SORRY MADAM (53)

Zephiline F Ezekiel
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
ILIPOISHIA...
“Ahaa sawa”
“Yule uliye kuwa unampiga ni nani?”
“Si ni mke wa baba”
“Ahaa na yule mwengine aliye pigwa risasi?”
“Ni mshenzi mwenzake ambaye walikuwa wakitembea pamoja na kumzunguka baba”

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
Tukiwa katika mzungumza ya kawaida tukazishuhudia gari mbili za polisi pamoja na gari moja za wagonjwa zikiingia kwenye geti kuu la jumba la baba na kusimama sehemu ya magari ya kusimama,Wakaingia ndani na baada ya muda madaktari wakatoka wakiwa na kitanda cha matairi na juu yake wakiwa wamemlaza mke wa baba na kumuingiza kwenye gari lao na wakaondoka huku wakiwa wanapiga ving’ora.Askari wawili wakatufwata sehemu tuliyo simama na mama na kutusalimia kwa utaratibu

“Tunaimani na nyinyi ni miongoni mwa wahusika kwenye hii nyumba?”
Askari mmoja alizungumza huku akituangalia usoni na mama akanitizama kisha akajibu
“Ndio labda tuwasaidie nini?”
“Kwa jina ninaitwa Afande Lawnrance ninawaomba kuwafanyia mahojiano ya nini kilicho tokea muda mfupi uliopita”
“Mimi ninaitwa Afande Martin

Kitu ambacho nimekigundua kuwa askari huyu anaukarimu mkubwa na nitofauti na baadhi ya askari wa Tanzania ambaye kwenye tukio kama hili atataka kukutingisha tingisha ilimradi iwe ni shida,Mama akashusha pumzi na kumtazama askari Lawnrence
“Kilicho tokea kwa ufupini kwamba yule mama aliye wahishwa hospitalini alimsukuma baba wa huyu kijana kutoka gorofani hadi chini ninaimani mumeona meza ya kioo iliyo pasuka?”
“Ndio nimeiona”
“Yaa hilo ndio kubwa ambalo limetokea na mengine mukawahoji wale wafanyakazi wa humu ndani”
“Asante mama je kijana una lolote la kuzugumza”
Kwa haraka mama akaniminya mguu pasipo askari kuono tukio hilo
“Hapana sina la kuzungumza”
“Haya asanteni kwa maelezo yenu”

Wakatupa mikono na wakaondoka na kuniacha nikiwa na wasiwasi mwingi juu ya tukio hili na sheria za hapa Afrika kusini hata kama una pesa kiasi gani ila kama umefanya kosa lazima ustakiwe
“Mama si watanikama wakiujua ukweli?”
“Ndio..ila cha kufanya sasa hivi nikupeleke kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo hapa na urudi Tanzania na mimi uniache nishuhulikie hili swala”
“Mama wewe ubaki.....!?”
“Ndio nahitaji kulishuhulikia kwanza hili swala la baba yako la sivyo wataanza usumbufu tena wa kukupeleka mahakamani na ikiwa hivyo ujue ni ishu nyingine tena ya kukuweka mmatatani”
“Sasa mama....”
“Hakuna cha sasa tena ngoja nizungumze na vijana wa hapa kazi hiyo ifanyike sasa hivi”
Mama akamuita mmoja wa walinzi wa baba na kuwaomba atupeleke ulipo ubalozi wa Tanzania

“Si unapajua?”
“Ndio mama ila mimi sihusiki na maswala ya usafiri na funguo zote za magari zipo ndani”
“Eddy si unajua sehemu zinapokaa funguo za magari?”
“Ngoja nikatazame ndani kwa baba”
Nikaingia ndani na kuwakuta askari wakipiga picha sehemu za matukio yalipo tokea,moja kwa moja nikaingia chumbani kwa baba na kuanza kufungua kabati moja baada ya jengine na sikufanikiwa kuona funguo hata moja.Nikafungua droo ya kitanda na kukuta funguo mbili za gari pamoja na saa mbili za dhahabu.Nikaziingiza mfukoni saa na kuzichukua funguo na kutoka nje,nikiwa ninashuka ngazi askari mmoja akanifwata na kunizuia

“Angalia usikanyange hiyo kwenye hilo sehemu lililo chorwa”
Alinielekeza nisipite kwenye sehemu ambayo wameichora kama ushaidi,Nikapita pembeni na kutoka nje na kuwakuta mama na mlinzi wakitusubiria.Tukafika sehemu yenye magari ya baba na kuitoa funguo moja na kuminya kitufe kilichopo kwenye gari kikiwa na matumizi ya kulifungua gari husila la funguo hiyo.Gari moja likatoa mlio na sote tukajua ndio gari husika la funguo hii.Nikamkabidhi mlizi funguo na sote tukaingia ndani ya gari na kuondoka.
Tukafika kwenye ofisi za ubalozi wa Tanzania na mama akashuka na kuniomba nibaki ndani ya gari na baada ya muda akatoka na kuniita kwa ishara na sote tukangozana hadi ndani ambapo akaanza kunitambulisha kwa balozi wa Tanzania Afrika kusini bwana Marki Msuya na baadi ya wafanyakazi wa ofisi hii.

“Tena mumekuja muda mzuri kwa maana leo ndio siku ya wale vijana wa Tanzania walio zamia huku na kukamata ndio wanarudishwa”
“Wanatumia usafiri gani?”
“Serikali ya hapa imetupa ndege tuwarudishe vijana wetu wapo kama 248 hivi”
“Si kijana wangu anaweza kupata nafasi kwa maana mimi ninahitaji kubaki huku kuna ishu nitaishuhulikika kabla ya kurudi nchini”
“Ndio nafasi zipo.....Za masiku dada yangu kwa maana ninayo taarifa kuwa umetekwa na Al Shabab?”
“Ahaa tutazaungumza baadaye kaka yangu ila kikubwa kwanza tumshuhulikie huyu kijana wangu”

Mipango ya mimi kurudi Tanzania ikaanza kushuhulikiwa na jina langu likawa ni miongoni mwa majinina ya vijana wanao rudishwa Tanzania kwa kuingia nchini Afrika kusini pasipo kuwa na kibali maalumu.Mida ya saa nane mchana tukafika uwanja wa ndege wa O.R. Tambo International uliopo Johannesburg na nikajumuishwa na baadhi ya vijana nilio wakuta katika sehemu za kusubiria ndege muda wa kuondoka huku wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari.Mama akanikumbatia kwa ishara ya kuniaga

“Ukirudi hakikisha humuambii mtu yoyote ni wapi nilipo na hakikisha kuwa unafwatilia nyendo zima za baba yako na utakuwa unawasiliana na mimi”
“Nitawasilia vipi na wewe kwa maana sina simu?”
Mama akamuita balozi wa Tanzania na akamuoma namba yake ya simu ambayo akaiindika kwenye kikaratasi na kunikabidhi mimi
“Hiyo utaitumia kuwasiliana na mimi kwa maana mama atakuwa kwangu”
“Sawa”

Muda wa kuondoka ukawadia na tukaongozwa hadi kwenye ndege ambayo ndi maalu kwa sisi kuondoka na tukaanza kuingia kwa majina na mimi nikawa mtu wa mwisho kwenye orodha ya majina na kuingia ndani ya ndege na kukuta wezangu wote wamekaa kwenye siti zao.Nikaanza kutafuta siti niliyoa ambiwa na muhudumu nikae.Kila abiria akawa ananitazama na macho yangu yakagongana na macho ya Sheila akiwa amejifunga kitambaa kichwani na pembeni yake amekaa jamaa mwengine
“Sheila?”
“Bee”

Nikampa mkono nikataka kuanzisha mazungumzo ya kujua ni nini kimempata ila muhudumu akaniomba nikakae kwenye siti yangu iliyopo nyuma kabisa kwani ndege imebakisha dakika chache kabla ya kuondoka.Nikakaa kwenye siti yangu na kujufunga mkanda na nisita ambayo pembeni hapakuwa namtu yoyote na mashine za ndege zikawashwa taratibu,Kwa kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona Askari Lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu

Kutokana tayari injini za ndege zilishaanza kuata moto haikuwa rahisi kwa kuisimamisha ndege ambayo taratibu ilishaanza kuondoka kuzipisha ndege nyingine ambazo zinasubiri kutua na kila kitu katika uwanjwa huu wa ndege vinakwenda na muda wanao jipangia.Macho yangu yakashuhudia jinsi tunavyo ziacha gari za polisi na ndege inavyo ongeza mwenza na kuitafuta njia ya kurukia
“Ehee mola niokoe mimi mja wako kwa maana mmmm”

Nilijizungumza kimoyo moyo na kweli ndege ikakaanza kunyanyuka taratibua na kuiacha ardhi ya Afrika kusini hadi ndege inakaa sawa angani ndio nikapata amani na kajasho taratibu kakanishuka huku kwa mbali nikijasikilizia jinsi mapigo ya moyo yanavyo punguza kasi yake,safari ikaendelea kwa amani na kutokana na uchovu mwingi nikajikuta nikilala fofofo pasipo na kitu kilicho nistua ni kipaza sauti cha rubani akituomba tufunge mikanda yetu vizuri kwani ndege inajiandaa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyata nchini Kenya
“Mmmmmmm”

Nikajikuta nikiguna kwani sijazoea kuziona ndege zinazo toka nchini Afrika kusini kutua Kenya ili kwenda Tanzania na isitoshe kwa maelezo niliyo yasikia wakizungumza mama na balozi wa Tanzania ni kwamba ndege inakwenda moja kwa moja Tanzania.Moyo wangu ukaanza kupoteza amani tena ikanilazimu kumiya muhudumu wa ndege na hakusita kunifwata sehemu nilipo na kunisikiliza haja yangu niliyo muitia

“Sijui nimesikia vibaya au....? Ni kweli tutatu Kenya?”
“Ndio kuna mzigo tunaishusha kwanza na pia kuna mmoja wa abiria nanhitajika kurudisha Afrika kusini kwahiyo tunaiwahi ndege ya shirika letu inayo ondoka Kenya saa sita usiku na tutamkabidhi abiria huyo kwa askari.”
Moyo ukawa kama umelipuliwa na bomo,kuzungumza nikajikuta nikishindwa na kubaki nikimtazama muhudumu kama sanamu la kushangaza
“Halloo mr”

Nikastuka na kumtazama muhudumu wa ndege ambaye alikuwa akinipungia mkono mbele ya uso wangu baada ya kuniona nikiwa nimegandishwa kama sanamu
“Umesema kuna mtu anashushwa?”
“Ndio hiyo ni taarifa tuliyo powa tukiwa njiani”
“Ni mwanume au mwanamke”
“Kusema kweli hatujatajiwa ni jinsia gani?”
“Nashukuru”
“Na wewe pia”

Muhudumu akaondoka na kuniacha nikitawaliwa na mawazo na laiti ingekuwa nipo kwenye gari nigeweza kuruka na kufilia mali.Kitu cha ndege ni ngumu sana kujirusha,rubani akatutangazia kuwa zimesalia dakika tano kwa ndege kutua na kila mto ahakikishe kuwa amejifunga vizuri mkanda wake hapo ndipo nikakumbuka na mimi kujifunga mkanda.Ndani ya dakika tano ambazo rubadi alisema ndivyo jinsi iliyo kuwa na ndege nikaanza kushuka chini kwa kasi na matairi yake yakaanza kukanyaga ardhi ila gafla tukasikia mlio wa ‘KWAAA’ kama kitu kilicho katika na kuifanya ndege kuegemea upande wangu niliopo na wezangu tulio kaa upande huu.Milio ya vyuma kukatika katika tukazidi kuisikia na si mimi mwenye niliye anza kupiga kelele za kumuomba Mungu ila hadi wezangu nao wakafanya hivyo huku kila mmoja akiomba kwa lugha anayo ijua yeye mwenyewe

Ndege ikazidi kulala upande wetu na kazidi kuserereka na mbaya zaidi moto mwingi ukaanza kuwaka sehemu ya nyuma mita chache kutoka ilipo siti yangu na kunilazimu kuufungua mkanda ili kuyaokoa maisha yangu kama wanavyofanya wezangu.Nikawahi kuishika siti ya mbele yangu ili kujizuia na upepo mwingi unao nivuta nyuma kutoka katika sehemu ulipo moto ambao umepasua sehemu nzima ya nyuma.Nikajikaza kwenda mbele na watu walio shidwa kujishikilia walivutwa nyuma kwenye moto.Kelele na vilio vikazidi kutawala na kila sehemu na watu wengi wakawa wamebanwa na siti zao kiaisi kwamba baadhi yao walijigonga vibaya kwenye vyuma na vichwa vyao kupasuka vibaya na wengine kukatika viungo vya miili yao

Ndege ikagonga sehemu na kusababisha mtikisiko mkubwa na kupinduka kichwa chini miguu juu jambo lililosababisha mikono yangu kushindwa kuhimili kuishikilia siti niliyo kuwa nimeishika na nikajikuta nikiachia na kuanza kuvutwa nyuma na upepo mkali uliochanganyika na moto ambao ni mkali sana

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni