SEHEMU YA KWANZA
Maisha safari japo si lazima ianzie stend. Dunia ina mambo tena vijambo toka kitambo. Eti ikisimama panda, ukipendwa penda.Mimi sio fumbo usiangaike kunifumbua mimi ni zawadi ikiweza nifungue.Nimezaliwa na ulimbo ukigusa utanata,ukinitaka utanipata.
Pesa ndo kila kitu ukiwa nayo utakula kuku mpaka bata. Maisha si lele mama ukishikwa shikamana.Dunia kweli kizingumkuti japo si jumba la makuti. Mungu nikijikuta nimeathirika nipe hata umauti maana sitaki kukonda kama kijiti. Yaani Sukari nigueke ugali, hili silitaki hata kwa mali.
Mungu nipe heri,niepushe na shari, nataka kutoa funzo kwa Watanzania na walio mbali.Ukiona ghali gharama basi tafuta vya kuparama.Ila chunga sana usije kuniparamia maji utaita mmmmaaa.Mimi sio wa jana wala juzi mimi ni wa enzi nakula visivyoliwa na ninanyoa zaidi ya kinyozi.
Aaaaaaaaaaah wacha nicheke mie eti unielewi kwa yangu misemo.Mimi sio mzaramo mimi ni mpogoro wa kule Mahenge Morogoro. Mimi sina soni kama mvivu wa kusoma, leo utakoma,sikuchambi wala sipiki tambi,sitaki rambi rambi, refa kashapiga filimbi weka sikio nikupe na moyoni.
Najua ushadata kwa Eliado kunipa nafasi kwenye ukumbi huu matata wa visa na visasi. Wacha nijinafasi mie, maisha yenyewe mafupi,kuna utamu uchungu na ukakasi.Mimi ni mshabiki wake wa mda mrefu japo si mrefu napenda sana kusoma simulizi zake kwa kina na marefu.
Leo nimeona si mbaya bishosti mimi mama la mama, mutoto ya mujibu kuwasimulia yaliyonikuta maishani .Japo si mabaya wala mazuri ila naamini mtajifunza yanayojiri huku duniani. Naitwa Bambucha, ndio Bambucha kinachokufanya ushangae ni nini?.
Bambuha maana yake kubwa kuliko (Extra-large).Ndio hivyo nimejaliwa mwenzenu yaani ya kwangu kumbwa kuliko alafu tamu kama asali. “Mwone ushaanza kuwaza ujinga japo ni mjanja”,mwenzio nimetania maana fupi tamu ndefu inakera ila hii simulizi ni Bambucha.
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
Kama huna pesa weka mbali na watoto wenzio wananijua ikisimama panda si kuku mimi ni bata mzinga. Ila majina yote haya si niliyopewa na wazazi wangu bali ni niliyopewa kutokana na kazi yangu.Sasa sitaki maswali subiri nikupe asali.Siunajua tena nzi naye akiacha ujinga siku moja atatengeneza asali. Sina shombo la samaki, mimi ni nanasi wewe nipe nafasi, nisome mwanzo mpaka mwisho.
Mimi wa kitambo kidogo maana nimezaliwa miaka 30 iliyopita kaatika kijiji cha Kwiro huko Mahenge Ulanga Morogoro.Wazazi wangu waliponizaa tu waliniita Vaileth.Nasikitika jina hili limekufa, kuzikwa na kusaulika.Sasa naitwa Bambucha mama la mama, bishosti wa mujini ninayekula kwa akili.
Mwenzenu nilizaliwa kwenye familia ya kimasikini sana. Familia ya mzazi mmoja tu yaani mama yangu ambaye alikuwa maarufu kwa jina la mama Vai kifupi cha Vaileth. Sikuwahi kumjua baba yangu mpaka leo hii nimefikia umri huu.Mama yangu naye ni moja ya watu ambaye historia yake nayo ilikuwa ngumu sana.
Kwa mujibu wake ni kwamba hata yeye alikuwa hawajui wazazi wake.Inasemekana walifariki yeye akiwa mdogo kabisa. Baada ya hapo alilelewa maisha ya kuunga unga mpaka hapo alipojitambua. Hakuweza kusoma zaidi alipata tu elimu ya kufuta ujinga na kwa maneno mengine naweza kusema aliishia darasa la saba.
Katika harakati zake za kutafuta maisha ndipo akaamia hiyo sehemu ambayo kilichompleka hapo ni shughuli ya kuuza chakula.Yaani alikuwa ni mama ntilie maarufu sana ukanda huo ambapo pia shule ya sekondari ya wavulana Kwiro ilikuwa ikipatina.
