SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Zena anaweza kuwa na mwanaume kwani kwa jinsi alivyo nifanyia vutu vyote ni sawa na mtu asiye na mwanaume kwani kila kitu amekifanya kwa kujiamini.SASA ENDELEA...
“Poa ninashukuru kwa taarifa yako”
“Ila usije ukamwambi dada kwa maana ninaweza kupoteza kibarua changu na kwetu mimi ndio ninaye tegemewa”
“Sawa sinto mwambia.....Ila na wewe asubuhi ilikuwaje hadi ukawa unanilazimisha kufanya mapenzi?”
“Nilivyo ivaa hiyo pete yako sikuwa ninajielewa nikawa ninahisi kuwa na hamu ya kufanya ma-penzi na wewe ila nakuoma unisamehe kwa hilo pia”
“Sawa”
Nikaondoka na moja kwa moja nikaenda hadi nyumbani kwangu na nikasimama kwa mbali ki-dogo kuangalia kamwa kuna ishu yoyote inayo endelea nyumbani kwangu ila sikuweza kumuona mtu wa aina yoyo akiwa nyumbani kwangu.
Nikapiga hatu za umakini hadi getini kwangu na kukuta geti langu limerudishiwa,nikachunguliwa kwa ndani na sikumuona mtu wa aina yotote.
Nikasukuma geti taratibu na kuingia ndani huku nikizidi kuwa makini kwani endepo kutakuwa na mtu wa aina yoyote asiweze kuniona,nikaingia sebleni na kukuta kukiwa kama nikivyo kuacha nikapitiliza hadi ndani kwangu na kuikuta hali ni ile ile ya jana,
Nifungua kabati langu na kuanza kuchukua nguo moja baada ya nyingine na kuziingiza kwenye begi langu kubwa la mgongoni.
Nikaanza kuitafuta simu yangu na kuikuta ipo chini ya uvungu wa kitanda kwa umbali kidogo na ikanilazimu kuinama na kuanza kuunyosha mkono wangu ili kuutona na nikafanikiwa na kabla sijanyanyuka nikahisi kutu kigumu kikinigusa kichwani kwangu
“Simama hivyo hivyo la sivyo niakuchangua kichwa chako”
Nikasikia sauti nzinto ikizungumza nyuma yangu na kujikuta nikianza kutetemeka na kujutia ni kwanini nimekuja nyumbani kwangu
“Simama”
Nikasimama na kuwasikia watu wawili watatu wakiwa wanajadiliana kitu cha kunifanya
“Ila bosi amesema tumpeleke akiwa hai kwa maana anataka kumuua kwa mkono wake yeye mwenyewe”
“Huyu bila kumpiga hatuto weza kumpekeka kwewe unamuonaje mtu mwenyewe?”
Nikageuza shingo yangu nyuma na kwakutumia pembe ya jicho langu la kulia nikawaona watu watatu wakiwa wamevalia vinyago vilivyo yaacha macho yao kuwa wazi ila sehemu nyingine za uso zao zikiwa zimezibwa na mmoja akiwa ameshika bastola.
Nikageuka gafla kabla sijachukua maamuzi ya kumpiga aliye shika bastola yake nistukia kitako cha bastola kikitua kichwani kwangu na kunifanya niangukie kitandani na kupoteza fahamu
Nikastuka nikiwa nimening’inizwa kichwa chini miguu yangu ikiwa juu na imefungwa na kamba ngumu ambayo sio rahisi kwa mimi kuweza kuanguka kirahisi,Mikono yangu ikiwa imefungwakwa nyuma na kamba pia na sikuweza
Kuona ni sehemu gani ambayo mimi nipo kwani nip ndani ya chumba chenye sakafu iliyo chakaa huku kwa juu kukiwa na kijikidirisha kimoja kidogo kinacho ingiza mwanga hafifu wa jua na kadri muda unavyo zidi kukatika ndivyo jinsi giza lilivyo tawala ndani ya chumba hichi hadi mwisho wa siku sikuona kitu cha aina yoyote kutokana na giza nene
Baada ya masaa mawili mbeleni kikahisi mngurumo wa gari ukisimama nje ya kibanda na baada ya muda gari lilazima,Nikastukia taa ya mshumaa kiawaka ndani ya chumba kisha mlango ukafunguliwa na akaingia jaa mmoja mweusi sana kiasi
Kwamba nikaanza kuogopa kwani mwili wake ulivyo tanuka ninaweza kuwafananisha na wale wanao cheza michezo ya myereka nchini Marekani.Wakafwatia wazee watatu wa kiarau wakiwa wamevalia kanzu nyeupe na mmoja nikamfahamu kwa haraka kwani ndio baba yeke Rahma ambaye jana nilimpiga kikumbo getini
Wakaanza kunong’onezana vitu ambavyo sikuweza kuisikia kisha kwa ishara akamuamrisha jamaa mweusi na nistukia ngumi nzito ikitua tumboni mwangu na kuifanya kamba kuzunguruka na mimi mwenyewe nikazunguka ngumi mvululizo
Kutuka kwa jijamaa hili ambalo linaonekeana kuwa na haruma hata kidogo zikazidi kutua mwalini mwangu na unaweza ukasema ni Mayke Tysona anavyochuka mazoezi ya kulipiga ‘Panch beg’ la mazoezi.Mwili wangu wote ukazidi kutawaliwa na maumivu makali huku nikitoa makelele ya kuomba msaada
“Wewe huwezi kumtia mimba mwanangu.....sitaki azae na watu weusi”
Baba Rahma alizungumza na kumfanya jamaa kuzidi kunipiga ngumi zilizo zidi kuulainisha mwili wangu na maumivu yakazidi kunitawala na damu za puani zikaanza kunimwagika
“NAOMBA UNISAMEHE MZEE WANGU”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika na kumfanya baba Rahma kumuamrisha jamaa kuacha kunipiga kisha akamuomba anivue shati langu na jamaa akalivuta na likachanika vi-pande vipande.Baba Rahma akatoa kisu cha kukunja kwenye kanzu yake na kukiminya sehemu kikafyatuka kisha akanisogelea na kukogoa kuhozi
Kubwa na kunitemea usoni,Akaniguza na kumuachia mgongo na akaanza kinichana chana kwa kutumia kisu chake na kujikuta nikipiga kelele za kumba msaada ila sauti yangu haikupata msaada wa mtu wa aina yoyote.Akanigeuza na kauendelea kunichana chana na kisu chake kwenye kifua changu na nikaizidi kulia huku maumivu makali yakendelea kuutesa mwiki wangu.
Kazee kamja ka kiarabu kakamzuia baba Rahma kuendelea kunichana kwani mwili wagu mzima ulilowana damu zilizo uchafua uso wangu hii ni kutokana na kiwa kichwa chini miguu juu.Mzee aliye mzuia baba Rahama akaishika
Bakora yake na kuanza kunichara mikwaju mingi isiyo naidadi kiasi kwamba nikajikuta nikilia hadi nikaanza kucheka kwa uchungu.Mzee anaye nichapa akazungumza maneno ya kufoka kwa kiarabu kisha akaitupa fimbo yake chini na kunishika masikia yangu na kuaza kuyavuta huku akinitingisha tingisha kichwa changu
Akaniamchia na wakazungumza na kutoka ndani ya chumba na kuniacha nikiwa ninalia kwa uchungu kiasi kwamba nikamuomba Mungu aweze kunichukua kwa wakati huu niweze kupumzika mahali pema peponi,Taa ikazimwa na nikaendelea
Kuvuja damu na nikalisikia gari likiwashwa na kuondoka.Ndani ya robo saa nikahisi kufuli la mlango likifunguliwa nikajua wanarudi tena ila nikaona mtu akiingia akiwa amevalia nguo nyeusi kutokana na damu zilizo tanda usoni na giza kali sikuweza kuona ni nani
“Ohhh Eddy mpenzi wangu”
Nikajua ni Rahma baada ya kuisikia sauti yake kisha akanikumatia huku akiwa analia kwa uchungu,
“N....ifungue”
Nilizungumza kwa shida na kumfanya Rahama kuanza kutafuta swichi ya kuwashia ndani ya chumba ila hakuiona,
“Ra...hma unatafuta nini?”
“Semehe waliyo ifunga hii kamba”
Rahma kwa bahati nzuri akaiona sehemu niliyo fungwa na kutokana na ugumu na kukazwa kwa kamba hii ikamlazimu kutoka nje na nikastukia taa ikiwashwa na akaingia huku akiwa ameshika jiwe lenye ncha kali ila baada ya kuniona jinsi nilivyo akabaki akiwa ananishangaa kiasi kwamba akazidi kulia
“Rah...ma”
Rahma akastuka na kuanza kupiga hatua za haraka hadi sehemu yenye nondo iliyo kitwa kutani na ndipo kulipo fungwa kamba iliyo kwenda kwa juu na kupita kwenye chuma kingine na kunining’iniza.Rahma akaanza kuipiga piga kamba kwa kutumia nguvu zake hadi kamba ikaanza kukatika taratibu
“Jika...ze....Ba...by”
“Sawa mume wangu”
Rahma akajitahidi kukata hadi kamba ikakatika yote na kunifanya nianguke kama mzogo na ni-zidi kapata maumivu mengi.Rahma akanifwata na kunikumbatia huku akiwa analia kisha akanza kunifungua kamba za mikononi nilizo fugwa kwa nyuma.
Rahma akaninyanyua na kutokana na kipigo kikali nikajikuta ninakosa hata nguvu za kuniwezesha kutembea.
Rahma akauchukua mkono wangu mmoja na kuupitisha begani mwangu na kuninyanyua na taratibu tukaanza kutembea taratibu kutoka nje na kuuona msitu mkubwa na kwa mbali tukaziona taa za gari zilija eneo la chumba kilichopo.
“Mungu wangu ni gari ya baba.....Eddy jikaze tuondoke”
Rahma akanihimiza na nikajikaza japo mwili wangu umepoteza nguvu na tukaanza kutokomea msituni na mwendo wa dakika kama tano nikakuta gari ambayo Rahma mara nyingi huwa hui-tumia.
Akaniingiza kwenye siti ya mbele kisha na yeye akaingia upande wa dereva na akaiwasha gari na kuotoa kichakani alipo ificha na kwa kasi ya ajabu akaingia barabara ya vumbi iliyopo ndani ya msituu huu na kuendelea kuliendesha gari na sikujua tunaelekea wapi.
Galfa nimamuona Rahma akitoa msunyo mkali kiasi kwamba kwa shida nikakinyanyua kichwa changu na kuangalia nyuma na kuona gari ikijakwa kasi huku ikiwa imewasha taa zake zenye mwanga mkali na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kunienda kasi
Gari tuliyomo ikaanza kutoa mlio ulio ashiria mafuta ya gari kuisha na kadri tunavyozidi kwenda ndivyo gari lilivyozidi kupungua mwendo na kuliruhusu gari la nyuma yetu kutufikia kwa ukarubu zaidi na mwish wa siku gari ikasimama kabisa na kumuona Rahma akitetemeka mwili mzima na asijue nini anafanya.
Gari ya baba Rahma ikasimama kwa nyuma yetu na kumuona baba Rahma akishuka huku mkononi mwake akiwa na bastola,Wakafwatia wazee wawili wa kiarabu pamoja na lile jijamaa jeusi.Nikashika kitasa cha mlano na kukifungua na kudondoka chini kisha kwa tabu nikasimama huku nikiwa nimelishaka gari kwa msaada wa kuto kudondoka
“Eddy nini unafanya?”
“Nipo tayari kufa Rahma siwezi kuishi tena.....Niache nife mbele yako”
Nilizungumza kwa uchungu huku nikiwa nimejishika tumboni kwenye maumivu malali na kumfanya Rahma kushuka kwenye gari kwa haraka na kusimama pembeni yangu huku akilia na kumuomba baba baba yake asifanye kitu anachotaka kukifanya.
Baba Rahma akaikoki bastola yake na kunielekezea mimi huku akiwa amesimama umbali kidogo na sehemu tuliyo simama sisis akimsikiliza mwanaye kitu anacho kizungumza
“Baba kumbuka kwamba mimi ni mwanao na ninauhuru wa kuchangua na kufanya kila ninachi kihitaji na siwezi kumuacha mwanaume ninaye mpenda katika maisha yangu”
“Nyamaza wewe mshenzi...mwanaharamu siwezi kukuruhusu kuwa na watu kama hao”
“Mzee wangu fanya unacho kifanya nipo tayari kwa lolote utakalo liamua”
Maneno yangu niliyazungumza kwa uchungu huku nikiwa ninatokwa na machozi na nikapiga hatua mbili mbela na kustukia mlio wa bastola na kujikuta nikiwa nimeanguka chini huku tara-tibu nikimshuhudia
Rahma akianguka huku akiwa amejishika tumboni akitoa kilio cha maumivu makali hii ni baada ya Rahma kunivuta mimi pembeni na yeye kupigwa na risasi ambayo baba yake aliifyatua kwa lengo la kunipiga mimi ili kuniua
Sote tukabaki tukimshangaa Rahma anaye anguka chini taratibu,nikajikongoja taratibu huku nikitambaa taratibu nikijaribu kuunyoosha mkono wangu mmoja ili kumshika Rahma na kabla sijamfikia nikastukia miguu yangu
Ikishikwa na lile jitu jeusi na kuanza kuniburuza kwenye majani na kuwaacha wazazi wa Rahma wakimbeba mtoto wao na kumuingiza kwenye gari huku damu zikimvuja.Jamaa likazidi kunivuta na kunitokomeza msituni na mbaya zaidi kila anavyo
Niburuza ndivyo jinsi ninavyozidi kupata michubuko huku miba mikali aina ya mbigili ikiingia mwilini mwangu na kuzidi kuniogezea maumivu makali.Jamaa akaanza kunipiga mateke ya tumboni kiasi kwamba nikahisi ndio mwisho wa maisha yangu
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA