MUUZA UBUYU (19)

0
Mwandishi: Micky Mejah

SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
Nililala baada ya kumaliza kila kitu mpka nikasahau kuzima simu iliimba mpaka asubuhi nilishtuka alarm ilipoita ambao ni muda niliojipangia kuamka kusoma.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Muda uliyoyoma na simu yangu ilizima chaji kabisa nilipokuja kushtuka ilikuwa imetimu saa moja kamili, niliamka nikafanya usafi wa mazingira wakati natoka nikamuona fatuma/mam bakari.

"Shoga mzima wewe? Aliongeaa mama bakari

" mzima vipi kwema huko?

"Kwema za kutususa? Aliongea mam bakari

" tuyaache hayo hivi huyu ni muda gani toka ametoka hapa? Niliongea kwa sauti ya chini

"Mmh mwenzangu ngoja nikung'ate sikio hata mimi sielewi hapa ndo ameama au ila kiukweli ana muda mrefu hajalala hap muda wote yupo uko ila uja mara moja moja sana" alinifumbua macho sasa

"Nakuomba nikutafute kesho tuongee na ile ishu ya biashara pia tutaijadili"
**********

Nilitazama mazingira yalivyo nikajua kwa hakika kuna watu wameingia pale ndani, nikajua kumbe ile simu ya jana niliyopigiwa na mamdogo kuwa unafanya nini kumbe alipanga kuja kuniangamiza(machozi yakitoka) sikudhani kuwa mama mdogo anaweza kunifanyia unyama huu ila mungu pekee ndio mlinzi wangu. Nilitaka nimpigie simu ila moyo ukakataa, nikairudisha simu kwenye chaji nikawa siamini kila kilichopo ndani, chakula nikakimwaga maana wanaweza kuweka hata sumu, nilitazama kila kona isije ikawa wameweka hata bomu "yani watu awalali wanatafuta roho yangu" niliwaxa cha kufanya nikakosa.

Nikiwa pale nikawaza juu ya ile ndoto nikapata maswali mengi "ina mana hawa watu wamedhamiria kuniua kabisa kama ni hivi inabidi nimtafute elibariki nimuombe msamaha maana ataniua kweli"

(TURUDI KWA CINDY)

Emmy: hivyo ndivyo ilivyokuwa best nikamtafuta elibariki ilikuwa ni jumapili jioni tukazungumza na kuyamaliza mpka leo unaniona hivi

Cindy: vipi kuhusu kaka rafiki na ukweli juu ya mamdogo na salma waliokusaliti?

Emmy: cindy kiukweli sielewi nipo nao peace tu ila kumbo nsyafatilia chini kwa chini maana hata huyu elibariki nipo nae lakini simuelewi elewi yani mguu nje mguu ndani.

Cindy: sawa best mimi naenda basi nina udobi kule hostel si utakuja jioni?

Emmy: sijui mamie namsikiliza shem wako maana weeknd anapenda tutoke sana nadhani anything can happenning sema tutawasiliana.

BAADA YA NUSU SAA.
Nilikaa nikatazama picha zangu za graduation ya form six moyo wangu ulifurahi sana nilikumbuka mengi ila kikubwa isingekuwa kumuomba msamaha elibariki hata kufa ningekufa kwani aliniandama sana 'lakini je ni kweli amenisamehe au ananilia timing aniangamize? Nitajua ukweli kupitia kwa kaka rafiki na mamdogo" nilijipa moyo uku nikizidi kufungua albam yangu nikaona picha ya sam akiwa amebeba beg lake roho iliniuma sana nikaanza kutoka machozi 'sam ni kaka rafiki kabisa ananificha tu kaka rafiki ni sam" nilipata wazo nimtafute maana ni moezi sita imepita pasipo kuwasiliana nae

Kila nikijaribu zile namba hazipatikani kichwa kilizidi kuniuma maana kuna sifa za sam ndani ya kaka rafiki. Wakati napiga namba moja iliyoanziwa na +254 ile simu ilipokelewa lakini hakuwa kaka rafiki, niliongea nae nikajua hakika si yeye.

" dada niko kwa job huyo chalii simfahamu wa kuitwa hivyo' aliongea rafudhi ya kikenya
"Amekuwa akinipigia kwa muda mrefu sana kaka nisaidie"

"Ni muda gani sasa?

" miezi sita imepita"

"Anhaa huyo aitwi kaka rafiki anaitwa abdulrahim alikuwa hapa ila alirudi tz uko miezi kumi iliyopita ila nilisikia tena yupo uku mombasa ila sijapata kumet nae"
Alitaja jina la abdulrahim akanichanganya kabisa

"Samahan kaka yupoje huyo abdulrahim?

" ni mrefu yuko na musculurs/misuli ni mtu wa it na anafanya kazi na shirika moja linaitwa MFS(MUSLIM FREE SOCIETY)"

"Ndio huyo huyo kaka nitakuja mombasa kaka"

"Noo nitakupa web yao uwasiliane nao ila wana matawi duniani hata zanzibar wapo pia" aliongeza yule jamaa

"Sawa kaka naomba nitumie kwa email yangu emmyqueen@gmail.com

Nilimalizana nae nikaketi mezani nikaanza kuwaza ni maswahibu gani yamemkuta sam hadi kubadilisha jina/dini nikaapa nitafanya kila niwezalo nipate details zake zote, nilianza na kumtafuta baba yake kule kijijini.

Nakumbuka nje na elimu yake sam alikuwa ni mtaalamu sana wa computer mambo ya internet na maintanance kitu kilichokuwa kinampa kipato pia cha kuendesha maisha yake ya chuo.

Ilikuwa ni jumatatu niliweza kupata taarifa ya kutoka kijijini kwao na sam kuhusu uwepo wa baba yake, taarifa nilizopata ni kuwa kwa kipindi kirefu baba yake na sam hayupo pale kijijini na wati hawajui alipoenda ila inasemekani yule mzee alipata ugonjwa wa kansa.
Taarifa zile zilinifanya nizidi kuumia inakuwaje hii ikanibidi nifikirie kufunga safari nikamtafute sam huko mombasa ila kabla sijaenda nilichukua laptop yangu nikatafuta jina la hiyo MFS na kazi zao na uongozi wao.

MFS.
dealing with social matters/wanajihusisha na mambo ya kijamii, kujenga shule, visima, misikiti na kutoa sponsors kwa wanafunzi na scholarshp.

>uongozi, meneja musin a musin, ahmed zakir, eli-babu, abdulrahim rahim, rashishi aziz, mohamed omar.

Haya ndio yalikuwa matokeo ya nilichokitafuta nikaangalia majina mawili nikawa na hofu nayo ils nikaapa kuyafatilia kwa kina.
*******""""""""""

Nilifikia sehemu inaitwa severin sea lodge mombasa, hapo kabla sikuwahi kufika uku nyuma nilimdanganya elibariki naenda field arusha. Niilipata chumba baada ya hapo nikatoa line zangu za tz na kuweka safaricom mtu wa kwanza nilimpigia ni yule mkaka wa juzi.

,"hallo upo wapi brother?

"Niko bamburi"

"Kuna umbali gani na hapa severim sea lodge?

" aaah ni mwendo wa dakika 20 nitafika"
*********"""""

"Unaweza kuniambia ilikuwaje mpaka ukakutana na abdulrahim?

" dada ni simulizi ndefu kidogo ilikuwa hivi.

ENDELEA NA FLASHBACK.

Nilikuwa nipo gengeni napata chakula muda ya jioni nikakutana na mtu yuko na singlend/vest na suruali chini yuko na maviatu yaliyopishana color/papa na ngulu inaonekana alichoka sana na hakuwa na pesa yeyote kwa pocket vyenye inatosha kubay chakula. Moyo wa huruma ulinijaa mno nikaamua kumsaidia kwa siku hiyo ikapita kwa kunishukuru sana "kaka mungu akubariki sana kaka yangu" nilimuacha na kuenenda zangu.

Sikutokea mahali pale kwa siku mbili kutokana na kaxi zangu za electricity nilikwenda mji unaitwa kakamega kufanya uko kazi baada ya siku hizo nikarejea tena. It suprise me kumuona yule kijana akiwa anafanya kazi ya kusafisha vyombo ili hapate yale mabaki ya chakula waty wanachoasha roho iliniuma mno nikamuendea.

"Bro naweza xungumza nawe" nilisema

"Sawa twaweza" alijibu

"Najua wewe ni mgeni kenya lakini mbona wapata shida zote hizi?

" kaka ni story ndefu" alijibu kwa machozi

"Naweza kukichukua mpaka nyumbani?

" nitashukuru kaka"

Niliweza kuishi nae pale nyumbani baada ya siku sita kupita nikamuuliza juu ya historia yake.

ILIKUWA HIVI.

Nilijitahidi kila pesa ninayoipata kumsaidia baba maana yeye ni mtu alipigana mimi nisome, tayari nikiwa chuo kikuu mwaka wa pili kuingia wa tatu ikagundulika baba ana ugonjwa wa figo mtoto pekee ni mimi nami kesho yangu sijui itakuwaje sikuwa na pesa mfukoni ikabidi nijaribu kuomba msahada wa matibabu ila dawa inabaki kupata figo nyingine. Nilipambana mpka nikafanikiwa kumtolea mzee figo ila haikusaidia mzee wangu alipoteza maisha...

