NIFANYE NAMIMI KAKA (1)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
SEHEMU YA KWANZA
Nilikutana naye Mlimani City supermarket. Alionekana kuwa msichana mrembo sana, kuanzia sura yake ya kuvutia, umbo la namba nane, chuchu saa sita yani alikuwa ni mrembo kwelikweli. Kwa mara ya kwanza nilipomtazama nilijikuta nikitamani kuwa naye kimapenzi, akili yangu ikanituma nimfuate na kumwambia kile nilichokuwa nakitamani lakini moyo wangu ulisita, sikutakiwa kukurupuka kufanya hivyo.
Alionekana kuwa makini kufanya ‘shopping’ lakini hilo halikunitisha hata kidogo nilichoamua kukifanya ni kuanza kujongea kuelekea pale alipokuwepo huku kimoyomoyo nikijisemea ‘liwalo na liwe’.
“Mambo,” nilimsalimia huku nikilitengeneza tabasamu pana.
“Safi,” alinijibu huku akionekana kuwa bize kuchagua bidhaa aliyokuwa akiitafuta.
“Unaonekana kuwa bize sana vipi naweza kukusaidia?”
“Hapana asante.”
“Asante maana yake nini?”
“Nashukuru kwa msaada wako.”
“Ok vipi naweza kukufahamu kwa jina?” nilimuuliza huku nikijifanya kama ninayetafuta kitu fulani hivi kwa kuzuga.
“Kwani kuna ulazima wa kulifahamu jina langu?” alinijibu kwa kuniuliza swali lililonifanya nimuone kuwa msichana wa matawi ya juu sana. Alikuwa hapendi mambo ya uswazi uswazi sijui kila mtu unayekutana naye unaanzisha urafiki naye mara sijui unakutana na mtu unaanza kumchekea chekea kwake haikuwa hivyo, alikuwa ni msichana fulani hivi wa gharama, wazungu wanapenda kumuita “Expensive Girl.”
“Sio lazima kulifahamu lakini kama hutojali ningependa kulifahamu?”
“Wewe kaka vipi, hivi utafahamu wangapi wanaoingia supermarket hii au wewe ni mwizi nini?”
“Ndio mimi ni mwizi nataka kuliiba jina lako,” nilimjibu kwa kutania na kumfanya atokwe na kicheko cha bila kukitegemea.
“Wewe kaka umetumwa?”
“Ndiyo nimetumwa na moyo wangu nikuulize kuwa unaitwa nani?”
“Sitaki.”
Mpaka kufikia hapo nilikuwa nimeshafahamu kuwa alikuwa ni msichana wa aina gani, alikuwa ni miongoni mwa wale wasichana ambao wanapenda kubembelezwa, yani wao kila kitu ni kubembelezwa tu. Nilikwisha lifahamu hilo na sikutaka kulifanyia kazi niliamua kuendelea kumsumbua mpaka pale uvumilivu ulipomshinda.
“Haya naitwa Evadia,” alijitambulisha huku akionekana kuchoshwa na usumbufu wangu.
“Nafurahi kukufahamu,” nilimwambia kisha nikampa mkono lakini hakuupokea, aliupuuzia. Hilo halikwa tatizo kabisa, niliendelea na usumbufu wangu.
‘Naitwa Dickson lakini wengi wanapenda kuniita ‘Dick mapenzi’,” nilijitambulisha kisha nikaanza kuondoka eneo lile kimtego.
Sikumbuki ni nini kilitokea lakini nilishangazwa na mshangao uliomkumba Evadia mara baada ya kumtajia jina langu. Alinitazama mara mbilimbili kisha akawa kama mtu ambaye haamini kile alichokuwa akikishuhudia kwa macho yake. Alilirudia kuliita jina langu halafu akanitazama usoni, safari hii ule ubize aliokuwa nao ulimuisha, akanitazama tena huku akiwa haamini kabisa kukutana na mimi mahali pale.
Labda nikuambie kitu ndugu msomaji, nilikuwa na jina kubwa sana mitandaoni, hakukuwa na mtu ambaye alikuwa ni mtumiaji wa mtandao wa Istagram au facebook halafu akawa halifahamu jina langu. Wengi walikuwa wakinifahamu sana kutokana na hadithi zangu aina ya chombezo nilizokuwa nikiziandika katika mitandao hiyo, nilikuwa nikiongoza kwa kuwa na wafuatiliaji wengi wa machombezo nilizokuwa napost.
“Dick!” aliniita kwa mshango.
“Naam!” nilimuitikia halafu nikamgeukia, alizidi kunishangaa sana.
“Ni wewe?”
“Yeah! Ndiye,” nilimjibu huku nikimrudia, safari hii nilijifanya kubadilika kidogo, sikutaka anielewe kwa haraka kuwa nilikuwa ni binadamu wa aina gani.
“Kwani unanifahamu?” nilimuuliza huku nikijifanya sifahamu lolote.
“Ndiyo nafuatilia sana simulizi zako mitandaoni yani kila siku nilikuwa natamani siku moja nikuone maana sio kwa simulizi zile za mapenzi unazotunga,” aliniambia kisha akaja na kunikumbatia kyumbato ambalo lilinifanya nijione tayari nimeshang’oa mtoto.
“Siamini jomoni,” aliniambia kwa kisauti fulani hivi kama kile cha watoto wadogo.
“Hahahaha sasa huamini nini?” nilimuambia.
“Yani kukutana na wewe kwangu ni bahati kubwa sana.”
“Usijali,” nilimwambia kisha nikajitoa katika kumbato.
Evadia hakutaka kuamini kama alikutana na mtu kama mimi ambaye nilikuwa nikisifika sana, wasichana wengi walikuwa wakitamani kuniona ‘live’ lakini lilikuwa ni jambo gumu sana kutokana na ubize niliyokuwa nao nilishindwa kukutana nao, mazungumzo mengi yaliishi kwenye simu, nilikuwa nikichat na wasichana wengi sana na kila mmoja alikuwa akionyesha kunipenda, hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana wote ambao walijilengesha mtegoni sikuweza kuwaacha nilihakikisha nawapa dozi. Alichoamua kukifanya Evadia ni kuitoa simu yake aina ya Iphone 6 yenye gharama ya zaidi ya shilingi milioni moja za kitanzania kisha akaanza kupiga selfie na mimi.
Nilichokuwa nakiwaza kwa wakati huo ni kwa jinsi gani ningeweza kumpata Evadia ambaye alikuwa amenivutia sana, nilimtamani sana kiasi kwamba mtarimbo wangu ukashindwa kuvumilia mwisho ukajikuta umesimama dede.
“Unajisikiaje?” nilimuuliza huku nikimtazama, alionekana kuwa mwenye furaha sana.
“Najisikia vizuri sana.”
“Nipe namba yako,” nilimwambia kisha akaingiza mkono katika pochi yake, akatoka na ‘business card’ halafu akanipa.
“Utanitafuta.”
“Muda gani?”
“Muda wowote kuwa huru Dick,” aliniambia.
Nilichoamua kukifanya ni kuondoka eneo lile, sikutaka kuendelea kubaki kwani nilikuwa nazidi kujiumiza tu, mtarimbo wangu uligoma kushuka, kila nilipokuwa nikimuangalia Evadia ndiyo kwanza ulizidi kusimama dede.
“Acha mi niondoke,” nilimwambia.
“Unaenda wapi?
“Kuna sehemu natakiwa kwenda.”
“Kwahiyo umeghairi kufanya shopping?”
“Hapana nitafanya nikirudi,” nilimuambia kisha nikaanza kuondoka, Evadia alizidi kunitazama sana, nililifahamu hilo pale nilipoamua kugeuka na kumuangalia, alikuwa akinitazama muda wote.
Niliamua kuondoka lakini akilini nilikuwa nikiwaza ni kwa nmna gani ningeweza kumpata Evadia. Niliamini kupitia kipaji changu cha kuandika machombezo kingeweza kunirahisihia kazi yangu.
“Lazima nikupate tu!” nilijiambia kisha nikatabasamu.
Nilitoka eneo lile la supermarket na sasa nilikuwa nje, macho yangu yaliendelea kushuhudia wasichana warembo wengi waliyokuwa wakiingi ndani ya supermarket ile.
Macho yangu yalitua kwa mwanadada mmoja ambaye alikuwa akilielekea gari aina ya Land cruser prado lenye rangi nyeusi. Alikuwa na mwili wa wastani uliyogubikwa kila aina ya sifa unazozifahamu. Alikuwa na rangi nyeupe iliyofuatiwa na uzuri wa sura yake ya kitoto. Lipis pana za kunyonya, umbo matata, nyuma alikuwa na chura kubwa. Kwa kweli nilipomtazama nilimtamani ghafla! Na ni hapa ambapo mawazo yangu yalihama kabisa mahali pale, yakanipeleka tayari nipo chumbani kitandani sita kwa sita na yule mwanadada tukijiandaa kwa ajili ya mechi.
“Wewe kaka vipi?” sauti nyororo ya yule mwanadada ilinishtua kutoka katika yale mawazo yangu.
“Yes! Naam,” niliitika katika namna ya kukurupuka huku nikijishtukia, mtarimbo wangu ulikuwa tayari umesimama.
“Mbona unanitumbulia mimacho muda wote?” aliniambia kwa sauti laini iliyozidi kuniamsha hisia zangu zilizowahi kulala usingizi wa wahenga.
