SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Maisha yaliendelea na nakumbuka siku hiyo flaviana pacha wake flavian ambae ni shem wangu alikuwa amemaliza masomo yake kenya akawa amerejea tanzania baada ya kukaa siku mbili akanipigia simu kuwa anakuja kututembelea kwani akujua kuwa dada yake hayupo pale nyumbani.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikamuelekeza funguo zilipo na kumuahidi baada ya nusu saa nitakuwa nimerejea.
Mishale kama ya saa kumi nilirejea pale home na kumkuta flaviana anaangalia cd za bongo movie aliponiona alinirukia kwa furaha maana mara ya mwisho tulionana siku ya ndoa yangu na dada yake. Tulipiga story pale nikamletea kinywaji tukawa tunakunywa pale.
"vipi dada yupo chuo au"
"dada yako bwana we acha tu"
"amekuaje tena?"
Kabla sijamjibu aliingia ndani wala akushtuka kama pale kulikuwa na watu akapitiliza hadi chumbani.
"shem nini kinaendelea?"
"yani hata sijui nikwambie nini"
Wakati huo alitoka na beg lake la nguo akawa anaburuza huku ameshika viatu vyake vya kuchongoka skuna. Nilikimbia na kumzuia asiondoke tukawa kama tunapambana akanipiga na skuna ya kichwa na damu zikanitoka palepale nikadondoka na kupoteza fahamu yeye akatokomea anapopajua yeye.
Hakuna nilichokijua baada ya pale kwani nilikuwa nimepoteza fahamu kabisa.
Takribani wiki nzima sikuweza kupata afuheni kwani nilipoteza damu nyingi na hata hivyo nilipata mshtuko mkubwa kwenye kichwa niliitaji kuchangiwa damu na pia gharama za matibabu niwapo pale hospitali sikuweza kuyajua haya yote mpaka niliposimuliwa hapo baadae.
Nakumbuka kuna mzee anaishi jirani na ninapokaa ndiye aliyetoa gharama za matibabu akiangaika na shem wangu flaviana muda wote huo flavian akukanyaga pale hospitali hata mama mkwe pia hakukanyaga japo walikuwa na taarifa zote. Watakuja kufanya nini kwangu mimi fukara nisiye na nyuma wala mbele ni flaviana ndo alikuwa na moyo wa upendo.
***
Ilikuwa ni jumatano jioni ndipo nilipopata nafuu na kumbukumbu zikanilejea na mbele ya macho yangu alikuwepo flaviana, mzee yasin na mchungaji. Niliona kichwa kizito sana na ikabidi niulize.
"kwani nimekuaje jamani mpaka mmekuja kuniona?"
Wote walitabasamu na baba mchungaji akaongea maneno haya "ooh haleluya achukuliwe mungu kwa kukupa uzima ooh asante mungu"
Yale maneno yalinifanya niamini kuwa kweli nilikuwa ni mgonjwa niliposhika kichwa nikajikuta nina bandage kubwa kichwani nilitamani kulia na kumbukumbu zikanilejea mpaka siku ile nilipogombana na flavian mke wangu nikaanza kulia baada ya kuambiwa ajakanyaga pale hospitali toka nimeumwa. Daktari aliingia na kunikuta nalia.
"jamani msimwambie kitu chochote kibaya huyo apaswi kulia akilia itamletea maumivu makali ya kichwa ebu muacheni apumzike basi"
Wote walitoka nje na kuniasha mimi na daktari. Alinibadilisha dripu na kunichoma sindano nikalala baada ya dakika mbili.
Nilikuja kupata nafuu baada ya kuamka kwa mara ya pili na hapo nilimuona flaviana akiwepo pale tena nikajifikiria kwani huyu ana moyo gani?
"flaviana shemeji wangu nashukuru sana, umeonyesha upendo mkubwa sana kwangu"
"usijali shem wangu hilo ndo jukumu langu amka basi ule leo nimekuletea ndizi nyama"
"asante sana naamini huyo atakaye kuoa wewe atakuwa amepata mke bora kuwahi kutokea ila usije kubadilika ukawa kama dada yako"
"hapana shem siwezi badilika mimi hapa unaponiona nimepitia maisha yote unayoyajua wewe mpaka nimeamua kuokoka nimetoka mbali sana"
Mara nesi akaingia na kumkuta flavian akiosha kijiko na kunilisha
"dada wewe unakula kweli maana unapaswa kula sana mboga za majani na juice uongeze damu si unajua umetoa damu nyingi nawe unatakiwa kupata muda mwingi wa kupumzika ebu jaribu kuongea na ndugu zako wengine waje kukaa na mgonjwa wewe nawe ukapumzike maana kutwa kucha upo hapa"
"sawa nesi nimekuelewa"
Nilipata picha nzima kumbe flaviana amenitolea damu mimi na kumbe amekuwa anakb na mimi muda wote, nilimuona ni mtu wa kipekee kwangu tena sana.
Baada ya kupata nafuu niliruhusiwa kutoka hospital na mzee yasin ndo alikuja kunifata na gari lake pale hospitali wakati nataka kupanda niliona gari aina ya nissan murano ikiingia na palepale akatoka mke wangu akiwa amependeza sana ndani aliongozana mwanaume mnene mwenye pesa zake. Nilipata mshtuko mkubwa.
Nilimtazama mke wangu flavian akishuka kwenye gari aina ya nissan murano na ndani kulikuwa na mwanaume mnene mwenye pesa zake. Nilimuona flavian jinsi alivyopendeza sana akawa anakuja kwenye lile gari nililokuwepo.
SONGA NAYO.
Nilipatwa na uchungu baada ya kuona mke wangu anachukuliwa tena mbele ya mwanaume mwenzangu nilitoka na kumfata vile vile nikiwa na bandage yangu kichwani.
"kaka nakuomba shuka mara moja tuongee kiume"
"we mark unataka kunitibua ebu rudi kwenye gari" alinijia flavian
"ebu niache wewe niongee na mwanaume mwenzangu"
"mwanaume mwenzako umemjulia wapi? Ebu toka hapa"
"niache nakwambia niache"
Nilimsukuma akadöndoka huku chini maana nilikuwa na hasira nae pia kwani yeye ndio chanzo cha yale yote. Nilifungua mlango na kumtoa yule jamaa na mtumbo wake nikamvuta hadi nikiwa na hasira sana.
"kaka wewe ni mwanaume mwenzangu na unajua uchungu wa mwanamke kweli unanifanyia hivi mimi na unajua huyu ni mke wa mtu tena mke wa ndoa?"
"hapana kaka me sikujua kama ni mke wako nisamehe sana nakuahidi nitakuachia mke wako"
Niliondoka na kupanda ndani ya gari nikawa nataka kuondoka mara flavian akanifata na kusimamisha gari nikafungua kioo kumruhusu aongee.
"mark kweli umenisukuma mimi na umeamua kuniharibia sasa kwako sitarudi na kamwe usijisumbue hata kufikiria kama una mke kama mimi pete yako hiyo hapo sikutaki pumbafu"
"sawa mimi pumbafu kisa nimekusukuma wewe uliyenisababishia majeraha? Sasa hata mimi nimechoka pia na nipo tayari twende kanisani tukavunje ndoa yetu"
"sawa kesho nitakupigia twende kanisani kwaajiri ya kuvunja hiyo ndoa"
Niliachana nae nikaenda zangu nikiwa na flaviana shem wangu nae alichangb kwa jinsi dada yake alivyobadilika lakini mimi nikamwambia "hata mimi sikutarajia kuwa atabadilika lakini ndo ameshabadilika sio flavian yule mke wangu wala yule dada yako huyu ni mwingine kabisa ila tumuombee atabadilika lakini mimi nimechoka na manyanyaso"
Tulifika nyumbani nikiwa nipo huru kwani moyoni mawazo ya flavian yalinitoka kabisa hata sikumpa nafasi tena na akili yangu iliwaza maisha kabisa.
Ilikuwa ni hatua ndefu sana kuvunja ndoa ile lakini tulifanikiwa na mimi na flavian hatukuwa mke na mume tena nilimpa kilicho chake na pia nikaanza mipango yangu na mara zote nilikuwa naongea na flaviana shemeji yangu aliyekuwa ni mwenye upendo kwangu na tokea nilipokuwa naumwa na kamwe sikuweza kumdharau wala kuonyesha kuna kitu kilitokea na dada yake. Sikutaka kujua maisha flavian kwani yangenifanya nimkumbuke na nitamani kuwa nae kitu ambacho sikukipenda kabisa.
Niliendelea na kazi yangu ya kujichikiza nikiangalia kama kuna uwezekano wa kupata kazi sehemu nyingine. Ilikuwa ni ijumaa moja mtoto mmoja wa kike alikuja na baba yake akiwa kwenye gari akaniita.
"mwalimu mark nakuomba mara moja samahani" aliniita yule mzee
"bila samahani mzee shikamoo"
"marakhaba pole na kazi lakini nikuja hapa kwa lengo moja, binti yangu amekuwa akipenda kusoma hapa na sasa anaingia kidato cha nne nakuomba sana umsaidie kwenye masomo ya biashara maana ameniambia unafundisha vizuri sana mimi nipo tayari kukulipa kwa kiasi unachotaka"
Nilijisikia vizuri kupata ile nafasi hata hivyo sikujua niseme nini maana kwangu ilikuwa ni bahati iliyoje. Nilikubaliana bei na yule mzee niwe namfundisha mwanae kila jioni na kesho yake ndo ilikuwa nianze kazi.
***
Siku ya tatu toka nianze Kazi ya kumfundisha jesca yule mzee alikuja na kuanza kuniuliza baadhi ya mambo baada ya kuzoeleka na kuwa moja kati ya wanafamilia.
"mwalimu hivi unafundisha shule gani?"
"dah mzee mimi sijasomea ualimu kabisa ila nimesomea accountancy/akaunti"
"eh bwana mbona unafundisha kama mwalimu kabisa sasa mbna ufanyi kazi ya professional yako/kazi ya taaluma?"
"shida tu mzee ndio maana unaniona hivi"
"mimi nitakusaidia ebu kesho niletee vyeti vyako"
Nilitoka pale nikiwa mwenye furaha sana na nilijua fika wakati wa mungu kunibariki umefika baada ya mimi kupitia wakati mgumu baada ya kufukuzwa kazi.
Nilifika nyumbani na kuanza kazi ya kutafuta vyeti vyangu mahali nilipoviweka nilifanya kazi hiyo kwa saa nzima nikakumbuka vyeti vyangu na vyeti vya flavian vilikuwa pamoja palepale nikampigia simu flaviana.
"hallo shem naomba unisaidie kuangalia vyeti vyangu kwenye vitu vya flavian"
"mmh sijui kama vyeti vyake ameviweka humu ndani ngoja nikutafutie shem wangu"
Niliketi pale nikingoja ripoti kutoka kwa flaviana, ulikuwa usiku wa saa nne simu yake ikaingia na kunifanya nipagawe na taarifa nitakazopewa nikapokea simu.
"uwiiii! Nimeshoka kweli wangu, yani hvyo vyeti nimekuja kuvipata chumbani kwa mamdogo"
"nashukuru sana kwa kuvipata flaviana maisha yangu yatabadilika muda si mrefu ooh asante mungu"
kesho yake palipokucha nilioga vizuri nikaweka kila kitu sawa nikaingia kazini na kuanza kufanya kazi yangu ya kufundisha watoto.
Ile jioni nilimkabidhi yule mzee vyeti vyangu palepale akampigia simu sijui meneja gani wa bank na kumueleza kuwa kijana mwenyewe anazo quality zote za kuajiri hata akiwa na haja na interview nikawa nashangilia moyoni na kumrudishia mungu sifa na utukufu maana hakuna sehemu ningeweza kupata kazi kirahisi namna ile tena kumbe kazi yenyewe na mhasibu mkuu msaidizi kwenye bank stanbic bank ilikuwa ni kitu ambacho sikukifikiria katika maisha yangu tena jiji la arusha sehemu ambayo niliiota kuwa siku moja nikaweke makazi yangu.
***
*upande wa flavian*
Maskini mimi flavian maisha yangu yalianza kuwa magumu bada ya kumdanganya derick kuwa sijaolewa na Leo amegundua ukweli achana na hilo nimemvumilia mengi sana kwani ana wanawake wengi sana huko nje na wengne nimewahi kumfuma nao lakini sina ubavu wa kumuasha kwani itakuwa fedheha kwangu kwani mark nimeachana nae na huyu tena nitaonekana mimi ndo nina matatizo. Ila kuna siku uvumilivu ulinishinda ni baada ya kumkuta ametembea na msichana wa kazi ilikuwa ni kitendo cha aibu kumwambia ukweli ikawa tatizo alinipiga na kunichania nguo nilizovaa.
"derick kweli unathubutu kunipiga kwa kosa ulilofanya wewe me naondoka derick naondoka"
"we mpumbuv ondoka tu hapa penyewe unazibia nafasi malaya tu wewe na ndio maana mwanaume wako amekushindwa nitakuweza mimi tena nilishndwa nitakufukuza kwa kosa gani kwani mke wangu na watoto wanatoka durban wanakuja wiki ijayo bora uondoke na unirudishie gari langu mchenzi hauna adabu unanijia juu mimi"
"nipo chini ya miguu yako derick nisamehe nitachekwa mwenzio sina msahada mwengne derick na hata hvyo sikujua kuwa umeoa kama ningejua nisingekubali"
"ndo umejua ondoka me nilikuwa nakupima kama unamsimamo nimegundua hata nikiwa na wwe siku nikishoka utanikimbia nakuomba toka"
"derick nakuchukia wewe mwanaume kwani umenìharibia maisha me naondoka ila mungu atanilipia"
"hahaha fungu la kukosa wa kupenda vya dezo, alafu nakusihi nenda kapime afya na ufate ushauri wa daktari kama mimi mwenzio natumia vidonge vya arv sina wasiwasi"
"haina aja ya kushuku mara zote tumekuwa tukifanya mapenzi bila kinga nahisi inaweza kuwa tatizo hapo baadae"
"toka huko mwanaume we mnafki yani nakuchukia kama shetani kweli umeniambukiza ukimwi"
Niliondoka pale nikiwa nimechanganyikiwa nilifika balabalani hata nikakuta watu wakisubiri kuvuka mimi nilitamani kuwa nikajikuta navuka ghafla bajaj ikanigonga mgongoni palepale nikapoteza fahamu sikujua kilichotokea baada ya hapo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com