SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
Alice akaanza maishaya usingle huku akaimchukua Stela rafiki yake waishi woe kwenye chumba alichoachiwa na Gaston.Gaston alikuwa na roho nzuri sana kwani alimuachia Alice kila kitu kilichokuwa chumbani na hapo yeye aliondoka na begi lake tu.SASA ENDELEA...
Kwa hiyo Alice hakuangaika tena kununua vitu vya ndani bali walikuwa wakilipa kodi tu. Masiha yaliendela na kuna kipindi Alice alifanikiwa kukutana na Dulah na kama unavyojua awali ni awali na hakuna awali mbovu. Waliweza kuombana msamaha na kila mtu akaendelea na maisha yake.
Kuna siku Alice alikwenda chuoni kwa kina Dulah kulikuwa kuna sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wapya.Hiyo ikawa fursa nzuri ya wawili hao kucheza disco liloandaliwa. Alice alipata nafasi hiyo kama mwakilishi kutoka kwenye chuo chao. Basi baada ya mziki kumalizika Dulaha alimshawishi Alice alale hasirudi chuoni kwao.
Alice akajikuta akimkubalia na kwenda kulala kwenye chumba cha Dulah. Ilikuwa ni usiku mzuri sana kwa wawili hao wakni walikumbushia enzi zao wakiwa wanapendana kwa dhati.Hapo kila mmoja alionesha ujuzi wake wa kufanya mapenzi na kufanya usiku huo kuwa usiku wa kumbukumbu ya msiha ya raha ya mapenzi waliyowahi kupitia.
Mazoea na mahusiano yasiyo na kichwa wala miguu baina ya Dulah ana Alice yakawa yameanza upya.Baadaye Dulah aligundua pamoja kuwa walikuwa wakikutana na kupeana mapenzi moto mooo lakini bado hawakuwa na future ya aina yoyote ile. Hivyo Duha alianza kuyafubaza mahusiano hayo kwa madai kuwa anampenda sana mpenzi wake huku akitumia picha za yule binti waliyokutana naye kwenye gari maarufu kwa jina la Fetty.
Ingawa Fetty hakuwa mpenzi wake lakini walikuwa wakiishi kama wapenzi, wakitumiana picha za kimahaba, wakichati sms za mapenzi na pia wakikutana sehemu mbali mbali za starehe wakifurahia maisha yaani kilichobaki ilikuwa ni kuvuliana nguo tu. Dulaha alikuwa na imani sana na binti huyo huku akiiamini kuwa ndiye atakaye kuwa mke wake wa ndoa.
Alice aliamini manenoo hayo na akaamua kuachana na
Dulah na kuendela na maishayake ya kila siku huku akiamua kuyakabidhi maisha yake kwa mwanaume ambaye alikuwa na umri mkubwa kuliko yeye. Alice aliamua kutumia ule msemo wa kiingereza uliosema “Age is just a number”. Ilibidi tu ampende mwanume huyo ambaye alikuwa akimsumbua kwa mda mrefu sana. Mapenzi yao yalizua majanga kwa Alice kupata mimba na safari hii hakutaka kuitoa bali aliamua kuzaa. Kwa hiyo katika mwaka wa mwisho wa masomo bintii huyo alikuwa ni mjazito.
Utata ukaja kwa wazazi wake Alice alipotaka kuolewa na mwanaume huyo waliktaaa. Kikwazao kikubwa walichokiweka wazazi wake ni kwamba mwanaume huyo alikuwa ni mkubwa sana kwake na pia walitofautiana itikadi za dini. Inasemekana mwanaume huyo alishawahi kuoa hapo kbala na akaazaa watoto watutu kabla ya kuachana na mke wake wa awali.
Baba yake Alice alitishia kutomtambua kama mwanaye endapo Alice atabadilisha dini na kuolewana mwanaume huyo. Baba yake alisema yupo tayari kumlea mtoto atakaye zaliwa.Mzee huyo mwenye misimamo mikali pia alimshauri mwanye aendelee na masomo na yupo tayari kumlipia ada. Misuko suko ilikuwa mingi sana mpaka Alice akajifungulia nyumbani kwao.
Baadaye Alice alisalimu amri kwa kuamuaa kurudi chuo kuendelea na masomoya elimu ya juu. Akawa anasoma huku analea mtoto.Dulaha alikuwa akienda mara kwa mara kumsalimia huku akiamini kuwa hayo pia ni matunda ya usaliti. Mda ulizidi kwenda mtoto akazidi kukua na Dulha naye alimaliza chuo na kurudi mtaani. Tofauti na matarajio yake kuwa akimaliza tu chuo atapata ajira na kuachana na kuwategeuea wazazi wake la asha mambo yalikuwa magumu.
Dulha akifikiria mamamilioni ya fedha aliyotoa kwa ajili ya kusoma alafu ajira anakosa ilimumia sana.Ilimbidi Dulha aendelee kusimamia baadhi ya biashara za baba yake. Hiyo nayo ikawa nafasi yake ya kuendela na mapenzi ya kisirisiri na Alice ambaye sa hivi mtoto wake alikuwa mkubwa na alimwacha kwa bibi yake. Mapenzi hayo yalimfanya Alice ajisahau na kuamini eti Dulaha anaweza kuwa mme wake.
Jambo ambalo lilikuwa ni zaidi ya ndoto za mchana kwa upande wa Dulah.Dulaha naye kutokana na stress hizo za kukosa kazi na kutopenda kutegemea mali za baba yake alianza kurudi kwenye hali yake ya starehe na anasa za dunia. Akarudia pombe na akawa mtu wa kupenda wanawake.
Safari hii akawa hachagui bali yeye ni yeyote atakayejitokeza mbele yake basi itakuwa ni halali yake. Hali ilikuwa mbaya zaidi pale alipokuwa akitembea mpaka na wahudumu wa bar. Kuna kipindi alipata binti ambaye alikuwa ni mlokole binti amabaye alitoa masharti magumu sana ikiwa ni pamoja kufika nyumbani kwao kabla hawajajuana au kukutana kimapenzi.
Dulaha alimdanganya binti huyo kuwa yeye ni mkiristo.Binti wa watu naye akadanaganyika kwa sababu Dulaha alikuwa akienda naye kanisani siku za jumapili.Baadaye alikwenda mpaka kwa wazazi wake kwenda kujitambulisha.Hatua iliyofuata ambayo ilikuwa ni ngumu sana kwa Dulaha ilikuwa ni kwenda kupima afya.
Dulaha aliwaza sana wasichana ambao alishawahi kutembea nao akajikuta anaingia hofu sauala la kwenda angaza kujitangaza.Yaani vigezo vyote alishinda lakini hicho cha kwenda kupima afya kilimtataiza.Siku zikazidi kwenda baadaye Dulaha alikubali kwenda kupima afya lakini na yeye alitoa sharti moja kuwa siku watakayopima ndo siku hiyo hiyo watakayofanya mapenzi.
Binti huyo akaona isiwe tabu akamkubali wakaenda angaza kujitangaza. Ilikuwa ni siku ya hofu sana kwa Dulah lakini kwa bahati nzuri alijikuta ni mzima jambo amabalo hata yeye akuliamini. Huo ndo ukawa ukurasa mpya wa mapenzi baina ya binti huyo wa kilokole na
Dulaha.Binti wa watu akawa amefungua moyo wake wote na akawa yupo tayari kumpa chochote Dulaha kwa wakati wowote aliohitaji.Binti huyo alitokea kumwamini sana Dulaha kwa sababu alishindwa vikwazo vyote alivyomuwekea na vilivyokuwa vikiwashinda wanaume wengi. Mapenzi yakaendelea kwa mda huku Dulah akijifanya yeye ni mkiristo.
Baada ya miezi mitatu Fetty binti ambaye takribani ya mda wa mwaka mzima alikuwa na mapezi ya simu na Dulah alimaliza masomo yake ya unesi katika cho cha KCMC na akaajiriwa hapo hapo.Kama alivyomuhidi Dulah kuwa atakuwa yupo tayari kuingia kwenye uhusiano pindi tu atakapomaliza chuo na kupata kazi. Kwa hiyo sharti lingine lilikuwa ni kupima afya.
Kwa Dulha haikuwa sharti gumu tena kwa sababu alaishapima afya na akaapa kuacha umalaya.Mapenzi rasmi baina ya Fetty na Dulaha yakaanza huku pia akiendelea na uhusiano na binti wa kilokole kwa jina Neema. Dulaha kazidi kuwa njia panda siku hadi siku hasijue amuache nani na awe na nani. Ikabdi aombeushauri kwa ndugu jamaa na marafiki kwa maaana wasichana wote alikuwa akiwapenda kutoka moyoni.
Ushauri wa kwanza aliopewa namarafiki zake ni kuwa amwambie ukweli Neema kuwa yeye ni muislamu hivyo kama bintii huyo atakuwa tayari basi abadili dini ili wafunge ndoa. Dulaha akafanya kama alivyoagizwa akamwambia ukweli binti wa kilokole.Ukweli huo ulikuwa ni zaidi ya maumivu ya sindano kwenye kidonda.Neema aliumia sana na alijuta kukutana na mwanaume huyo yaani Dulha ambaye yeye alimjua kwa jina la David.
Hakuwa na jinsi zaidi ya kumshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea na kuamua kuachana na Dulah.Basi kujitoa kwa binti huyo kwenye uhusinao kukawa ndo mwanzo wa kukolea kwa mapenzi baini ya Dulaha na Fetty. Dulaha akaamua kufuata taratibu zote za kuoa ikiwa ni pamoja na kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa Fetty.
Ikumbukwe hakuwaikufanya mapenzi na binti huyo zaidi ya romance tu. Wakati wakiwa kwenye michakati hiyo ya kufunga ndoa Dulaha naye alipata kazi jambo ambalo lilichagiza nia ya wao kuoana. Basi kwa kuwa ndo ulikuwa ni mwanzo wa mwaka waliamua kusogeza ndoa yao mbele yaaani mwisho wa mwaka.
Mwaka mmoja ulitosha kabisa kwa Dulaha kujipanga na kwa kuwa wazee wake walikuwa tayari kumsapoti kwa hali na mali kijana huyo ambaye alishaonekana hafai katika familia kwa kuwa alikiuka imani ya dini yao na kujigeuza na kuwa muhumini wa dini ingine. Maana ilifika mahali jina la David likawa maarufu kuliko jinala Dulah.Hapa naweza kusema Neema yule binti wa kilokole alifanikiwa kabisa kumbadilisha Dullah.
Hivyo wazazi wake walifurahi sana Dulah kurudi kwenye maadili ya familia na kuwaletea binti safi anayejua maadili ya dini yao. Wazazi wake walikuwa na furaha sana na walikuwa wapo tayari kumpa hata nyumba ya famili ailimradi tu aoe atulie. Basi mambo yakaenda kama yalivyopangwa na kabla ya harusi kadi zilisambazwa sana na kutokan ana umaarufu wa famaili yake alipata michango mingi sana na kufanya harusi yao kuwa na bajeti kubwa sana na kuingia kwenye historia za harusi ya kifahari.
Habari hizi za yeye kuoa ziliwafikia wanawake wote ambao alishawahi kuwa nao katika kipindi chake cha mapito ya safari ya mapenzi. Mtu ambaye alimuia sana na habari hizo alikuwa ni Alice msichana ambaye kweli alikuwa akimpenda sana Dulha kutoka moyoni. Alice aliamini kuwa hiyo ndo ilikuwa ni bahati yake lakini yeye aliichezea.Dulaha naye aliamini kuwa kama sio Alice basi hasingekuwa na historai ndefu ya mapenzi.
Hatimaye siku ya harusi ilifika, watu walikusanyika na baada ya kufunga ndoa msikitini walikwenda ukumbini. Zoezi la sherehe na shamrashamara za harusi ziliendelea salama lakini ilipofika mda wa kwenda kupeana mikono kwa bwana na bibi harusi Alice uzalendo ulimshinda akajikuta akipiga kelele za majonzi kama vile mtu ambaye alimpoteza au alifiwa na mtu wake wa karibu. Alice alidondoka chini huku akitupa tupa miguu.Watu wote wakageuza macho sehemu ambayo Alice alikuwa amekaa.Kamera zote ziliamia kwa Alice jambo lilonifanya na mimi Eliado mwandishi wa simulizi hii kumsogelea.
Tofauti na watu wengine ambao walikuwa bize kumpiga picha Alice akiwa chini akitupatupa miguu huku mdomoni akitokwana povu mimi nilikuwa bize kumuhoji Stela rafiki wa karibu wa Alice. Maelezo yake yalinifanya pia kwenda kwa bwana harusi kupata ufafanuzi.Alice alikimbizwa hospitali ili kupatiwa huduma ya kuokoa maisha yake.
Tukio hilo lilinifanya mimi Eliado kumfuatilia kwa karibu na kwa maeleozo ya Alice, Stella, Dullah, Gaston na Jesca nikafanikiwa kuandaa simulizi hii ya PENZI PENZINI au matunda ya Usaliti kama Alice alivyopenda iitwe...Kweli mapenzi ni mchezo kama mchezo wa kuigiza.Mapenzi ni safari iliyojaa visa, usaliti uwongo na msamaha baina ya wapendanao.
Kwa upande wa Gaston yeye baada kurudi kutoka Ulaya alipoenda kusomea masomo ya juu alimtafuta Jesca mpenzi wake ambaye alimpenda kwa dhati ili pengine waweze kurudiana lakini alimkuta Jesca akiwa tayari ni mke wa mtu tena mwenye mtoto mmoja wa kike mrembo kama yeye. Gaston na yeye akaona kweli kuna matunda ya usaliti maana hata huyo Beatrice msichana aliyesababisha yeye na Jesca waachane tayari alikuwa ni mke wa mtu.
Gaston baadaye alimtafuta Alice na alimpata wakakumbushia penzi la shemeji la kipindi kile wakiwa chuoni.Alice alimuueleza ukweli Gaston kuwa tayari alishazalishwa na mwanaume ambao wazazi wake walimkataa.Gaston akaamua kufunga mikanda na kuishi na Alice.Mishowe walifunga ndoa na kwa sasa wana mtoto na maisha yanaendelea.Kweli mapenzi ni safari yenye visa na matukio ya kufurahisha na kuhuzunisha.
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
MWISHO