SORRY MADAM (112)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA MIA MOJA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
"Karibuni mabibi na mabwana kwenye mnada wetu wa uzinduzi wa gari ambalo nilakipekee"
Sauti ya dada huyo ilizungumza huku picha ya gari hilo kikionyeshwa kwenye Tv kubwa, iliyopo mbelw yetu.
"Hili gari, sifa ya kwanza haliingii risasi, hwala likipigwa bomu halilipuki"
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
Si mimi tu niliye guna, bali hata wapembeni yangu aliguna.
"Gari hii niyakisasa, kwani unaweza kuigeuza na kuwa katika muundo wa ndege, na likapaa angani kwa umbali wa mile nne kwenda juu."
"Mmmmm"
Na spidi yake likiwa angani linakwenda kwa mwendo kasi kama wa ndege za jeshi Jet"
Mwanadada huyo aliendelea kutupa sifa za gari hilo lililo zidi kutushangaza sote tuliopo ndani ya ukumbi huu. Kila alicho tueleza ndicho kilicho kuwa kikionyeshwa kwenye tv hiyo kubwa, jinsi gari hilo linavyo fanya kazi. Kusema ukweli lilinivutia, mbaya zaidi gari hilo limetengenezwa moja tu.
Taa zote zikawashwa baada ya dada huyo kumaliza kulielezea sifa zakumwaga gari hilo, lililo tengenezwa kwa vyuma vigumu, pamoja na madini ya dhahabu. Muda wa gari hilo, lililetwa mbele yetu, kila mmoja akapata fursa ya kuliona, kwa macho yake.
Watu wakaanza kutaja bei za kulinyakua gari hilo, akiwemo John.
"Paund laki nne"
John alizungumza nakuwafanya watu kumtazama. Kwani ni pesa nyingi.
"Paundi laki nne na nusu"
"Paundi laki tano"
"Paundi laki sita"
John aliendelea kuminyana na vigogo matajiri wenye peaa zao waliomo ndani ya ukumbi huu.
"Paundi laki nane"
John alizungumza nakuufanya ukumbi mzima kuzizima, huku sauti ya dada anaye pigisha mnada akihesabu taratibu.
"Pauni milioni moja na nusu"
Nilizungumza kwa kujiamini sana, watu wote wakageuka na kunitazama. John na Sheila wakanitazama kwa macho yamshangao.
"Kwa mara ya kwanza kwa bwana nani?"
"Henry Derulo"
"Kwa mara ya kwanza kwa bwana Henry"
"Kwa mara ya pili kwa bwana Henry"
"Milioni mbili paundi"
John alizungumza huku akinitazama.
Nikamuona Sheila akitabasamu sana.
"Pauni milioni nane"
Nilizungumza kwa kujiamini nikamuona John akifumba macho yakukaya tamaa, kwani pesa niyo itaja nikubwa sana katika ulimwengu wetu huu. Nilitaja pesa hiyo huku nikiwa sina pesa hiyo.
Nikamuona John akinong'onezana na Sheila.
"Paumi milioni kumi"
John alizungumza, na kunifanya nimpigie makofi kwa ishara ya kumpongeza.
John akafanikiwa kuwa mshindi wa gari hilo. Baada ya zoezi hilo kila mtu akaendelea na kujipa burudani ya kutembea popote ndani ya ukumbi huo na ujipatia burudani tofauti tofauti.
"Eddy wewe ni nani?"
Pretty aliniambia baada ya kunifikia.
"Mimi ni Henry, kwani vipi?"
"Pesa yote umeitoa wapi uliyo kuwa umeitaja?"
"Usijali ni pesa ndogo"
"Ndogo mmm.."
"Nakuona upo na tajiri"
John alizungumza baada ya kutufikia tulipo akiwa na Sheila
"Hapana wewe ndio tajiri,"
Nilimjibu John huku nikitabasamu.
"Naitwa John huyu ni mke wangu Coletha"
Nikatabasamu kwanu ushindi wa kuwateketeza John na Sheila.
"Naitwa Henry"
"Tunaweza kuwa marafiki na kushirikiana katika biashara kama hivi?"
"Ndio tunaweza kuwa"
John akanipa mkono huku akinikumbatia pasipo kujua mbaya wake nimerudi.
"Basi tuwasiliane kwa namba hii"
John akanipa kikadi chenye namba yake ya simu. Sauti yangu nilizidi kuibadilisha ili wasizidi kunigundua.
"Henry, tangulia nyumbani, mimi nitarudi baadaye"
"Prety kwani unaishi na Henry!?"
Shamsa aliuliza huku akishangaa
"Ndio, ni rafiki yangu wakipindi kirefu sana"
"Ahaaaa sawa"
Prety akanikumbatia, akanibusu shavuni kisha akatuaga na kurudi kwa zee lake lililo kua likizungumza na watu wengine.
"Hivi Henry wewe unajishuhulisha na nini?"
"Mimi ni mfanya biashara wamagari, nimewekeza kwenye baadhi ya nchi kubwa duniani"
Niliongopea kila nilicho kizungumza, ili kuzidi kuwaleta John na Sheila wake karibu.
"Ahaaa mimi ninamiliki hotel kubwaAfrika kusini, Tanzania, Uganda, Kenya"
"Ahaaaa, hivi biashara ya Hotel inalipa sana?"
"Inalipa tena sana, tukikaa vizuri tutazungumza kuhusiana na biashara hiyo. Vipi wewe magari yanalipa?"
"Kwakiasi chakr yanalipa. Unakua kama hii teknolojia iliyo tengeneza hili gari. Kama ningelinunua mimi, ningelipeleka kwa mainjinia wangu wakaliunda kama hili, na pesa ingeendelea kuingia"
"Ohoooo basi tufanye dili lakibiashara kwenye hili gari, kwani mimi ndio mmiliki halali wa teknolojia nzima kwa sasa, hata mtu ukihitaji kutengeneza gari kama hili basi utakuja kwangu kuomba kibali"
"Sawa tu..."
Kabla sijamalizia sentensi yangu, dada mmoja alimnong'oneza John kisha akaondoka.
"Jamani ngoja nikazungumze na hawa wauzaji, so baby nisubiri nakuja"
"Sawa"
John akambusu Sheila mdomoni, kisha akaongozana na dada huyo aliye mnong'oneza. Tukabaki na Sheila, aliye kuwa akitabasamu kila alipp kua akinitazama machoni.
"Vipi?"
Nilimuuliza Sheila baada ya kumuona akinitazama sana.
"Ahaaa hakuna"
"Unaonekana una wivu sana ehee?"
"Kwanini Hery?"
"Naona unawasi wasi na mumeo?"
"Hapana ila kila mtu na chake bwana"
"Hahaa haya, ngoja mimi niondoke. Jamaa akija muambie nimeondoka"
"Jamani nioe nipe japo kampani, hadi arudi tupige stori mbili tatu"
Nilimtazama Sheila kwa macho yauchokozi wa kimahaba, nikamfanya atazame chini huku akitabasamu.
'Laiti ungekua ninavyo kuchukia, wala usinge jichekesha. Malaya mkubwa wewe'
Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiweka tabasamu feki usoni mwangu.
"Mumeo anajishuhulisha na nini kingine ukiachilia mbali na biashara?"
"Yeye ni mfanya biashara tuu, hana kazi nyingine"
"Ahaa samahani lakini kwa kukuuliza hivyo"
"Hapana, mbona nikawaida tu. Wifi yangu mbona hujaja naye?"
"Sijabahatika kuwa na mwanamke"
"Kwanini?"
"Ahaaa, wanawake wanamatatizo mengi sana, kwahiyo nisinge penda sana kuumizwa kichwa katika mapenzi"
"Mmm ila inabidi utafute mwanamke, kama Prety ili kidogo uwe na familia"
"Sawa ila itachukua muda sana kuwa na mwanamke"
John akarudi akiwa na tabasamu usoni mwake, huku mkononi mwake akiwa na bahasha. Akamkabithi Sheila.
"Jonh mimi ninaondoka"
"Sawa, ila fanya tuonane hata kesho"
"Sawa kaka, nikutakie usiku mwema"
"Nawe pia, alafu kuna kadi ya harusi nitakupatia hapo tukionana"
"Sawa kaka, shem mapumziko mema"
"Nawe pia"
Nikawapa mkono kila mmoja waki, nikaondoka huku nikimiacha John na Sheila wake.
"Nahitaji wafe taratibu, bila wao kukijua"
Nilizungumza mara baada ya kukaa kwenye siti ya dereva, ya gari la Pretty tulilo kuja nalo. Nikaliwasha na kuondoka kwa mwendo wa kawaida. Nikafanikiwa kufika kwenye hotel anayo ishi Pretty pasipo kupotea njiani. Nikaingia ndani kwa Pretty na kujitupa kwenye sofa. Nikavua koti la suti na kubakiwa na shati, nikasimama na kukaa kwenye kiti kimoja cha matairi kilichopo kwenye computer zilizomo humu ndani.
