafla tu wakati mjukuu wake kazikwa jana tu hata matanga hayajaisha, baba akamuuliza “mama aibu gani hii tena unaileta hapa ndio kwaanza tumezika jana leo hii unaondoka kweli?"
sikia Juma nikwambie kitu Hafidhi hajafa kama unaamini kafa ni wewe nikae hapa sijui msiba wakati mmeenda kuzika mgomba wa ndizi naenda iringa nikirudi ndio mtaujuwa ukweli embu nisindikize kituoni huko,
baba hakuwa na budi kumsindikiza bibi
baada bibi kuondoka wakiwa wamekaa kwa kupata msosi wa mchana huku wakizungumza hili na lile cm ya shangazi Fetty ikaita akaicheki na kusema “whao mama huyoo akaiweka cm sikioni hallo..wapi..? cm ikamtoka na kuanza kugalagala kwa kilio mamaa weeee mama yanguuu... baba akaenda mbio kuiyokota cm akaicheki bado ipo on hallo,' ndio...wapi hukoo? nae akamwaga chozi na kusema mama hatunae tena....
Nikastuka,"
“Kwanza kabisa nilistuka kusikia taarifa zile sikuweza kuamini masikio yangu, vilio vikaanza upya yani kama kidonda ni kibichi kimetoneshwa tena, baba akishilikiana na marafiki zake ambao walikuwa bado hawajaondoka kwenda mjini wakafunga safari mpaka hospital ya kilwa masoko ndio sehemu mwili wa bibi umehifaziwa nikiwa ni mmoja ya watu walikwenda huko kwanza nikataka kuzibitisha ni kweli au uongo, ni mwendo wa dakika kama 30 hivi kutoka kilwa kiwawa mpaka kilwa masoko tukafika huku kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kujuwa kilicho tokea kusema kweli watu walikuwa wengi, kila mtu alikuja kutaka kujuwa habari ya ndugu ndugu zake au jamaa zake baada kufika mapokezi kutokana na kombati zake alizo zivaa baba hatukukawia kupata maelezo ya kwamba
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU