TWIN SISTERS (9)

0
Mwandishi: Michael Mejah

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Niliondoka pale nikiwa nimechanganyikiwa nilifika balabalani hata nikakuta watu wakisubiri kuvuka mimi nilitamani kuwa nikajikuta navuka ghafla bajaj ikanigonga mgongoni palepale nikapoteza fahamu sikujua kilichotokea baada ya hapo.

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Nilikuja kujikuta nipo hospitali ya moe nikawa nataka kunyanyuka nikashindwa mbele yangu alikuwa mama nikamuomba anisaidie kunikarisha nae akafanya hivyo nikaketi lakini nilikuwa sijielewi kuanzia mgongoni hapa mpaka chini. Mara akaingia daktari.

"mama nadhani kama nilivyokwambia wewe nenda kakamilishe malipo na mtoto wako kisha uchukue wilchair/kiti cha walemavu"

"sawa dokta nimekuelewa"

"mama ina maana nimekuwa mlemavu?"

"hapana mwanangu umepalalaizi ila nitaongea na baba yako utaenda kutibiwa india usijari"

"hapana mama msipoteze hela kwa ajiri yangu mimi wa kufa tu hapa nilipöina ukimwi na tena mlemavu sistahili kuishi mama nimemkosea sana mungu sistahili kuishi laiti ningejua ningetulia na mume wangu mark nimeamini majuto ni mjukuu naombeni mtafuteni mark nimuombe msamaha kabla sijafa"

"we flavian usiseme hvyo ebu"

"mama ni lazima nisime ninapaswa nitubu ili nikifa mungu anipokee"
***

*Upande wa mark*

Maisha yalikuwa mazuri nilikuwa mhasibu kwenye bank ya NBC nilipewa nyumba na gari la kutembelea na niliishi njiro mji wa arusha.

Flaviana alikuwa mtu wa karibu kwangu na taratibu tulijikuta tukiwa wapenzi na mara zote tulikuwa tunaongea mara kwa mara akiniuliza umekula, umeamka, umetoka kazini, unafanya nini now? Haya yalikuwa maswali yake kila siku ila leo nilishangaa toka aliponisalimia asubuh akuweza kunijulia hali tena mpaka nilipompigia.

"hello honey leo mbona kimya sana unaumwa au?"

"hapana! matatizo mpenzi sema siwezi kukwambia ulisema uhitaji kujua"

"hapana mpenzi niambie"

"dada flavian ameashana na yule mwanaume na amemuambukiza ukimwi na hakapata ajali iliyopelekea kupalalaizi hapa alipo anataka uje akuombe msamaha"

"dah masikini mimi nilijua hayo yatampata ndo wanaume wa mjini lakini mungu atasaidia nitakuja wikiendi hii na kama nitakuvisha pete ya uchumba kabisa"

"mpenzi mama ataki unioe"

"amesema kwanini ataki nikuoe?"

"eti nitaitia familia yetu mikosi kwanza eti wewe maskini una nyuma wala mbele pili wewe ndo umepelekea hata flavian amepelalaizi yani anakuchukia sana lakini mimi nimemwambia ukweli kuwa sitakuacha kamwe"

"sasa huo mtihani sema nitakuwa wikiendi hii nijue mbivu na mbichi"

"hapo itakuwa vyema baby i should wait for you/nitakusubiri wewe"

"okey baby usiku mwema"
******

Sikuamini kama itafikia siku nitakuwa mzigo kwa familia kama nilivyo leo hata sioni raha ya kuishi maisha yamebadilika na kunifanya nikumbuke enzi zile ambazo nilikuwa na msimamo haswa mwanaume akuweza kunichezea kama alivyoniraghai lile janaume na kunisababishia matatizo makubwa namna hii nalia na moyo wangu.

Mama alinibadilikia hakuwa yule tena alikuwa mbogo kwangu kuna wakati alinipa kazi ngumu za kumfulia, kupika na kuosha vyombo wakati anajua nina matatizo ya kupalalaizi kwanzia huku chini, namshukuru pacha wangu flaviana ndo Amekuwa msahada mkubwa mkubwa kwangu hasa ninaposhndwa unilisha na kunipeleka chooni na kuniogosha mara zote nilipohtaji msahada kutoka kwake. Sikuwa flavian wa kugombaniwa na wanaume tena ule urembo wote ulipotea nilikuwa kama kituko hata muda mwingne mama kama ana wageni wake ataki mimi nitoke pale sittingroom/sebureni anahisi nitamchafulia mambo yake sijui?

"flavian mdogo wangu nasikia umepata mchumba anataka kukuvalisha pete"

"aah ahapana dada bado bado ila ikiwa tayari atakuja tu"

"mbona kigugumizi flaviana au upendi dada yako nijue mambo yako ya ndani sana?"

"hapana dada we ni dada yangu unapaswa sana dada ila wakati ukiwadia nitakwambia usijari"

"sawa mdogo wangu ila jitahidi utulie usije kufanya kama mimi nilivyomtendea mark wa watu matokeo yake napatwa na matatizo haya nakuomba mdogo wangu"

"saaawa daada nimekuelewa"

Nilishndwa kuelewa ni kwanini flaviana alikuwa anapatwa na kigugumizi lakini nikayaasha yale nikawa namtazama tu akicheza game kwenye laptop aliyotoka nayo shule kenya.

"hvi sista flavi bado unampenda mark?"

"khee wee flaviana umefikiria nini mpaka unaniuliza swali kama hilo?"

"nataka kujua dada"

"ndio nampenda xana sema sina nafas tena ndani ya moyo wake hasa kwa yale niliyomfanyia isitoshe hata akitaka turudiane haitawezekana leo mimi mremavu na tena nina ukimwi siwezi kuwa flavian yule tena labda mungu aniumbe tena"

"dada jamani unanitia huruma jamani mpaka natamani kulia hata sielewi nifanyaje"

"flaviana flaviana flaviana nini tena"

Flaviana aliongea yale maneno huku anatokwa na machozi akatoka na kukimbilia nje. Nilipoona ile hali na mimi nikaendesha kigari changu kuelekea alipo lakini wakati natoka nilisahau kama pale sebureni nilikatazwa nisikanyage mimi nikaenda nilipoinua macho nilimuona mark akiwa na rafiki zake nilishtuka sana nikaburuza kiti kwa mbele kumbe pale kuna ngazi nikajisahau na kuanguka vibaya nikaangukia mikono na kichwa.

"mama mama mama mama dada flavian ameanguka"

"mpumbav huyu nilimkataza hakutaka kusikia yeye anajijua ana matatizo lakini bado anatusumbua yani sijui nimtupie nani huu mzigo"

Roho iliniuma sana japokuwa flavian niliashana nae lakini yale maneno ya mama yake yaliumiza sana. Tulienda kumnyanyua na kichwani alikuwa anavuja damu na muda ule alikuwa uncouscious/ametoza fahamu.

Kufika hospitali walimpeleka chumba maalumu cha wagonjwa mahututi maana hata pumzi ilianza kuisha, muda wote flaviana analia sana maana flavian ni pacha wake kabisa na kama ujuavyo mapacha wanauguaga sana mateso ya mmojawapo ndo alivyokuwa flaviana nilikuwa nambembeleza atulie mara zote lakini yeye anajua dada yake amekufa.

Kama kunakipindi flaviana nilimshuhudia akilia ni leo na muda wote nilikuwa nikimnyamazisha ananyamaza lakini akikumbuka tu anaendelea kulia nilipata shida sana nilipumzika aliposinzia kwenye mapaja yangu.

Mama alikwenda pembeni na kumpigia mume wake aliyepo nairobi akamwambia kila kitu na kumjaza maneno ya uongo kuwa mimi ndie chanzo na nimekuja kuivuruga familia yao. Mzee aliongea maneno makali juu yangu na la mwisho nilisikia akisema "mwambie asiniletee upumbav nitamtwaga risasi" niliyasikia maneno yote japokuwa nilijifanya kama sijui kitu kumbe masikio yangu yanasikia mbali sana. Mama alipomaliza alikuja pale akiwa anatabasamu lakini nilishajua ni la kinafki.

"khee huyo amelia wee mpaka kapitiwa na usingzi"

"yeah unajua tena hana uchungu na dada yake"

"yani hapa nimechoka kweli nasubiri taarifa za dokta niende nikalale zangu maana"

"ni kweli"

Nilijikuta namuitikia ili mradi tu lakini moyoni mwangu nilishamjua vizuri yule mama ni mtu wa aina gani.
***

Flavian alipata nafuu akiwa na bandage kichwani alitoka hospital nikampakia kwenye gari kumrudisha nyumbani muda wote huo flavian alikuwa anaongea mwenyewe nikajua tayari atakuwa kachanganyikiwa maana alianguka vibaya na isitoshe alikuwa ameshapalalaizi na yale mawazo ya kuashwa na mwanaume na mimi kuwa na mdogo wake yalimchanganya sana kweli mapenzi yanaua na yanauisha.

Tulimlaza kwenye sofa akawa amepumzika na sisi tukawa tunaongea mawili matatu mara mlango ukafunguliwa nikaona miwani ya macho khee mara mwili wote alikuwa ni baba mkwe aliyekuwa na nyuso ya hasira na jazba kama mbogo aliyejeruhiwa, nilitamani kukimbia lakini nisiwe.

"nilikuwa hospital kumbe tumepishana nyie mmeshafika nyumbani"

"ndio dokta alimruhusu" alijibu mama mkwe

"khee kabla sijasahau, hivi wewe kijana unaitafutia nini familia yangu? Sasa leo utanijua mimi ni mtu wa aina gani"

Mzee alitoa bastora na kunielekezea mimi wakati huo nilikuwa nimekaa kiti kimoja na flaviana mkojo ulianza kunitelemka kwa kasi ya ajabu.

Nilitetemeka na mkojo ukaanza kunitoka sikuamini kama mzee anaweza kuniönyeshea silaha ya moto na kwa pale nilivyokuwa sikuweza hata kujitingisha hata kidole.

"dady please don't commit adultery he is innocent men/baba tafadhari usiue huyo hana hatia"

"wewe flavian unanijua vizuri huwa sipendi kuingiliwa kwenye mambo yangu sasa wewe sogea nitakuamishia wewe ili balaa pumbav"

"lakini baba subiri nikwambie ilivyokuwa itakuwa mama ajakwambia, mimi ndio nimekosea baba na mungu ameamua kunipa pigo hili unaloliona mimi sikuzaliwa na tabia hizi kweli nimeamini ule usemi asiyefunzwa na mamae ufuzwa na ulimwengu baba ulimwengu umenifunza kamwe sitakuja kusahau mpaka naingia kaburini"

"flavian ebu nieleze nini kilitokea?"

"dady wakati fulani mark alifungwa kutoka na wizi uliotokea kwenye kitengo chao na mimi nilijaribu kila njia kumtoa ikashindikana nikaenda kumueleza mama nae akaniambia mimi ni mtoto wa kike inabidh nijue kutafuta pesa kwa namna yeyote ile kwani yeye ataweza kunilisha mimi na mume wangu mark kama vile yeye ametulazimisha tuoane, nilishanganyikiwa nikaondoka wakati nipo chuo bwana mmoja alinifata na kuja kunishawishi atimae akanibaka na huyo ndo chanzo cha haya yote kwani nilivunja ndoa na mark kumbe na yeye alikuwa ameoa tayari akaja akanisaliti ndo niliposhanganyikiwa na kupata ulemavu huu yani najuta kwanini nilikuwa na tamaa namna hile"

"mama flavi unaona haya hivi flavian angekuwa mwanao wa kumzaa ungemfanyia ulivyofanya au kwasababu ni watoto wa kaka yangu wewe hawakuhusu, ni mara ngapi nimetuma hela kwaajiri ya flavian na mwenzie? Me nakuomba ondoka niachie familia yangu"

"hapana dady mama asiondoke huyu ndo mlezi wetu kama angekuwa mtu mbaya usingetukuta tulivyo sasa, me ninachoomba tujadili ndoa ya flaviana na mark itakavyokuwa haya yameshaisha sasa majuto ni mjukuu hakuna lenye mwanzo lisilo na mwisho mama na baba"
***

Nilifurahi sana kukubaliwa kumuoa flaviana na hiyo yote ni kwa juhudi za flavian mzee alishakataa katakata kuwa haiwezekani mwanaume mmoja amuoe mtu na dada yake lakini mwisho alikubali na harakati za ndoa zikaanza na ndoa ilipaswa kufungwa nairobi kenya anapoishi mzee kikazi na hata mimi nilipata michango karibu mil11.4 niliyoipata kutoka kwa marafiki zangu kule kazini na hata mabosi na wafanyakazi wenzangu ni kumbukumbu nzuri sana katika maisha.
***

Siku ya ndoa iliwadia na ukumbi wa kanisa ulifurika watu mpaka nje wapo rafiki wa mzee na marafiki zangu kutoka arusha nilifurahi sana ila wakati tunafunga ndoa kumbe huku nyuma flavian alitoka nje kama anaenda chooni akatafuta sehemu tulivu akajifungia na kutoa sumu ya panya kwenye pochi yake akanywa na kupoteza maisha. Huku ukumbini sherehe ilipamba moto tulikunywa tukala sasa wakati uliposonga tukapata taarifa kuna mwili umekutwa chooni watu wote walitoa kilio hasa baada ya kumtambua alikuwa ni flavian.

Miezi mingi ilikatika baada ya ule msiba na mke wangu alikuwa amekaribia kujifungua lakini aligundulika ana kifafa cha uzazi, nilikuwa kama chizi kichwa kinauma kwani niliogopa kumpoteza mke wangu.

Ilikuwa jumapili jioni mei 23siku ambayo sitakuja kuisahau mke wangu aliyopoteza maisha na kuniashia katoto ka kike ambaye amenipa shda katika malezi yake ila kila ninapømuona huwa namkumbuka mama yake kwasasa yupo standard four lakini mungu amesema tushukuru kwa kila jambo. AMEN!!!

*KILA JAMBO NA WAKATI WAKE KUNA WAKATI WA KUZALIWA NA WAKATI WA KUFA JIANNDAE NA NYAKATI ZOTE*

MWISHO

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)