SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
Roho iliniuma mno machozi yalinitoka nikakumbuka jinsi nilivyokuwa nashindwa masomo ya arts kama histry alikuwa akinifundisha na kunipa mbinu za kufahuru hayo masomo maana mimi nilitilia sana mkazo masomo ya science yeye ndiye aliyebadilisha mindset yangu juu ya masomo haya.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Haikuwa kazi rahisi kusahau wema wake kwa familia na ushauri wake pia japo ametenda kwa ubaya mwishoni mwa maisha yake ila bado ni icon yangu the first born. Nilikumbuka vitabu vyake alivyonipa nikavikusanya vyote na madaftari yake "kupitia haya nitatimiza ndoto zangu promise you brother i will never let you down(nakuahidi kaka sitakuangusha)" nilibeba yale yote nikamuonyeshe dada clementina nilipofika pale sikumkuta mtu zaidi zile cd zilikuwa pale mezani
"Shangaziiiiiiiiiiii" niliita kwa nguvu nikiogopa uenda dada katoroka
"Abeeeeeeeee mwana weee njoo huku" alijibu shangazi
"Shangazi dada hayupo" niliongea huku macho yananitoka
"Aaha yupo chumbani kwake usijari, kama unahitaji kuongea naye kamgongee" alitoa ushauri wake shangazi
***************
Tulitazama kwa muda bila kuzungumza lolote nilimuona dada akitoka machozi na mimi machozi yalianza kunitoka nikamkubatia dada naye akanikumbatia tukawa tunalia wote, hapo ndio alipata fursa ya kutoa ya moyoni mwake.
"Clinford nimekata tamaa ya maisha najuta yaliyokwisha tokea, nilikuwa tayari kumsamehe clement maana hata mimi ni mchafu kuliko, lakini amekufa clement, clinford nimetembea na wewe, clement, mlinzi na kibaya zaidi baba mzazi nina laana ya mzazi ona sasa nimejiharibia hata kizazi sina tena mimi ni wakufa tu clinford"
"Noo cleme mungu ni mwenye rehema atakusamehe, usione watu wanatembea barabarani vifuani mwao wamebeba makubwa hayo madogo cha msingi kuomba rehema, kisha tuungane kuwauguza wazazi wetu naomba usiweke mawazo haya mabaya maana si ewewe ila shetani ndani yako yaepuke hayo"
*************
Niliumia nilipomuona mama yangu awezi kutembea tena alipararaizi upande wa kushoto roho iliniuma mno kwani mimi nilikuwa chanzo, tulimsukuma na kibaiskeli huku moyoni najishuhudia mengi ya kunihukumu, ila niliendelea kusukuma kile kibaiskeli mara nilisikia nesi wawili wanakuja kwa mwendo.
"Ni yule au* nesi mmoja aliuliza
" ndiyo huyo mvulana" alijibu mwingine
"Kaka samahani unaitwa na baba yako" alisema yule nesi wa kwanza.
*************
Kwa unyenyekevu mkubwa nilikaa chini kusiiliza maneno ya mzee.
"Mwanangu clinford nakuomba msamaha kwa yote yaliyotokea kweny familia yetu ila ni nyie kuwa hapo mlipo ni historia ndefu huko nyuma baba yenu nilikuwa sina kazi mjini zaidi ya kuangaika kwenye maofisi kutafuta kazo bila kupata ikawa siku moja nilipopata kazi hali haikuwa vile nilivyodhani.
Nilikuwa na kiu ya kuendelea kujua kuhusu maisha ya mzee ila kikohozi kilipunguza concentration/umakini wa kufatilia jambo lile nilichukua maji kwenye chupa nikampa baba akanywa angalau kikohozi kikatulia.
"Baada ya kuangaika zaidi ya miaka miwili bila kupata ajira nilikata tamaa nikaamua kuondoka dar na kurudi simiyu(sehemu aliyokuwa akiishi awali) hata huko sikujua naenda kufanya nini ila rafiki yangu niliyewahi kusoma naye tabora boys nilikutana naye kwenye msafara wa kukata tketi tazara, nilishangaa maana ni muda mrefu umepita toka tulipoachana kwa mara ya mwisho"
**********
JINSI ILIVYOKUWA..
"vipi ndugu yangu za siku nyingi? Aliongea Billy
" wouw! Ni muda sana bila uko wapi siku hizi? Sikujibu kile nilichoulizwa zaidi ya kuunganisha mazungumzo.
"Nipo na wizara ya ujenzi nafanya kazi kama injinia msaidizi katka miradi ya miundombinu ya barabara" aliongea billy kwa bwebwe.
"Oooh kweli mungu amtupi mja wake billy naomba nishike mkono usiniache ndugu yangu hapa unaponiona narudi simiyu nimetafuta kazi bila mafanikio yeyote"
Niliongea kwa masikitiko
"Kwa sasa nasafiri kikazi naelekea shinyanga wewe nenda nikirudi nitakutumia barua ya kuja kufanya kazi wakatu nimeshatengeneza nafasi sawa" aliongea billy kwa namna nilivyomtazama alikuwa ni tofauti na billy wa kipindi kile shule kwani alikuwa mjanja mjanja kipindi hiki ikabidi niitikie tu.
Tulibuku tiketi kabla ya kusafiri yeye billy alikata daraja la kwanza mimi kwakuwa sikuwa na fedha nilikata daraja la mwisho, tuliachana pale nikiwa sina imani kamq billy atanitafuta tena.
********
Maisha mwanza hayakuwa mazuri nilikuwa nafanya biashara ya kutengeneza bakoroboi na kuuza angalau nipate fedha ya kula.
Muda ulizidi kusonga sikupata barua kutoka kwa billy mpaka nikapoteza imani na hiyo kazi.
Maisha yalizidi kuwa magumu zaidi ilikuwa siku hiyo jioni sikufanikiwa kuuza koroboi hata moja ambayo nilikuwa nayapanga sokoni. Nilirejea nikiwa mnyonge maana kiasi cha fedha nilichokuwa nakipata ni kidogo mno nacho nilikihifadhi ili endapo nitahitajika nirudi mjini nisichelewe. Mambo yalizidi kuwa magumu kuna wakati nalala na njaa au kula hata mlo mmoja kwa siku ili mradi mambo yaende sawa.
Hali ya simiyu ilinishinda na ule ukimya wa billy ulinifanya nifikiri kurudi dar-es-salaam ili kama kazi nihisubiri hukohuko.
*********
Sikuwa na cha kula njiani ndani ya treni, hapa pembeni nilikuwa nimekaa na msichana mzuri aliyeonekana ametoka shule anarudi nyumbani. Muda wote tulikuwa kimya kwa ile safari toka imeanza. Siku hiyo jioni watu walikuwa wamelala kutokana na uchovu wa safari mimi sikupata usingizi kwani nilikuwa na mawazo kichwani kwangu juu ya hatma ya maisha yangu na uko niendako. Nilisiikia mtu anavuta begi(yule msichana) nilimvizia na kumkamata tuliangaishana mpaka watu waliamka*
**********
Safari ilikuwa ndefu ila michale ya saa kumi jioni tulianza kuingia dar nilitabasamu sana yule mdada ndiye aliyekuwa akinisaidia katika ile safari alinipa anuani ya kwao na kuniahidi pindi nitakapomtafuta atanijibu kwa wakati. Aliniachia kiasi kidogo cha fedha shilingi kumi, ilikuwa ni kiasi kikubwa sana cha fedha hata alipotoa alikificha sana maana nyakati za nyerere hapakuwa na ubadhilifu wa fedha kama nyakati hizi hivyo ukionekana na kiasi kikubwa cha fedha hukumu yako ni jera umepata wapi kiasi kikubwa cha pesa kama hicho(socialism era)..
Nilifikia manzese maana ambapo palikuwa na nyumba chache sana, hapo nilimtafuta mjomba wangu akiyekuwa anaishi hapo toka nikiwa dar nyakati zile nilikuwa naenda kumsalimu.
Nilishtushwa niliposikia kuwa mjomba tayari alikuwa ameama mazingira yale nilichoka nikakaa chini na kushika kichwa "nitaenda wapi mimi?
Nilikosa mtu wa kunisaidia nikaanza kufanya biashara ndogo ndogo ili kujikwamua kimaisha haikuwa rahisi mpka siku zilipotangazwa dhabuni nikaiona kupitia gazeti la the citezen nikaamua na mimi kujaribu bahati yangu ndipo nilipopata bahati ya kupata kazi...
Nyakati zile hapakuwa na changamoto kama nyakati za sasa ilipofikia kipndi nikawa nafanya kazi chini ya wizara ya ujenzi hapo ndipo yalianza mizengwe wakati huo tayari nina familia ya watoto wakubwa tu clement, clementina na cliford, rafiki yangu wa muda mrefu Billy alinieleza kuwa kama nahitaji kuongezewa mshahara au cheo kikubwa zaidi twende kwa mtaalamu(sangoma) ili afanye mambo na kunipa dawa za kuweza kunifanya nikubalike na wakuu zangu wa kazi.
Nilikubaliana na masharti yote kutoka kwa sangoma ila lilikuja suala moja lililonipa shida.
"Suala lipi baba" aliuliza clinford
"Mganga aliniambia km unahitaji kufanikiwa zaidi tembea na mtoto wako wa kike"
'Kheeee ili iweje sasa" alizidi kuhoji clinford
Ilikuwa ili nifanikiwe mambo yangu, nilipata shida sana ila mama yako aliposafiri ndipo nilipofanikisha malengo yangu hali ambayo ilinisaidia sana kazini na kipato.
**********
CLINFORD.
Nilimtazama baba akinisumulia kwa shida nikajikuta machozi yananitoka nikamtazama tena nikagundua hata kuhema kwake kulikuwa si kwa kawaida.
"Clinford mungu akusaidie mwanangu usome kwa bidii zile ndoto zako za kuwa daktari siku moja zitimie sisi kazi yetu duniani imekwisha penda familia yako na kamwe usiwasahau mimi nilipambana kote huko ilimuishi vizuri na isitokee siku mkakosa mahitaji muhimu, mungu"
Niilisikia neno la mwisho "mungu" ila hakumalizia akawa kimya nilimshika mkono wa kulia nikauweka kweny paja langu la kushoto kisha nikamfunika vizuri na shuka " daddy pumzika utanimalizia baadae najua umechoka" nilimkisi kwenye paji la uso nikatoka nje angalau kutafuta chakula maana nilikuwa na njaa mno.
Nilipokuwa kantini pale hospitali nilimpigia simu dada clementina kujua anaendelea nyumbani simu iliita bila kupokelewa nikampigia shangazi akawa anaongea kwa kutokuwa na utulivu.
"Shangazi ebu tulia kwanza una nini kuna nini?
" dada yako shangazi kwanini lakini clementina? Aliongea shangazi
"Amekuwaj sasa shangazi?
" anatokwa na mapovu na mwili wote unatetemeka"
Niliacha kula ili niende nyumbani tumuwaishe clementina hospitali maana shangazi peke yake asingeweza kumudu wakati nataka kutoka nikakumbuka kuwa sikuacha mazingira salama nikapitia wodini nilishangaa kuona pale kitandani baba kafunikwa shuka tofauti na lile.
**********
Maisha yangu yalibadilika kwa kiasi kikubwa sana toka niliposhuhudia ndani ya mwaka mmoja nampoteza baba na kaka huku nikimuacha mama akipooza na dada clementina akiondoka pasipojulikana baada ya kupona tatizo lake nilikuwa mpweke kila nikikumbuka familia ile leo nipo na mama pekee ndugu wengine siwaoni.
Niliishi maisha ya wokovu nikiamini mungu pekee anaweza kusaidia maisha yangu kwani yote yaliyotokea yalikuwa ni funzo kwangu.
MWISHO
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com