“Kwani kuna ubaya nikikutazama?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni, alikuwa na macho ya kurembua.
“Hakuna ubaya lakini wewe umezidi kha!” aliniambia huku akiibetua midomo yake, alizidi kuonekana mrembo sana.
“Duh! Siamini,” nilimwambia huku macho yangu yakiendelea kutalii vyema kifuani mwake, alikuwa na chuchu zilizochongoka vyema mithili ya kifuu cha nazi.
“Huamini nini?” aliniuliza kisha akawa kama ananitazama kwa kizembe.
“Hivi kumbe Tanzania bado kuna wasichana warembo?” nilimuuliza swali la kizushi lililomfanya anishangae kwa muda.
“Warembo, kwani umesikia hawapo?”
“Nina miaka kama kumi hivi sijawahi kumuona msichana mrembo kama wewe, wote naishia kuwasoma katika simulizi,” nilimuambia maneno yaliyomfanya atokwe na tabasamu pana lililotengeneza vishimo vidogo mashavuni mwake.
“Hee! Kumbe unajua kuficha siri hivyo?” nilimuuliza huku nikijifanya kama nimeshtuka kwa kuona kitu ambacho sijakitegemea.
“Siri gani?” aliniuliza.
“Nimesimama na wewe muda wote huo kwanini usiniambie kuwa una dimpoz?” nilimuambia katika namna ya kumuuliza swali la kizushi lililomfanya atokwe na kicheko.
“Mbona unanicheka sasa?”
“Hapana sikucheki.”
“Ila?”
“Umenifurahisha tu.”
“Halafu hujaniambia kitu?”
“Kitu gani?”
“Jina lako?”
“Oooh! Sorry naitwa Precious.”
“Precious ndiyo jina lako?”
“Ndiyo Precious Kamba.”
“Aliyekupa jina wala hakukosea yani limefit mahali pake.”
“Hahahaha kwanini?”
“Jina zuri wewe mwenyewe mzuri.”
“Asante na wewe unaitwa nani?”
“Mimi naitwa Akili za wote.”
“Ndiyo jina lako.”
“Ndiyo.”
“Unaishi wapi?”
“Tandale kwa tumbo.”
“Tandale?”
“Ndiyo kwani vipi?”
“Hamna!”
“Sawa.”
“Haya kwahiyo unaingia au unatoka.”
“Nipo katikati.”
“Niambie bhana ili nikupe lift kama hutojali maana naelekea Magomeni napitia Tandale.”
“Dah! Nashukuru Precious umeiokoa nauli yangu ya ngama maani sisi wengine kuja supermarket mpaka sikukuu kwa sikukuu,” nilimwambia Precious kisha akacheka. Tulipanda kwenye gari na safari ikaanza hapo, barabarani hakuna nilichokuwa nawaza zaidi ya mapenzi, Siku hiyo nilipanga niende na Precious mpaka nyumbani kwangu japo alionekana kuwa mwenye haraka mno.
Barabarani Precious alionekana kuwa ni mchangamfu sana, alikuwa akizungumza na mimi utadhani tulikuwa ni marafiki wa muda mrefu kumbe siku ile ndiyo ilikuwa mara yetu ya kwanza kuonana. Hahaha! Wanawake bhana ati! Ameniamini kabisa kiasi cha kunipa na lift.
“Hivi ulisema unaishi wapi vile?” aliniuliza hapa tulikuwa tumefika yalipo makutano ya barabara ya Mwenge kwa wakati huo tulikuwa tumeikamata barabara iliyokuwa inaelekea Makumbusho.
“Magomeni sijui,” nilijibu huku nikijifanya nimesahau.
“Hee! ni Magomeni au Tandale?” aliniuliza huku akinitazama kwa kujiibaiba.
“Kumbe unajua halafu unanichora,” nilimjibu kisha akatabasamu, tabasamu lilelile lililojenga vishomo mashavuni mwake ‘Dimpoz’, alizidi kuonekana mzuri mno.
“Hivi ulisema unaitwa nani?” aliniuliza tena hapa tulikuwa tumeshafika Bamaga.
“Sijui Dick?”
“Dick au Akili?”
“Yeah! Yote majina yangu hayo ila wengi wanapenda kuniita Dick mapenzi,” nilimjibu.
Sikumbuki ni nini kilitokea ila nilishangaa Precious akinitazama kwa mshangao, hakunisemesha chochote alibaki akiwa ameduwaa tu kama sanamu.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
TAZAMA KICHEKESHO HIKI KISHA BONYEZA SUBSCRIBE ILIYOPO CHINI YAKE WAKATI TUKIELEKEA KWENYE MUENDELEZO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni