Notification
Tidak ada notifikasi baru.

MUUZA MAZIWA (5)

Mwandishi: Gift Kipapa

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
“Ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu”
“limeharibika , ooh, mungu wangu!”
Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika.
“ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha”

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Aliongea Lisa haraka haraka.
“okey”[sawa]
Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa.
“nataka kuoga wifi”
“na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu”

Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa.
Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke nje kabisa ya nyumba hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo alisikia muungurumo wa gari, halikuwa gari lingine bali gari la Jerry mume wa Lisa.

Hofu iliwaingia kwa ghafla na haraka haraaka walirudi tena chumbani kwa penina , ambapo kama kawaida alimfungia muuza maziwa kabatini, hawakuwa na njia nyingine tena bali hile waliyoipanga awali, muuza maziwa asubiri mpaka usiku wa manane Penina atakapo lala ndipo atoke kwani Lisa atauacha mlango wa kutokea wazi.
Lisa alipomaliza kumfungia muuza maziwa katika kabati alitoka nje ya chumba hicho,akiwa koridoni aligongana ana kwa ana macho na mumewe. Wote wawili waliinamisha vichwa vyao chini. Kwani kila mmoja aliona aibu kwa kumsaliti mwenzake.
Lisa kwa muuza maziwa na Jerry kwa sekritari wake.

“Ah, mmh, wifi amekuja , kakaribu!”
Aliongea Lisa kwa kujiumauma huku akiwa na wasi wasi.
“ asante amekuja saa ngapi?”
“sio muda mrefu”
“aah yuko wapi sasa nimsalimie?”
“yuko bafuni anaoga”
“Okey” [sawa]

Aliitikia na kisha kuelekea chumbani kwake.
Lisa nae alimfuata mumewe nyuma hukubado akiwa na hofu juu ya kugundulika kwa uwepo wa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo.
“Pole na kazi dear”
Aliongea Lisa huku akijibaraguza kwa kumvua tai mume wake, macho yake bado yalikuwa na aibu sababu bado alikuwa na wasi wasi kwamba labda mumewe amegundua chochote.
“ah, asante mpenzi”
Aliitikia Jerry huku akitabasamu, lakina nae pia tabasamu lake liliishia mdomoni tu moyoni nafsi ilimsuta .

Maovu aliyoyafanya na sikritari wake ofisini kwake yalikuwa bado yakionekana katika kichwa chake.
Akavua nguo na kuingia bafuni kuoga lisa nae alimfuata na kujumuika nae kuoga . Alifanya hivyo ili Jerry hasihisi chochote.
Walioga huku kila mmoja akiwa hana habari na mwenzake. Kwani wote wawili walikuwa wamechoka, walipomaliza kuoga wakavaa na kasha kwenda sebuleni. Huko wakamkuta Penina akianga lia tv.
“mdogo wangu huyo!”
Jerry aliongea kwa furaha huku wakicheka.
“kaka!”
Penina aliitikia na kisha kumkimbilia kaka yake.

“waoo!!!”
Waliongea kwa pamoja na kisha kukumbatiana kwa furaha.

“habari za masomo!?”
“nzuri tu kaka, shikamoo!”
Aliitikia Penina na kasha kumwamkia kaka yake
“marhaba mdogo wangu>“
Aliitikia salamu.
“Penine kanenepa kweli safari hii, shule imempenda kweli.”
Aliongea Lisa.
“hapana wifi!?”

Penina aliongea na kasha kucheka, ukweli ni kwamba kweli alikuwa amenenepa na kujengeka shepu kwa mahipsi na makalio yaliyo fungashika kiinye plus gwedegwede.
Waliongea mengi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja tena. Upande wa Lisa moyoni hakuwa na furaha hata kidogo, muda wote alifikiria jinsi ya kumtoa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo.
Alifahamu fika jinsi swala hilo lilivyokuwa gumu kwani chumba alichomficha ndicho chumba atakacholala penina , hakuelewa angeweza vipi kumtoa muuza maziwa katika chumba hicho bila ya Penina kugundua.
“sijui nitafanya nini mungu wangu?”
Aliwaza bila kupata jawabu, hakuona aibu kumshikilikisha Mungu katika uovu wake.

“atalala tu lakini , na hivi alivyochoka, na huo ndio utakuwa muda muafaka”
Alizidi kuwaza,
Hiyo ndio ilikuwa njia pekee aliyoitegemea alitumaini Penina atakapolala ndio uwe muda muafaka.
“wifi vipi mbona utafikiri uko mbali sana!?”
Penina aliuliza baada ya kugundua kwamba Lisa hayupo pamoja nao katika maongezi.
“hapana nipo , mbona tupo pamoja!.“
Aliitikia Lisa haraka haraka baada ya kuzinduka toka kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo.
“kweli Lisa upo tofauti sana leo”
Jerry nae alikazi
“hapana jamani mbona nipo sawa!”

Lisa alizidi kujitetea kwa nguvu zake zote kwani hakutaka mtu yoyote ahisi chochote kuhusiana na swala hilo la muuza maziwa, alichokifanya baada ya hapo ni kujaribu kujichekesha na kuonyesha kuwa ana furaha ili kupoteza kabisa hisia za mumewe pamoja na wifi yake.
Waliongea kutwa nzima mpaka usiku ukaingia , baada ya chakula cha usiku kila mmoja alielekea chumbani kulala Jerry na mkewe chumbani kwao na Penina pia alielekea chumbani kwake.
Wakiwa kitandani kwao si Jerry wala mkewe aliyeonekana kumjali mwenzake, kila mmoja aligeukia upande wake , kila mmoja alirizika na usaliti alioufanya mchana wa siku hiyo. Jerry alipotembea na Sekritari wake wakati Lisa alipotembea na muuza maziwa.
Hakuna aliyejua maovu ya mwenzie kila mmoja alimuona mwenzake karanga bao na kumlalia mzungu wa nne.
xxxxx- - - - xxxxxx—- - — xxxxxxxx

Saa sita na nusu usiku Penina alishtuka toka usingizini , hii ni baada ya kusikia mlio wa kabati likifunguliwa , haraka alisogeza mkono wake kwenye swich ya taa na kuiwasha. Mwanga ulitanda chumba kizima . Penina hakuamini alipomuona mtu akiwa amesimama karibu kabisa na kabati huku kabati likiwa wazi.
“kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1”
Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri.
Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa.
“mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!”
Aliongea Lisa kwa mshituko

“Utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?”
Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa.
Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati.
“da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi”
Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi.

“kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1”
Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri.
Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa.
“mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!”
Aliongea Lisa kwa mshituko

“utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?”
Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa.
Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati.
“da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi”
Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi.

“kumbe wewe nan……….?”
Penina alijikuta anakatisha kauli yake baada ya kumuangalia vizuri muuza maziwa, hakuamini alichokiona alihisi kama vile yuko ndotoni.
“Karani!!!!”
Aliita Penina kwa mshangao huku akiwa ameduwaaa.
“Penina!!!”
Muuza maziwa nae aliita mara baada ya kumuangalia vizuri penina.
Wote walibaki wakishangaa huku wakiangaliana usoni, kumbukumbu zao zilirudi nyuma miaka miwili iliyopita.

Suji sekondari katika bweni la wasichana chumba namba ishirini na moja. Penina akiwa amelala kwenye kitanda cha dabodeka, ikiwa ni mara yake ya kwanza kulala ndani ya chumba hicho.
Sababu hiyo ilikuwa ni siku yake ya kwanza toka ahamie bwenini , mwanzo alikuwa akikaa kwenye nyumba ya mkuu wa shule.
Akiwa kitandani hapo alisikia mlio wa mluzi ukisikika kwa mbali karibu kabisa na dirishani sehemu ambapo alikuwa amelala.
“it ndizi time!” [ni muda wa ndizi]

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Muuza Maziwa Simulizi Z3`
Jiunge kwenye mazungumzo (2)
Maoni 2
  1. 25 Juni 2022, 23:53
    Profile
    Bila jina
    Said: Hasanibudeba
    Hasanibudeba