
SEHEMU YA MIA MOJA NA MBILI
ILIPOISHIA...
Kumbukumbu za wanakijiji walio vamiwa na John, na kuuliwa watoto wao kikatili, wasio na hatia yoyote. Ikapita kichwani mwangu kwa haraka, nikajikuta nikomuonea huruma binti huyu ambaye hastahili kifo kwa wakati huu. uzuri wa binti huyu, kidogo unaendana na Phdaya wangu, Macho yake, pua yake, midomo yake ni kama Phidaya.NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Nikawa katika dimbwi zito la kumtathimi binti huyu, nikastukia kuona mtu aliye valia sutlruali ya jeshi, akiingia ndanj ya chumba hichi, huku akimfokea binti huyu, akimuuliza mbona anachelewa kutoka.
Nikafyatua risasi kadhaa kwa jamaa, huyu na akaanguka chini. Binti akajribu kuchukua bunduki yake, ila nikawahi kujirusha na kuisukumia pembeni. Jamaa waliopo sebleni, wakaanza kufyatua risasi nyingi katika chumba tulichopo. Nikamnyanyua binti huyu aliye chamganyikiwa na kumsukumiza kwenye ukuta usio pitisha risasi. Nikaanza na mimi kujibu mashambulizi ya watu hawa.
"Babaa, Babaa usiniache mwenyewe"
Binti huyu alianza kulia, huku akimtazama mzee, huyu niloye mpiga risasi na kufa mbele ya macho yake.
Nikaendelea, kujibu mashambulizi ya jamaa hawa, walio sebleni wakakimbjlia nje. Nikatoka sebleni, huku nikiendeleà kujibu mashambulizi yao. Nikasikia sauti zikiwaashiria waondoke, haraka eneo hili kwani mkubwa wao amekufa. Ndani ya dakika tano, ukimya ukatawala nje ya nyumba. Nikarudi ndani ya chumba na kumkuta binti huyu akiwa amemuegemea baba yake, aliye jitahadi kumnyanyua hadi akamkalisha kitako.
Binti huyu akanyanyuka, haraka na kunifwata mlangoni nilipo simama. Akaanza kunipiga piga kifuani huku akilia.
"Umemuua baba yangu"
"Kwa nini umuue baba yangu?"
Aliendelea kunipiga kifuani, mwangu sikumjibu kitu chochote, akaendelea kunipiga kifuani mwangu, nikajikuta nikimtandika kofi moja la shavuni lililo muangusha chini, nakumfanya atulie kimya.
Nikakaa kitanda huku, nikiwa nimejichokea sana. Nikajihi maumivu kwenye paja langu la mguu wa kushoto, nikajichunguza vizuri na kugundua nina jeraha risasi, iliyo nikwaruza, ila haikuingia ndani ya mguu wangu.
"Mungu, hivi kwanini maisha yangu si yaraha?"
Nilijikuta nikizungumza mwenyewe huku nikitazama maiti mbili zililo lala chini, sikujua hata hii maiti ya askati imetokea wapi. Ubaya wa hii sehemu, nyumba ipo msituni, na imezingirwa na miti mingi, kiasi kwamba si rahisi kwa watu wa kawaida kupafikia.
Nikazitoa maiti zote mbili, nukuziweka sebleni, Nikaigia chini kwenye handaki, nikajitibu jeraha la risasi iliyo nipunyua. Nikachuku silaha na risasj zakutosha nikazipeleka kwenye gari, nililo likuta lipo salama salmin. Nikarudi na kuchukua masandukuvya pesa kabla sijatoka binti akapiga chafya. Nilayaweka chini nà kumsogelea karibu, nikamnyanyua na kumuweka kumkalisha.
"Unaitwa nani?"
"Eheeee"
"Jina lako ni nani?"
Akabaki akiwa amenitazama tu, pasipo kunijibu kitu cha aina yoyoye.
"Nipo wapi?"
"Upo duniani"
Nilimjibu hivyo kutokana ninatambua kwamba alipoteza fahami kwa kofi zito nililo mtandika. Akanyanyuka na kutazama mazingira ya chumba, nikamuona jinsi anavyo zitazama damu zilizo tapakaa chini.
"Kumetokea nini?"
"Hakuna, twende zetu"
Tukatoka chumbani, akafika sebeni, akaitazama maiti ya bana yake. Nikashangaa kumuona akianza kuupiga mwili wa baba yake mateke huku akianza kulia.
"Kufa kufa kufa"
Alizungumza huku akizidi kuutandika mateke mwili wa baba yake, nikabaki nikiwa nimeduwaaa nisijue nini kinacho endelea.
Ikanilazimu, kumshika huyu binti, nakumuweka pembeni ili asiendelee kupoteza muda wa sisi kuondoka katika eneo hili kwani hatutambui ni kitu gani kinaweza kutokea ndani ya dakika moja inayofwata mbeleni. Tukatoka nje huku binti akiendelea kumwagikwa na machozi mfululizo. Tukaingia ndani ya gari, nikaliwasha kama nilivyo liwasha mara ya kwañza kwa kuviunganisha vijiwaya hasi na chanya.
"Usiondoke"
Msichana alizungumza mara baada ya gari kuwaka. Akashuka ndani ya gari na kuzunguka nyuma, ikanilazimu na mimi kushuka. Akainama na kuchungulia uvunguni mwa gari, akaingiza mkono wake, alipo utoa nje, akawa amesheka bomu la kutega
"Limebakia dakika tatu lilipuke, tuondoke haraka kwani yapo mengi eneo hili"
Binti huyu alizungumza huku akiliweka taratibu chini bomu alilo lishika.
"Kwahiyo mengine yapo humu ndani?"
”Yapo kwenye nyumba"
Tukaingia ndañya gari, kitendo cha kuingiza gia, ili kuliruhusu gari hili kuondoka. Likazima gafla, nikajaribu kuviunganisha vijiwaya, ila gari halikuwaka.
"Endesha nisukumu”
Nilizungumza huku nikishuka kwenye gari, na kumpisha binti kwenye mskani. Nikazunguka nyuma, nikalitazama bomu lililopo karibu, linaonyesha imesalia dakika moja na sekunde kadhaa, kabla halijalipuka, wasiwasi wangu mwengine ni kwenye mabomu, yaliyo wekwa kwenye nyumba, sijajua yametegwa kwa muda gani. Kwa jinsi nilivyo jeruhiwa mwilini mwangu na kuchoka ikanilazimu kujikaza liume kusukuma gari, hili ambalo sikujua limepatwa na nini hadi haliwaki. Taratibu likaanza kusogea, nikazidi kujikakà mua kuendelea kulisukuma lizidi kwenda mbe, huku mara kwa mara binti huyu akijaribu kuliwasha. Kwa bahati nzuri, kwenye njia ya kuingilia nyumbani kwa Àmina kuna kiporomoko, kidogo, kilicho lifanya gari kuongezeka mwendo.
Gafla gari likawaka, huku likitoa moshi mwingi.
"Ingia twende"
Nikalikimbilia gari, lilipo, kwani lilikua limeniacha kwa umbali fulani baada ya kuwaka. Kabla sijashika kitasa cha kufungulia mlango wa gari, nyuma tulipo iacha nyumba ya Amina, tukaanza kusikia milipuko mikubwa ya mabomu
"Twete twende"
Binti huyo alizungumza huku, akinitazama, nikajitosa ndani ya gari na binti hiyu akaliondoa kwa kasi kwenye eneo tulilopo, na mabomu yakaendelea kulipuka nyuma yetu.
***
Tukafika kwenye moja ya kijiji, chenye nyumba chache sana, zilizo achana achana na kujengwa na udongo wa mfinyanzi. Akasimamisha gari kwenye moja ya kijumba, akashuka kabla hajafikka mlangoni mwa kijumba hicho akarudi nilipo ndani ya gari.
"Hapa ni kijijiji kwetu, ndipo nilipokua nikiishi”
Alizungumza huku akiwa anachungulia kwenye dirisha la gari hili upande wa siti ya dereva alipo kua amekaa yeye.
”Kuna usalama?"
"Katia nchi hii, hakuña eneo lenye usalama”
"Unaweza kushuka ñdani ya gari"
"Ahaaa wewe nenda, nitakungojea hapa hapa"
"Sawa ñisubirie"
Akaingia ndani, mimi nikashuka kwenye gari na lufungua kwenye buti ya gari, nikatoa bunduki, yenye risasi za kutosha kisha nikarudi kukaa kwenye siti niliyo kaa, muda wote mà cho yangu, yakawa yanatazama kila kona ya barabara, kuhakikisha ninapata usalama wangu, kwani niliyo yafanya dhidi ya watu nilio pambana nao nina imani wananitafuta kona zote za nchi hii ya Somalia.
"Mbona anachelewa kutoka huyu?"
Nilijiuliza baada ya zaidi ya lisaa zima kupita pasipo binti kutoka ndani ya kajumba haka kilicho kidogo sana.
Nikataka kushuka, ila mlango ukafunguliwa wa kijumba hichi. Binti akaja nilipo
"Samahani kaka yangu, kwa kuchelewa nilikua nikifanyà fanya usafi, kidogo nyumba ilijaa vumbi"
"Ahaaa, ulinipa wasiwasi, nikajua umepatwa na tatizo"
"Hapana karibu ndani"
Nikashuka kwenye gari, nikazunguka nyuma gari, nikatoa masanduku ya pesa, binti akabeba silaha tulizo nazo. Tukaingia ndani, nikaona vyumba viwili tu ndani ya kijumba hichi, nikabaki niliwa najiuliza ni usafi gani alikua akiufanya binti huyu, ulio chukua zaidivya lisaa zima.
'Au kuna njama kapanga?'
Nilijiuliza kimoyo moyo, huku nikiendelea kuchunguza eneo zima la humu ndani.
"Kaka twende huku"
Tukaingia kwenye moja ya chumba kati ya viwili vilivyomo humu ndani, kwenye chumba hichi kuna ngazi, zakushuka kwenda chini. Sikuamini macho yangu baada ya kukuta seble kubwa, iliyo pangiliwa vizuri na inamasoma makubwa. Kuna milango kadhaa kwenye kuta za seble hii ikiashiria kwamba, nimilango ya kuiñgilia ndani ya vyumba vilivyopo chini ya handaki hili.
"Karibu kaka"
"Asante"
"Jisikie upo nyumbani."
Nikayaweka masanduku yangu chini, huku nikiendelea kuchunguza sehemu nzima, iliyo tengenezwa kwa utadi wa hali ya juu. Huku kukiwa na taa nyingi, zaukutani zinazo waka kwa mitindo tofauti tofauti
"Kwa nini munapenda kujenga nyumba zenye mahandaki?"
"Nikutokana na usalama wetu"
"Duuu"
"Pasipo kufanya hivi, tunaangamia. Watoto wengi wanatwekwa na kwenda kufanyishwa kazi mbali mbali, ikiwemo ya kigaidi"
"Yule uliye kua ukimpiga ni nani?"
"Baba yangu"
"Baba yako!?"
"Ndio, ila si mzazi. Ni baba mlezi, yeye kwenye kundi la kigaidi, watoto hua tunamuita baba"
"Ahaaa"
"Alafu sijalijua jina lako, mimi jinairwa Shamsa Al Seif"
"Eddy, Eddy Godwin"
"Umetokea wapi?"
Shamsa alizungumza huku, akifungua friji lililopo hapa sebleni, akatoa soda mbili za kopo na kunirushia moja.
"Nimetokea Tanzania"
"Kweli?"
"Ndio kwani vipi?"
"Hiyo nchi ninaisikia tu, kwamba ina amani. Basi najua watu wake hawajui kutumia silaha kama ilivyo sisi."
"Ni kweli, watu wengi hawajui kutumia silaha, kutokana na amani iliyopo. Ila ukiwa na matatizo utaweza kujua tu"
"Ahaaaa, wewe ni askari?"
"Hapana"
"Mmmm mbona, unajua mbinu nyingi za kijeshi?"
"Kawaida tuu. Ila wewe imekuaje ukawa katika kundi la magaidi?"
"Kule, niliingia pasipo kupenda. Siku tulipo kua njiani kurudi nyumbani, kwenye ule msitu ule tulio upita, walituvamia na kumuua baba, na mama wakaniteka mimi, nikiwa na miaka tisa"
"Ndipo walipo niunga kwenye kundi lao, wakawa wakinitumia kwenye matukio kadhaa ya ualifu"
"Mmmm pole sana, ilikuwaje mukavamia pale?"
"Pale tulipewa mchongo na jamaa mmoja, kwamba wewe unapesa nyingi sana, baada ya kumpa yeye pesa nyingi"
"Ndipo jamaa, fulani wakawa wanakifwatilia pasipo wewe kujua. Ndipo ukafika kwenye ile nyumba. Kutokana hatukuwa mbali na ile nyumba. Ndio maama tulikuvamia mara baada ya wewe kuingia ndani"
"Duu!"
"Ndio hivyo, mara baada kupiga risasi nyingi, tukajua utakua umekufa ndipo tulipo amua kuingia ndani. Tulivyo zikuta zile damu sebleni, zikielekea chumbani
Tukajua utakua umejeruhiwa ndipo tulipo ingia ndani na kukuta ule mwili wa askari. Ila nilibaki nimeduwaa baada ya kukuona ukiwa unanitazama kwa macho ya guruma, pasipo kuniua"
"Baba alikua akinifokea nitoke nje kwani tayari walisha tega mabomu"
"Sasa kwa nini, wasizifwate pesa nilizo kua nazo?"
"Huwa wananitoa mimi kama chambo, laiti baba angeingia mule ndani, asinge kutana na tukio kama hilo basi tungesaka chumba kizima kujua ni wapi zilipo pesa, ila kutokana ulimuwahi basi ikawa kama hivyo ilivyo tokea"
Shamsa, alizungumza huku akikizungusha zungusha kikopo cha soda yake. Machozi yakaanza kumwagika taratibu.
"Sikupenda kuua, sikupenda niwe katili katika umri huu. Nilihitaji nisome nitimize malengo yangu ya kuwa Daktari"
"Ila sijajua kama yatatimia tena"
"Kwani una umri gani?"
"Miaka kumi na saba"
"Unataka kusoma?"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com