MUUZA UBUYU (18)

0
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
"Bwana bwana zungu kuna mdada mmoja jana katukimbia usiku wa manane boss anamuitaji sana yule dada maana inasemekana alikuwa mtu wa boss lakini boss anahofia michongo yake binti atamchoma hivyo anataka hampoteze, sasa hiyo jana alichotufanyia yule mwanamke mshenzi hasaaa hapa ndugu yangu babu hali yake sio mbaya" aliongea moja ya vijana mhalifu.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
"Sasa hapa sio salama kabisa kuendelea kukaa kama inawezekana tuondokeni maana polisi muda wowote watatia maguu, ebu nipe funguo ya ilo gari niangalie oil na mafuta" aliongea ford/zungu huku anapokea funguo

"Aisee zungu yule mwanamke mwisho sasa ngoja nimuamshe babu tuamshe maana tulikuwa tunamsikilizia bosi tu hapa"

Mr ford aliona ule ndio ulikuwa upenyo wa kutoroka na lile gari, alipoangalia kwenye dashboard akakuta simu mbili, pochi ya kike ndani yake kulikuwa na pesa na funguo nyingi pia na vipodoz vya kike "anhaaa sawa hapa naweza kwenda maana oil kila kitu kipo poa"
*************

UPANDE WA EMMY.
Baada ya kumaliza kuoga nilikaa kitandani nawaza jinsi ya kutoka pale guest tayari ilikuwa saa tatu na busy asubuhi. Usoni sikupaka mafuta wala make up yeyote nikawa nawaza nitaondokaje pale mara mlango ukagongwa.
"Mmmh wenye vyumba wanataka chumba chao mmh ngoja nivae viatu niwaachie room yao" nilijisemea baada ya kuvaa viatu nikaenda kufungua mlango sikuamini macho yangu kumuona yule ford akiwa na pochi yangy mkononi na simu zangu.

"Habari yako dada* alisalimia kwa bashasha

" jamaniiiii salama pole na asante jamaniii yani sina cha kukuripa mungu akusaidie" nilikuwa ni mwenye furaha mnooo

"Shukrani ila nimepigiwa simu na bosi wangu nikwenda kufata mzigo mimi ni dereva wa kampuni ya gsm naomba niende ila tutakutana mungu akipenda"
Aliongea na kuanza kunyanyuka kisha akageuka
"Nilitaka kusahau gari nimepaki hapo kulia nimeshaweka mafuta nakutakia siku njema.... No no no nimesahau unaitwa nani?

" jamani hizo haraka mpka utaki tujuane naitwa emmy nakaa kijichi ccm ukifika pale ulizia kwa dada emmy muuza ubuyu"

"Kheee kumbe ni mjasiriamali mkubwa hivyo najua kwa umaarufu huo sio ubuyu huu ninaouna ukiuzwa mtaan" alitania

"Kidogo hivyohivyo kaka yangu"
************

Nikiwa ndani ya gari nilikuwa nawaza mno juu ya yule mtu ndipo nikamkumbuka kaka rafiki nikaanza kuandika namba zake maana nimezikariri kichwani wakati nataka kubonyeza call simu ngeni ikaingia.

"Hello emmy harakati zako nimezielewa nakupa siku tatu uache hizo harakati la sivyo nitakuua" ilisikika sauti nzito upande wa pili.

Niliduwaa na kubaki nashangaa "jamani mbona mambo haya yananikuta mimi sasa ni harakati gani nazifanya mimi nataka niishi kwa amani lakini mbona huyu elibariki ananifanyia hivi sawa tu mungu atanisaidia tu" niliongea huku machoz yanatoka nikasahau mataa pale yaliruhusu nilichosikia honi nyuma yangu piiiii piiiiiii pooooooo!!!!
Nilikanyaga mafuta nikaanza kuendesha gari huku kichwani bado nina msongo wa mawazo sana, nilitamani sana kumuomba msamaha kaka rafiki maana dhamiri ilikuwa inanihukumu kwa nilivyomwambia ila kabla sijampigia namba ngeni iliingia nikapark gari pembeni.

"Halllo" niliongea baada ya kuweka sikioni

"Yes emmy mzima wewe" nilisikia sauti nene mno ya kunguruma.

"Mimi mzima nani wewe"

" mimi ni kaka rafiki" alijibu

"Mmh kaka rafiki mbona sauti sio yako au unaumwa?? Nilishangazwa na ile sauti.

" nina mafua kidogo upo wapi sasa?? Aliuliza

"Nipo sabasaba maonyesho nilikuwa nadrive nimepaki pembeni"

"Sasa nataka kuonana na wewe leo saa mbili" alizidi kuongea kwa sauti nzito mnoo

"Mmh wapi na mbona mida hiyo ya usiku huwa mimi sitoki"

" hii ni kwa manufaa yako na usalama wako njoo pugu road nitakuelekeza pa kwenda" aliongea na kukata simu.

Nilibaki na mshangao mkubwa nikajiuliza mambo mengi kichwani moja sauti ile haiendani na ya kaka rafiki hata kidogo, pili ongea yake ni ya command/kuamrisha ni tofauti na kaka rafiki, tatu namba ile iliyonipigia ni namba ambayo niliwahi kuiona mahali si ya kaka rafiki, jingine kubwa zaidi kaka rafiki hataki tuonane iweje huyu kaka rafiki wa leo hatafute tuonane kirahisi namna hiyo na wakati anachofanya mara zote kaka rafiki ni kunipa maelekezo na kukata simu sio kutaka tuonane.

Mambo haya yaliniumiza kichwa nikasema nooo nampigia kaka rafiki mwenyewe kwenye simu nina namba zake sita nikaanza kujaribu ya kwanza haipatikani mpaka ya tano haipatikani nikapata maswali "uenda ni kweli yule kaka rafiki lakini nitamsubiri anipigie kwa mara ya pili"
*********"*****

Nililala mnooo hata sikula japo nilipofika nyumbani nilipika nikawasha tv hapo kuangalia vipindi vya ubuyu matokeo yake usingizi ukanipitia, niliota kitu cha ajabu sana tena juu ya usaliti mkubwa.

ILIVYOKUWA.
nilikuwa nimesimama kutazama bahari nyuma yangu alikuwa mwanaume aliyenishika kiuno alikuwa ni mtu mwenye misuli..

"Vipi baby umepapenda hapa" aliuliza.

"Saana baby nimependa mandhari yake"

"Unajua najaribu kufanyq kila niwezalo hili kukusahaulisha yale matatizo yaliyokukuta"

"Baby kila siku unasema hivyo yalinikuta matatizo naomba nikumbushe kilitokea nini baby"

"Esta mpenzi wangu ni mambo mengi nasubiri hali yako itengamae nitakwambia usijari"

"Mbona hali yako ipo sawa pleasee baby niambie kilitokea nini??

Ilikuwa siku moja nikiwa nimetoka kazini usiku kwasababu ya mambo mengi na kazi iliitajika ndani ya siku tatu mbele ikamilike kutokana muda mdogo ulibaki ilibidi nitumie muda wa ziada kuifanya ile kazi.
Siku hiyo nilitoka kazini usiku wa saa nane ili nipumzike masaa manne kisha nirudi tena ofisini. Nikiwa njiani ghafla nililiona gari mbele yangu likiwa limebeba kitu kama gunia kwenye bonnet niliendelea kutazama ndipo nilipogundua alikuwa furushi tu ila ulikuwa ni mwili wa mtu baada ya kuona mkono mmoja ukining'inia nilizima gari na kuchomoa bastola yangu kiunoni, nilitazama mbele nikasikia wale watu wakisema.

" jamani mume hakikisha amekufa kweli maana kama akipona ushahidi wote utakuwa wazi" aliongea mmoja katu yao.

"Yeah kwa kipigo kile sidhani kama atakuwa hai ila jebu ebu hakikisha" aliongea wa pili

"Jamani heee muda mbya mtupeni baharini huko watu wa patrol watapita muda si mrefu"

Walikimbia wote na nilibaki peke yangu nikasogea mpaka eneo la tukio ndipo nikakuta furushi kuubwa lenye damu nyingi heee kumbe ni mwanamke ikabidi nimchunguze kwa hali ile nilijua amekufa lakini nilisikia akikohoa ndipo hapohapo kwa shida sana nilimbeba kwenye gari nq kufanikiwa kumuingiza ghafla polisi wa patrol wakatokea.

"Halllo unafanya nini hapa usiku huu wewe ni mwalifu" alihoji afande mmoja mweny mwili mpana mno.

"Aaha naomba tuokoe uhai wa binti yupo nyuma nikiwa natoka kazini nilikuta watu watano wakiutupa mwili huu hapa nilishindwa kuwatackle kwasababu walikuwa ni wengi hivyo nikawasubiri walipoondoka nikaenda kutazama ndipo nilipomkuta binti huyu akiwa mahututi mwanzi nilijua amekufa ila baada ya muda akakohoa nikaona nimuwaishw hospitali kwenye kitengo chq dharura naomba msahada wenu" nilioongea huku nafungua mlango wa gari niwaonyeshe jinsi ulivyokuwa.

"Haloo hili jamaa ni liongo naona hawa ndio walee afande ambao ni wauaji wanaowatelekeza wale ambao uwafanyia uhalifu sasa tumekukuta na kithibiti kesi imekamilika"

Nilitetemeka sana nikaanza kujitetea pale ila hawakutaka kunielewa kabisa.

JE NI KIPI KITAENDELEA KATIKA SIMULIZI HIYO YA EMMY.

KUMBUKA HIYO NI NDOTO YAWEZA KUWA KWELI AU NI MAWAZO TU YA EMMY.

ILA NINGEPENDA KUWAKUMBUSHA KUWA SIMULIZI HII IMEJENGWA KWA MFUMO TOFAUTI MAANA MATUKIO AYAENDI KWA KUFATA MPANGILIO ULIOZOELEKA, TUKIO MOJQ ALIISHI LINALUKIWA TUKIO JINGINE YOTE NI KUKUFANYA UPENDE KAZI UANDISHI NA KUZIFATILIA.

YOTE HAYA TUNAYOSOMA NI MATUKIO YA NYUMA EMMY ANAMSIMULA RAFIKI YAKE CINDY, EMMY WA SASA NI MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU KTK UHALISIA HIVYO TUWE MAKINI KUFATILIA HII SIMULIZI.

Suddenly simu yangu ikaita na kutoa kwenye ndoto nilishtuka sana maana tukio lile la ndoton ni zito sana.

"Hello"

"Yeah emmy mzima?

" mzima mamdogo, upo wapi mbona kimya' niliposikia nilitambua ni mama mdogo love.

"Nipo mwanangu hata nashaangaa hu mzima kabisa? Alionyesha mshangao kweli

" yeah ma kuna nini niambie" nilizidi kuhamaki pia

"Noo hakuna nilitaka kujua hali yako kama ni mzima basi nashukuru" alimaliza akakata simu.

Ilinibidi nikae kitako nifikirie nini kimetokea na mamdogo kunipigia simu muda ule ila tokea awali nilianza kuhisi kuna namna ambayo mamdogo love na salma wanashirikian na elibariki ambaye kwa sasa ni kama adui yangu. Akili haikunipa kabisa nikajisemea moyoni "hapa leo silali lazima nijue nini kinaendelea" niliamka japo nilikuwa na uchovu nikanawa uso nikapaka lotion yangu kidogo usoni kwa ule muda (00:23) niliona nivae pensi yangu ya kombati ambazo elikana aliniletea kipindi cha nyuma nikapiga na tshert, simple zangu nikachukua kadi zangu za benki na kiasi kidogo cha pesa nikaweka mfukoni, sikuwa nahitaji gari kwa muda huo, nilidhamiria kukodi bodaboda na kwakuwa kijiweni pale kijichi ccm ni maarufu kwangu haikuwa shida kufikiria nitafika saa ngapi.

Nilifunga geti nikaanza kutembea mwendo kama wa teja yote ilikuwa ni kujiami maana ile mida mibaya hasa kwa mimi mtoto wa kike lolote linaweza kutokea. Sikupiha hatua nyingi simu yangu ikaita nikajivuta kwenye mti nikapokea.

"Mamdogo"

"Yeah emmy umelala? Aliuliza mama

" yeah nimelala upo wapi? Nilimuuliza kwani safari ile ilikuwa ni kwake

"Nipo nyumbani nimelala" mmh nilishtuka kuniambia yupo nyumbani kalala na uku nilisikia sauti za watu wakiongea kwa pembeni yake tena inaonekana wapo bar au sehemu mojawapo ya starehe. Nilikata simu nikijua nitapata vipi.

"Aaha sista emmy"

"Niambie muddy mauwezo"

"Poa sista lake unaruka wapi now dada lake?

" nitaka unirushe temeke mikoroshini now ngapi pale mshizi wangu?

"Shingi saba/elfu saba dada lake"

"Poa nivushe mdau"

Nilijaribu kuongea slang za mtaani ili mradi niweze kuendana na muktadha na kurahisisha maongexi, muddy ni kijana ambaye nafahamiana nae muda sana toka naaminia kijichi na kabla sina gari alikuwa ananipeleka nitakapo kwa bei rahisi, maana hiyo elfu saba kwa mwingine angemwambia kumi na tano hadi elfu ishirini.
****************"""

Nilishangaa kutomkuta mamdogo na wakati aliniambia yupo nyumbani kalala, nilitazama mazingira kwa haraka haraka niligundua kile chumba hakikuwa na mtu kama sio siku tatu ni wiki kabisa kulikuwa na vumbi, shuka lilitandikwa vizuri na midori ililazwa kitandani, nilitumiq simu yangu kutazamia mule ndani. Nilianza kufanya usafi taratibu uku nasikiliza muziki kwenye simu yangu maana chumba chenyewe hakikuwa na umeme.

Nililala baada ya kumaliza kila kitu mpka nikasahau kuzima simu iliimba mpaka asubuhi nilishtuka alarm ilipoita ambao ni muda niliojipangia kuamka kusoma.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)