SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Zote za mji,Huku miale miale mingi ya kutisha ikiaanza kutoka ardhini huku ikiwa inafanana moto wa Volkano.Gafla jumba la kina Rahma likaanza kumeguka taratibu na kutufanya tuanze kukimbia kuelekea kwenye ngazi.SASA ENDELEA...
Kabla hatujaanza kushuka ngazi tukakutana na mtu aliye vaa mavazi meupe tupu akiwa amesi-mama mwazoni mwa ngazi katika sehemu ya kupandishia huku macho yake yakiwa yanawaka manga wa kutisha ulio ufanya mwili mzima kunisisimka,
Tukiwa tunaendelea kumshangaa mtu huyo nyuma yetu tukasikia kishindo kikubwa kitendo cha kugeuka tukakutana na jitu lenye mabawa na meno yake yakiwa ni makali na yakutisha,na nyumba ikaendelea kumeguka vipande vipande
Rahma akazidi kuning’ang’ani mkono wangu kwani hali inazidi kuwa mbaya kadri jinsi muda unavyozidi kwenda,Mtu aliye vaa nguo nyeupe tupu akantonyooshea mkono kwa ishara ya ku-tuita tumfatwe,
“Agrrrrrrriiiii”
Jitu la nyuma lilinguruma kwa nguvu na kutufanya tushuke kwenye ngazi kwa haraka pasipo kupenda.Hadi tunamkaribia mtualiye valia nguo nyeupe naye akanza kupandisha ngazi kutuf-wata
“Edddyyy”
Rahma alipiha kelele, akimuogopa jamaa anaye panda.Nikajaribu kuunyanyua mkono wangu na kumrushia ngumi na kustukia akiuzuia pasipo kuushika na akapita pembeni yatu na kulifwata jitu lenye mabawa, na yakaanza kupambana.
Tukashuka kwenye ngazi kwa haraka na kutoka nje ya jumba la kina Rahma huku tetemeko la ardhi likiendela tena safari hii likizidisha kasi,Ardhi ikaanza kupasuka vipande vipanda, kila sehemu inapo pasuka basi linatoka jidudu linalo fanana na ng’ee ila lina vichwa vyaviwili kimoja kikiwa cha simba na kingine kikiwa cha joka kubwa.
“Eddy mume wangu tunakufa”
Rahma alizungumza kwa wpoga huku akimwagikwa na machozi mengi
“Hatufi , futa wazo hilo”
Nilizungumza kumpa moyo Rahma ila ukweli ni kwama endapo tutafanya kitu cha kijinga nila-zima tufe tena kitakuwa kifo kibaya kupita vifo vyote vya watu walio tutangulia,tukaanza ku-kimbilia kuelekea baharini, huku tkijitahidi sana kukwepa mipasuko ya ardhi.Tukafanikiwa kufika kandokando ya bahari pasipo kujeruhiwa na madudu ambayo yanatisha kwa muonekano wake
“Kitabu kilisemeje?”
“Kilisema kuwa, damu imwage baharini”
Nikamtazama Rahma kwa macho makali kisha nikaanza kuangaza angaza chini kutafuta kitu chenye ncha kali, nikaokota kijiti cha mti wa mkoko chenye ncha kaliNikapiga hatua na kuingia ndani ya maji hadi sehemu ambayo, maji yananifikia kwenye magoti.
Nikaunyoosha mkono wangu wa kushoto mbele na kujichoma kijiti kwenye moja ya mshipa wa damu, Damu nyingi zikaanza kunimwagika na taratibu zikaanza kuingia baharini na kusababisha maji kuanza kubadilika gafla na kuwa rangi ya damu.Nikatoka na kutazama jinsi maji ya bahari yanavyo chemka na kusababisha upepo ulio mkali sana.
Tetemeko la ardhi likaanza kutulia huku ardhi ikianza kijirudi kama kawaida,Hali ya upepo ika-zidi na kutulazimu kuweza kulala chini,Madudu ya ajabu yaakaanza kupeperushwa na kvutiwa habarini.Tukabaki kushangaa kuona yale majini ya kutisha nayo yakiwa yanavutwa na kuingizwa baharini.Hali ikazidi kuwa kwa viumbe hawa wa ajabu kuvutiwa bararini na taratibu hali ya upepo wa baharini ikatulia.
Nikasimama na kumpa mkono Rahma na kumnyanyua, tukakumbatiana kwa furaha huku tuki-pigana mabusu mfululizo ya mdomoni.
“Eddy umefanikiwa mume wangu”
“Ndio baby”
Nikamkumbatia kwa nguvu Rahma na yeye akafanya hivyo huku akiwa na furaha kubwa iliyo pitiliza kikomo.Tukiwa tunaendelea kukumbatiana gafla nikaona kitu kikubwa kinachomoza baharini, nikagundua ni joka kubwa ambalo lina vichwa kumi na mbili
“Rahma”
“Mmmm”
“Nenda kanisubirie nyumbani”
“Ehheee”
Nilizungumza huku kichwa cha Rahma nikiwa nimekielekezea nyuma yangu huku tukiwa bado tumekumbatiana, sikutaka Rahma aone chochote kitakacho endelea
“Nakuomba uende nyumbani, usiangalie nyuma utakapo ondoka hapa”
“Eddy mbona sikuelewi?”
Rahma akataka kujitoa mwilini mwangu ila nikamrudisha kifuani kwangu huku kichwa chake nikiwa nimekikandamiza begani mwangu na sikumpa nafasi ya kutazama nyuma
“Eddy do you love me?”(Eddy, unanipenda?)
“Yes my wife.....ila ninakuomba uondoke”(Ndio mke wangu........)
“Eddy hunipendi”
Rahma alianza kuzungumza huku akuanza akilia kwa uchungu
“Rahma nisikilize mimi, nakupenda na mimi ndio mume wako.Ila ninakuomba uondoke kwenda nyumbani”
Nilizungumza huku nikilitazama joka jinsi linavyozidi kujitokeza kwenye maji na kuanza kujitokeza kichwa kimoja baada ya kingine.Hadi muda huu limesha jichomoza vichwa viwili na kila linavyozidi kuchomoza kuelekea juu ndivyo jinsi vichwa vyake vinavyozidi kuchomoza.Nikaanza kurudi nyuma huku nikiwa nimemkumbatia Rahma
“Rahma ninakuomba uondoke sasa hivi”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali na kumfanya Rahma anitazame usoni mwangu, nikamuachia na akaondola taratibu huku akiendelea kumwagikwa na machozi, Rahma akapiga hatua kadhaa na kugeuka nyuma, macho yale akayatoa kana kwamba amakebwa na kitu kwenye koo.
“Nenda”
Nilizungumza kwa sauti ya ukali huku nikimtazama kwa hasira
“Eddy mume wangu utakufa”
“Nimesema nenda, usije huku.Siwezi kufa niamini mimi”
Rahma akarudi kwa kasi na kunikumatia kwa uchungu, furaha ambayo ilitutawala muda mchache ulio pita ilitoweka.
“Eddy ninakupenda sana, siwezi kukuacha mume wangu ukafa.Ni bora tufe sote kuliko wewe peke yako”
“Rahma, niamini mimi, Siwezi kufa sawa”
‘Eddy unanidanganya”
“Sikudanganyi”
Joka likazidi kuchomoza vichwa vyake hadi sasa hivi tayari imechomoza vicha vyake vinavyo tisha sana.Nikambeba Rahma juu juu hadi sehemu ya mbali kidogo na bahari na kumnyonya midomo yake vya mwisho mwisho kwani kitabu kinaelezea ni lazima nife ili wengine wapone
“Rahma, niamini mimi siwezi kufwa hata kidogo.”
“Mimi ninajua tuu unanifariji”
“No sikufariji mke wangu, ninakuhakikishia siwezi kufa niombee kwa Mungu”
“Mishale utaitoa wapi?”
“Sijui, ila tafadhali ninakuomba unielewe.Kumbuka ukinisaidi ndio nitakufa, niache nifanye haya yote peke yangu”
Nilizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa upole na unyenyekevu mkubwa.Rahma akanikumbatia tena kwa uchungu
“Eddy nitakupenda maisha yangu yote”
“Hata mimi pia, nenda sasa”
Rahma akabaki akinitazama
“Nenda tafadhali”
Rahma akaanza kuondoka kwa mwendo wa taratibu huku akinipungia mkono, nikageuka na kukuta joka ndio linachomoza kichwa cha kumi.Nikaanza kukimbia nikielekea baharini kwa bahati mbaya nikajikwaa kwenye mizizi ya mti wa mkoko na nikaanguka chini kama gunia.
Nikiwa ninajinyanyua nikaona podo lenye mishale likiwa limening’inizwa kwenye moja ya mti wa mkoko huku pembeni yake kukiwa na upinde pamoja na baadhi ya vitu ambavyo hutumika katika kufulia,Kwa haraka nikaviendea na kuchukua podo lenye mishale na kuliuvaa mgongoni mwangu.
Nikaushika upinde mkono wa kushoto na kuvua shati langu na kubaki kifua wazi.Nilipo hakikisha nipo sawa nikachomoa mchale mmoja na kuuweka kwenye upinde, kitu kilicho nichanganya ni maneno ambayo yaliandikwa na sote hatukaelewa
“Vyovyote”
Niijisemea kimoyo moyo,huku nikitazama kichwa cha kumi na mili kikijichomoza kwenye maji, umbali mrefu kati yangu na joka kubwa ambalo nakumbuka nililiona kuzimu ukanipa ujasiri wa kijiamini zaidi ,nikataka kupiga hatua na kuingia
Ndani ya maji ila mwili wangu ukawa mzito kupiga hatua za kuingia ndani ya maji.Joka likaanza kutoa moshi mwingi kwenye pua za vichwa vyake na kilicho fwatia hapo akaanza kutoa moto mwingi kwenye midomo yake huku ukiwa unaelekea sehemu nilipo mimi
“In the name of Lord”(Kwa jina la bwana)
Nilijisemea huku nikiuvuta mshale nyuma kwa nguvu zangu nyingi huku nikitumia kamba ngumu ya manila iliyopo kwenye upinde.
Nilipo hakikisha uvutaji wangu unaweza kuufanya mshale kwenda kwa kasi na mbali zaidi nikaachia huku nikiwa nimeuelekeza kwenye kicha cha sita.
Kwa bahati nzuri mshale ukatua kwenye kichwa cha joka na kukifanya kichwa hicho kuanza kupaparika na kuchanguka na kusababisha joka kutoa ukelele Mkali na mkubwa wa maumivu.
Joka likazidi kutema moto mwingi kwa hasira, ambao hakunizuia kuifyatua mishale kuelekea vilipo vichwa vingine navyo vikapasuka
Joka likaanza kuja nchi kavu, huku likimwaga moto mwingi na sasa hivi moto wake akaanza kuutoa kwa mfumo wa madoge mabukubwa kama mpira yaliyo nfwata kwa kasi.
Nikaanza kujirusha pembeni huku nikiwa ninayakwepa kwa utaalamu mkubwa, Sikubaki nyuma na kuzidi kuendelea kuifyatua mishale yangu, na kufanikiwa kuviangamiza vichwa nane na kuzidi kulizidisha hasira joka
Joka likazidi kunifwata huku likinitemea madonge donge ya moto yalito anza kubadilika na ku-wa kama mishale iliyoanza kuja kwa kasi.Nikaendelea kufyatua mishale hadi nikafanikiwa kuua vichwa viwili na kubadi kimoja, Joka likaruka juu na likazama ndani ya maji na kupotea gafla.Nikabaki nikiwa nimesimama kutazama ni wapi lilipo joka.
Nikasimama kama dakika tano na sikuona dalili yoyote ya kuwepo kwa joka, bahari nzima ikawa imetulia na upepo ukarudi katika hali ya kawaida.
“Yeeahaa”
Nikaanza kushangulia huku nikiruka ruka juu, nikaanza kupiga hatua nikiondoka baharini hu-ku nikiwa nimejawa na furaha sana.Gafla nikasutkisha nikastukia nikirushwa juu na nikiwa angani nikalishuhudia joka likiwa limeufumbua
Mdomo wake, huku likiningojea niingie ndai ya kinywa chake.Nikaanza kurudi chini kwa kasi kubwa huku nikipiga kelele nyigi na moja kwa moja nikaingia ndani ya mdomo wa joka
Kwa, haraka nikachomo mshale ulipo kwenye podo langu nililo livaa mgongoni, Nikiwa ninaendela kushuka katika tumbo la mwili wangu, huku nikiwa nimeibana pumzi yangu.Nikaukita mshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza
kuuchana mwili wake huku nikimshale wangu kwenye tumbo la joka hili na kuanza kuuchana mwili wake huku nikiwa ninaendelea kushuka nao chini hadina kumfanya joka hili kuanza kubingiria bingiria huku maji mengi, ya bahari yakiwa yanakingia mwilini mwake
Wingi wa maji unao ingia mwilini mwa joka, yakanifanya niweza kupata nafasi ya kutoka nje ya joka hili ambalo bado linaendela kutapa tapa kwenye maji huku likitoa ukelele mkali.Jokaa likaanza kufutuka huku likiwa moto mkali,
Kwa bahati mbaya likanipiga kikumbo, kwa kutumia mkia wake kilichorusha mbali na eneo alilo kuwepo na kunitoa nje ya bahari na kwabahai mbaya nikangukia kwenye kisiki cha mti wa mkono, na kutulia tuli huku giza zito likitawala macho yangu
“Eddy......Eddy”
Kwa mbali niliisikia sauti ya Rahma ikiniita,nikayafumbau macho yangu taratibu na kukutana na mwanga mkali ulio nipiga kwenye macho yangu, huku nikiwa, nimelala kwenye kitanda nikipelekwa nisipo pajua na pembeni yangu akiwepo
Rahma naye akionekana akitembea huku machozi yakimwagika.Kila ninapojaribu kuyafumbua macho yangu, nikajikuta nikiona maruweruwe hata watu wanao kisukuma kitanda nilicho kilalia sikuweza kuwaona vizuri.Nikajikuta nikitawaliwa tena na giza kwenye macho yangu, na sikuelewa kilicho endelea.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA