UTAMU WA KITUMBUA (14)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
""why daddy.........!!! kwanini umeamua kufanya hivi tungekua masikini tusinge ishiii ona sasa yaliyo kukuta sita kuona tena baba yang....uuuu please nisaidieni......jamani baba azikwe hapa hapa nyumbaniiii ......."" aliongea errycah kwa uchungu mkubwa.SASA ENDELEA...
Akachukua simu yake na kumpigia mwanasheria wa mjomba simu haikuita.na baada ya mda mfupi tuliwaona wale (BHG) wakiingia ndani huku wakiwa wamepanga foreni walikua wengi sana.wake kwa waume nilipo jaribu kuwachunguza wengine niliwafahamu kabisa.kuna baadhi ya wasanii wa
Dini,bongo fleva,hiphop wa hapa nchini wachungaji matajiri wakubwa wandishi wa habari watangazaji wanasiasa hata baadhi ya wanafunzi wa vyuo walikwepo.tuliwekwa pembeni na police ili kuwapisha wale (BHG) kufanya ibada ya kumtoa ndugu yao jeneza la dhahabu lilitolewa mle ndani na likawa linapita mikononi mwao huku kila aliye libeba alilitemea mate.sikuelewa wana maanisha nini ila mlinzi alituambia ile ndo ibada yao ya mwisho ya kumuaga mwenzao na wakioka hapa wanapanda ndege na kwenda kuzika.
Errycah na manka wao ulikua ni mwendo wa kilio tu.Mimi na merry hatukuumia hata kidogo kutokana na madhambi aliyo tufanyia mjomba.kwa kutuondolea wazazi wetu.walipeleka jeneza kwenye gari na wote kwa mstari ulio nyooka waliingia kwenye magari yao na safari ya kuelekea airport iliianza tulibaki na viulizo kichwani huku mlizi akiendelea kutupa stori "wote unao waona hapo wanaenda Nigeria moja kwa moja hiyo ndio sheria yao lazima mwenzao akifariki wamzike na hao wote watazikwa Nigeria cha msingi nacho washauri wanangu. kaeni meza moja muongee myamalize na mjue mtaanza vipi maisha ""ACHENI WAFU WAWAZIKE WAFU WENZAO.""
"ama kweli mshahara wa dhambi ni mauti"alimalizia errycah huku tukielekea kwenye gari.tulipokua njiani tuliendelea kukumbushana mambo tuliyo yaona kule hospitali.mpaka tukaanza kubishana na Merry.ubishi wenyewe merry alisema kwenye ule msafara amemuona mwandishi wa story ya utamu wa kitumbua chas360tz nilimkatalia kwa sababu chas360 namfahamu vizuri Jamaa hapendi mambo ya kijinga kwanza saizi yupo zake studio anaanda kitabu chake.ubishi ule uliisha pale mlizi alipo ingilia kati na kusema chas360 ni baba yangu mdogo msimsingizie mambo ya ajabu ajabu.tushuka kwenye gari na kuingia ndani moja kwa moja huku wote nia ikiwa moja kwenda kufungua chumba cha siri.kabla ya kwenda kufungua simu ya mezani iliita tulitazamana huku tukisakiziana kila mtu apokee.kidume nikajitosa nika pokea na kuanza kusikiliza maelezo unaongea na OLOMO IGWE kutoka (BHG) samahani naongea na KENNY .J. SIMBULI nilishanguu kuona kalijuaje jina langu nika mjibu ndio.
"nadhani unatambua mjomba wako kafariki kuna baadhi ya document zake tumezipitia na tumeona kakuandika wewe ndie mrithi wake.unatakiwa kufika Nigeria kesho ili tukufanyie usajiri na kama ukikataa basi ukoo mzima mtakufa na Mali zote mtanyang'anywa mana ni Mali ya brotherhood gang (BHG). kuhusu usafiri na kupata utaratibu wote nenda horena hotel chumba namba #966 utakutana na agent wetu atakuelekeza kila kitu." uzuri simu niliweka loudspeaker kila mtu akasikia
Nili mjibu kwa dhalau "sikia bro nikwambie siogopi kufa mana hamna uwezo wa kuondoa maisha yangu hamuwezi kuiteteresha imani yangu.na kuacha kumua budu mungu wangu aliye juu.kama Mali njoeni mchukue bora nife masikini kuliko kua na Mali nyingi sio halali.kwa imani ya Mwenyezi Mungu hii vita nitaishinda na hamniwezi kwa chochote kile."
"sikia kijana naona ume panic sana bora uishi naisha mafupi yenye raha kuliko maisha marefu yenye shida.kama umekataa cha moto utakiona wewe na ndugu zako nikimaliza kuzungumza na wewe nakupa masaa 48 mkusanye kilicho chenu wewe na ndugu zako na mtoke kwenye nyumba.ila kitu chochote cha mjomba wako naomba chumba namba #966 msikifungue........nadhani nimeeleweka."alikata simu
Tulianza kujadiliana kutokana na ile simu iliyo pigwa.nikaonyesha msimamo wangu kama mwanaume hapa tunaenda kufungua kile chumba ili tujue kuna kitu gani tukitoka hapo tubebe kilicho chetu tuhame uzuri wa Mali za kishirikina kama ukichukua kabla ya marehemu ajafariki hiyo Mali ni yako ila ukichukua baada ya marehemu kasha kufa utakacho kutana nacho ni juu yako.zile million hamsini ndo
Zitakua Mali yetu ya uhalali mana tulichukua kabla ya mjomba hajafariki ukiangalia erycah na yeye alikua amewekewa hela toka utotoni mwake kuyumba hatuto weza.maumivu yalikua kwa manka yeye hakulipwa chochote kibaya zaidi alicho jiharibia ni ile tabia yake ya kutoa Tigo ningeweza kumuoa alijiharibia CV alicho kiomba yeye ni nauli arudi Rwanda akaanze maisha.mlizi hatuwezi kumuacha tumezoeana naye sana hata tukisema arudi kijijini tuta mtesa tu.
Errycah alileta ufanguo wa chumba cha siri nikauchukua na kwenda kukifungua.nilifika mlangoni wote walikusanyika pale kutaka kushuhudia kitu gani kipo kwenye chumba kile.nilianza kufungua kufuri la kwanza nikatekenya kitasa kitu kikajibu.nilifungua taratibu na kuona chumba kipo tupu tena kuna Giza Nene nilitangulia kwanza peke yangu nikawapa ishara waje ndani waliingia hatukufanikiwa kuona kitu chochote nisogea kwenye ukutu nilishangaa kuona kama mlango ukutani nilipo ugusa
Ulifunguka.kumbe kule ndio chumba chenyewe namba #966 tulipo ingia tuliona vitu vya ajabu tulikuta kabati mikufu ya dhahabu vibuyilu chungu na kiti cha kifalme errycah alifungua lile kabati tukaanza kusikia harufu mbaya nilipo mulika na vizuri na tochi ya simu yangu.oooooooh mungu wangu sikuamini nilicho kiona niliona mafuvu ya vichwa nilipo mulika vizuri niliona fuvu LA kwanza likiwa likeandikwa jina la baba na lingine jina LA mama nilianza kutokwa na machozi niliumia sana..hakukua na mtu wa kuvumilia wote tulianza kuangua kilio.hiyo ilikua ni flem ya kwanza.
Flem ya pili ya kabati tulikuta fuvu moja kuangalia pale juu kwenye paji LA uso lilikua limeandikwa jina LA shangazi mama yake mzazi errycah. errycah baada ya kuona vile aliishiwa nguvu kabisa alikaa kimya huku akitoa kilio...
Huku akisema ""baba kumbe ulimuua mamaaaaa.....""
Nikafungua flem ya 3 tukakuta mafuvu ma tano yaliyo wekwa pamoja kumulika vizuri tuliona majina kwenye mafuvu yale lilikua fuvu la vannesa nasma husna yule shangazi na dereva.......
""mungu wangu huyu dereva kafariki lini nakumbuka sikuile tulimkuta mwanza akiwa anaokota makopo.jamani duniani kuna watu wabaya.""aliongea manka kwa majonzi
Tukaendelea na fkemu ya 4 tutakuta viperushi vya majina yetu inaonesha na sisi tulikwepo kwenye list.
Mlinzi alituamuru tuvichukue kisha tukavichome moto ili hata wenzake wakija kuchukua madude yao majina yetu yasiwepo... uwezi kuamini nilisahau utamu wa vitumbua nilivyo kula na kujuta kuzaliwa mana si kwa vitu hivi.
Kutupa macho pembeni niliona nyele zikiwa kwenye kindoo na hapo ndipo nilipo gundua kwa nini mjomba hakua na nywele na sikuwai kumuona akienda saloon kunyoa.nilisogea mpaka pale kwenye kiti cha kifalme nikakuta bahasha niliichukua na tukatoka kwenye kile chumba.nilikifunga kama nilivyo kikuta tukaenda sebreni kuifungua ile bahasha na kukutaa ma dhambi yote aliyo yafanya mjomba kama kafara ya kuongeza Mali ameyaandika.kweli mjomba amewaua wazazi wangu mkewake (mapacha) husna na nasma na dereva .........
Karatasi ya pili tulikuta majina yetu yakiwa yameandikwa kwa rangi nyekundu.........niliumia sana ila nilijikaza kiume tukiwa bado tunasoma zile karatasi.walikuja ma agent wa (BHG) wakatumbia tubebe kila kilicho chetu na tuondoke la sivyo tujisajiri na chama chao wote tuligoma kila mtu akaingia chumbani kwake na kupaki nguo.nilifika ndani na kuanza kupanga kila kilicho changu nilipofungua kabati LA chumbani kwangu nilishangaa kuiona ile bahasha niliyo achiwa na sethi kule horena hoteli.sikupata mda wa kuifungua niliweka kwenye begi na kutoka nje kuwapisha wale ma agent wa BHG.kibaya zaidi tulimwona na yule wakili wa mjomba akiwa nao sambamba wale ma agent. alijifanya kama hamjui errycah.ama kweli MWISHO WA MAWINDO MBWA HANA THAMANI.
Hatuweza kuondoka na gari tulipotoka nje nilimwona yule boda boda aliye nileta juzi.tuka salimiana nika muulizia hamna nyumba inayo uzwa ?
"bro hapa umefika Mimi ndo dalali wa mijengo sema ikifika mida kama hii napiga boda boda jina langu naitwa dalali kiongozi kuna mjengo masaki hii hii unauzwa million 450 kama upo vizuri unaingia leo leo."
Nilidata kuisikia ile bei.nilishangaa kuona errycah akidakia ok twende hela ipo.ndo ikawa nafuu yetu alimwita mwenye nyumba baada ya lisaa limoja tulikamilisha kila kitu na kuingia kwenye nyumba mpya huku zile million 50 tulizo mwibiaga mjomba alikua Nazo merry.niliingia ndani na kufungua begi langu ili nipange vitu vyangu niliiona tena ile bahasha nilipo ifungua sikuamini macho yangu nilikuta majibu ya hospitali ya sethi ya kipimo cha damu na kuonyesha ni mwathilika nilihisi Ku data mana yeye alikua msichana wangu wa kwanza Ku lala nae ukiangalia sikutumiaga condom.
"""ina maana na mimi nimeathilika Mungu nionee huruma Mimi sito ludia tena kwaiyo kama Nina HIV inamaana wote nilo lala nao na wenyewe wanao oooohh mungu wangu nimekwisha nikianza kulia kwa sauti mamaaaaaaaa.........nimekwishaaaaaa.............sethi..........umeniponza........ .kwanini...........Mimi.....nimesha......upoteza u padri........na nimewaua ndugu zangu..........nime muua mpaka mdogo wangu..........bora nife siwezi kuendelea kuishi kama nimewaua ndugu zanguuuuuu"""
Kumbe kina merry walikua wana nisikiliza lakini hawakuelewa walipo fika waliniuliza sikua na mengi ya kuongea zaidi ya kuwaonyesha Yale matokeo na kuwaambia Huyo ndo alikua msichana wangu wa kwanza kutembea nae........
"Kenny kwaiyo umetuua woteeee"wote watatu waliniuliza kwa Mara moja
Niliumia sana niliwaomba samahani ila mlinzi alitushauri twende hospitali tuka hakikishe hatukua na mda wa kupoteza tulienda hospitali kwa yule doctor wa Rwanda bahati nzuri tulimkuta yupo zamu ya usiku nilimwelezea akachukua vipimo vyetu.akatuambia turudi baada ya wiki tatu hapo ndo tutapata majibu ya uhakika alinichana ukweli mda ule ule na kuniambia hauto kua na uwezo wa kumpa mimba mwanamke yoyote yule labda muujiza wa mwenyezi mungu niliona dunia ngumu na kujilaumu sana kwa kunogewa na UTAMU WA KITUMBUA...............
MWISHO WA SIKU KENNY NA WALE WOTE ALIO FANYA NAO MAPENZI WALIPATA UKIMWI (NGOMA) ILA MAISHA HAYAKUISHIA HAPO YALISONGA MBELE KENNY HAKU BAHATIKA KUPATA MTOTO
ALISHINDWA KURUDI SEMINALINI ALIMRUDIA MUNGU ALIFUNGUA KANISA LAKE NA KUA MCHUNGAJI.......!!!!
ERRYCAH NA MERRY WALIOLEWA
MANKA ALILUDI NCHINI KWAO
NA MLINZI ALIRUDI KIJIJINI KUANZISHA BIASHARA YAKE
KWA WATUMIAJI WA APP KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
MWISHO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni