SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
Siku ya tatu toka nifike pale rohoni nilikuwa nawaza nisingeweza kukaa kimya bila kumwambia mama mdogo yaliyo moyoni maana ananifanyia vitu vya ajaby mno yeye na salma, siku hiyo nilipanga nimtafute nikitoka chuo japo najua fika sasa haishi temeke maana hata majirani pia nao wanasema hivyo. Nilimpigia simu yake ikawa inatumika.
"Halllo mbona bize hivyo mama yangu?.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Hamna mwanangu si unajua mjini hapa kuangaika, vipi mzima?
"Mimi mzima mama nina shida na wewe sana"
"Ipi tena na lini unahitaji tuonane"
"Sasa nipo chuo ubungo ila saa nane mchana nakuomba tuonane hapo tcc chang'ombe"
"Mama nipo sehemu kwa leo sijui kama itawezekana"
"Mama kuwa casino na mimi kuna umuhimu?
" emmy emmy naona unanipanda kichwan nipo casino mimi?
"Mama umezidi nakuhita unasema upo busy sasa nashukuru endelea na huo ubusy hatq nikifa utakuwa busy ww" nilimaliza nikakata simu
Sjui alijifikiria nini akanitumia ujumbe "samahani mama yangu nitakuja na utanikuta wa kwanza" niliisoma mara mbili mbili sikuamini kama anaweza kuniandikia vile.
************
Nilifika pale tcc nikatazama pande zote sikuweza kumuona mamdogo nikajua uenda amechekewa kufika ikanibidi nivute subiri. Nikawa napitia social network ghafla nikaona breaking news ajari imetokea ya gari dogo na lori maeneo ya veta. Nilifungua ile taarifa maana lile gari dogo lilipondwa mno kiasi alifai tena kwa matumizi.
Ndani ya lile gari inasemekana alikuwa mwanaume na mwanamke wenye majina ya loveness hamis na rude peter ambaye ndiye alikaa kwenye seat ya abiria na mwanamke alikuwa ndiye dereva. Kilichonishtua kwenye ile ajari ni jina la loveness hamis ni sawa na la mama mdogo lakini najua fika mama ana gari hilo lilinipa matumaini. Nilinyanyua simu nikampigia, simu ikawa inaita bila majibu nikawaza mmh huyu ndio kaniingiza mjini.
"Hello emmy"
"Vipi cindy mambo"
"Wapi hiyo shosti?
" nipo tcc hapa"
"Baby nimeona taarifa hapa ya habari kweny tv ya ajari mbona mtu yule kama mama mdogo aliyepata ajari!
" aaha bby unasema??
"Nimeona hivyo mamy ndio nimekupigia"
"Mungu wangu mama yangu....
" emmy emmy emmy
Simu ilisikika bila majibu.
Nilinyanyuka baada ya kuongea na cindy nikaanza kutembea taratibu huku macho yangu yakijaa machozi nilitazama kama nitapata msahada isingewezekana nilifika mpkastend ya daladala nikapata gari inayopitia keko. Niliona kama wanapoteza muda nikashuka na kuanza kutembea baada ya kuona pale napoteza muda.
Nikiwa njiani akapita bodaboda nikamsimamisha.
"Wapi dada?
" naenda keko hapo"
"Ni buku tu dada"
Nilipanda na kuanza safari mpka eneo la tukio sikuamini nilipoliona lile gari hasa upande wa dereva uliharibika mno nilifanikiwa kuliona breakdown likinyanyua lile gari kutoka kwenye msitimu wa umeme. Niliulizia pale nikaambiwa majeruhi wamewaishwa muhimbili hospitali.
"Samahani kaka naomba nipeleke muhimbili"
Niliongea huku nikitoka na machozi na makamasi mepesi yalianza kunidondoka, yule kaka aliponitazama akuongea lolote akawasha pikipiki tukaanza safari.
Kiukweli alijitahid kuendesha kwani tulitumia dakika 20 tu kutoka veta mpka muhimbili. Kichwani nilijua nina pesa kwenye sidiria baada ya pochi yangu kuiasha kule bar, sikuwa na akili kwa wakati ule sasa nilipokosa pesa kichwa kikaanza kuuma
"Samahani kaka naomba nikuchukulie pesa ndani nakuja unanidai shilingi ngapi?
"Elfu kumi na tano" alijibu.
"Samahani kwa usumbufu nakuja"
Niliingia ndani kwasababu ulikuwa ni muda wa kuona wagonjwa pia, nilikuta watu pale kwenye bench sikuwasalimia nikapitiliza mpka reception nikaongea na yule dada akaniambia wamepokea wagonjwa saa mbili iliyopita hivyo nirudi kusubiri majibu ya daktari. Nilirejea pale nikiwa hoi nilitamani kuingia ndani lakini nilishindwa ikabidi nikae pale lakini niliona aibu sana maana nilipita bila kusalimia. Nilisalimia na kuketi nisubiri daktari aje pale.
Nilipitiwa na usingizi kidogo nikuja kushtuka sikuwaona yule kaka na mmama nikajua wameingia kwa dokta na mimi nilinyanyuka nikaenda kule kwa dokta sikugonga niliingia tu. Nikakuta mazungumzo nami niliketi kusikiliza.
"Mwanamke ameumia sana kifuani hivyo sasa ameamishiwa icu, ila mwanaume anaendelea vizuri na matibabu nadhani baada ya muda tutawapa taarifa hali inaendeleaje"
"Mama yangu yupo wapi dokta namtaka mama yangu" nilianza kulia pale.
"Pole dada pole" alininyanyua yule kaka na tukawa tunatoka nje ghafla akatokea dereva wa bodaboda. Alikuwa amekasirika mno
"Dada nataka pesa yangu tafadhari naona sio mstaarabu wewe" aliongea kwa hasira na mimi sikuwa na pesa
"Kakaa sina pesa hela zote nimeasha tcc kule kaka yangu naomba nivumilie nimpigie rafiki yangu anitumie pesa"
"Akutumie pesa! Wewe dada vipi umesema vitu vyako umeasha uko atakutumia kwenye mikono dada usinitibue naomba hela yangu" alizidi kufoka
"Unadai kiasi gani kaka" aliuliza yule mkaka aliyenisaidia tulipokuwa chumba cha dokta nikaona wanatoka pembeni mimi nikabaki na yule mama akiyekuwa na yule kijana.
"Pole mdogo wangu love ni nani yako? Aliuliza yule mama
"Ni mama yangu"
"Kheee wewe kwa love mbona haifanani umri kama mmepishana ni miaka 8 si chini ya hapo"
"Ndio ni mama yangu mdogo ila roho inaniuma akiniacha peke yangu".
*******"""""""********
Nilimtazama mama mdogo alikuwa yupo hoi sana nilitamani kulia kwa maneno aliyokuwa anaongea maana alionyesha kukata tamaa na maisha.
" emmy mwanangu, mdogo wangu, rafiki yangu nakupenda emmy" aliongea huku machozi yakimtoka
"Nakupnda pia mama naomba usilie"
"Emmy kuna siri kubwa ambayo sikuwai kukwambia juu ya mama yako, na naomba nisamehe mwanangu niliyokufanyia najua nimekuumiza sana"
"Hapana mama hayo yamepita naomba yapite mama tujadili hali yako mama"
Nilipatwa na haja ndogo ikabidi nitoke kwenye msalani maana nilivumilia kwa muda mrefu.
Nilimaliza na kurejea sikuamini nilimkuta mama mdogo ameanguka chini alipojitahidi kujigeuza nilitoa kelele za nguvu nesiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!
Nilitazama chini sikuamini mama alikuwa anaanguka damu ikimtoka nilishindwa kuvumilia nikapiga kelele nesiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!.
Nilitapatapa nataka kwenda nje mara nirudi ndani nilikosa maamuzi mara ghafla cindy akaingia na nesi wakaja kunisaidia kumnyanyua mamdogo kumrudisha kitandani.
"Nesi imekuwaje mgonjwa kaanguka jamani? Aliuliza cindy
" mimi sikuwa zamu humu dada sijui ila kitandani hakikuwekwa vizuri"
"Huu ni uzembe kazi yenu ni nini sasa sisi tunalipia pesa hapa na hii hospitali ya serikali ila gharama zipo juu na bado huduma mbovu huyo dokta yuko wapi? Alikasirika sana cindy nikamvuta mkono
" hapana cindy acha" nilimzuia huku machozi yakinitoka
"Watazoea hawa emmy subiri"
Alinitoka na kuondoka nikabaki pale na mgonjwa akitapatapa na mikono alikuwa anairusha uku damu zikiendelea kumtoka nilipata hofu maana nilipokuwa namuita aliitikia "mmmmh" bila kuongea lolote, nesi nae alitoka nyuma ya cindy. Nilitoa kanga yangu na kumuwekea kichwani kupunguza damu isienee mwilini mwake. Hapo ndipo dokta na cindy wakaingia.
"Ona dokta hiki nini kiukweli hapana siwezi hivi dokta huduma zenu ovyo bora tumpeleke private tu" aliongea cindy kwa hasira.
"Tusamehe bure dada tatizo wagonjwa wengi wahudumu wachache tuvumiliane dada tutagharamia huduma hiyo dada usijari" aliongea dokta akasogea na kumpima macho na kumuagiza nesi amsafishe na kumfunga vidonda wakiendelea kuangalia hali yake.
Niliendelea kulia tu cindy akanichukua mpka nje na kunipa vitu vyangu ambavyo niliviacha kule tcc chang'ombe.
Alijitahidi kunipa moyo akanibembeleza pale kisha akaniomba nisubiri kidogo akaingia ndani sijui alifata nini ila takribani dakika tano zilipita nikiwa pale ndani ya gari yangu, nilifungua pochi yangu sikuamini kukuta pesa yote ipo kama ilivyo nikajua pale ni waaminifu sio rahisi kukutunzia mali yako.
"Emmy ebu twende tukatembee kidogo tutarudi mgonjwa wanamshugulikia sawa dear? Aliongea cindy polite
" isiwe mbali cindy nina shida na mama jamani"
**********"""
Sikujua chochote juu ya kilichotokea nyuma lakini cindy ndiye alikuwa anafatilia mambo yote kule ndani hospitali, kumbe mama alikuwa na hali mbaya akaamishiwa chumba mahututi/icu mimi sikujua hilo mpka alipokuja kunieleza.
"Emmy unajua toka muda ule mchana hali ya mama ilikiwa mbaya akaamishiwa ICU lakini sasa hivi wanasema hali yake ni nzuri kidogo, ila wale ndugu zake yule mwanaume ambaye naye alipata ajari wamesema mgonjwa wao ataruhusiwa saa tatu hii" aliongea cindy
"Wacha waende wameshamtoa mama yangu kafara mimi nataka nikamuone mama yangu"
"Mmh cindy usiende kwanxa" alikataa cindy
"Cindy mbona unanikataxa hapana naenda kumuona mama yangu"
Nilinyanyuka na kuanza kuelekea ndani, huku nyuma cindy naye alikuwa ananifata kwa nyuma, niliingia kule ndani nikakutana na nesi akanizuia "samahan dada muda umeisha" nilijaribu kumuomba sana hata kwa dakika tano tu niingie. Kutoka na kulia kwangu akanionea huruma na kuniruhusu kuingia nilinyanyua macho yangu kutazama vitanda pale moja kwa moja jiccho litamuona mama mdogo.
Nilisogea taratibu nikashika mkono wake eeeeh mungu wangu mkono ulikuwa wa baridi na ulioregea kabisa
Nililia "cindy cindy njoooo nisaidie mama kapatwa na nini huyu jamani mbona hivi lakini??
Sikujua kama mama yu hai pale au amekufa, nilitamani iwe ni ndoto alafu niamke nikute kila kitu kipo sawa maana ktk dunia sijawahi kuwa na ndugu mwingine ila huyu tu, machozi yalinitoka mithiri ya matone ya mvua nilinyong'onyea mwili yote na kukaa chini kabisa "kama nisingejiingiza kwenye mahusiano na bonge yasingenikuta haya tamaa mbaya jamani tamaa inaua haya mama nawe ni kwanini uliingia uko sasa? Unajua mwanao nipo nae nawe unaingia uko, haya ulisema utaniambia ukweli sasa mbona umeondoka bila kusema ukweli? Sawa bwana sawa tu" niliongea kwa machoz nikiwa chini uku nimeshika mwili wa mama mdgo.
Laiti kama mungu angewapa wafu nafasi ya pili ya kuishi duniani uenda wengibadilisha maisha yao nikikumbuka naumia sana mamdogo wangu amepotea kama choz la samaki baharini, ameyayuka kama moshi angani sitomuona tena sitamgusa tena, wala kuzungumza nae tena. Niliwaza mbali saana hata sijui ila ghafla nilianza kuhisi maumivu makali ya kichwa nikaanza kuita tu majina ya watu pale mara nesi mara cindy mara mamdogo love sikujitambua kabisa.
*************
"Emmy! Emmy! Amka basi ule hata kidogo" sauti nyembamba ilipenya kweny ngoma ya masikio yangu
Nilifumbua macho na kutazama nikajikuta napata nguvu nikajivuta na kukaa, alikuwa ni cindy hata hivyo alikuwa na rafiki wengine tunaosoma nao chuo pale udsm. Wote kwa pamoja walisema "eehe pole sana emmy"
"Asante lakini kawaida tu" nilijibu kisha nikatulia.
Moyoni najiuliza sasa "ina mana ni nini kimetokea mbonaa niko hapa na hawa wamekuja kwa ajiri yangu ina maana naumwa au? Niliendelea kujiuliza hapohapo nikashtushwa tena
" mmh emmy kunywa basi hata kidgo uji" aliongea cindy kwa kunibembeleza
"Cindy bhana ninywe uji wa nini? Unajua nasikia njaa nileteeni hata chipsi kuku nina njaa cindy" niliongea kwa kujiamini kitendo kilichowashangaza wote pale.
"Eheee mungu mwema rose nenda kafate chipsi basi" aliongea cindy
"Cindy kwani nilikuwa naumwa nini? Niliuliza maana sikuwa na kumbukumbu zozote
" mamie nitakweleza baadae ngoja ule kwanza"
"Chakula si bado tunaweza kuendelea kupiga tu story" nilizungumza
"Haaa sawa ila... Mmh... Eeh .. Emmy aah.. Unajua" aliongea cindy kwa kujibaraguza tayari nikaanza kuvuta kumbukumbu nyuma nini kilitokea,
Nilimkumbuka sam kwa harakaharaka nikawaza sana, nikashindwa kuuliza maana pale hakuna anajua details zake nikabaki nawaza kimenitokea nini?
MWISHO
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com