MUUZA UBUYU (15)

0
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
"Emmy usije ukagombana na ndugu yako kisa mwanaume mimi huyu baba bakari huyu siye mwanae ni mtoto niliyezaa na baba yangu mzazi na sijawahi kuona ajimnyanyasa wala kumtenga hata nilipomzaa halima(mdogo wa bakari) bado ameonyesha upendo kwao wote"

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
"Ndio huyo salum uliyesema alikusaidia? Ilibidi niulize baada ya kutoamin labda huyu ni mwanaume mwingin

" ndio huyu salum au kwasababu kazoeleka kwa jina la baba bakari? Aliongea huku anatabasamu kidogo

"Ahaaa dah ni wanaume wachache wanaweza kufanya hivi mama bakari, kwani una miaka mingapi sasa hivi? Nilitokea kumpenda sana mama bakari

" nina miaka 21 sasa hivi nakumbuka bakari nilimzaa nikiwa na miaka 17 na huyu dada yake ni mwaka jana nikiwa na miaka20 ndio hivyo sasa tunapambana tukamilishe nyumba yetu mbande uko tuamie" alizidi kuongea mama bakari uku namsikiliza kwa makini.

"Haaa pole dada jamani unafanya kazi gani sasa?
Niliendelea na maswali mengi

"Nina kazi wapi zaidi ya ususi huo nikipata wateja wawili watatu nina elfu 60 nacheza na michezo minne hapa kwahiyo nina uhakika wa kila mwezi kupokea laki 3 hadi na nusu zote nazipelekwa kwenye ujenzi nasaidiana na baba bakari nae akiangaika akaa!! Tunasogeasogea" alionyesha cheko lako nami nikatabasamu pia

"Sasa dada nashukuru kwa ushauri wako japokuwa zamani nilikuwa nakuona mnoko na wale rafiki zako hasa mke mdogo wa mzee yule(mzee mashaka father house) nakushauri lakini ule urafiki sio mzuri na ukiangalia rika lako bado mdogo wewe wa kukaa na wale miaka 30 watakushauri nini zaidi ya umbea" niliamua kumpa la rohoni maana nakumbuka yeye na wenzake kipindi hicho walikuwa awanipendi mno

"Mmh mdogo wangu we acha tu, hivi kwani emmy una miaka mingapi? Aliuliza dada fatuma

" miaka ishirini nadhani nafikisha mwezi wa tisa"

"Kheee basi hatujapishana sana, ila mwenzangu yale makundi nimeshaachana nayo sasa ndio kama unavyoniona na hapa nikipata kazi tu mambo yatakuwa sawa" aliongea dada fatuma na kunipa akili

"Sikia nikwambie kitu mimi nina biashara zangu nina sambaza ubuyu kwenye supermarket na mwezi ulioisha nimefungua cafe ya kuuza vinywaji na vyakula mbalimbali nina ndoto za kuwa mjasiriamali mkubwa sasa niweke kwenye nafaka ila tatizo niliyempa asimamie ananiibia sana" aliongea kwa masononeko

"Nani tena??
Aliuliza mama bakari/fatuma

" si huyo salma anayeishi karibu na mtendaji"

"Kheeee yule jamani yule msichana anahonga yule sijawahi ona mbona alikuwa anamtaka baba bakari nimegombana naye juzi tu na yule mwanaume wako yule bonge(alibariki) nahisi anatembea nae" aliongea kwa mshangao mkubwa

"Aaha sawa naomba niende nitakutafuta dada, halima.mama njooo chukua ya soda hii" niliamua kupotexea ile mada maana nilijua yatakuwa mengine pale nilitoa noti mbili za elfu kumi nikampa halima mtoto wa mwisho wa fatuma/mama bakari.
****************

Katika maisha yangu nimejifunza vitu vingi hasa kuishi na watu vizuri fatuma/mama bakari akuwahi kuwa rafiki yangu alikuwa ni miongoni mwa maadui zangu ila historia ya maisha yake imenipa hatua moja mbele ya kutafakari ni wapi nilipotoka, nilipo na wapi nitaka kuwepo. Mtu ambaye nilimuona ni adui kwangu sasa anekuwa rafiki ila yule ninayekula nae na kuishi nae na kumpa siri zangu(salma) kumbe utoka na kuzitoa nje kasahau kuwa mimi ni emmy na sio salma na asichokumbuka pia mimi ni rafiki na hatuna bloody relationship/uhusiano wa damu hivyo muda wowote naweza kuamua nichukue hamsini zangy nae achukue zilizobaki kwenye mia moja. Kinachoniumiza zaidi ni kutumia nafasi ya urafiki na mimi kufuja pesa zangu kwa kuhonga wanaume, amesahau kuna maisha baada ya hapo ni bora angefuja pesa na kufungua biashara au kumalizia upande wa pili wa nyumba yao ulikosa kuezekwa hata kwa makuti ili yeyw haondokane na aibu ya kulala na wadogo zake wa kiume hali inayomlazimu anapotaka kubadili nguo kuwatimua nje wadogo zake.
Mimi emmy kwa kuona matatizo hayo nilikubari kumsaidia rafiki yangu wa utoto mpka ukubwani salma nikijua labda atabadili.

Haya ndio malipo ya salma sasa anatembea na elibariki, ameshanitia hasara ya zaidi ya milioni sita, kibaya zaidi anasambaza taarifa za uzushi kuwa mimi namroga mamdogo ili nipate pesa, je mimi emmy ningekuwa na akili za kufuja mali leo hii nisingesoma maana hapa nilipo namiliki nyumba japo ya kupewa na mwanaume yenye thamani zaidi ya milioni mia mbili, nina kiasi cha shilingi milioni 35 benki, nina usafiri binafsi japo nimepewa na mwanaume lakini bado sijadharau shule maana najua nilipotoka na siku zote najua kusimamia ndoto zangu.
Nilikaa huku machozi yananitoka nikimkumbuka salma ninayemjua mimi roho inaniuma, acha huyo sasa nakuja kwa huyu aliyezaliwa tumbo moja na mama mdogo wake wa mwisho/mama mdogo rose. Sikatai amenilea mpaka najitambua ila ilifikia wakati wa yeye na mimi kuungana ila siku zote akutaka, mara nyingi nimekuwa nikimsihi tuanzishe biashara au hata aje kijichi tuishi pamoja amekuwa akikataa sijui ni kwanini lakini kumbe jibu ni jepsi tu hata wewe mama mdogo unatembea na mkamwana wako ashilia mbali na wetu kutopishana saana ila bado haiondoi heshima kati yetu roho inaniuma kusikia nawe unashiriki kusema eti "emmy ananiroga ndio maana mambi yangu hayafanikiwi" nimekuwa nikikaa na kutafakari nikapata jibu kuwa elimu ni mkombozi na hapo ndio unaweza kumtofautisha aliyesoma na asiyeenda kabisa darasani na watu hawa wawili uwezi wao wa kufikiri hauwezi kuringana.

Emmy huyu wa leo sio emmy wa nyakati zile asiye na elimu, emmy yule alikuwa ana kifua akisikia jambo akawii kukurupuka na kwenda kumkanyaga aliyelizungumza kwa maneno makali yaliyojaa vitisho, na hilo baba mwenye nyumba analijua na wapangaji wengine, unajua ni kwanini? Siku mama bakari aliponisimulia juu ya tabia ya mama mdogo na salma alitegemea ningekasirika na kuwafata tayari kuharibu uhusiano lakini si hivyo nataka nihakikishe kwa macho yangu na si kuruhusu masikio yawe shahidi pekee..
***********

Baada ya kutoka hospitali jioni nilimchukua mama mdogo nikamrudisha nyumbani hapo nilipata fursa pia ya kuonana na salma nilifanikiwa kusikia kauli moja ambayo ilinichanganya "pole shoga yangu sikujua kama yamekukuta ya kukuta au ni zile pombe za juzi zilikuzidia? Mie unavyoona mguu huu ndio narudi nyumbani kutoka uko las vegas nimekesha, nimekunywa ila nimeliwa laki tisa na uchee japo nimepata jibosi limenihonga laki tatu siku hizi mbili" alisikika salma wakati huo nilitoka nje kujisaidia aja ndogo. Nilipoingia ndio ukimya ulitawala.

"Salma mzima" nilimsalimia

" nipo poa mambo best, poleni kwa kuuguza" alijibaraguza hapo nikimuangalia usoni kama kahaba amejipodoa hamna mfano na amevaa cheni za gold, eleni za gold chini vikuku vya gold na bangili za gold nilijawa na ghadhabu juu yake ila nikakituliza kifua changu

"Jamani me naenda kama kutakuwa na tatizo mama utanipigia naomba usikae kimya au usitume message wewe nipigie tu" aliongea nikamuachia kiasi cha fedha kama laki na nusu kisha nikawa naondoka

Kitendo kile kiliwachangaza hao wanaosema mimi simjali mamdogo wala kumtunza, kabla sijaingia kwenye gari nikamsikia salma anakuja kwa kukimbia
"Emmy emmy sikia nisubiri" aliita uku ana kimbia
"Samahani naomba niazime laki sita nitakurudishia jumanne" aliongea bila hata chembe ya aibu hajui wenzie tumeenda shuke kuliko anavyodhani

Nakumbuka wakati anamuahadhia mamdogo love alimwambia ameliwa laki tisa na kapata jamaa kamuhonga laki tatu hivyo nikimpa laki sita itakuwa laki tisa hivyo basi mwisho mwa wiki iliyoisha akuleta mahesabu ya biashara ambayo ni kama laki tisa na nusu kwa mawazo yake ile pesa nimpatie kisha afanye kama hesabu ya wiki hiyo. Nilicheka kidogo kisha nkamjibu

"Hesabu ujanipatia bado na ni laki tisa na nusu si ndio" nilimuuliza kwa mtigo maana wadaiwa wote waliniambia tayari wameshalipa

"Kheeenheeee ndio" alijibu kwa kigugumizi

"Sasa katika pesa hiyo uliyonayo nakukopesha hiyo laki sita unaweza kunipa laki tatu na nusu hapo? Niliamua kutumia ujanja

" aahaa ndio" alijibu pia kwa kusitasita huku anatoa pesakwenye poshi yake kulikuwa na laki tatu kamili zilizofungwa kwenye lababendi alinikabidhi na kurudi ndani kwa spidi nahisi alienda kumuazima shoga yake mama mdogo amuazime elfu hamsini
Dakika kumi nyingi alirudi akiwa na fedha hizo, akanipatia kisha nikamtazama alivyotokwa jasho

"Naomba ndani ya wiki ijayo uwe umenipatia hizo laki sita nilizokuazima" niliamua kuwa mkali

"Sawa lakini.."

"Nataka ndani ya wiki hii tafadhari hatutaelewana salma kuwa makini" niliongea nikaingia ndani ya gari na kuondoka.

Nilikuwa bado siamini kama love(mamdgo) na salma wanacheza kamari kwenye casino za hapa mjini nikawa nafikiria siku moha niwafumanie.
*************

Sikumpa tena mzigo salma nilifanya hivyo kwasababu niliitaji anirudishie fedha zangu kisha nimkabidhi rasmi kazi fatuma/mama bakari maana angalau yeye anajua maana ya maisha ni nini.

Jioni ya siku hiyo nilikuwa nimetoka darasani nikawa naondoka kurudi nyumbani niliona namba ngeni inaingia "mmmh nani tena huyu" nikapokea

"Hallo nani" niliuliza

"Kaka rafiki naongea" sikushtuka sana maana nilianza kumuelewa sana huyu kaka japo simjui ni nani

"Heee mzima kaka rafiki? Nikiongea kwa furaha

" emmy hapohapo ulipo njoo new africa hotel nipo na mama yako mdogo na rafiki yako salma hapa tunacheza kamari za nguvu" alinishtua kaka rafiki palepale nikageuza gari


Niliendesha kwa mwendo kidogo kuwahi huko casino maana nilikuwa natamani sana kujua salma na mamdogo love wana issue gani vinazowaunganisha, ndio kama bahati kaka rafiki akaniambia niwahi kule casino.

Pamoja na kuwa na foreni za hapa na pale nilibahatika kufika hiyo casino, sikujua cha kufanya maana sikuwahi kuingia casino toka nazaliwa ila kitu nilichokiwaza kwa wakati ule kwenye pochi nilikuwa na laki sita, sasa kwa vyovyote vile nikisema niingie nazo ninaweza kupoteza zote maana mambo ya kishwetani haya yana ushawishi mkubwa. Nilipiga hatua kama tatu mbele nikawa namkaribia mhudumu wa kiume aliyekuwa nje ya hotel ile kubwa ya kifahari nikamkumbuka kaka rafiki nikaamua kumpigia simu.
Simu iliita bila majibu nikawaza "huyu ameniingiza choo cha kiume nini?" Sikukata tamaa nikapiga tena mambo yakawa kama mwanzo simu haikupokelewa sasa wakati naendelea nilishangaa yule mhudumu anakuja kunifata.

"Hello madam welcome" alikuwa ni mkarimu mno km ni customer care ya hali ya juu

"Hello! Samahani kaka kuna mtu namsubiri hapa" niliamua kujidefend kidogo

"Anhaaa sawa ila kuna mtu ameniagiza kwako dada"

"Kheee! Kakwambia anaitwa nani?"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)