TANGA RAHA (32)

0
SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Niburuza ndivyo jinsi ninavyozidi kupata michubuko huku miba mikali aina ya mbigili ikiingia mwilini mwangu na kuzidi kuniogezea maumivu makali.Jamaa akaanza kunipiga mateke ya tumboni kiasi kwamba nikahisi ndio mwisho wa maisha yangu
SASA ENDELEA...
Jamaa akatoa kamba aina ya manila na kunifunga kwenye miguu na mikononi kisha akarudi se-hemu walipo wazazi wa Rahma na nikaanza kujaribu kujifungua kamba kwa kutumia meno ila kutokana na kwa jinsi alivyo ikaza nikajikuta nikishindwa kujifungua,

Nikamuona jamaa akirudi huku mkononi mwake akiwa ameshika chepe na sururu na nikazidi kuogoa na sijujua analengo gani.Jamaa akaviweka vitu vyake pembeni na kuanza kuchangu majani kwa kutumi mguu wake wa kulia ulio valia buti kubwa.

Nikapata jibu la jamaa kuja na vifaa vyake baada ya kuanza kuchimba shimo kwa kutumia sururu huku chepe akilitumia kwa kutolea ichanga.
“Ohhh Mungu wangu ninakuomba uniongoeze wewe ndio kila kitu kwagu na kuomba huyu ja-maa abadilieshe mawazo asinizike nikiwa hai mimi”

Nilizungumza kwa uchungu huku machozi yakinimwagika nikajaribu kujifungua kamba ila nikashindwa na kujikuta nikiwa nimetulia huku nikilia na kujutia ni kwanini nimekuwa na mahusianao na Rahma.
“Kaka....Kaka....Kaka”

Niliita na jamaa akaniangalia kwa macho makali ambayo kwa muonekano wake anavuta bangi kiasi kwamba macho yake ni mekundu kiasi,
“Ndugu yang...u tambua kuwa m...imi na wewe ni wa..tanzania...Pia sisi ni wanaume haya mambo leo hii yana..nipa..ta mimi ila kesho yanaw...eza ya katokea kwako kwa m....fumo mwengine nakuoma ndugu yangu nifu..ngue niweze kuondoka”

Jamaa akanitazama kwa jicho kali kisha akashika chepe lake na kuendelea kutoa mchanga kwani tayari ufefu wa shimo analo lichimba umefikia usawa wa kiono chake,Jamaa akavua shati lake kabisa na kubaki kifua wazi na kuendelea kuchimba shimo huku akifanya haraka.
“Mungu atak....upa swa...wabu zake pale utaka....po nisaidia mimi ni sawa na ndugu yako...kwani sisi ni wa Afrika na hao waarabu japo wana pesa ila sio wa Afrika...Kaka....KAKA...!!”

Nilizungumza kwa shida sana ila jamaa akawa kama hanielewi kiasi kwamba akazidi kuchimba shimo na akiwa anaendelea nikasikia mngurumo wa gari ukipita maeneo ya barabara ilipo na nikaanza kupiga kelele na kumfanya jamaa kutoka kwenye 

Shimo haraka na kunishika kichwa changu kwa mkono wake mmoja kisha mkono mwengine akiwa na kazi ya kunisokomeza shati lake alilo livua kiasi kwamba likaingia karibia nusu ya shati na kujikuta sauti ikiwa haitoki kabi-sa

Jamaa akarudi kwenye shimo na kuendelea kuchimba na safari hii akatumia nuvu nyingi sana hadi nikamuona akizidi kwenda chini kiasi kwamba akawa anaonekana kichwa na kwa jinsi alivyo mrefu nikajua kabisa shimo ni refu kiasi kwamba hata nikifukiwa humo sio rahisi kwa mtu kuja kuiona maiti yangu kiurahisi.

Jamaa akatoka ndani ya shimo na kupiga hatua za kuja eneo nililopo kisha akaninyanyua na kuniweka begani kwake na kabla hatujalifikia shimo tuka-muona mzee yule wa kiarabu aliye nicharaza bakora nyingi akija akiwa peke yake hadi sehemu yulipo simama
“Pumbavu sana hiyo kijana weka ndai shimo zika potelee humo changani....Peleka Rahma Hos-pital acha baba yeke kule na jomba yake mimi rudi kuja angalia kazi jinsi inavyokwenda”

Mzee alizungumza kwa sauti ya ukali huku Kiswahili chake kikiwa ni kibovu kiasi kwamba nikajikuta nikisali sala yangu ya mwisho huku nikitubu zambi zangu zote nilizo zofanya duniani kwani huu ndio mwisho wangu wa maisha na sina ujanja zaidi ya kusali
“Pesa yangu ipo tayari?”

Hapa ndipo nikaishikia sauti ya jamaa na kushangaa ni sauti ya upole na ninzuri tofauti na ni-navyo muona.
“Ndio ipo ndani kula ya gari hembu ngoja kwanza mimi chungulia ndani hii shimo ona kama refu ridhisha”

Mzee akalisogelea shimo na kulitazama huku akiwa amekitanguliza kichwa chake kama mtu anaye hofia kudumbukia ndani ya shimo hilo.
“Wewe pumbavu sana shimo dogo hili chimba refu sana hata mbwa polisi nusa shindwa pata harufu yoyote”
“Mzee nani mpumbavu?”
“Wewe pumbavu sana lipa pesa chimba shimo dogo hata zika panya harufu toka nje”
“Eti ehee”

Nikastukia jamaa akitingishika na kusikia kilio kikali cha mzee wa kiindi kilicho ambatana na kishindo kizito cha kisha jamaa akanishusha na kuniweka chini na kwa haraka akaokota chepe lake na sikumuona mzee kwenye usawa wa ardhi na nikaisikia sauti yake ya kulia ikitokea kwenye shimo.

Jamaa akachota mashepe wawili yaliyo jaa mchanga na kujatumbukiza ndani ya shimo na mzee akaendelea kupiga kelel huku akitoa matusi yaliyo changanyikana na lugha ya kiarabu,Jamaa akaweka chepe lake chini na kunyanyua sururu na kuitupa ndani ya shimo na kumsikia mzee akitoa ukelele mkali na nikajua kabisa sururu hiyo itakuwa imempata vizu-ri.

Jamaa akaanza kuzunguka huku na kule kama mtu aliye changanyikiwa na akazunguka nyuma ya mti na ndani ya muda mchache akarudi akiwa amebebe jiwe kubwa na linalo onekana zito sana kwani japo jamaa ana misuli mikubwa ila akaonekana 

Kupata shida sana katika kulinyanyua jiwe hili na akafika sehemu ya lilipo shimo kisha akazungumza maneno ya kilugha Kitukuyu kisha akalitupia ndani ya shimo na kuusikia mlio mmoja wa mzee na ukimya ukatawala

Jamaa akachukua chepe na kuanza kufukia kwa haraka shimo na ndani ya kama dakika kumi akawa amemaliza kulifuka shimo kisha akachukua matawi ya mti na kuyaweka juu ya sehemu ya shimo kisha akapiha ishara ya msalaba na kunisogelea sehemu nilipo na kunifungua kamba alizokuwa amenifunga kisha akanita shati ambalo alikuwa amenikandamiza nalo mdomoni
“A....saante”
“Powa na hii iwe siri yako na ole wako nisikie kitu chochote kitakacho husiana na hili tukio nita-kuua na nitatoka tena Kenya na kurudi Tanzania kwa ajili yako”
“Siwezi kuzungumza kwa mtu”
“KIMBI”

Nikajaribu kukimbia na kujikuta nikianguka kama mzingo na kujikuta nikianza kutembea kwa kutumia msaada wa miti iliyopo ndani ya huu msitu ambao unatisha sana.

Nikajikaza na kuongeza mwendo hadi ikafikia hatua viungo vyote vya mwili vikakataa kwenda sehemu yoyote na nikajikuta nikikaa chini na kujiegemeza kwenye mti mkubwa na kutokana na uchovu mwingi na kajiupepo kalichopo kwenye eneo la huu msitu nikajikuta nikilala na usingizi mzito ukanipitia

Nikasushwa na kitu kikubwa chenye ubaridi mkali kikinizunguka kweye mwili wangu huku ki-kiwa na ngozi inayo laini.

Nikayafumbua macho na kukuta ni joka kubwa likiwa limeziningira mara mbili kwenye mwili wangu na sikukiona kichwa chake kipo kwa wa-pi.

Nikajikaza mwili wangu na kuyafumba macho yangu huku nikijaaribu kuzibana pumzi zangu mara kwa mara.

Mwanga wa jua ukatawala anga na sehemu yote ya msitu nikaioa kw azuri huku nikitumi kona za macho yanga kuliangalia joka lililo nizingira,Sikuyaruhusu mapigo yangu ya moyo ku-nienda mbio kwani ndio ugekuwa ndio mwisho wa maisha yangu kwani ninaamini joka hili linanisikilizia na kitu kingine kilicho nichanganya zaidi sikujua mwili wake upo kwa wapi.

Nikaanza kuhisi ute ute ukiniangukia kichwani na kwajinsi ulivyo na harufu kali nikatambua kabisi kichwa chake kitakuwa kipo juu ya kichwa changu.

Nikazidi kujikausha na masaa yakazidi kunikatika ila joka likaendelea kunijikausha huku likiwa linaendelea kunidondoshea ute.

Nikazisikia kelele za umbwa wakilia na wakijawa wapo sehemu ya karibu na eneo hili na gafla nikasikia mlio wa bunduki na damu nyingi zikinimwagikia huku joka likiniachia na na kuanza kugara gara chini,Nikawaona watu wapatao sita huku wawili wakiwa na bunduki aina za magobore na wengine wakiwa na mishale na mikuki.

Wakaanza kulishambulia jo-ka wa mishake hadi likatulia kimya.Jamaa wakaanza kushangilia huku wakipiga vigele-gele na nikagundua ni wamang’ati wanao ishi huku Tanga.Cha kumshukuru Mungu ni joka hili kuwa linaonekana limeshiba sana kwani sehemu ya tumboni kwake imefuka na kama sio hivyo ningekuwa kitoweo cheke.
“Wewe vipi?”

Jamaa mmoja aliniuliza huku akinishangaa,Sikuweza kumjibu kwani hata uwezo wa ku-zungumza uliniishia.Jamaa wawili wakaninyanyua na ninibeba na kuondoka msituni huku nikiwaacha jama wengine wakiwa msituni wakilipasua joka.

Tukafika kwenye moja ya kijiji chenye nyumba nyingi za udongo na zilizo ezekwa na nyasi huku kikiwa na maboma mengi yaliyo kusanya idadi kubwa ya ngombe.

Wanakijiji walio valia nguo ambazo sio nzuri sana wakaanza kunishangaa na nikaingizwa kwenye moja ya kijikibanda na kumkuta bibi mmoja mzee kiasi na wakanilaza kwenye kijimkeka kilicho shonwa kwa aina yake
“Bibi huyu jamaa tumemuokota huko porini tulipokuwa tunaliwinda lile jijoka lililo kuwa lime-luka ndama jana usiku”
“Mumefanikiwa kuitumia ile dawa niliyo wapa?”
“Ndio bibi tumefanikiwa kuitumia kama ulivyo tuelekeza na tumwefanikiwa kuliua joka hilo na tulilikuta likiwa limejiviringisha kwenye mwili wa huyu jamaa”

Bibi akanitazama kwa umakini kuanzia juu hadi chini na macho yake yakasimama kwa muda kwenye mkono wangu wa kushoto kisha akaushika na kuunyanyua na kuiangalia pete niloyo ivaa kisha nikamuona akikitingisha kichwa chake na sikujua ana maana gani.
“Kanichoteeni maji kisimani nije kumpaka dawa huyu kijana”

Jamaa wakaoondoka na nikabaki na bibi na kumuona akifungua fungua vikopo vyak vingi am-bavyo vimejaa dawa za kienyeji za kila aina na akabandika maji yaliyomo kwenye chunga cheusi tii kwenye jiko lake ambalo limetengenezwa na udongo na kwa utaalamu mkubwa na japo ninajisikia vibaya ila sikusita kulishangaa na linatumia kuni.

Bibi akaanza kunivua suruali yangu na nikabakiwa na boksa,Jamaa wakarudi wakiwa wamebebe ndoo mbili kubwa zilizo jaa maji mengi na kuziweka pembeni na bibi akawaruhusu waondoke na kutuacha peke yetu.

Akaanza kunifuta damu zilizo ganda mwilini mwangu kwa kutumi spoji ambalo analichovya mara kwa mara kwenye maji aliyo yachangaya kati ya maji ya moto aliyokuwa akiyachemsha na maji yaliyo toka kisimani na kusababisha uvuguvugu wa maji hayo.

Akamaliza kuniosha kila sehemu ya mwili na akanifuta na kitambaa licho kauka kisha akachu-kua mafuta ambayo harufu yake inaendana na kondoo na kunipaka kila sehemu yenye kidonda na akachanganya dawa zake za unga kisha akaanza 

Kuninyuzizia mwili mzima na kujikuya mwili wangu ukiwa unachemka kwa maumivu makali na kujikuata nikipata shida ila nikajikata katika kumwaga machozi.

Akachukua maji ya moto aliyo yachota kwa kutumia kikombe cha plastiki kilicho chakaa kiasi na kuweka vijiko kadha ya dawa zenye asili ya unga zinazo fanana kama majani ya chai kisha akaanza kuninywesha kilazima

Sikuwa na jinsi zaidi ya kunywa japo ninaungua tumboni ila nikajikaza kiume kwani huduma nyenyewe ninayo fanyiwa ni ya msaada
“Ndio jikaze mwanaume huwa halii...Hiyo dawa inakwenda tumboni kusafisha uchafu wote na-kuachia misuli iliyo na maumivu”

Tumbo likaanza kunikoroga kiasi kwamba nikaanza kuhisi kichefu chefu na kila nilivyo jikaza ili kukipotezea kisije nikajikuta kikiongezeka hadi mwishowa wa siku nikajikuta nikitapika hadi nikaanza kutapika vidonge vidogo vidogo vya damu iliyo ganda

KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)