Kwa Mujibu wa mama yangu ambaye kwa sasa ni marehemu ni kwamba eneo hilo pia kwa mbele kunapatikan madini aina ya Ulanga na rubi. Hivyoo kufanya watu wengi sana kuja huko kujitafutia maisha.Hivyo mama yangu alifanikiwa kukutana na bwana mmoja mchimba madina ambaye alitokea kumpenda sana.
Mama yangu anasema kipindi hiko kilikuwa ni kigumu sana kwake hivyo ikamlazimu pia kuwa mjanja mjanja ili kufaya maisha yake yasonge. Anasema hakuwa akijiuza maana tayari alikuwa na biashara yake ya kuuza chakula na kujipatia kitu kidogo. Lakini kama alitokea mwanaume mwenye fedha za kutosha hakuacha kumchuna na kuendelea kupambana na maisha.
Katika miangako hiyo ndipo alikutana na mwanaume wa mgodini.Upendo ukakolea na hatimaye akabeba mimba yangu. Anasema bwana huyo siku za mwanzo alionesha upendo wa hali ya juu sana lakini baadaye alipomwambia ana ujauzito bwana huyo aliruka viunzi.
Mama yangu alikomaa hivyo hivyo mpaka akajifungua. Basi nilivyozaliwa mama yangu akaendelea kupambana na maisha. Mama yangu naye alikuwa ni mzuri tena mzurii wa asili. Hali hii ilimfanyia pia wanafunzi wapapatike sana naye. Pia hakuacha kuwachuna.
Ikawa mradi tu mwanaume na pesa nzuri basi alimkubali. Mama yangu aliaapa kunilea na atafanya lolote ilimradi tu nisome na nije kuwa mwenye mafanikio makumbwa sana duniani. Maiha yakaendeea na mimi nikaendelea kukua.
Lakini kadiri nilivyokuwa nakuwa mkumbwa kuna tofauti kidogo ilitokea.
Yaani mwili wangu ulikuwa ni mkubwa hata matiti na makilio yaliaanza kuonekana nikiwa kwenye umri mdogo sana. Hali hii haikumshangaza sana mama yangu maana hata yeye alikuwa si haba alijaliwa kiukweli kwa maneno mengine yaliyomo yamo. Nikiwa tu darasa la tano nikaanza kuwa kivutio cha wanaume wengi sana hasa hao wa kutoka Kwiro Boys.
Mama yangu kwa kuwa alikuwa akizijua tabia za wanafunzi hao na kwa jinsi wanavyoweza kutumia fedha zao kumlaghai alianza kunipa mafunzo ya kiutu uzima ambayo aliamini kuwa yatawea kunisaidia na kujitambua. Alinambia kuwa wanaume ni watu wabaya sana na ndio maana hata baba yangu alinikataa.
Taratibu taratibu akaanza kunijenga kisaikolojia na kuanza kuwachukia wanaume.Kwa hiyo nikawa wa kujitenga na kuwaepusha na wanaume wasio kuwa na aibu ambao walianza kuninyemelea nyemelea bila hata aibu. Hatimaye Mungu naye akawa ananilinda mpaka nikafanikiwa kumaliza darasa la saba salama.
Hapo sasa uzuri wangu huu wa kibantu ulianza kuonekana.Mtoto mdogo makalio makumbwa,chuchu ndo usiseme kama embe dodo. Miguu mizuri wenyewe waliita ya bia, sura kama ua ukicheza utajichua,umbo lenye mvuto mapozi utafikiri mtoto wa kishua.
Kweli asante Mungu maana ulininyima vingine ukanipa uzuri.Mimi mzuri bwana,niliumbwa nikaumbika,sipigi napigiwa. Aaaah mshaanza kuona wivu vingine utani tu.Sasa hapo ndipo nilianza kuyastaajabu ya dunia, mibaba mijitu nzima ilianza kunisumbua. Nikawa naachiwa mpaka chenchi hapo kwenye kibanda cha mama.
Kule shuleni Kwiro ndo usisme nikifika mimi na utoto wangu wauzaji wengine ilibidi wasubiri mpaka nimalize. Mama yangu alikuwa mwenye furaha sana maana biashara yake ilichanganya. Jina la Vai likawa kubwa sana na hakuna hasiyenijua. Kibalehe cha kwanza na chenyewe kiliniwahi sana nikajikuta naanza kusahau maonyo aliyokuwa akinipa mama.Nilitaka na mimi nijaribu hayo mambo ambayo mama kila siku alaikuwa akinikataza.
Kipindi hicho cha kusubiri matokeo ya darasa la saba kilikuwa kigumu sana kwangu. Wanafunzi wa Kwiro, walimu na hata wananchi wengine kila mmoja alikuwa akinitaka ili anionje na kuniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi. Ilikuwa ngumu sana kwao kutokana na uwoga ambao mama yangu alinijaza.
Mama yangu alidiriki kuniambia kuwa yeye ni muathirika hivyo nikicheza na mimi nitapata ukimwi. Nikweli mama yangu alijikwaa lakini kwa bahati nzuri mimi alinizaa nikiwa salama bin salimini.Siku moja majira ya sa mbili usiku ilisikika sauti kutoka shule ya sekondari ya wasichana St Agness ambayo ilikuwa ikiangalia na hiyo ya Kwiro Boys kuwa kuna moto ulikuwa ukitokomeza majengo yao.
Basi Mama yangu na yeye alitoka kwenda kushuhudia na kuniacha mimi nikiwa nimelala. Kwa bahati nzuri au mbaya na mimi nilishtuka kutoka usingizini na kusikia kilele hizo za wanafunzi wa kike.
Basi kwa kiherehere changu na mimi ilibidi nitoke ili kujua nini kinaenelea. Uzalendo ukanishinda kelele za mabinti hao zilikuwa juu nikasema ngoja na mimi niende kujionea sio kesho nasimuliwa. Siunajua tena mwanamke umbea babuu eeeeh. Sasa kwa mahali ambapo sisi tulikuwa tunaishi ilikuwa ni lazima uzunguke Shule ya Kwiro au upite katikakati.Kwa kuwa nilikuwa na haraka haraka zangu niliamua kupita katikati japo ilikuwa ni usiku.
Ile nakatisha kwenye migomba nilisikia kama sauti za wanaume lakini niliona kwa kuwa wananjua hamna shida ngoja niende tu. Masikini ya Mungu nilishtukia nimepigwa mtama nikadondoka chini na kabla sijakaa sawa nikavutiwa migombani..Walinibeba wanaume kama watatu juu juu na kuanza kunipeleka nisipoapajua. Nilipiga kelele lakini kelele zangu zilizuiliwa na wanaume hao ambao walikuwa wamejazia vizuri misuli utazani wacheza mieleka.
Kuna kama dawa walinipulizia na nikaanza kuona wenge wenge. Nilishangaa nikilazwa kwenye kigodoro kidogo kwenye moja ya chumba. Masikini ya Mungu wale wanaume wakaanza kubishana kuwa “naanza mim, naanza mimi”.Sikujua wanaanza nini lakini nilipojiangalia mikono yangu ilikuwa imefungwa juu ya kitanda cha chuma mkono mmoja kaskazini na mwingine kusini.
Nilipojaribu kutingisha miguu nayo ilikuwa imefungwa kwa staili hiyo.Nililia sana lakini haikusidi maana ni dhairi kuwa mtego huo ulishapangwa siku nyingi. Mabishano yakaendeea kati ya wanaume hao watatu nani aanze.Kila nikijaribu kutupuputa miguu nilishindwa na sasa nilianza kumuomba Mungu hanisuru na watu hawa wasiokuwa na Utu.
Wale wanaume nao hawakufikia muafaka na wawili kati yao walianza kupigana. Kwa macho yangu niliona mmoja akivua shati na kuanza kumpiga mwenziye. “Mimi huwezi kunipiga hivi hivi njoo hapo nje tuzichape na wewe utakuwa refa atakayeshinda ndioa ataaanza’.Aliasema mmoja wao ambaye tayari alishapigwa ngumi na yule aliyevua shati.
Basi ugomvi ukaanza na wanaume hao ambao walionekana kujazia vizuri na watu wa mazoezi wa kunyanyua vitu vizito wakaanza kuoneshana umwamba.Wakati wakiendelea kupigana sijui hata nini kilitokea maana nilisikia kama kuna mtu amekuja na wale wanaume wote watatu walikimbia.
Sijui hata huyu aliyekuja alikuwa ni nani lakini nahisi alikuwa labda ni kiongozi.Akaingia kwenye kile chumba na alishangaa sana kunikuta mimi nikiwa nimefungwa kamba.Aliniangalia na kuniita Vai.Na mimi nilimwanagalia na kumwambia “tafadhali naomba unisaidie”.
Kweli kwenye kundi la mamba pia kenge wamo sio watu wote ni mashetani bali kuna wengine ni malaika. Maana kaka huyu ambaye alikuwa ni kiranja wa Ulinzi hapo shuleni kwao alianza kunifungua kamba zote za mikononi na miguuni. Niliponyanyuka ndipo nilipogundua alikuwa ni moja ya kiongozi ambaye na yeye pia alikuwa akinifuatilia na kunitongoza kwa mda mrefu sana. Nikaingiwa tena na hofu nakuona kuwa nimetoka mikononi mwa Simba na sasa nimeigia mikononi mwa Chui.
“Walitaka kukufanyaje?”, kaka huyo aliniuliza kwa upole”.
“Hata siju naomba tu unisaidie nifike nyumbani salama”,nilimjibu huku machozi yakinitoka. Basi akanipa mkono nikamshika na tukatoka nje.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA