SEHEMU YA MIA MOJA NA MOJA
ILIPOISHIA...
Masanduku yenye pesa yakaanza kunishiñda nguvu, ikanilazimu kuyaachini, yakazidi kwenda chinni. Taratibu nikaanza kujilegeza mwili wangu na kuanza kw, hadi nikatolea usawa wa bahari.
Nikailuta meli ikiendelea kuteketea kwa moto mkali, nikatazama sehemu nilipo waacha Amina na wezake ila sikuzioa gari mbili zilizo kua zimewabeba.
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Wasiwasi wangu, ukawa juu ya Phidaya, ikanilazimu kuogelea kuelekea ukingoni mwa bahari. Kitendo cha kufika ukingoni mwa bahari, kundi la watu si chini ya saba, wamesimama mbele yangu huku wakiwa na bunduki mikononi mwao. Nikajikuta nikiishiwa ujanja nisijue nini nifanye
"Toka nje ya maji"
Jamaa aliye valia kilemba kichwani mwake aliniamrisha niweze kufamya alicho agiza. Nikawatazama vizuri, nikagundua hawa ni miongoni mwa wale wali mteka mke wangu Phidaya. Nikatoka huku mwili wangu wote ukiwa umelowa kwa maji.
"Piga magoti kabla hatujakumwaga ubongo"
Nikapiga magoti taratibu, sikuwa na ubishi kwani tayari nipo chini ya ulinzi wao. Wakaanza kunong'onezana, walizungumza kisomali. Macho yangu yakatazama kila pande ila sikuona magari yote mawili.
"Umeharibu biashara yetu mshenzi wee"
Jamaa alizungumza, huku akinipiga teke la kifua lililo niangusha chini. Sauti ya simu ya upepo ya mmoja wao ikasikika ikizungumza
"Mkuu wasichana wametukimbia tayari wamefika kwenye mikono ya wanejeshi wa UN. Over"
Nikuona mkuu wao akianza kuzunguka zunguka mithili ya mwenda wazimu aliye changanyikiwa. Akaanza kujipiga piga kichwani kwa mkono hadi kilemba kikaanguka chini, akanigeukia, huku akiwa amenikodolea mimacho mikali iliyo jaa hasira kama chui.
Akaanza kunisogelea sehemu, niliyo piga magoti chini, huku mkono wake mmoja ukichomoa bastola aliyo ichomeka kwenye mkanda wa suruali yake. Nikamtazama kila hatua anayo ipiga kumifwata nilipo, hatua moja kabla hajanifikia. Nikauvuta mguu wake kwa nguvu, akaanguka chini, kwa kasi ya akabu nikamuwahi, kumpiga kabali, iliyo wafanya watu wake kuzikoki bunduki zao wakiwa tayari kwa kufyatua risasi
"Waambie watu wako waweke silaha chini, lasivyo nakuvunja koromeo lako"
Nilizungumza huku, nikizidi kuliminya koo la jamaa huyu, mwenye mwili mwembamba kiasi ila ulio komaa. Watu wake wakashusha silaha zao chini, hapakuwa na sehemu nyimgine ya kukimbilia zaidi ya kurudi nyuma, kuelekea kwenye maji.
"Musitufwate"
Nilizungumza kwa sauti ya ukali, iliyo wafaya watu wake kusimama wakinikodolea mimacho. Nikafika ukingoni kabisa wa bahari. Nikawatazama jinsi walivyo duwaa, pasipo kusubiri kitu chochote, nikaizungusha shingo ya mkubwa wao, na kuivunja kabisa, nami nikajirusha kwenye maji. Nikawacha wakimkimbilia bosi wao, niliye muacha akiwa eanguka katika sehemu tuliyo simama.
Mwanga wa moto, wa meli inayo endelea kuteketea, ukanisaidia kuona vitu vilivyomo ndani ya maji. Nikayaona masanduku ya pesa. Nikaanza kuyafwata sehemu yalipo angukia. Kabla sijayafikia, mikawaona jamaa wakijirusha ndani ya maji mmoja baada ya mwengine, lengo lao kubwa ni kunifwata mimi sehemu nilipo. Ikanilazimu kubadili muelekeo na kuachana na masanduku ya pesa.
Kasi yao ya kunifwata ikazidi kuongezeka. Nikapanda juu kwa kasi ili kupata pumzi itakayo nisaidia kupambana na jama hawa
Nilastukia mmoja wao akinivuta ndani ya maji huku akiwa amenishika miguu. Nikaanza kupambana nao, huku wezangu wakiwa na visu vikali. Japo katika maisha yangu nimekutana na mambo mengi sana kuhusiana na kupambana na maadui, ila hawa wasomali ni mziki mwingine. Sikutaka kukubaliana na kushindwa japo, visu vyao mara kadhaa vimejikata kata maeneo ya mikononi, kila nilipo kua nikijaribu kuvizuia visinifikie mwilini mwangu.
Nikafanikiwa kupata kisu cha jaa, mmoja niliye mtoboa macho, kwa vidole vyangu, ikamlazimu kukiachia kisu hicho. Nikazidi kupambana nao pasipo kukata tamaa, Nikazidi kuwapunguza hadi nikawamaliza kabisa. Nikaogelea taratibu hadi eneo nilipo zama mara ya kwanza na masanduku ya pesa. Nikavuta pumzi yakutosha kisha nikazama tena ndani ya maji. Nikayachukua yote, hivyo hivyo nikajikaza kupanda tena juu, na nikafanikiwa kutokeza juu kabisa. Nikatoka nayo hadi nchi kavu, nikatazama usalama wa kila eneo, nilajiridhisha hakuna mtu atakaye nidhuru. Taratibu nikaanza kujikongoja, huku mwanga wa mbala mwezi ukinisaidia kuona niendapo. Japo mwendo wangu ni wakuchoka sana, ila nikajika kutembea hivyo hivyo.
"Baba mwema ni yule anaye ipigania familiavyake"
Nilijifariji hulku nikisonga mbele, nikafanikiwa kufika sehemu tulipo liacha gari la Amina. Kwa bahata nzuri nikalikuta. Nikayaingiza masanduku yote ndani ya gari. Sikuikuta funguo ya gari, ikanilazimu kukata nyaya mbili za hasi na chanya, zilizopo pembeni ya mskani. Nikazikutanisha kwa pamoja gari ikawaka.
"Hahaaahaaaaa"
Nilianza kucheka mimi mwemyewe baada ya gari kuwaka, nikaligeuza kwa haraka na kurudi katika sehemu tulipo toka na Amina
Gari ikaanza kutoa mlio wa kuishiwa na mafuta, kwa kumbulumbu zangu, kuna sehemu niliona sheli, na sehemu niliyopo hadi sheli ilipo si mbali sana. Nikafanikiwa kufika ilipo sheli, saa ya kwenye gari inaonyesha ni saa kumi na mbilo asubuhi. Nikafungua sanduku moja nilachomoa noti kadhaa za dola mia, japo zimetota kwa maji, ila hazijaharibika.
Nikazungumza na muhudumu, akanijazia tanki la gari. Nikampa noti tatu za dola mia, kisha nikaondoka na kumuacha akishangaa kwani nikiasi kikubwa sana cha pesa ukilinganisha na mafuta aliyo niwekea kwenye gari.
Safari ya kurudi, kwa Amina ikaanza, njia nzima nikawa makini kwa kila gari lililo karibu yangu.
Nikafanikiwa kufika nyumbani kwa Amina, nikalisimamisha gari sehemu anapo lisimamisha, nikashuka ndani ya gari, nilitizama kila kona ya yumba, nikaridhika na usalama. Nikashusha masanduku ya pesa ndani ya gari. Nikaingia nayo ndani.
Niajikuta nikiyaweka chini, kwa haraka, hii nibaada ya kukuta damu nyingi zikiwa zimetapakaa kwenye sakafu, pamoja na sehemu ya ukutani. Mapiga ya moyo yakaanza kuniendaa mbio. Nikaanza kufwata michuruziko ya damu iliyo elekea chumbani mwa amina kabla sijufikia mlango wa chumbani kwake, kitu kizito kikangia kupitia dirishani. Kikaanza kutoa moshi mkali ulioa anza kunipalia, nikagundua ni bomu la machozi, lililo ambanata nailio ya risasi iliyoanza kusikika ikitokea nje.
Ikanilazimu kulala chini haraka haraka, risasi zikazidi kumiminika zikipigwa kupitia maditishani, ambayo ni yaviol na tayari yamesha vunjika vibaya mno. Kitu kilicho nichanganya sikujua risasi hizo zinatokea upande gai, na mbaya sijajua watu hawa nj waaina gani, na wanamalengo ganjni kwangu.
Nikatamba haraka na kuyachukua masanduku ya pesa nikaufungua mlango wa chumba cha Amina, nukayasukumia ndani, na mi nikaingia nikiwa ninatambaa, japo moshi huu, mkali uliendelea kunipalia na kuyafanya macho yangu kumwagikwa na machozi mengi. Nikamkuta polisi akiwa ameuawa ndani ya chumba cha Amina, huku risasi kadhaa, zikiwa zimekichangua kichwa chake vibaya. Nikafunga mlango kwa ndani, nikaatafuta maji ya kunawa usoni, ila sikuyapata.
Nikavua shati langu nililo livaa, nikalikojolea na kulitotesha vizuri kwa maji mengi. Nikajifunika usoni, kidogi hali ya kumwagikwa kwa machozi ikapungua. Risasi zikaendelea kurindima, nikawa ninajiuliza watu hawa huwenda wakawa ni wendawazimu, kutokana risasi zao wanazimalizia katika kuzifyatua pasipo malengo, isitoshe ukuta waa nyumba hi, kidogo ni imara sana, na risasi kupenya si rahisi sana.
Nikatafuta kila koa ya chumba kama kuna kitu cha kuweza kunisaidia kuepukana katika adha hii ya kuingia mikononi mwa watu amwa watu ambao hadi sasa hivi sijajua kama ni poliai au laa. Katika kuyembea tembea ndani ya chumba cha Amina, nikahisi mlio fulani kutokea chuni ya kapeti lililo tandazwa chumba kizima.
Nilalifunua kwa haraka na kukuta, mfuniko wa chuma, ulio fungwa kwa kufuli. Nikaanza kutafuta jinsi ya kuufungua mfuniko huu, kwakutumia ncha ya sanduku moja wapo, ñikafanikiwa kulivuñja kufuli. Nikalifungua, nikakuta ngazi ya kushuka chini, kwa haraka nikashuka japo kuna giza totoro, ila nikajiamini. Kufika chini ya ngazi, nikahisi kuna kitu, kinanigusa kichwani, nikaupeleka mkoni wanguna kushika, nikakuta kijikamba, katika kukivuta chini, taa karibia nne, zilizopo ndani ya chumba hichi zikawaka.
Bunduki nyingi za kila aina nikaziona zikiwa zimepangiliwa vizuri kwenye kuta za handaki hili, nikapnda juu haraka, nikayasukumia ndani masanduku ya pesa, nikajibanza kwenye moja ya kuta, yenye dirisha, nikachungulia nje. Nikaona watu wakikatiza katiza kwenye miti mingi ya hii, nyumba. Mikononi mwao wakiwa na silaha. Kitendo cha wao kukimbia kimbia kwenye miti hii, ni kubadilishana nafasi za kufyatua risasi. Kitu kilicho nifanya nigundue hawa si polisi, hii nikutokana na vilemba vyao walivyo jifunga, pamoja na mavazi yasiyo na sare maalumu.
"Jamaa wamekuja hadi huku"
Nilijisemea, mwenyewe huku nikiendelea kuwatazama jinsi wanavyo fyatua risasi zinazo piga kwenye kuta ya nyumba hii.
'Wameanza mimi, nitamaliza'
Nilizungumza, huku nikishuka kwenye ngazi za kuingia kwenye handaki. Nikanza kufungua makabati manne yaliyopo humu ndani, nikayakuta yakiwa na bunduki pamoja na silaha kadhaa, nikakuta kisanduku cha kuhifadhia, vitu vya huduma ya kwanza.
Nikafungua na kuchukua clip bandeji, nikajifunga sejemu nilizo pata majeraha ya kukatwa na visu. Nilipo hakilisha nipo salama, nikachukua bunduki, aina ya SMG, nikachukua na magazine kumi, zilizo jaa risasi.Nikachukua shati langu, nililo lilowanisha kwa mikojo, nikajifunga kichwani. Nikapanda juu, nikakuta hali ikiwa imetulia. Nikaanza kusikia minong'ono ikitokea sebleni, iloashiria jamaa, wamesha ingia ndani. Nikajibanza pembeni ya ukuta wenye mlango, taratibu nikakifungua kitasa, Na kuuvuta mlango taratibu, nikauachia, nikañza kusikia hatua za mtu akija chumbabi.
Nikashañgà à , kunuona mtoto mdogi wa kike mwenye umri chini ya miaka kumi na tato, akiwa ameshika bunduki huku akimshangaa, polisi aliye lala chini.
"Amefia huku"
Alizungumza pasipo kuniona nyuma ya mlango, nilipo simama. Akaiweka bunduki yake chini na kuanza umpapasa askari huyu, nikasogea pembeni kidogo, ili asinione, kwa bahati mbaya nikagusa kikopo chenye poda kilichokua juu ya 'dreasing table'
na kikaanguka chini na kumfanya binti huyo kugeuka haraka, tukakutana macho kwa macho.
Kumbukumbu za wanakijiji walio vamiwa na John, na kuuliwa watoto wao kikatili, wasio na hatia yoyote. Ikapita kichwani mwangu kwa haraka, nikajikuta nikomuonea huruma binti huyu ambaye hastahili kifo kwa wakati huu. uzuri wa binti huyu, kidogo unaendana na Phdaya wangu, Macho yake, pua yake, midomo yake ni kama Phidaya.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com