Notifications
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (11)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MOJATULIPOISHIA...“Orion,” Seidon akamwambia Amatagaimba huku akikimbia. Amatagaimba akasimama na kugeuka nyuma huku tayari akiwa na upanga wake mkononi, Seidon alizidi kukimbia bila kutazama nyuma. Amatagaimba alipigwa kikumbo kikali kabla hajautumia upanga wake, kwani kasi ya Yule farasi alishindwa kabisa kuidhibiti kwa upanga wake huo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (10)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMITULIPOISHIA...akaeuka ghafla na kukaa upande wa Seidon tayari upanga wake ulikuwa umekwishaondoa kichwa cha Yule jamaa, vurugu ikazuka kati ya watu wale na akina Amatagaimba, mapigano makali yakazuka, kila walipowakata kata na panga zao wale watu walizidi kuwa wengi na makelele yao yalikuwa yakiwasumbua masikio ya Amatagaimba na Seidon.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (9)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA TISATULIPOISHIA...“Seidon, hapa kuna kazi,” Amata ga Imba alimwambia Seidon, akageuka kumtazama akamuona ametulia kimya kama mtu anayetafakari kitu fulani. “Seidon, unawaza nini?” akamuuliza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Amata ga Imba, tutafika hii safari kweli, maana naona vikwazo ni vingi sana, na ninaanza kukata tamaa,” Seidon alijibu.“Usikate tamaa, hakikisha unafika…

WEKA YOTE (14)


JINA: WEKA YOTE
Mwandishi: Gaooh Musah

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
"Kwani kuna ubaya si ninajua tu jamani."

"Sawa."nikajibu kifupi kabisa.

"Ester nani yako.?"aliuliza tena hapo ndio kabisa nilimchoka kwa maswali yake yasio na mbele wala nyuma basi hata katikati hayana.

TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE

SASA ENDELEA...
"Kwani wewe unataka nini.?"na mimi nikavaa upolice sasa nikampa swali.

"Amna napenda kujua tu."

"Ili,?"

"Nijue tu."

"Alafu ukishajua upate nini.?"

"mmmgh"aliguna hapo nikaondoka bila kuendelea kuongea mana mpaka wakati huo tayari giza lilianza kuumeza uso wa dunia na kuutawala.

"Gao unaenda wapi, yani nakuuliza unaondoka si ndio sawa dawa yako ndogo."alisema hapo nimetia pamba sikioni niliyaona ni maneno ya mkosaji tu yale.

"Ngoja dawa yako wewe ni kumwambia mama yako, mlichofanya na ester ngoja."alizidi kusema, hapo akijia shangazi ni mama yangu, pengine hiyo ni kutokana na kutomwambia uhusiano wetuimi ba ester pale alipo uliza labda anajua ester ni ndugu wa mule.
Nilimwacha akibwata maneno mengine ambayo hata sikuyasikia vizuri hiyo ni kutokana na mtamkaji kuwa mbali.
Nilitembea mwendo wa kijeshi jeshi kuwahi nyumbani zilikuwa ni kilometa kadhaa kufika nyumbani ila kwa mwendo ule wa hatua ndefu na kuimbia kimbia nilizidi kupunguza umbali hadi kufilia naiona nyumba yetu vilivyo, imewashwa taa usiku umefika.
Nilitembea mwendo mdogo dogo kwa tahadhali nisije kanyaga mbwa usiku mana yanapenda kulala hapo uwanjani karibia na kwetu.

Nilifanikiwa kipita hima hima mpaka nikaufikia mlango wetu mkuu kuibwa geti niksingia kwa kunyata nyata kama mwizi anaevizia nguo azianue na kuondoka nazo.
Hadi kufika katika dilisha la valandani pale, nilisikiliza kama baba yupo hajaondoka.
Nikalisogelea dirisha usawa wa karibu kabisa huku nikiyaamuru masikio yangu yote kuaikiliza ndani, nilisikiliza kwa muda nako olaa hakuna niliemsikia hata baba niliedhani yupo nae sikumsikia nilivuta nguvu na kuufata mlango kwa kunyata nyata ile nafungua tu uso kwa uso na shangazi.

"Haya, watoka wapi.?" nilikumbana na swali moja moja tokea kwa shangazi akishangaa muda alioniita na mpaka muda huo ndio naonekana.

"Nilikuwepo pale juu."nilijitetea

"Yani,nimetuma neema akuite na kakukuta amekuambia nakuita hukuja kwanini?"alizidi kuongea.

"Nisamehe shangazi nilijisahau sijaitikia wito baada ya kuona kimya."nilizidi kujitetea ila shangazi alikuwa kakasirika kwa muonekani wake tu, nilimtambua kakasirika yani mpaka hata sauti yake ilibadilika.
Muda huo tumesimama pale mlangoni, hakuendelea akaondoka zake nje.
Hapo mimi kiange ange sikiwa na chakufanya nilielekea chumbani kwangu kutulia mana mufa huo amani nilipoteza kwa nilivomchukiza shangazi.
Sikukaa ndani sana kukisahau nikazichukua nguo zangu na kutoka nazo nje tayari kwa kuzifua.
Japo hali ya hewa haikuwa rafiki ila nilizifua tu.

"Gao, mpenzi."sauti ya kike nyororo ya kuvutia iliniita na kunipa cheo cha upenzi.

"Gao si ninakuita baby wangu."alizidi kuongea hapo nikageuka moja kwa moja nikakutana na CAREEEN alieko kwenye tabasamu akimulikwa na taa nyeupe ndefu ya mshumaa,inayo angaza pale.
Nilishangaa sana Careen kuniita vile.

"Wewe ndo nini sasa hivyo."niliuliza kwa wasi wasi ulionijaa.

"Kwani nini mpenzi wangu si kawaida tu jamani."

"Kwanza nani mpenzi wako,?"nilimgeuzia kibao sasa.

"Jamani si wewe hapo."alisema huku akikaajuu ya kiti nilichokuwa nimekalia baada ya kusimama kuanika nguo, hapo na mimi nimesimama huku mkononi nimeshika nguo ya pili niliyokuwa namaliza kusuunza nikaanike.

"Wewee, ishia hapo hapo mimi sio mpenzi wako,"nilisema kinaga ubaga, yani nilimtolea uvivu.

"yan, gao leo unanambia hivyo mimi."alisema huku akitaka kulia.

"Jamani wewe si mtoto wa dhangazi ni ndugu yangu."

"Gao, unanambia mimi hivyo sawa."alisema na kuondoka huku akilia kwa kufika fina, hapo mimi sina hata habari nae tena ndio kwanza nikamaliza kufua na kuanika.
Baada ya kumaliza nikaelekea ndani moja kwa moja, na kukaa kwenye makochi pale nilikuwa peke yangu sikuona mtu wakati huo ule upweke ukapelekea na mimi niingie ndani, nikiwa na dhumuni la kuandaa vitu vya shule pamoja na kupitia pita kidogo madaftali yangu, nililitafuta begi mpaka kulitoa kisha nikaanza kusoma moja moja ili kupoteza muda na kuondoa upweke niliobaki nao pale, yalipita masaa kadhaa, ndipo jina langu likaanza kuitwa kama kawaida yake ni Ester sikucherewesha nilitoka haraka, nikijua fika chakula tayari mana hata tumbo lilianza kusononeka kwa njaa.

Nilitoka haraka ndani nikifata sauti ilipotokea,
Nilienda mpaka sehemu maalum ya kulia chakula.
Wenzangu walishaa kaa tayari ambao ni Neema,doreen,careen na ester shangazi hakuwepo, yani japo wote kasoro doreen, niligundua tabia zao za hovyo lakini mbele ya watu wengi wanaonekana wanaheshima hasa Careen.
Tulikuwa kwa kucheka kwa maongezi yaliokuwa, yakiendelea ila careen hakuwa na furaha, hata ulaji wake wa kimadoido doido ila sio ya yamoto band, ni madoido ya careen.

"Mnakula wanangu."shangazi aliongea baada ya kuja muda huo mkononi kashika mfuko mweusi unaonekana wazi unavitu ndani.

"Ndio."waliitikia baada ya kuilizwa hapo na yeye akajiunga na sisi.
Kusema ukweli Ester alikuwa mpishi sana, hasa kwa kuwa ametokea tanga yani alipika wali mtamu alioutia nashki ya iliki hivyo kuufanya unoge zaidi, hayo maharage ndio usiseme unaweza jing'ata ulimi kwa utamu.
Shangazi alifungua mfuko wake na kuzitoa ndizi alizogawa kwa kila mmoja wetu.
Na kuzipokea hapo shangazi ndio alimaliza utamu wa wali na ndizi zile nilitamani kisiishe ila tumbo nalo linamwisho nilipomaliza sahani ilitosha kabisa, tumbo kujaa.
Niliaga na kuingia chumbani kwangu, nikavaa taulo muda mchache nikaenda kuoga haraka na kuja kulala.

**************
Asubuhi na mapema nilidamka sikusubili usumbufu wa Ester kuniita itaa. Hivyo niliamka tu mwenyewe na kujiandaa kisha nikazinyoosha nguo na pas hadi kumakiza muda wa kwenda shule tayari.
Niliongoza heya heya mpaka kufika shule kumepoa siku hiyo ya ijumaa yani siku hiyo watu wengi huichanganya ni weekend. Hawafiki shule mahudhulio yanakuwa machache sana.
kwakuwa jana yake nilitoroka hivyo nilitembea kwa makini nikiwa sina habari wala taarifa mara nasikia nyuma mtu akiongea.
"Aaaaah, headmaster huyo yani ukiamua kutoroka unatoroka tu."niliikunbuka sauti hiyo haraka nikazungusha shingo kumwangalia................

..Niligeuza shingo upesi upesi nikiwa mwingi wa wasi wasi iliyonijaa vilivyo, kitendo cha kugeuka hapo uso kwa uso na sir lusinde, akivalia suti nyeusi na viatu vyake vyeusi vilivyoendana kabisa na suti yake huku mkononi akiwa kaishikilia briefcase(mkoba), aliyoshikilia na mkono wake wa kushoto.
"Aaaah, hapana sir.'",nilibabaika baada ya kumuona, hakuongea zaidi akaondoka tu na kuniacha nimesimama kama mtu aliyeshushwa na gari baada ya kufika sehemu asiyo ijua akiwa akishangaa shangaa, na ugeni wake.

Nilimpotezea na kuanza kuelekea darasani muda huo namba imekwisha hesabiwa wanafunzi ndio wanatawanyika mmoja mmoja.
"Oi gao niaje mkale"ni sauti ya jamaa yangu wa muda mrefu ambaye hatukuweza kuonana kwa kipindi kirefu hiyo ni baada ya kupata matatizo kidogo ya kifamilia.
"Safi ni vipi, frank upo poa"nilimjibu baada ya salamu yake akionekana mchangamfu.
"Niko poa jamaa,nambie."

"Safi vipi mama anaendeleaje ndugu.,"nilimuuliza swali ambalo ndio chanzo cha kumfanya abaki nyumbani.

"Daah, kaka nashukuru mungu, mama amepona kabisa na afya yake ipo imara."
"Aseeh, hongera sana jambo la kushukuru hilo." Tuliendeleaa kuongea maswala machache, kisha kwa pamoja tukaelekea eneo letu maalum la usafi.
Njiani tuliendelea kupiga soga mbili tatu za kukumbukana mana karibia miezi miwili hakuwepo shule, baada ya matatizo ya mama yake.

Tulifika eneo letu na usafi kuendelea, muda ulipepea haraka mpaka kuisha ndipo tukaelekea paredi kea matangazo na vipindi vya wakati huo. Nayo yalienda barabbara na uimbaji wa wimbo wa shule, siku hiyo ilikuwa tofauti sana walimu wote walifika paredi hapo mimi niliweka gutu kwa kuvibebanisha vidole vyangu cha katikati na cha pili kutokea gumba, waliopitia hatua hiyo wanajua.
Nilikuea nikiomba mungu nisitumbuliwe mana nilijisihi ni jibu tena lililoiva tayari, muda mchache mwalimu wa zamu akaanza kuongea kwa niamba ya walimu wengine ambayo pengine walikuja tu au wana ya kwao ya kuongea.

"Good morning scholar."alisalimia kimombo.

"Good morning teacher's"tuliitikia kwa pamoja wanafunzi wote. Baada ya salamu ndio akaanza kuongea.
"Wanafunzi leo ni siku ya ijumaa, mshudhurio yeni ni machache mno karibia nisu ya waafunzi hawapo sasa uongozi wa shule tukiambatana na mwalimu mkuu, tumeona tuandike majina ya wanafunzi wote mliohudhulia leo kwa kila mkondo a baada ya kuandika majina kutaendelea matangazo mengine. Aliongea hapo walimu karibia wote kasoro mwalimu mkuu, walimu walipita kwa kila mwanafunzi kuliandika jina lake mpaka wanamaliza hapo wakajisogeza mbele na karatasi zao walizo andika majina.

"Nadhani zoezi limeisha kila mwanafunzi jina lake tumeliandika, ambaye hajaandikwa atanifata sawa." Alisema mwalimu, yule na kumkaribisha mwalimu mkuu aseme alichokuja nacho siku hiyo.
"Habari zenu wanafunzi"alianza kwa kusalimia kama kawaida tukamwitika wote kwa pamoja, nae hakusita kuendeleaa kuongea.

"Wanafunzi,tunategemea kuanza mitihami yetu jumatatu, mitihani ya nusu mhula ambayo inaanza mwezi wa sita hivyo taarifa kwenu mjiandae mapema, pia taarifa kwa wale wote wenye madeni hamtafanya mitihani hii ikiwa mnadaiwa, hivyo leo mkirudi mchana mkawape taarifa wazazi wenu sawa."aliendelea kuongea huku gutu langu sijatoa, mana nilimuona kama lusinde ananitafuta.
Nilianza kujificha mana alitafuta kwa macho hivyo alinipa wepesi wa kujizuia kwenye vichwa vya wenzangu.
Baada ya mwalimu mkuu kumaliza tuliruhusiwa kuingia darasani hapo nikijiona mjanja bila kujua kinakuja nini.

Nikiongozana na frank kuelekea darasani huku story za kiujamaa zikiendelea kumwagika mana nilimkumbuka sana rafiki yangu huyo.
Tulitembea mpaka kuingia darasani, nilikuta kashapata makazi yani kiti na meza alikaa sehemu yake karibu na mimi. Muda mchache mwalimu akaingia tena lusinde na viboko vyake mkononi.
Walimsalimia baada ya kusimama, mimi sikufungua hata kimya changu niliweka gutu kama kawaida nikijua kila siku ijumaa kumbe kuna jumamosi mpaka alhamis, mimi nilijua siku ni moja tu.
Baada ya kumsalimia wote tukakaa pamoja na mimi.

"Wanafunzi nitakae mtaja hapa atakuja mbele kama hayupo mtasema nimuweke hayupo"aliongea sir lusinde.

"Maamaa,hivi sipo kweli pale nipo lazima"nilijisemea kimoyo moyo nikijua fika nipo,wanafunzi walikaa kimya wote hata kelele zilinyamaza.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

ENJOY WAKATI UKISUBIRI MUENDELEZO, SUBSCRIBE KAMA HAUJAJIUNGA NA CHANNEL YETU

Subscribe channel hizi ili usipitwe na video za Vichekesho


28 Simulizi Weka Yote
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni