SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Maelezo ya Pretty yalijitosheleza vizuri hadi kuyaelewa.
"Umechukua hatua gani juu ya hizu video?"
"Sijafanya lolote kutokana sijui lakufanya juu ya hizo video"
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
"Alafu John anafunga lini ndoa yake"
"Zimebaki siku kama tatu"
"Ahaaa"
"Kuna kazi nitahitaji unisaidie"
"Kazi gani"
"Nitakuambia"
***
Mchana mida ya saa saba, nikampigia simu John, akaniambia nimtembelee kwenye chumba chao wanapo ishi na mke wake. Kutokana chumba chao kinatazamana na chumba cha Pretty nikamuomba Pretty kwenda naye. Tukagonga kwenye mlango wao, Sheila akatufungulia, akafurahi sana kutuona. Akakumbatiana na Pretty. Tukaingia ndani na kumkuta John akiwa sebleni akitazama katuni.
"Ohooo karibuni sana wapendwa"
John alitukaribisha huku akiwa na furaha sana.
"Asante kaka"
"Alafu mumependezana musitake kuniambia kwamba nyinyi si wapenzi"
"Ndio tupo kwenye mpango wa kuvishana pete"
Ptetty alijibu huku akinishika kiuno. Tukakaa kwenye kochi, Sheila akatuandalia vinywaji. Taratibu tukaanza kuvinywa huku tukipiga stori za jana usiku.
Kipindi cha kinacho onyesha makatuni kikakatwa na kurusha habari iliyo wafikia hapo studio kwao(Breaking News)
"Ndege ya shirika la KLM imelipuka"
Niliyasoma maneno hayo yaliyo niatua kiasi cha kunikosesha raha.
"Yes mpango umekwenda vizuri kama nilivyo panga"
John alionekana akiwa amefurahi sana kwa habari hiyo. Iliyo onyeshwa kwenye kituo hichi cha habari. Hii ni baada ya muandishi huyo kudai kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea nchini Brazili, kwenda bara la Afrika. Abiria wote waliomo ndani ya ndege hiyo wamekufa kwenye mlipuko huo wa ndege ulio tokea majira ya mida hii ya mchana, jambo lililo nipa wasiwasi mwingi, hadi nikajihisi mwili mzima kuishiwa na nguvu.
Pretty akamtazama John kwa umakini huku akionekana kuwa na mshangao mkubwa.
"Unafurahia nini?"
"Kuna mpango niliupanga na vijana wangu, kuhusiana hiyo ndege"
"Unataka kusema wewe umehusika kwenye mpango wa hiyo ndege kulipuka?"
Pretty alimuuliza John huku akimkodolea macho ya wasiwasi. Mimi hata nguvu ya kunyanyuka kwenye kochi sikuwa nayo hii yote ni kwakuiwazia familia yangu.
"Ndio"
"Kwanini?"
Kuna mjinga nilimuua, sasa ulikua muda wakuiteketeza famia yake"
Nikastukia kumuona Pretty akinyanyuka kwa hasira na kumrukia John, hadi sofa alilo likalia wakaaanguka nalo. Sheila akasimama kwa haraka na kumchomoa Pretty aliyekuwa akimshambulia mumewe kwa kumpiga kwa makofi mfululizo.
"Wewe ni gaidi"
Pretty alizungumza kwa hasira, huku mimi nikiwa nimepigwa na bumbuazi lililo nifanya nishindwe kufanya kitu cha aina yoyote.
"No no nakudanganya Pretty"
John alizungumza huku akicheka.
"Muongo wewe"
"Kweli Pretty siwezi kufanya kitu kama hicho. Kwanza nitaanzia wapi. Eti Henry kweli ninaweza kufanya jambo hili?"
Nilitabasamu tu, hata kinywa changu kikashindwa kufunguka. Tangu nizaliwe sijawahi kukumbana na hali ya mshangao kama hii, iliyo nimaliza nguvu zote.
Pretty akafungua mlango na kutoka huku akiubamiza kwanguvu. Jambo lililo nistua na kurudi kwenye hali yangu yakawaida. Nikanyanyuka kwa haraka na kumfwata Pretty ndani kwake
"Nilazima nimpeleke polisi nikamstaki"
Pretty alizungumza kwa hasira huku akiingia chumbani kwake. Nikamfwata na kumkuta akiwa amekaa kwenye kitanda huku akilia.
"Pretty nisikilize, kitu kimoja"
"Nahitaji zile video mbili kama una flash zihifadhi sawa"
Pretty alibaki akiwa amenikodolea macho. Nikatoa simu mfukoni na kuingiza namba za Blanka. Ikaita kwa muda mrefu, kisha ilapokelewa.
"Blanka wamefika?"
"Hawajafika"
Jibu la Blanka likanifanya nizidi kuchanganyiliwa, hadi mwili ukawa unanitetemeka kwa woga kwani swala la akufiwa nafamilia tena kwa wakati mmoja, sikuliwazia kichwani mwangu.
"Hawajakupigia?"
"Hapana hawajanipigia"
Nikakata simu nakushusha pumzi kubwa, nikabaki nimesimma pasipo kuzungumza kitu chochote na Pretty. Nikamshika mkono Pretty na kumnyanyua juu.
"Twende kwangu"
"Kufanya nini?"
"Twende tu"
Tukatoka sebleni, Petty akaziingiza video zote mbili kwenye flash, kisha akachukua begi lake lenye laptop.
Tukaondo hadi nyumbani mwangu. Kitu cha kwanza nikaifwata simu ya chumbani kwangu. Nikamiinya kitufe cha kusikiliza ujumbe wa sauti, ili kutambua kama kuna ujumbe wowote wa suti ulio ingia nikiwa sipo.
"Eddy mume wangu, mbona hupokei simu?"
Ilikuwa nisauti ya Phidaya, kwenye ujumbe wa kwanza wasauti
"Tumeamua kubadilisha safari, tupo Marekani kwa sasa. Shamsa ndio alitoa pendekezo la sisi kubadilisha safari. Ukipata ujumbe huu usiwe na wasiwasi, tupo salama na kesho tunakwenda Tanzania. Nakuupenda mume wangu"
Ujumbe wasauti, ukawa umekwisha. Nikashusha pumzi nyingi, huku tabasamu pana likiwa usoni mwangu. Nikatoka sebleni na kumkuta Pretty akiwa anaminya minya batani za laptop yake.
"Unafanya nini?"
"Nachapisha habari za kumchafua John kwenye mtandao na kuituma hii video ya mauaji"
"Hapana usifanye hivyo"
"Kwanini?"
"Nataka kumuua John taratibu"
"Kumuua taratibu!?"
"Ndio"
Nikaanza kumuadisia historia nzima ya maisha yangu. Kuanzia nilivyokua shule na John hadi leo ni adui yangu.
"Sasa kwanini hutaki tumuue sasa hivi?"
"Pretty mpango wangu ni mrahisi sana. Nataka kumuua kwa kifo chakumzalilisha na kumtesa sana."
"Ila familia yangu ipo salama"
"Kweli?"
"Ndio"
Pretty akanikumbatia kwa furaha, huku machozi yakimwagika kwani historia yangu ilimuuzunisha sana.
Siku ya pili, tukakutana na John na Sheila wakiwa kwenye maandalizi. Ikamlazimu Pretty kuwaomba msamaha kwa kile kilicho jitokeza jana mchana. Hii ikiwa ni moja ya mpango wetu wa kumteketeza John na Sheila, pasipo wao kujua chochote.
"Nilijua tu nihasira, mimi nimemsamehe"
John alizungumza huku akimpa mkono Pretty.
Ikawa ni furaha kubwa sana kwa John, na Sheila wake. Wakiamini urafiki wetu utaendelea kama kawaida na laiti wangejua wasinge ruhusu kujipendekeza kwetu.
***
Siku ya harusi ya John ikawadia, mimi na Pretty tukawa nimiongoni mwa waalikwa kwenye sherehe hii ndani ya kanisa hili kubwa la Roman katolic.
"Kila kitu umekipanga sawa?"
Nilimuuliza Pretty mara baada ya kufika kanisani, tukishuka kwenye gari yetu aina ya BMW, tulilo linunua jana kwa kazi moja tu iliyopo mbele yetu.
"Kila kitu kipo powa mpenzi"
Kabla sijazunguza chochote simu yangu ikaita kwa namba ya Blanka, ndio inayo nipigia.
"Nipigie bwana"
Blanka alizungumza kwa furaha, ikanibidi nikate simu na kumpigia.
"Ndio kaka Eddy. Kweli wewe nikiboko"
"Kwanin?"
"Yaaani toto lako nikopi na wewe yaani umefanya kazi kubwa kulitafuta"
"Kwani wamefika?"
"Ahaaa ndio nipo hapa uwanja wa ndege nimewapokea yaani weee acha tuu. Ninafuraha yakufa mtu"
"Hembu mpe Junio simu nizungumze naye"
"Dady tumefika Tanzania"
"Umemuona antie?"
"Ndio, ila kuna joto kali"
"Poleni mwanangu, mpe mama simu"
Nikasikia sauti ya Junio ikimuita Phidaya, furaha ikazidi kuongezeka moyoni mwangu, nakujiamini zaidi kwamba kazi yangu inazidi kuwa nyepesi zaidi.
"Mume"
"Niambie mke wangu"
"Safi, tumesha fika Tz yaani hapa nijoto"
"Sasa hivi nisangapi?"
"Saa.....saa tano inakwenda saa sita usiku"
"Poleni kwa uchovu"
"YÃ ani wee acha tu, yaani tumetoka Marekani jana alfajiri, tunashukuru Mungu ndege tuliyo panda haikupita kwenye nchi nyingi"
"Ilikuwaje mukaenda Marekani?"
"Hilo swali muulize mwanao Shamsa"
"Mpe simu"
"Vipi wewe"
"Ahaaa safi baba"
"Hembu sogea pembeni uniambie nini kilitokea?"
"Wee acha baba, kipindi tupo uwanja wa ndege kuna jamaa nilikua ninamtilia mashaka, sasa tulipo maliza kukaguliwa. Kipindi sasa tunaelekea kupanda basi lile linalo wapeleka watu kwenye ndege"
"Ndio"
"Basi roho yangu ilisita, nikamuambia mama hatuwezi kuondoka. Nashukuru mama alinielewa ikatulazimu kuuza tiketi kwa kisingizio tumepata msiba wa gafla Marekani"
"Tukaweka booking kwa ndege iliyokua inaondoka saa moja usiku, basi tukaondoka"
"Duuu umefanya la maana sana mwanangu. Una habari?"
"Ya nini?"
"Ile ndege, mulio kuwa mukitaka kupanda. Imelipuka"
"Weeee"
"Na mtu uliye kua unamtilia mashaka ndio huyo John"
"Yupoje?"
"Mrefu kiasi, mweusi si sana na ana macho makubwa hivi"
"Ahaaa nilimuona pale ulivyo ndoka basi akawa anatutizama sana"
"Mimi aliniona?"
"Hakukuona kutokana alikuja dakika kama tatu hivi baada ya wewe kutuacha"
"Hei ibada inataka kuanza"
"Pretty alizungumza kwa sauti ya chini huku akinionyesha ishara nikate simu.
"Ok nitawapigia baadaye"
Nikakata simu, shamsa akanishikaa mkono, tukaingia kanisani. Tukakaa viti vya mbele huku, tukiwa na hamu yakuwashuhudia maharusi wetu. Mlio wa kinanda, wakuwaruhusu maharusi kuingia kanisani, taratibu ukaanza kulia. Vitoto vidogo vipatavyo kumi, vitano vikiwa vya kiume na vitano vikiwa vya kike wakawa wametangulia mbele, huku John na Sheila wakifwata kwa nyuma.
"Mpango mbona kama utaaribika?"
Nilimuuliza Pretty kwa kumnong'oneza kwa sauti ya chini, pasipo mtu mwengine kusikia nilicho kizungumza.
"Usijali, naiaminia timu yangu"
Pretty alinipa matumaini makubwa ya kuifanya kazi yangu. John na Sheila wakafika mbele yakanisa. Ukubwa wa hili kanisa ukanifanya niwe makini sana kutazama walinzi wa John ni wapi.
Ibada ikaanza huku nasi tukipiga ishara za msalaba, kama wafanyavyo waumini wengine.
Maubiri ya hapa na pale yakafanywa na mchungaji, anaye fungisha ndoa hii. Huku akituahusia tusilipize baya kwa ubaya.
'Kakosa chakuhubiri huyu'
Nilijisemea kimoyo moyo, baada ya kusikiliza maubiri yake kwa umakini, na yote nikahisi yananihusu mimi.
Muda wakuvishana pete ukawadia, Prettyakatoa simu yake kwenye pochi yake.
"Unataka kufanya nini?"
"Subiri uone"
"Coletha Agray upo tayari kumpokea John, kuwa mume wako wa maisha, kwenyeshida na raha, afya na magonjwa hadi pale kifo kitakapo watenganisha?"
"Ohooooo aiiiiii mmmmmmmmm"
Sauti za mahaba zilisikika kutokea kwenye vipaza sauti vilivyomo humu kanisani. Kila mmoja akawa amekodoa mimacho kila upande. Gafla tv zote zilizo kuwemo ndani ya kanisa hili, zikabadilisha picha kutoka katika matukio yanayo endelea humu kanisani hadi kwenye video ya ngono, aliyo cheza Sheila miaka kadhaa ya nyuma.
Kila mtu akajikuta mdomo wazi, ila tukio hilo ninatambua Pretty ndio amelifanya litokee. Nikamuona Sheila akitazama chini, huku mchungaji akiweka miwani yake vizuri, akitazama tv iliyopo pembeni yao. John akaanza kuhaha, huku akizungumza na msimamizi wake hata kama kuna jinsi ya kuzisimamisha video hiyo ifanyike.
Sheila akashindwa kustahimili kusimama, akadondoka chini na kutulia akazidi kumchanganya John, aliye livua koti lake kwa kuchanganyikiwa. John amampokonya kipaza sauti mchungaaji
"Wewe mshenzi uloye ziweka hizi video zitoe kabla sinakuua"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK