SORRY MADAM (109)

0
SEHEMU YA MIA MOJA NA TISA
ILIPOISHIA...
Nikamfwata Phidaya alipo, akanionyesha video aliyo rekodi, goli lililo pita katikati ya miguu yangu
"Mwanao amekupiga tobo"
"Huyu mtoto, ananguvu za miguu kama hadi ananiogopesha, skija golini"
"Ndio hivyo tumepata mchezaji, mzuri tusubirie atakaye kuja sijui atakuwaje"

NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU

SASA ENDELEA...
"Huyo naomba awe wa kike"
"Kweli ehee"
"Au wewe unataka aweje?"
"Vyovyote Mungu atakavyo tubariki, nenda uwanjani wamesha rudi na mpira"

Mechi ikaendelea huku mipira mingi ikielekezewa golini kwetu, baada ya wachezaji wangu kuchoka sana. Ikanikazimu mara kadhaa nikaiokote mipira inayotoka nje ya goli letu. Mpira mmoja ukapigwa na mchezaji wa timu ya Junio, ukaenda mbali kidogo. Nikaanza kuukimbiza kwa bahati mbaya ukagonga glasi mbili za juisi zilizo wekwa kwenye kijimkeja, huku pembeni yake akiwa amelala, kifudifudi msichana mmoja, aliye valia chupi na sidiri, akiota jua na juisi zikamwagikia ubavunini.

"Ahaaaaa jamani"
Akanyanyuka, kitendo cha kunitazama usoni akastuka, kwani ni Sheila. Macho yake akabaki akiwa amenitumbulia. Sikuonyesha dalili yoyote ya kustuka kwani tayari ninatambua kitu kinacho endelea na anatambua kwamba mimi ni marehemu niliye zikwa wiki kadhaa za nyuma.
"Am sorry Madam"(Samahani bibie)
Nilibadilisha sauti yangu na kuifanya ya besi. Nikauokota mpira na kuondoka pasipo kutazama nyuma. Nikafika uwanjani, muda wa kucheza ukawa umeisha. Nikamuona Sheila, kwa mbali akiondoka akielekea kwenye hoteli ya pembeni yetu, huku akiwa amejifunga kipande cha mtandio kiunoni mwake. Akaingia kwenye hoteli hiyo yakifahari kama ya yakwetu.

'Sipo nao mbali'
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiondoka na familia yangu. Tukafika ndani na kumkuta Shamsa akiwa anatusubiria sisi, ili tupate kifungua kinywa.
"Jamani mbona mumejaa michanga hivyo?"
Shamsa alituuliza baada ya kutuona mimi na Junio tukiwa tumechafuka sana.
"Si hiyo mijimipira yao. Nendeni mukaoge la sivyo hamuli leo"
"Jamani ndio munatutelekeza na mwanangu"
"Ndio nendeni mukaoge"
Nikataka kuokota soseji moja ila Phidaya akaniwahi kunidaka mkono

"Hembu tuachie uchafu wako, nenda ukaoge tunasikia njaa wezenu"
"Tangu lini njaa ikasikika"
"Banaa ehee hivyo hivyo"
"Sema nahisi njaa, sio nasikia njaa"
"Eddy mbona mchokozi lakini, unakuka kuniudhi mapema yote hii"
"Naombaaaa"
"Nini?"
"Kasoseji kiduchuuuuuu"
"Jamani huyu mwanaume mmero ahaaaa"
Phidaya akanikatia kipande kidogo cha soseji na kunilisha.

"Mambo si ndio hayo, kamuogesheni Junio nasikia maji yanamwagika tu huko bafuni kwake."
Nikaingia bafuni kwetu na kuanza kuoga, huku nikiwa na furaha ya mpango wanguy wa kumteketeza John, unaanza kukamilika, kutokana Sheila hajanistukia kwamba ni Eddy mimi na sio Fredy waliye muua.
Nikarudi sebleni nikiwa nimevalia nguo nyengine. Tukapata kifungua kinywa. Tukapamba eneo zima la sebleni kwa ajili ya kesho, siku ya kuzaliwa kwa Junio. Phidaya na Shamsa wakasaidiana kutengeneza keki kubwa. Nikavaa sweta lenye kofia pamoja na miwani nyeusi. Nikawaaga kwamba nakwenda kununua vitu baadhi kwa ajili ya kesho. Nikafika kwenye hoteli ya jirani yetu, inayo onekana mmiliki akiwa ni mmoja kutokanana kufanana majengo yake kufanana sana.

Nikaikuta gari ya John kwenye maegesho ya hoteli hii, nikatafuta sehemu ya watu kukaa, nikajipatia kinywaji taratibu nikaanza kushusha tumboni mwangu, huku nikitazama anayetoka na kuingia kwenye hoteli hii yenye watu wengi tofauti na yakwetu, iliyo tulia sana.
Hadi kagiza kanaingia sikumuona John wala Sheila wakiwa kwenye eneo hili, nikahisi kukata tamaa ya kuwaona. Nikapiga fumba la mwisho la juisi yangu ninayo kunywa. Nikasimama na kujiweka sawa, kabla sijatoka nikawaona John na Sheila wakiitoka ndani ya lifti, iliyo toka gorofa za juu, wakielekea hadi sehemu ilipo kaunta ya vinywaji. Wakaagizia vinywaji, baada ya muda kidogo John akambusu Sheila na kwenda maeneo ya vyooni.

Nikaelekea sehemu alipo Sheila, nikasimana upande wake wa kushoto. Taratibu nikavua miwani na kuiweka juu ya meza kubwa iliyopo hapa kaunta.
Nikamuonyesha muhudumu mzinga wa whayne ninao uhitaji, jambo lililo mfanya Sheila kunitazama huku akiwa amenitumbulia mimacho. Mwili mzima ukaanza kumtetemeka kwa woga, hata simu yake kubwa aliyo ishika ikaanguka chini.

Nikalipa pesa ya mzinga huo, nikamuona John, akiwa anatoka kwenye mlango wa chooni. Nikavaa miwani yangu, taratibu na kuanza kuelekea mlango wa kutokea nje. Huku John akipita nyuma yangu bila ya kunijua. Kwakupitia kioo cha mbele yangu, nikamuona Sheila akininyooshea kidole, mimi huku, akizungumza na John, aliyekua akimbembeleza kutokana, analia kwa woga. Nikatoka nje ya mlango wa hotel. hii.

"Am sorry brother, please wait for me"(Kaka samahani naomba unisubirie tafafadhali)
Niliisikia sauti ya John, ikiniita kwa nyuma na kunifanya nisimame huku chupa yenye whyne, nikiishika vizuri, kwa lolote litakalo tokea kati yetu, huku nikimsubiria kwa hamu anifikie nilipo.

Nikawaona polisi wawili wakija mbele yangu, jambo lililo nifanya nishindwe kufanya kile nilicho hitaji kukifanya mbele ya John. Nikapiga hatua kwenda mbele, huku nikiipuuzia sauti ya John inayo niomba nisimame. Sikuelekea kwenye hoteli yetu kuepukana na kugundulika sehemu ninayo ishi. Nikafika kwenye kundi la watu wanao elekea barabarani, nikajichanganya nao. Nikageuka nyuma na kumuona John akiendelea kunifwata kwa nyuma

'Ngoja nimpeleke peleke huyu mwehu'
Nikazidi kutembea kwa mwendo wa kawaida, hadi nilipo fika kwenye moja ya eneo lililo tulia. Nikasimana na kugeuka nyuma na kumkuta John akiwa ananikaribia kunifwata.

"Brother....."(Kaka.....)
John hakumalizia sentensi yake na kubaki akinitumbulia mimacho.
"Can i help you?"(Ninaweza kukusaidia?)
Nilimuuliza John anaye nishangaa, huku sauti yangu nikiifanya nzito, tofauti na sauti ninayo itumia siku zote na iliyo zoeleka na watu wengi.

"You... you kno......"(Una.....una jua)
John alibabaika kiasi kwamva hata hata alicho kipanga kuzungumza kilimtoka kichwani.
”Samahani nilikufananisha"
John alizungumza huku akiondoka kwa aibu, na kutazama tazama chini. Kitu kilicho nifanya nishindwe kumdhuru John ni kamera za ulinzi zilizo fungwa barabarani. Ambazo zipo kwa ajili yàkuchukua matukio yote yatakayo tendeka barabarani hususani ya madereva wanao kwenda kwa kasi. Na endapo ningefanya lolote baya ingekuwa ni viguu kwangu kutoka nje ya nchi hii ya Brazili.

Nikamuona John, akirudi Hotelini, ambapo si mbali sana na sehemu tulipo. Ikapita taksi, nikaisimamisha na kuingia ndani, mikamuomba dereva anifikishe kwenye hoteli niliyo fikia jambo lililo mshangaza dereva taksi kwani umbali huo, mtu anaweza kutembea kwa miguu.

"I will pay you"(Nitakulipa)
Dereva taksi akafanya kama nilivyo muagiza. Njiani tukampita John, akirudi hotelini, wala hakuweza kuniona mimi ndani ya gari. Nikafika hotelini. Nikampa dereva kiasi anacho kihitaji. Kabla sijashuka nikamuona John akiingia kwenye hoteli waliyo fikia huku, akitembea kwa mwendo wa haraka akionekana kumuwahi mpeñzi wake Sheila.
***
Nikaingia ndani na kuwakuta Phiday na wanae wakitazama movie kwenye tv, kubwa iliyopo sebleni.
"Mbona umechelewa kurudi?"
Phidaya aliniuliza huku akinyanyuka kwenye sofa, akanipokea chupa ya whyne niliyo ibeba. Akanibusu mdomoni.

"Nilikya nashangaa shangaa mji tu"
"Mmmm masaa yote hayo?"
"Ndio, pia kuna kazi nilikua nikiifanya, nitakuambia nikiwa nimetulia"
"Sawa, muda wa chakula, tulikua tunakungoja wewe"
"Dady umesha wahi kuiona movie ya Death Race?"
"Hapana"
"Njoo uicheki"
Nikakaa sehemu alipokua amekaa Phidaya, katikati ya Shamsa na Junio

"Jimovie lenyewe ndio wanauana hivyo?"
Nilimuuliza Junio baada ya kushuhudia tukio la filamu hiyo, ikionyesha mtu akiuliwa vibaya na gari moja kubwa, lenye watu wanao piga risasi.
"Yeaaah wamelipuka, dady cheki kule cheki"
Junio alizidi kupendezewa kwa tukio la gari hilo kubwa kugonga kwenye vyuma vyenye ncha kali na kulipuka vibaya.

"Sasa Junio mwanangu, hapo ni kipi kinacho kufurahisha?"
"Dady lile jigari likubwa lilikua likiwashambalia Frank Sting na Joe"
"Eddy narudia tena kukuambia, kwamba umeniharibia mtoto. Hapo hajaanza shule, anawajua masteringi wa movie hizo kama ndio wazazi wake"
"Usimlaumu hata mimi nilivyo kua mtoto nilipenda kutazama sana movie. Junio stering anaitwa nani?"
"Jansan Stathan au Frank Sting"
"Mmmm haya baba, nyanyuka ukale movie yako naiwekaa pause, ukimaliza utaendelea"
Tukanyanyuka sote, na kukaa meza yachakula.

"Shamsa mbona kama haupo sawa?"
"Najisikia sikia kichwa kinauma"
"Umekunywa dawa?"
"Hapana, ila kitapona. Nahisi ni jinsi tulivyo tazama tv muda mrefu, imechangia kichwa kuuma"
"Mmmm pole fanya ule, kisha ukameze dawa. Sawa mwanangu?"
"Sawa baba"
Kwa mara ya kwanza Shamsa kuniita baba, jambo lililo nishanga
za sana kwani siku zote alizoea kuniita Eddy. Furaha ikazidi kuongezeka moyoni mwangu. Kwa kuona Shamsa akiniheshimu kama baba yake mzazi.

"Shamsa utaniambia nikupe dawa gani, kwa maana mimi ni dokta"
"Kweli mama?"
"Ndio nilikua dokta, muulizeni huyo baba yanu, tumetokea wapi?"
"Natamani nisome kwa juhudi, ili niwe dokta kama baba na mama yangu"
Shamsa alizingumza kwa sauti yaunyonge iliyo jaa huzuni.
"Usijali utakuwa, tutahakikisha tunakupa chochote utakacho kutoka kwetu"
Phidaya alizungumza huku akimshika shingo Shamsa kumfariji, kutokana Phidaya anatambua historia nzima ya Shamsa baada ya mimi kumuadisia, tukiwa ndani ya ndege tukija Brazili.
Tukamaliza kula, kabla kila mtu hajaendelea na shughuli yake nikawaomba wanisikilize kwa dakika chache.

"Nilipotoka, nilikwenda kupiga simu. Kuwasiliana na nyumbani nchini Tanzania."
Niliwaongopea kutokana simu nilipila siku mbili za nyuma.
"Nilitaka kujua hali ya mama, ila nikaambiwa kwamba ni mgonjwa sana, amepalalaizi na hawezi kufanya kitu chochote"
Nikamuona Phidaya akistuka kwa taarifa hiyo.
"Sasa imekuaje!?"
"Matatizo nahisi ni mambo yao yakisiasa, wamechezeana."
Ilibidi kuficha kwamba John ndio chanzo wa tatizo la mama, baada ya kumuua Fredy ninaye fanana naye sana.

"Dady wamemchezea bibi mziki?"
Swali la Junio likatuashiria kwamba haelewi kitu tunacho kizungumza kwa wakati huu.
"Eheee"
"Kina nani hao?"
"Watu tu utakwenda kuwaona mukienda Tanzania"
"Ngoja Eddy, umesema tukienda Tanzania, ina maana wewe hauendi?"
"Kuna kazi itanilazimu kuifanya hivi karibuni, itawalazimu nyinyi kwenda kabla yangu."
"Kazi gani?"
"Nilikuambia nitakuambia, nikitulia mke wangu"

Tukamaliza mazungumzo, nikaondoka na kuingia chumbani kwetu, nikafanya maandalizi ya kulala, baada ya muda Phidaya akaingia na kukaa kitandani
"Baby ni kazi gani inayo kufanya ubaki huku peke yako"

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI

KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)