SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Siku zilisonga huku nikiwa napata wakati mgumu sana wa kuoanana na babu G. Ratiba zilikuwa zikipishana lakini wikiendi moja niliamua kumbana na kubaki anga zake. Niliongea naye habari nyingi sana na niliamua kumgusia habari za mapenzi. Hapo mzee alicheka sana na kusema ni ajabu kwa kijana mdogo kama mimi kumuulizia habari za mapenzi. AlinSambaia yeye kwa umri huo hana jipya zaidi ya kulea wajukuu.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Mjukuu wangu habari za mapenzi waulize vijana wenzio ila kwa sisi ujana wetu ulishaisha”. Hpao na mimi nilianza kucheka na kuonesha kuwa alikuwa akinidanganya. Kwa kuwa nilikuwa nikihitaji kupata habari zake zaidi niliamua kutoa simu yangu na kumsikilizisha lile tukio lake la kwanza lilofanya mpaka mimi kutamani kuwa karibu naye.
Babu G alisikiliza kwa umakini mkumbwa sana na alikuwa mpole. Ilibidi sasa tutafute sehemu tufanye mazungumzo. “Mimi sikuwa na nia mbaya kukurekodi mzee wangu ila ninachotaka kujua ni mbinu unazozitumia kuwapata hawa mabinti hili hali ni ngumu sana”.Nilimtoa hofu kwa kumwambia kauli hiyo.
“Sasa nitakupa mbinu na pia ujuzi wowote utakaotaka kwenye sekta hiyo ya mapenzi.Lakni sasa kunirekodi tu ni kunishtua na kunifanya niwe na wasiwasi juu ya kusambaa. Ujue siku hizi teknolojia imekuwa sana hivyo ikitokea ikasambaa basi uje nitakuwa nimepoteza kibarua changu. Ujue mjuku wangu katika vitu ninavyoviogopa na nisingependa vitokee kwa wakati huu ni kupoteza kazi katika shule hii ya wasichana.Sio kwa sababu ya kuwa wananilipa vizuri la hasha ni kwa sababu nafaidi vitu vizuri sana ambavyo vinanipa raha huku duniani”. Alisema kama akizikosa raha hizo basi atawahi kufa mapema.
Nilitamani kucheka lakini nilicheka kimoyomoyo na nilikuwa bize nikimsikiliza. Leo na mimi nilimkamata pabaya. Na nilataka kujua vitu vinavyomfanya kwa umri huo kuendelea kuwapagawisha wajukuu zake. Hili kwangu lilikuwa ni jambo la muhimu sana kuliko vyote. Nilimuahidi kumtunzia siri kama atanipa siri tutafanya siri. Mzee akatabasamu tabasamu lake ambalo linamfanya aonekane bado kijana. Wakati tukiwa hapo huku utamua wa mazungumzo ukikolea mara alikuja binti mmoja ambaye naye alikuwa si haba. Nilibaki nimemkodolea macho na kusubiri kwa hamu ataongea nini na babu G. Hama kweli dunia ina mambo na tembea uyaone maana binti huyo alifanya kitu ambacho kilinishangaza sana. Alifika na badala ya kuonge ana Babu G alinijia moja kwa moja na kunisalimia kwa kunikumbatia. Alining’ang;ania kwa nguvu na alininong’oneza masikioni kuwa ananipenda. Nilibaki njia panda nikishindwa kuelewa nifanye nini.
Mapigo ya moyo yaliongezeka na nilikuwa sielewi nimjibu nini mara baada ya kuniambia kuwa alikuwa akinipenda. Sikuwahi kufikiria akilini mwangu kuwa inaweza kutokea binti huyo nikawa naye. Alikuwa ni mrefu sana na alijaliwa wembamba wenye mvuto. Sura alijaliwa na alikuwa ni binti ambaye inatosha kumwita mrembo. Baada ya kumbatio hilo lilonihamisha kutoka uliwengu huu na kunipeleka ulimwengu mwingine binti huyo aliniachia. Akanipa kikaratasi ambacho alikuwa ameandika namba zake. “Babu G naomba unisaidaie kazi yangu na mimi nipate ninachokipata”. Alisema binti huyo na kuzidi kuniacha njia panda.
Kwachu kwachu binti huyo kwa mwendo wa madaha alianza kuondoka. Nilibakia nimeshangaa na kushindwa kuelewa nini maana ya mchezo huo. Wakati nimeendelea kushanaga na kutafakari jambo hilo la kukumbatiwa na kutamkiwa maneno hayo yenye mvuto baba G aliniondoa kwenye mawazo.
“Mjukuu wangu umeonesha udhaifu wa hali ya juu. Kumbe ndo dhaifu hivyo. Sina uhakika kuwa una mpenzi au umeshawai kuwa na mpenzi.”
“Kwa nini babu G kwani nimefanya nini cha tofauti..?”Nilimuuliza huku nikiendelea kutafakari kauli zake.
“Mjukuu wangu lazima utambue kuwa mwanaume haitakiwa kuwa dhaifu. Mwanaume inatakiwa utambue kuwa mwanamke ni zawadi na si fumbo. Zawadi siku zote inahitaji kufunguliwa na fumbo linahitaji kufumbuliwa. Mjukuu wangu futa zile picha nikufundishe ujanja.
Wanawake wameumbiwa wanaume.Wanawake ni zawadi na mwanamke siku zote ni dhaifu. Mimi kwa kuwa hapa shuleni wananilipa mishahara midogo hivyo huwa najilipa..Haya ebu futa hizo picha zangu ili tuende sawa”. Aliongea babu G na kutulia.
Nilifikiria sana kufuta picha zile huku nikiwa na hofu huenda nikizifuta hawezi kunipa siri zake. Nilimwambia kuwa kwa kuwa giza limeshaingia ni vizuri kama nikawahi nyumbani maana babu atakuwa na wasiwasi. Hapo mzee huyo aliangua kicheko na kuniambia kumbe bado ni mtoto. “Mjukuu wangu kwa umri wako huo hutakiwa kuwahi nyumbani kulala mapema kama kuku. Au unawahi kupika? Babu G aliuliza huku akinikazia macho.
“Hapana siwahi kupika na wala mimi sio kuku ila ni kifaranga. Bado ni mdogo hivyo nahitaji kufuata sheria za huko. Babu yangu namweshimu siwezi kumpanda kichwani”. Wakati nikitoa ufafanuzi huo mara mwalimu wa nidahamu alitujia. Alifika hapo na kutusalimia. Baada ya salamu aliniita pembeni tuzungumze kidogo.Alinambia kuwa kama nitaweza nimsaidie kuwasimamia wanafunzi muda wa prepo ambao unaaanza saa 2 usiku mpaka saa 4. Alinambia kuwa yeye siku hiyo alikuwa hajisikii vizuri hivyo alihitaji msaada. Mwalimu huyo alieleza kuwa wanafunzi hao wasiposimamiwa huwa hawasomi na muda mwingi huwa wapo bize wakichati na kutumia simu ambazo zinakatazwa.
Niliangalia saa yangu ndo kwanza ilikuwa saa moja na wanafunzi muda huo walikuwa vipindi vya dini. Nilifikiria ombi hilo na nilimwambia kuwa ngoja niende kwanza nyumbani kwa kuwa nilikuwa sijaenda. Kwamba nilikuwa na hofu kuwa babu yangu atakuwa na hofu juu yangu. Alinikubalia na hapo nilimwaga babu G nikimwabia kuwa nitarudi. Alifurhi maana ilionekana na yeye alikua akipenda kampani yangu. Huyo nilianza kuondoka na kuelekea nyumbani. Nilimkuta babu akiwa nje huku akisikiliza kipindi cha michezo. Nilimsalimia na kujiunga naye hapo. Nilimweleza nahataji kurudi kule kwa maana mwalimu wa taaluma alinambia nimsaidie jambo. Babu alaionesha wasiwasi wake na kuniuliza kwa nini napenda mambo y
Nilimwelewesha babu kuwa hasiwe na wasiwasi maana kama anaogopa mimi kutembea usiku nitalala kwa babau G. Babu hapo akatabasamu na kuniambia huyo mzee atakupoteza mjukuu wangu. Ataanza kukufundisha mambo ambayo yataharibu maisha yangu. Nilijaribu kumdadisi babu ili nijue mambo gani hayo lakini babu hakuwa wazi. Alichonambai kuwa mzee huyo hapaswi kuwa na urafiki na vijana maana anajua vitu vingi sana ambavyo ni sumu kwenye ubongo wa vijana. “Ujue Babu G si mtu mzuri na huenda ni mchawi kwa sababu mambo anayoyafanya kwenye shule hiyo ni mambo mazito sana lakini hatukuwahi kusikia kuwa amesimamamishwa kazi au kufukuzwa kabisa”.
“Tatizo babu unapenda sana kuaamini kuhusu uchawi. Wewe mara ya kwanza uliwahi kuniambia kua mzee huyo ni mchapa kazi anayejituma sana na hiyo ndio sababu ya wao kumwamnini.”
“Mjukuu wangu sio kila kitu nitakwambia vitu vingine havijengi vina bomoa. Mimi ni mtu mzima siwezi kukuambia mambo ya kipuuzi lakini nikiona unataka kukengeuka nitakueleza kila kitu.Lakini kama uanenda kwa ajali ya mambo ya shule wewe nenda mjukuu wangu. Ila kama ni kwa ajili ya mambo mengine jua sijabariki. Bado tunakupenda na tunataka uwe na maisha mazuri huko mbeleni.”
“Babu usijali nitaenda na kurudi..Na nimekuelewa sitofanya mambo mabaya na wala sitokuwa rafiki wa babu G”.
Nilimwabia hivyo na kuingia ndani.Muda ulikuwa umeenda niliongea na bibi na nilimuomba chakula aniwekee chumbani kwangu. Bibi yangu alikuwa mzungu hakuwa mtu wa kuhoji hoji sana aliniitikia na alinambia kaa kizungu take care. Niiondoka hima hima na kueleka huko shuleni. Nilikuwa natafakari sana kauli za babu huku nikitafakari pia mtazamo wake kuhusu babu G.
Bado wazo kuwa eti niache urafiki na Babu G alikuniingia akiliini. Kwanza nilikuwa nawaza jinsi ya kujifunza ufundi kwenye mapenzi.Maana mpaka nafika chuo nilikuwa simjui mwanamke. Nilikuwa muoga na wala sikuwahi kutongoza. Mabinti wa chuoni walikuwa wakinipenda sana na nilikuwa nikiwasaidia kwenye masomo lakini sikuwahi hata siku moja kuwatongoza.
Hali hii iikuwa ikininyima sana raha na kwa bahati mbaya wale ambao mimi binfasi nilitokea kuwapenda na kutaka wawe wapenzi wangu wote walikuwa wakinikataa. Nilishawai kukataliwa zaidi ya mara tano na siku zote nilijihisi mwenye mkosi. Kila ikitokea naona mwanamke ananikubali na kujilengesha siku nitakayomtamkia kuwa nampenda basi ndo siku hiyo hiyo ambayo atanikataa na siku urafiki utkwisha. Hli hii ilinijengea uwoga na niliacha kabisa kuwatongoza wasichana. Hayo ndo maisha ambayo niliyachagua. Nilikuwa nawaogopa sana na kila siku nilikuwa natafuta mbinu ya kuwajua na njia ambazo wanaueme wanatumia kuwapata wasichana. Sijisifii lakni nimekulia kwenye maadili ya dini.
Kuna kipindi nilipokuwa sekondari walikuwa wananiita Jose Paroko. Yaani nilikuwa mshika dini sana. Basi nilienda mpaka shuleni lakini wakati naingia nilikumbuka yule binti aliyenipa namba zake. Niliingiza mkono mfukoni na kukichukua kile kikaratasi na kuzisevu zile namba kwenye simu. Niliingia na niliongea maneno machache na Babu G kisha nikaingia kwenye bwalo ambapo watu walikuwa wakisoma. Niliingia na kukaa kiti ambacho nilionekana. Nia ni kuwafanya wanafunzi watambue uwepo wangu ili wasome na kuacha kupiga kelele. Walitulia na mimi nilichukua mitihani ambayo nilikuwa nikisahisha. Mara Boke alikuja na kunishika bega. Niligeuka na kumuuliza alikua akihitji nini. “Sahamai mwalimu nina tatizo je naweza kukaa hapa ili unielekeze?” Ilibidi kufunika ile mitihani yao. Sijakaa sawa yule binti aliyenipa namba naye alikuja na yeye alinishika bega. Hapo pozi likaisha. Nilipogeuka tulikutanisha macho na alinikonyeza. Kuduuuu kuduuuuu moyo wangu uliongeza mapigo
Mara wakaja tena mabinti wengine wawili na wao walionesha kuwa walikuwa wanahitaji msaada wa jambo. Bado nilikuwa sijajua ni jambo gani walikuwa wakihitaji niwasaidie. Wakazidi kuongezeka na kuongezeka. Wengine walikuwa nyuma yangu wengine walikuwa mbele yangu. Sikujua nini cha kufanya maana mimi nilikuwa mgeni wa mambo hayo. “Mwalimu kuna swali ya hesabu yametushinda tunataka utusaidie.”Aliongea mmoja wao.
Kidogo moyo wangu ukatulia na nikawaambia basi wasinizunguke sana nitakosa hewa. Walivuta viti wakakaa na kuanza kuwaelekeza. Cha ajabu yalikuwa ni maswali yale yale ambayo niliyarudia mchana. Nilijua kabisa walielewa basi ndo hivyo huenda vipururu vilikuwa vikiwasumbua. Maswali yalikuwa mengi na kwa jinsi walivyokuwa wakiuliza maswali ya kuvuta muda tulijikuta saa nne imetufikia. Wanafunzi wengine walianza kuondoka tukabaki sisi. Ili kutokuvunja sheria za hapo ilibidi niwaambie waende kupumzika.
Ni kawaida kwa hapo ikifika saa nne kila mtu anatakiwa kuingia kitandani na saa nne na nusu taa zinazimwa.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com