Nilishika kichwa nikawaza mengi kuhusu maisha na kikubwa nilitaka kutambua inawezekana vipi baba nimetoa figo na bado amefariki. Nikikumbuka miaka ya nyuma ni yeye pekee alisimama kutetea maisha yangu kwani nilikosa msahada kwa ndgu wengine kwenye masuala yangu ya shule lakini yeye aliuza mifugo akauza nyumba ndogo ili nisome.
*****""""

Hivyo ndivyo ilivyokuwa na alinisisitiza kuwa lengo lake kubwa ni kuja kuchunguza chanzo hasa cha baba yake japokuwa tayari alishamzika.
Miezi iliyopita alipata kazi huku kwenye hilo shirika la kiislamu hivyo ameamua kwenda kutafuta pesa huku.

Emmy: unaweza kunisaidia nikamuona tena?

Humud; sidhani dada yangu kwasababu toka amekwenda uko mpaka sasa namba zake zote hazipatikani ila dada una lengo la kumsaidia?

Emmy: ndio maana nipo hapa

Humud: nitakukutanisha na mtu ambaye huyu atakusaidia kumpata yeye.
*****************

EMMY.

nilitazama saa yangu ya mkononi nikagundua muda ulikuwa umeenda sana, nakumbuka huku nyumbani nilimuacha elibariki akiwa naye kasafiri kuelekea kikazi sijui saudia, hiyo kwangu ilikuwa nafasi ya kipekee kufanya yangu ila najua ninachofanya ni kujihatarishia maisha yangu.

Nilikubaliana na humud yule rafiki yake sam/kaka rafiki tuonane jioni ya siku hiyo maana nilikuwa na siku 6 tu kuendelea kuwa mombasa. Wakati nafikiria mengi nilisikia simu yangu inaita.

"Hello" ilisikika sauti

"Yeah heloo"

"Emmy upo wapi? Umeondoka tanzania umeelekea wapi? Ilinitia shaka ile sauti japo sikujua ni nani

" no nipo kilosa nimekuja kufatilia mambo ya biashara"

"Sawa kumbe bado unaendelea na hayo mambo sawa"
Alikata simu.

Niliogopa sana nilijaribu angalau kumpigia tena lakini sikuweza kutokana na ile namba kuwa ni ya nje ya nchi za uarabu "huyu elibariki mungu wangu kapata wapi namba yangu hii ya safari com, aaah jana niliongea na mama mdogo atakuwa kampatia lakini amejuaje nipo kenya?' Nilijiuliza maswali nikasahau safari com ni ya kenya hivyo kujua ni rahisi na pia kama ana kifaa cha kutambua mahali nilipo ina maana atakuwa amejua kwa namna hiyo.
" haaa kesho narudi tanzania haya mambo mimi basi" nilijisemea moyoni nikavaa viatu vyangu kushuka chini kuelekea mapokezi.

"Sorry dada naweza kujua njia za kukatw tiketi ya ndege kweny mtandao" niliuliza

"Aaah it simple dada ngoja nikupe karatasi ila hapo nje kuna office ya kenya airway ni hatua ishirini tu na hapa"

"Oky thank you"
**************

Nilikuwa ni mtu mwenye upweke sana kwa kipindi hiki sikuwa na furaha kabisa kitendo kilichonifanya nione hakuna raha ya maisha maana ni heri kipindi kile sina pesa lakini nilikuwa na amani kuliko sasa pesa imeshindwa kutatua matatizo mengine, sikujua elibariki angenisababishia matatizo haya, nakumbuka siku ya kwanza nakutana naye tandika alinionyeshea kuwa ni mtu mwenye upendo na mwenye msahada kwangu ni nni sijui kimeingia hapa kati? Ila mungu pekee ndiye anaweza kusaidia maana katishia maisha yangu, katembea na mama yangu na rafiki yangu na bado ananitishia maisha. Sikuwa na wa kunisaidia nilikuwa safarini niliomba mungu niwahi kufika mapema hiyo airport kwakuwa sikuwa na amani hata rubani wa ndege sikumwamini pia.

Nilisinzia nlikuja kushtuka niliposikia sauti ya yule mtu wa kwenye ndege akizingumza "sasa tunakaribia tunatua kwenye kiwanja cha mwalimu julius kambarage nyerere... Nilijiweka sawa nikawa natazama namna ndege ilivyokuwa inatua moyoni nikawaza " hivi ndivyo maisha yalivyo sijui vita hii kama nitashinda eeeh mungu nisaidie".

Nilimuona rafiki yangu cindy na boyfriend wake wakija kunipokea nilifurahi mno nilimuona cindy kama ndugu kwangu maana wale niliowaona marafiki leo wamenigeuka huyu mweny kuonyesha upendo nilimuomba mungu anisaidie asibadilike.
*************"

Siku ya tatu toka nifike pale rohoni nilikuwa nawaza nisingeweza kukaa kimya bila kumwambia mama mdogo yaliyo moyoni maana ananifanyia vitu vya ajaby mno yeye na salma, siku hiyo nilipanga nimtafute nikitoka chuo japo najua fika sasa haishi temeke maana hata majirani pia nao wanasema hivyo. Nilimpigia simu yake ikawa inatumika.

"Halllo mbona bize hivyo mama yangu?.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)