BAMBUCHA (26)
Jpt
6 min read
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
TUPATE BURUDANI KIDOGO KISHA TUENDELEE
SASA ENDELEA...
Pamoja na mambo ya maisha utotoni nilikulia kwenye malezi ya dini hii.Mama yangu japo alikuwa hapendi kwenda kanisani na alikuwa akiishi maisha ya kipagani lakini alijitahidi sana mwanaye niwe mfuasi mzuri wa dini.
Kwa kiasi fulani nilikulia kwenye dini na baadhi ya misingi ya dini ya kikristo niliielewa sana. ingawa ukubwani nimekuwa nikiishi maisha ya kipagani tu lakini bado nilitambua uwepo wa Mungu. Niliamini kuwa mimi ni mkristo na ipo siku moja nitakuja kuujua mlango wa kanisa kama ilivyo kuwa zamani.
Sasa Msimamo wa mpenzi wangu huyu kuwa lazima nibadili dini na tufunge ndoa kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ulikuwa ukiniweka njia panda. Moja ni kwamba nilikuwa sina misingi yoyote ya dini ya kiislamu na mbili nilikuwa bado sijajua ndugu wa huyo mwanaume.
Nilijaribu kuomba ushauri kwa jamaa wa karibu ikiwa ni pamoja na Sabrina juu ya kubadili dini. Sabrina alinambia nisihofu kwa kuwa Mungu ni mmoja ila njia ndo mbalimbali za kufika huko kwake.Pia walisema eti mara nyingi mwanamke hana dini. Walinishauri sana na mwisho wa siku nilikuwa tayari kubadili dini ila kwa masharti kwanzaalazima niwajue ndugu wa mme wangu huyo matarajiwa.
Basi kwa kuwa mwezi mtakatifu ulikuwa umekaribia kabisa maandalizi yalifaywa na tulitakiwa tuende huko mahali ambapo ndugu zake wapo. Kwa nini nilitaka kuwajau ndugu zake kwanza kwa sababu wanaume huyu hakupenda sana kuongelea ndugu zake.Kwa mda wote huo niliokaa nao sikuwahi kumsikia akiongelea kuhusu ndugu zake.
Ingawa mimi nilikuwa wazi nikamueleza kinagaubaga kuwa mimi ni yatima nisiyekuwa na baba wala mama. Pia nilimweza kuwa ndugu pekee ambaye nilikuwa namjua ni mama ambaye naye kwa bahati mbaya alifariki na kuniacha nikiwa mpweke.Yeye kila nikimuuliza habari za ndugu zake hakuweza kabisa kunijbu na zaidi alinambia nisubiri tu.
Basi siku hiyo ya kwenda kwa ndugu zake ilifika na tulindoka kuelekea huko ambapo alikuwa hataki kupataja kwa jina. Hiki kitu ndicho kilichokuwa kinanipa wakati mgumu.Siku hiyo tuliweka gari yake mafuta na akanambia nivae kiheshima tayari kwa safari.
Hakuna safari mbaya huku duniani kama hii.Yaani unasafiri hujui mahali ambapo unaenda. Nikaona tunafuata njia ya Morogoro na tulivyofka mjini tulipitia mahali tukapata kifunga kinywa.Safari ikaendelea na sasa tulifuata njia ya kwenda Mikumi.Hapo nikawa nafikiri labda tunaenda Iringa au Mbeya.
Lakini tulipofika mikumi badala ya kufuata barabara ya Iringa tulikuja na kuingi sehemu hiyo. Iikuwa ni mikumi sehemu ambayo ina historia nzito sana kwenye maisha yangu.
Si unakumbuka nilipotoka Mahenge breaki ya kwanza ilikuwa ni hapa na ndipo ramani yangu yamaisha yangu ilipoanzia.Hapa ndio nilimwibia yule mama na kutokomea.Kumbukumbu za matukio ya miaka mimgi sasa zilikuwa zimetawala ubongo wangu. Nilimkumbuka sana yule mzee aliyenisaidia alikuwa mlinzi ambaye kwa namna moja au nyingine ndiye alinipa akili ya kuiba. Ninakumbuka pia jinsi maisha yao yalivyokuwa yakufurahisha na kuhuzunisha.
Yaani mtu na mkwe waliishi vyumba tofauti na mwanamke ndiye aliyekuwa na nguvu kuliko mwanaume.Niliona pale stend pakiwa pamebadilika kidogo na kuvutia kuonesha kuwa mji unakuwa na watu wanaongezeka. Alikunja kushoto akaenda mbele na alikuwa kama mtu ambaye alikuwa hana uhakaika na sehemu ambayo alikuwa akienda.
Mara hasimame mara ashuke kuangalia angali mazingra.Nilitamani kucheka maana ni kwamba huyu mtu alipasahau kwao. Baada ya kuangalia mazingira aliingia na sasa alinyoosha moja kwa moa mpaka kwenye nyumba Fulani. Hapo aliniacha akashuka na ni kama mtu ambaye alikuwa akienda kuulizia. Baadaye akaja na kuniambai nisiwe na hofu alipita kusalimia jamaa zake. Akawasha gari na tuliekea huko kwao.
Kadri alivyokuwa anaenda ndivyo hivyo nilianza kupata wasiwasi kwa maana alikuwa akinipeleka sehemu ile ile ya mama la mama. Mapigo ya moyo yaliongezeka baada ya yeye kushuka na kuniambia nisubiri hapo kwenye gari. Baada ya dakika kadhaa alikuwa yeye na kijana mwingine ambaye alionekana kama kumuelekeza na kumuonesha wapi tunatakiwa tuende.
“Aise ni miaka mingi sana yaani sisi ulitucha wadogo mpak aleo tumekuwa. Kweli aaisee damu haipotei” aliendelea kusema kijan huyo huku akionesha furaha yake.Tulienda mbali kidogo na naweza kusema ilikuwa ni nje ya mji huo.Huko kulikuwa na nyumba mpya mpaya na hatimaye gari lilipaki sehemu yenye nyumba ambayo ilkuwa ikionekan ni nzuri sana kwa nje.
Nasema ilikuwa ni nzuri kwa sababu nyumba ilikuwa ina hadi geti.Tulifunguliwa geti nakuingia ndani.Nilishuka na hapo sasa nilitamani kuzimia maana mtu wa kwanza kuonana naye ni yule mama la mama ambaye nilimwibia. Nilijikaza na kujifanya kama sijamkumbuka kabisa.mama huyo alienda kumkumbatia mwanaye na wote kwa pamoja walimwaga chozi kuonesha kuwa hawakuonana kwa mda mrefu.
Mara baada ya salamu hiyo nikajua kabisa huyo atakuwa ni mama yake. Mama alinikaribisha kwa furaha sana na alionesha kunishau kabisa. Kwa kuwa hanikumbuka na mimi kimyoyo moyo nilifurahi. Basi Mudrik akanitambulisha kwa mama yake kuwa mimi ni mchumba wake.
Mama aaifurahai sana na akasem hiyo nihatua nzuri sana.Hapo hapo akanyanyua simu na kumpigia mtu. “Baba Muddy nakuomba uje maana leo nina furaha sana mwanetu amekuja”, alisikika mama huyo. “Mnakunywa nini wanangu?” aliuliza mara baada ya kukata simu.
Mama alionekana kuchanganyikiwa maana hiyoo furaha ilpiitiliza mipaka. Akamwita binti mmoja na kumtuma dukani.Basi stori ziliendelea na baada ya kama nusu saa kuna mzee alingia. Hapo sasa ndo nilitaka kuanguka maana mzee huyo alikuwa ni yule mlinzi ambaye alinisaidia kumwimbia huyo mama.
Baba huyo alikuwa amevaa miwani na alipovua aliniona laivu. Hata yeye alionesha kushtushwa maana aliponiangalia tu sura yake ibadilika sana. Akasema Bambucha ni wewe au macho yangu yananidanganya. Hapo sasa akayapikichapikicha macho yake kama vile alikuwa ndotoni. Mama akashangaa imekuwaje tunajuana.
Mudriki yeye alinyanyuka na kwenda kumkumbatia baba yake.Basi baada ya salamu kila mtu alikuwa na hofu moyoni. Na mama sasa baad ya kusikia jina Bambucha ilionekan kuwa ni dhairi kuwa amenikumbuka. “Hata mimi nimekukumbuka ni miaka mingi sana lakini sura yako na umbo lako la Bambucha bado linaonekena”.
Tena hili jina ni mimi nilikupa sasa nasema hapa hakuna ndoa. Mwanangu huwezi kuoa mwanamke mwizi mwanaizaya hasiye na haya”. “Mama ebu tulia kwanza punguza nchecheto yaliyopita si ndwele watu hatuna makucha basi tusiombe upele”,aliongea Muddy kwa sauti ya upole iliyojaa hekima na busara.
Baba naye akaunga mkono hoja hiyo na sasa utulivu ulikuwepo. Baada ya mama kushusha jazba alitamka neno moja ambalo lilimshangaza kila mtu. Hiyo ni mara baada ya mimi kuomba msamaha. Alisema mwanangu dunia ni duara binafsi nimekusamehe ila nasisitiza ndoa hapa haipo”.
“Ujue kuna siri nzito ambayo nilitaka nikuambie mara baada ya wewe kunisimulia historia yako ya amisha siku ile ulipokuja hapa kwangu. Kwa kifupi wewe ni mtoto wa Jenifa ambaye alikuwa ni rafiki yangu”.Hapo nilishtuka kidogo kwa maana Jenifa ndilo likuwa jina la mama yangu.
“Jenifa alikwua ni rafiki yangu sana na wewe ulipatikana mgodini. Kipindi hicho tunafanya kazi huko migodini kama mama ntilie. Kwa bahati mbaya kuna wamnaume ambaye alikuwa na pesa sana alitokea kutuchanganya. Yaani alikuwa akitembea na mimi na pia akitembea na mama yako kwa wakati mmoja.Huyo wamaune ndo ilikuwa chanzo cha mimi na mama yako kugombana. Mwisho wa siku mama yako alikubali kuniachia huyo mwanaume na yeye aliondoka na kwenda huko Mahenge kuanza maisha yake”.
Kila mtu alaikuwa kimya kumsikiliza mama huyo ambaye alikuwa akionge kwa hisia sana. “Mama yako aliondoka akiwa na mimba yako na mimi pia niliondoka nikiwa na mimba ya huyu Mudrick.Sasa kidume kilichotupa mimba ndo huyo hapa”.Hapo alisema huku akimnyooshea kidole mme wake.
“Kwa hiyo wewe na Modrick ni mtu na dada yake”. Hapo nilishindwa kwa kweli nilihisi radi ya masikio ilipiga na kupasua ngome ya masikio yangu na nilijikuta nikianguka na kuzimia.Nilikuja kushtuka nikajikuta nipo hospitali nimetundkiwa dripu za maji. Sikuamini kama kweli ndoa ya mtu ambaye nimempenda sana imeingia mdudu.Niliwaza kuhusu hiyo mimba yangu kwa kweli sikuwa na jibu la kufanya.
Kulikwua na taarifa pia za huzuni kuwa baba na yeye baada ya tukio hilo ambalo lilkuwa na aibu alikunywa sumu na kujiua. Ilikuwa inauma sana maaana kama unakumbuka mimi na baba tulishawahi kufanya mapenzi siku ile ambayo alinisaidia kuiba zile pesa.
Sasa nilianza kuvuta kumbukumbu kuwa ndo maana ile picha ya Bambucha ambayo baba huyo aliichora alikuwa akiifanana na mimi.Kumbe msichana wa ndoto zake alikuwa ni mama yangu. Niliumia sanana na sikutaka hata kukumbuka yaliyotokea.Kwenye msiba kila mtu alikuwa akilia lakini mimi nililia zaidi maana nilimpoteza baba.Tuliombolezwa na baadaye mzee yule tulimwihifadhi kwenye nyumba yake ya milele.
Mpaka nafika kwa Eliado nilikuwa nimeshachanganyikiwa nisije kuwa nifanyaje yaani hiyo mimba niilee au niitoe. Niolewe na kaka yangu au la. Nipo kwa Eliado mshauri najaribu kumsikiliza kwa umakini naamini nitafikia muafaka.Nataka kupona kiroho na kiakili.
Nipo njiapanda na ndo maana niliomba fursa hii ili na nyinyi wafuatiliaji wa story muweze kunishauri..Pia nimeamini dunia ni duara na inazunguka.Hili ni funzo kwa wanaume wanaowachanganya mabinti na kuwaapa mimba bila mpangilio. Jamani kama mwanaume una watoto hata wan je ya ndoa basi watafute maana mwisho wa siku ndo kama haya watoto wanakuja kuona.
Nawashukuru sana naamini kuna vitu mmejifunza kuhusu maisha ya Bambucha.Naombeni ushauri wenu nimekwama mwenzenu.Mudrick na yeye amechangnyikiwa yupo yupo tu kama zuzu hasijue wapi pa kushika. Naamini mwisho wa simulizi hii utatokana na ushauri wa wasomaji na aliyenipa nafasi hii yaani Eliado.
Niwatakie tafakari njema ya jambo hili,Mungu awabariki na kuwalinda.Kweli maisha safari.Nimebaki kama kunguru niliyekimbiza bawa langu na sasa limenidondosha bila kupenda. Mungu nisamehe kwa yote,nifanye kiumbe kipya niendelee kuishi nisijikatili uhai kama baba yangu.
Kalamu inagoma siwezi kuandika tena karatasi imejaa machozi sina mbele sina nyuma.Sioni pa kushika, jua la saa sita limenichoma utosini, mishale yenye sumu yote kwa pamoja imejeruhi nafsi yangu.Sijui mimi nitakuwa mgeni wa nani hakiyanani niombeeni kwa Mungu nipone na kupata faraja ya moyo.
"SIJAKATA TAMAA NAAMINI YUPO MUNGU MSEMAJI WA MWISHO"
KUNA MATANGAZO YANATOKEA KWENYE APPLICATION YETU HIVYO UKIYAONA NAOMBA BONYEZA HAPO NDIO UNANIPA SAPOTI MIMI, UKIBONYEZA UNAWEZA KUCANCEL SIO LAZIMA UENDELE ULIKOPELEKWA, KIKUBWA UBONYEZE HATA MARA 2-3 KILA UKIFUNGUA APP YETU
MWISHO
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni