SEHEMU YA MIA MOJA
ILIPOISHIA...
Manka akanyanyuka na kuingia ndani, kwa Amina. Amina akamfwata kwa nyuma kwenda kuzungumza naye. Nikawasha Tv, ila nikaikuta tarifa hiyo ikiwa imekwisha, nikajaribu kuitafuta kwenye chanel tofauti, pia sikuipata.
"Oya mtu wako amekataa bwana, tujiandae twende tukapachunguze, kisha usiku twende"
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Poa"
Tukajiandaa, nikavaa miwanani pamoja na kofia, tukaingia kwenye gari la Amina na kuondoka.
"Hilo begi lina nini?"
Nilimuuliza Amina, Ã liye beba begi la mgongoni, alilo liweka siti ya nyuma.
"Lifungue"
Nikalichukua, nikalifungua. Nikakuta kamera moja aina ya Canoon, bastola tatu, magazine kumi na mbili, na mabomu manne yakurusha kwa mkono.
"Mmmmmm"
"Mbona umeguna?"
"Kazi leo ipo"
"Ahaaa ulizani nimchezo, hii ni Somalia bwana, kuingia nirahisi ila kutoka ni ngumu"
Amima alizumgumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake. Chakumshukuru Mungu, htukukutana na polisi barabarani. Mwendo wa dakika arobaini na tano, tukafika kwenye majengo ya magorofa machakavu, yaliyopo nje kidogo ya mji wa Mogadishu. Amina ajasimamisha gari pembeni na kuitoa simu yake, akaniomba namba ya simu ya jamaa aliye nipigia, akaipiga, baada ya muda ikapokelewa, akaanza kuzungumza na jamaa kisomali, ambacho sikielewi kabisa.
"Amesemaje?"
Nilimuuliza Aminà baada ya kumaliza kuzungumza na jamaa huyo.
"Anasema yupo hapa"
"Ulimuambia kwamba wewe ni nani?"
"Hapana nimemuambia nahitaji kufanya nao biashara ya mafuta"
"Kwahiyo watakuja hapa tulipo?"
"Hapana nilitaka kufahamu kwamba wapo hapa"
Tukakaa ndani ya gari zaidi ya nusu saa, sikuwa ninaelewa nini maana ya Amina.
"Tunasubiri nni hapa?"
"Usiwe na hataka utaona"
Tukaendelea kusubiri zaidi ya masaa mawili, magari makubwa aina ya Scania yakatoka yakiwa na matela nyuma. Yakaingia barabara ya lami, na kuondoka kwa mwendo wa taratibu. Amina akawasha gari, taratibu tukaanxa kuyafwata.
"Tunaelekea wapi?"
"Tunayafwatilia hayo magari moja wapo ndipo alipo mke wako?"
"Umejuaje?"
"Hawa jamaa huwa wanafanya biashara ya kuuza wañawake wanao wateka katika nchi za ulaya, ambapo huku wanakwenda kuuzwa kwenye makasino na mabaa makubwa kwa ajili ya ngono"
"Sasa hapa wanawapeleka wapi?"
"Hii moja kwa moja wanakwenda baharinia à mbà po wanawasafirisha kutumia meli"
"Mmmmmmmm"
"Usigune hii ndio dunia bwana"
Amina alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari"
Nikaanza kuzitoa bastola moja moja, na kuanza kuzikagua kama zina ubora kwa maana nimatambua chochote kitatolea muda wowote tuliwa kwenye hio safari ambayo hadi sada hivi sitambui kama kuma udhibitisho wowote wa Phidaya kuwa ñdani ya magari haya yenye makontena makubwa.
Kadri tulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mahari hayo yalivyo zidi kuyoyoma, Amina hakukata tamaa, kila magari yalipo kunja naye akakunja pasipo kuhofia kama wahusika wameugundua, uwepo wetu wa kuwafwatilia kwa nyuma.
"Usiyafwate kwa ukaribu zaidi watatustulia"
"Usiogope"
"Kivipi"
"Hakuna kitakacho jitokeza"
"Mmmm"
Kitu ninaçho kiamini maishani mwangu, ni kuto kumuamini mtu yoyote, mbaya zaidi wale nilio waamini wote walinifamyia unyama wa hali ya juu, nikajikuta nilihangaika na kuteseka vibaya mno. Akili yangu ikaanza kumfikiria Amina, sikuhitaji kumpa uaminifu wa aina yoyote. Magari tuliyo yafwata, tukayashuhudia yakikunja kushoto mwa barabara na kuiacha barabata ya la lami na kuingia barabara ya vumbi. Amina akasimamisha gari
"Mbona umesimamisha gari?"
"Huku walipo ingia ni hatari sana"
"Kwahiyo itakuaje?"
"Itatulazimu kwenda kwa miguu, kutokana sio mbali saña na hapa"
Tukashuka kwenye gari, tukachukua silaha zetu, kila mmoja akachukua silaha yake, tukaanza kuchanja mbuga kwa kutumia miguu. Kigiza kwa mbali kilisha anza kujitokeza, huku saa yangu ya mkononi ikinionyesha ni saa kumi na mbilo na robo. Tukatembea zaidi ya dakika kumi. Tukafika kwenye moja ya fensi , iliyo zunguka majengo machakavu, ambayo yapo pembezoni mwa bahari. Tukapenya kwenye fensi hii, iloyo na uwazi mkubwa kidogo.
Kwa mwendo wa harà ka, wenye umakini, tukafanikiwa kufika kwenye moja ya nyumba. Tukashuhudia jinsi watoto wengi wa kike wakishushwa kwenye magari hayo. Amina akachukua kamera yake, na kuanza kurekodi matukio yote yanayo endelea, huku akizivuta karibu sura za wasichana hao, weñgine walipaswa kuwa mashuleni, ila ndio hivyo wametekwa.
Nikamuona Phidaya akisukumwa, kitoka kwenye gari alilo kuwepo, kuanguka kwake chini, kukanifanya nitake kujitoa muhanga, ila Amiña akaniwahi
"Umataka kufanya nini?"
"Mke wangu yule"
"Kwahiyo? Hembu tumia akili, wewe huoni walivyo wengi. Unadhani utapona?"
Amina alizumgumza huku akiwa amenikandamiza ukutani kwa nguvu zake zote.
Nikamshuhudia askari mmoja akimpiga Phidaya mgongoni kwa kutumia kitako cha bunduki mgongoni, baada ya Phidaya kukataa kunyanyuka, chini.
"Amina tunasubiria nini?"
"Ngoja kua mvumilivu"
Amima akiwa anaendela kurekodi, nikalichunguza eneo zima, nilawaonà askari wote katika maeneo walio kaa. Nikachukua kiwambo cha kuzuia sauti na kukifumga kwenye bastola yangu. Nilipo hakilisha kila kitu kipo sawa, sikuhitaji kusubiri, nikaanza kufyatua risasi kwa askari mmoja baada ya mwengine, nilianza kuwamaliza pasipo wao kujijua wanakwisha, kutoka na bastola yangu kuto kutoa mlio wa aina yoyote. Ñikaanza kusonga mbele pasipo kuhofia kitu cha anai yoyote, huku nikowa nahasira kali dhidi ya askari walio mtesa mke wangu
Askari hao wakastuka, baada ya Amina kumlenga mmoja, kwa bahati mbaya akamkosa na risasi ikapiga katika tairi la gari moja na kulifanya litoe mlio. Yakaanza majibizani ya rusasi kati yetu na watekaji hawa, haikuwa kazi rahisi kwani, wengine waliongezeka wakitokea kwenye meli waliyo kua wakiisubiria kuja kuwabena Phidaya na wezake.
"Nimezaliwa siku moja, nitakufa siku moja"
Nilizungumza baada ya kuona mashambulizi yakianza kutuelemea upande wetu, isitoshe risasi zilitupungukia. Ikatulazimu kuokota baadhi ya bunduki za askari walio fariki, Kusema kweli, Amina anajua kujituma, jinsi anavyo piga risasi unaweza kuhisi ni mwanaume, kumbe ni mwanamke. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi tulivyo zidi kuanza kuwamiliki maadui zetu, wengi tuliweza kuwaua, hadi tukafanikiaa kufika katika eneo wipo lala chini Phidaya na wenzake. Maadui zetu wakaanza kukimbia ovyo, baada ya mashambulizi kuwa makali sana. Ikawa ninafasi kwetu kuhakikisha wanaondoka kabisa, wengine wakaingia kwenye meli yao.
"Unakwenda wapi?"
Amina aliniuliza baada ya kuniona nikikimbili kwenye meli hiyo, ambayo hadi kuwashwa kwake na kuondoka ni shuhuli kubwa sana.
"Walinde hawa"
Nikadi kukimbia, huku mkononi mwangu nikiwa nimebeba bumduki aina ya AK 47, walizo kua wakitumia hawa maadui. Nikafanikiwa kuingia ndani ya meli, Kazi yangu ikawa ni moja tu, kuhakikisha haondoki adui hata mmoja katika eneo hili. Nikafanikiwa kuwateketeza karibia wote.Taratibu nikaanza kunyata kuelekeà chumba cha manahoza, kitendo cha kufungu mlango, nikastukia nikirudishwa nyuma kwa kupigwa teke la uso. Kwa bahati mbaya nikajikuta nikiiachia bunduki na ikaangukia mbali nami.
Nikanyanyuka na kukutana na jitu refu kwenda juu. Nikamtazama vizuri jinsi alivyo jazia misuli yake, kwa haraka haraka nikamfananisha na mwana mereka mmoja nchini Mareni, anayevitwa 'BIG SHOW'. Likanza kurusha makonde ambayo nilianza kuyakwepa, kutokana na urefu wake, ninamfikia kiunoni, kwa kimo changu. Katika kukwepa kwangu, akanibahatisha kunitandika teke moja, la miguu. Nikajikuta nikianguka kifudi fudi. Akaninyanyua na kuñirusha kwenye mapipa yaliyopo karibu nasi, nakunisababishia maumivu karibi mwili mzima.
Likanifwata na kujaribu kuniinua, ila nikalikwepa. Kwa haraka nikanyanyuka, nikaanza kumpiga mateke ya miguu. Likanza kuyumba. Nikazidisha juhudi ya kulipiga miguuni hadi likaà nnguka chini. Ñikaiokota bunduki yangu, nikataka kufyatua risasi ila hapakuwa na risasi iliyo toka.
Likaanza kucheka kwa dharau. Huku taratibu likinyanyukà . Nikaitoa magazine na kuikuta haina risasi hata moja. Nikaanza kurudi nyuma kwenda kilipo chumba cha manahoza. Nikaingia ndani, nalo likazidi kumifwata. Ndani ya chumba hichi nikakuta, masanduku mawili yaliyo wazi, huki yana pesa nyingi dola za kimarekani. Ninaamini mtu huyu ndio alikua mnunuzi wa wasichana hawa. Likaanza kunirushia mskonde mazito. Sikutaka kurudi nyuma zaidi ya kukabiliana nalo, kufa na kupona.
Baadhi ya ngumi zake zikawa zinanipata kisawa sawa mwilini mwangu. Sikulaza damu, na mimi nikazidi kujituma kupigana, huku ngumi zangu nikijitahidi kupiga kwenye sehemu za viungio vya mwili wake. Taratibu likaanza kulainika, hata ngumu kurusa likaanza kushindwa kwani, nilimpiga sana kwenye viungio vya mabega, tena kwa kujaribu kupanda kwenye baadhi ya meza, ili kumfikia kwenye mabega yake.
Nikafanikiwa kuona sime mbili zikiwa zimechomekwa kwenye moja ya kabati la vioo. Nikazichukua zote mbili na kusimama, nikilisubiria jitu hili kunyanyuka, baada ya kuanguka chini.
Likafungua moja ya droo, likkatoa bomu la kutega kwa sekunde
"We are going to die, kid”(Tunakwenda kufa mtoto)
Lilizungumza huku likiminya minya batani za bomu hilo, kwa haraka nikakimbia, mguh mmoja nikakanyaga kwenye meza, nikajinyanyua juu, sime moja nikà ishusha kwenye mkono wake ulio shika bomu na kukatika, bomu likaangukia pembeni, jamaa akaanza kulia kwa maumivu makali huku damu ikiwa inà mtoka kwa wingi, mkononi mwake.
Nikaliokota bomu, nikakuta zimebaki dakika mbili, kabla halijalipuka. Nikamkata mkobo wake wa pili, na kumzidishia maumivu. Nikatupa sime pembeni, nikachua masanduku ya pesa na kuyafunga, bomu likawa limebakisha dakila moja na sekunde kumi.
"Your going to die grand paaa"(Unakwenda kufa babuu)
Nilizungumza huku nikilichukua bomu na kulidumbukiza kwenye mshati wake. Nikayabeba masanduku haya yenye kilo kilo moja zsidi ya ishirini. Yakanifanya nishindwe kutembea kwa kasi. Nikazidi kujotahidi kukimbia huku nikiwa nimeyabeba. Mlipuko mzito ukaanza kusikika nyuma yangu, ukitokea kwenye chumba cha manahoza. Pembeni nikaona dirisha la kioo, nikalivunja kwa kutumia masanduku haya ya chuma, nikajirusha kwenda chini, kwenye maji huku nikiiacha meli ikizidi kulipuka kwa moto mkali.
Kitendo cha mimi kuzama, ndani yà maji ikawa ndio pona pona yangu, kwani moto mkubwa ulizidi, kurindima juu ya maji, Masanduku yenye pesa yakaanza kunishiñda nguvu, ikanilazimu kuyaachini, yakazidi kwenda chinni. Taratibu nikaanza kujilegeza mwili wangu na kuanza kw, hadi nikatolea usawa wa bahari.
Nikailuta meli ikiendelea kuteketea kwa moto mkali, nikatazama sehemu nilipo waacha Amina na wezake ila sikuzioa gari mbili zilizo kua zimewabeba.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com