SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
"Hello madam welcome" alikuwa ni mkarimu mno km ni customer care ya hali ya juu
"Hello! Samahani kaka kuna mtu namsubiri hapa" niliamua kujidefend kidogo
"Anhaaa sawa ila kuna mtu ameniagiza kwako dada"
"Kheee! Kakwambia anaitwa nani?"
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Ahaa hakunitajia jina ila kaniambia una watu wengine wawili pia mpo msafara mmoja" yule mhudumu alizidi kunishangaza ina maana huyo kaka rafiki yupo kweli mule ndani
"Unajua alipo huyo kaka? Niuliza kwa shahuku
"Najua alipo" alijibu kwa haraka kidogo
"Nakusihi unipeleke" nilionyesha unyenyekevu
Safari hii hakujibu chochote aligeuka na kuanza kutembea mimi nae nikaanza kumfata nyuma nyuma kama mkia na mbuzi, cha kunishangaza ni atmosphere/hali ya hewa ya mule ilikuwa ni nzuri ajabu, zile lights/taa zilikuwa zinawaka mng'aro wa kipekee kiasi kwamba kama una saa unaweza usijue majira kabisa, kilichozidi kunishangaza ni jinsi tulivyokuwa tunateremka chini zaidi km andaki ni ngazi tu kushuka chini. Ilishukua takribani dakika nane kufika kule mandhari ilikuwa amazing, watu walikunywa na kucheza kamari kuna sehemu hasa zile zilizokuwa na machine za kuchezea kamari zilikuwa na mwanga ang'avu ila zile ila kule kwenye pembeni mwanga wake ulikuwa hafifu, nilimtazama yule mhudumu usoni nikamuona nae akinitazama mimi.
"Yupo wapi sasa kaka? Niliuliza
"Alikuwa hapa mara ya mwisho sasa sijui kaenda wapi, labda msubiri hapahapa" alizidi kunishanganya yule customer care
"Hivi kaka rafiki mbona unanifanyia hivyo lakini, au utaki nikuone sura yako? Nilijisemea nikiwa nabembekeza machozi cha ajabu hata nikilia ili nionewe huruma bado mhusika hayupo ni bure tu ilibidi kujikaza
" dada kama unahitaji kinywaji caunter pale pia mambo mengine unaweza kuuliza pale" alinionyesha upande wa kulia niliokaa nikageuza shingo nikatazama sekunde kumi hazikufika nikageuza shingo kama awali sikujua niende wapi ila sasa nilipotazama mule kwa harakaharaka vinywaji vilivyokuwa vinanywewa ni whisky, savannah, champagnee na pombe nyingine kali, kwa akili yangu ya haraka haraka nikawa najua vyote vile vina kilevi hivyo niliwaxa kuagiza soda au juice za kopo au za glass nilianza kusogea taratibu huku kichwani nikiwa na mambi mengi yananitatiza. Kabla sijauliza kinywaji tayari nilipewa juice kwenye glass ndefu nyembamba "karibu dada" alinikarihisha dada aliyekuwa pale counter.
"Dada haina kilevi" ilibidi niulize kwa woga kidogo
"Noo ni juice hiyo dada" alijibu yule dada
"Sawa juice ila haina kilevi" niliuliza kwa mara nyingne maana sikuwa na imani kabisa
"Hapana hatuwezi kumpa mteja kitu asichokipenda hata hivyo ni mkaka mmoja ndio aliyekuja na kutuagiza tukupatie kinywaji hicho alivyosema pia km utahitaji chakula ameshalipia kadi yako hii hapa" aliongea hukuanatoa kadi kutoka kwenye droo zake kwa ndani
"Nashukuru, naweza kukaa popote dada" niliendelea kuuliza
"Yeah upo huru dada ubanwi"
"Asante nashukuru"
Nilirejea nikaketi sasa pembeni yangu kulikuwa na wadada wawili na mvulana mmoja na mwingine inavyoonesha ndiye alikuwa anacheza kamarialiyo mbele yetu kidogo, ni kamari ya machine ambapo unabonyeza namba ya bahati kisha unasubiri majibu yako, nilipotazama vizuri nilimuona kwa mbali mamdgo alaaaaa!! Bado kichwa hakikukaa sawa niimuona na salma pia alivyovaa mungu anajua wanaume walikuwa wanamshika makalio mara wanchezee maziwa yake, cha ajabu kuna jamaa alikuwa anacheza akashinda nahisi huyo ndio alikuwa bwana wake aliruka akambeba juu na kuanza kumnyonya ulimi kwa macho yangu nashuhudia, nilisikia vibration kwenye mkoba wangu nikajua napigiwa nikafungua zipu ya mkoba nikatoa simu alikuwa ni kaka rafiki.
"Yeah emmy"
"Mbona umendoka?
" emmy nimekuita uwaone ndugu zako mimi siku ya kuonana na wewe haijafika ikifika nitakuita sehemu ya heshima sio kama hapo" aliongea kaka rafiki
"Sawa hao watu nimeshawaona ila nitajua cha kufanya asante sana kaka rafiki ama kweli wewe ni zaidi ya rafiki" nilimsifia kidogo
Niliendelea kuongea mengi kumbe alishakata simu mimi sikujua.
***********"""
Niliendelea kunywa kinywaji changu ile juice ila kadri muda ulivyozidi kwenda niliona nguvu zinaanza kuniisha "mmh hii juice kweli au??? Niliona niamke pale nikaanza kutembea taratibu kurudi parking ila nguvu nazo hazikuwepo mwilini nilijikuta natambaa kwa kutumia ukuta nilipoangalia nyuma niliona wakaka wawili wanakuja na pale nilipo ni kichochoro nikawa na wasiwasi juu ya usalama wangu
Niliona kizunguzungu na wale watu nyuma walizidi kunikaribia niliogopa mno ila nitatumia njia gani kuokoka? Nilishikiria ukuta nikawa nashuka nao taratibu huku moyoni nasema "heee yesu nisaidie niokoke na ili"
"Oya zigo lenyewe si ndio hili ebu limulike? Aliongea kaka wa kwanza(mrefu mweupe)
" ndio tunafanyaje sasa na tumepewa kazi dada mwenyewe kazima/unconscious/kapoteza fahamu" aliongea wa pili (mfupi mweusi)
Nilijifanya nimezimia kweli ila bdo nilikuwa macho sema hali yangu haikuwa nzuri, nilifikiria ni nani aliyenifanyia haya yote "ni kaka rafiki kweli kaniingiza kwenye huo mtego kweli" kabla sijapata jibu mmojawapo alipokea simu.
"Hallo eheee ndio tumempata, sawa bosi enheee ndio" alikuwa kaka yule mfupi mweusi
"Ni nani huyo? Aliuliza yule mwingine
" bosi elly huyo, tumpekele au tule mzigo tu, maana kule ana mawili kufa au kupona" alitoa tahadhari yule mweusi.
"Ila kiukweli bosi elly mimi namuheshimu tu anawajali malaya zake yule sijui love na salma na kale kadada kasalma sikapendi ila namtaka sana yule love" aliongea yule mrefu mweupe
"Ila nikwambie kitu francis? Niligundua yule mrefu mweupe alikuwa anitwa francis
" ndio"
"Bosi anajalia sana kuhonga wanawake ila sisi mishahara na pesa zetu atulipi mimi nimeshoka" aliongea yule mfupi
"Hamna juma hii kazi ya kumpeleka huyudada inakuwa?? Aliuliza yule francis
Kwa lengo moja walikubaliana wasinipeleke ila mungu ni mkubwa maana kabla walipanga kunibaka sasa nilipoteza imani na elibariki nilivyokuwa najua alikuwa nje ya nchi kumbe yupo hapahapa dsm anakula bata casino na kuamua kutembea na rafiki yangu na mama yangu mdogo.
" tumsaidie juma uwezi jua ya mungu mengi"aliongea francis
"Kweli ila tuzime simu zetu ili wasitutafute tuhakikishe uyu dada anafika kwake kwa namna yeyote" aliongea juma?
Nilikuwa sijiwezi nakumbuka hatua ya mwisho niliwapatia funguo ya gari baada ya kujua ni watu wazuri walifanikiwa kunifikisha mpk nyumbani lakini wakati huo sikuwa najiweza.
**************
Nilishtuka nipo kwenye usukani wa gari nje ya geti langu jana yake mpka nafika pale nyumbani nilikuwa najielewa japo sio sana ila ilitokeaje mpaka nikawaruhusu waondoke na wakati awakuchukua namba zangu za simu??? Nilijiuliza maswali mengi ila bado jibu sikuwa nalo "ooh shit!! Nimeharibu"
Mgongo ulikuwa unauma sana nilihitaji kupata hata message hapo ndipo nikakaa nikawaza juu ya vipi ninaweza pata message ingekuwa ni kipndi kile cha samson nisingewaza maana hata mimi mwenyewe ni mtaalamu wa mambo hayo since nafanya kazi saloon kwa elibariki enzi zile sina kitu kabisa.
Niliwaza mengi hasa juu ya kufungua saloon ya kike na kiume ambazo zitakuwa na message ndani yake ila sitamani kufanya kazi na wanawake tena kama salma mtu wa pekee ni mama bakari tena ni kwasababu ana shida zake bila hivyo nisingeweza kufanya nae kazi maana wanawake kwa wanawake tundharauliana sana.
Nilishika simu yangu nijaribu kumpigia rafiki yangu jenifa wa shule maana tulikuwa na group discussion siku hiyo, wakati naingia kwenye phonebook mara simu inaingia "mmh namba ngeni jamani nani huyu tena??"
"Hello Juma naongea, hu mzma dada??
" jumaa yule wa jana?? Wow! Me mzima niambie juma" nilishangamka mno
"Mzima unaendeleaje?? Alizidi kuongea juma kwa uhuru zaidi
" safi tu sijui nyie, tena afadhali umenipigia francis yupo wapi??
"Nipo nae pia" alijibu juma
"Sawa ninaweza kuwapata lini kwaajiri ya maongezi na nyie??
" siku yeyote dada wewe tu sisi hatuna kazi tupo tupo" alijibu juma roho ikaniuma vile kusema tupo tupo
"Kwanini lakini juma?? Niliuliza kwa upole mno
" ni story ndefu dada yangu ndio maana tunajiingiza kweny hizi kazi dada yangu" aliendelea kuongea juma
"Basi msiwe na shida nitawatafuta kesho jioni sawa?? Nilibidi nitoe promise
Ni ngumu kuonana na watu kwa wakati huu lakini nitafanyaje na inaonekana kuna siri nzito wanaweza kuijua juu ya watu watatu yani elibariki, salma na love(mama mdogo) ambao kwasasa ni watu wa kushinda casino na kucheza kamari na kunywa pombe kali, hiki kitu nilianza kukihisi mapema maana salma nilikuwa nikimpa pesa lei keshokutwa hana kitu na yeye kila pesa haimtoshi.
********************
Siku zilizidi kwenda kwa kasi na tarehe za kufanya mtihani wangu wa kidato cha sita ilikaribia, niliwaza mno kule nilipotoka haikuwa rahisi " yule emmy niliyeishia la saba huu kwangu ulikuwa ni mlima mrefu kuupanda mpk hapa nilipo ni mungu tu, ila sasa nazidi kumuomba anifanikishe nifaulu mtihani wangu niende chuo kikuu, huu mwezi mmoja uliobaki inapaswa niutumie vizuri mno"
Nilikuwa najitazama kwenye kioo nguo zangu nyingi zilizokuwa hazinitoshi mpk nikawa nafikiria kumpa salma sasa zilianza kunitosha na kupungua kuliko " eeh mungu wangu nina mawazo hivi mpka napungua namna hii" nilijisemea moyoni na ni siku hiyo nilikuwa na appointment/ahadi ya kukutana na juma na francis.
Gari yangu ilikuwa na vumbi ilibidi niipitishe kwa car washing mtongani wakati huo mimi niliingia cafe ya jirani nipate juice maan siku za karibuni sikuweza kutengeneza juice wala kununua supermarket.
"Hallo emmy"
"Kaka rafiki ulivyonifanyia juzi sijapenda hata kidogo" niliongea kwa lawama baada ya kupokea simu yake
"Emmy dhumuni langu sio hilo ninachotaka kukwambia naomba hiyo safari usiende" alinishangaza sana kaka rafiki
"Hapana nashukuru kwa ushauri wako ila mimi naenda wale watu nimeshakubaliana nao*
"Emmy siku zote nimekuwa nikikushauri mengi ukifata unafanikiwa hata hili nakuomba tafadhari usiende kuna mtego upo mbele yako' aliongea kaka rafiki
" najua na nakuheshimu na asante kwa huo moyo wako ila juzi ulivyonifanyia umepoteza iman yngu kwako tafadhali nakuomba niache na mambo yangu samahani" niliongea kwa hasira mno.
"Saw utakaponihitaji usisite kunitafuta, call me kaka rafiki" alimalizia hivyo.
"Toka uko kaka rafiki bongo? Yani ili kaka eti anawaambia watu waniwekee dawa kwenye kinywaji ili nibakwe sijui ili afaidike nini? Niliongea peke yangu baada ya yeye kukata simu
Nilikaa takribani dakika kumi mbele nawaza juu ya hiyo safari moyo ukawa unakataa tena nisiende nikapata visingizio vingi ila kikubwa nilishaweka mihadi ni ngumu kuvunja, nilipokuwa pale iliingia message
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com