Nikawasha computer niliyo onyeshwa picha za John na Pretty.
"Password"
Computer hiyo, ilihitaji niingize namba au neno la siri, ili iweze kuwaka kuelekea kwenye program, zilizo hifadhiwa ndani ya computer hiyo. Nikatoa simu mfukoni na kumpigia Pretty
"Henry vipi?"
"Poa, naomba unisaidie kitu"
"Kitu gani?"
"Namba za siri za computer ile uliyo nionyesha picha za John"
"Ahaa poa nitakutumia kwa meseji, ila umefika?"
"Ndio"
"Nakutumia"
Pretty akakata simu, ndani ya dakika moja meseji nikaingia. Nikaingiza neno la siri computer ikafunguka yote. Nikaanza kufungua baadhi ya mafaili, nikaziona picha zile zile za John na Sheila wake. Nikiwa katika kufungua mafaili mengine, nikakuta faili moja likiwa limeandikwa kwa herufi kubwa 'STOP' Huku likihitaji neno la siri ili kufunguka. Nikaingiza namba ya siri aliyo nitumia Pretty. Ila likakataa kufunguka. Nikaandika neno lenyewe la Stop, kwabahati nzuri likafunguka.
Nikakuta video mbili zikiwemo kwenye faili hili, nilalifungua video ya kwanza, ikaonyesha baadhi ya maneno yaliyo andikwa kwa lugha ya brazili nisiyo ielewa. Nikaona watu wawilii wakiwa wamesimama pembeni ya dada mmoja aliye valishwa kipande cha gunia kichwani mwake. Mijamaa hiyo, nayo imevaa vinyago vilivyo wabakisha macho na tu, huku wakuwa wameshika bunduki mikononi mwao.
Mlango wa chumba hicho walicho kuwemo ukafafunguliwa. Nikamuona John akiingia huku mkononi mwake akiwa ameshika bastola.
"Mfunueni"
Jamaa mmoja akamfungua binti huyo, nikamuona Victoria sura yake ikiwa imechakaa kwa majeraha ya kupigwa.
"John wewe ni mshenzi mpumbavu mkubwa wewe"
Victori alizungumza kwa hasira huku sura akijitahidi kunyanyuka kwenye kiti.
"Yap mimi, ndio ni mshenzi tena niliye pitiliza. Hivi ulidhani sinto kukamata?"
"Victoria nahisi hunijui mimi vizuri, kwa jina ninaitwa John Ngemela. Labda nikuambie kitu kimoja ambacho ulikikosea kwenye maisha yako."
"Sina haja ya kuju...."
John akamtandika kofi zito Victoria na kumfanya atoe ukelele wa maumivu makali aliyo yapata. Huku baadhi ya damu zikimtoka mdomoni.
"Victoria sikukupenda, nilihitaji mali zako na marehemu baba yako ambaye ulimuua kwa kumnyonga wewe mwenyewe"
"Sikuhitaji umtoroshe Phidaya na mwanae. Nilihitaji waendelee kunisujudia mimi kama Mungu wao. Nikiamini nilazima nimpate kaka yako Eddy"
Mapigo ya moyo yalianza kunienda mbio, huku hasira ikipanda taratibu.
"Sina kingine zadi ya kukuondoa duniani"
John akampiga Victoria risasi zisizo na idadi mwili mwake hadi akakata roho. Machozi yakanitiririka usoni mwangu, kwani kifo alicho kufa Victoria nichakikatili sana, japa ni haki yake kupata kifo kutokana na dhambi ya kumua baba yangu mzazi.
"John, siku zako zina hesabika"
Nilizungumza huku nikiitazama video hiyo iliyo simama baada ya kuisha. Nikashusha pumzi na kufungua video ya pili. Nikajikuta nimechoka kabisa baada ya kumshhudia Sheila, akifanya mapenzi na wanaume wawili kwa pamoja. Kumbukumbu zikanirudisha hadi siku Sheila alivyo wahi kuniambia, alishawahi kufanya mapenzi na wanaume Wakimarekani, walio mzawadia gari aina ya BMW.
"Ptetty ni nani?"
Nilianza kujiuliza maswali mengi baada ya kuzitazama video zote mbili, swali jengine ni kuhusiana na wapi alipo zitoa hizi video, ila sikupata jibu kabisa.
Asubuhi na mapema Pretty akaingiandani, huku akionekana akiwa amechoka sana.
"Hujalala Eddy?"
"Nilikua ninakusubiri nina mazungumzo na wewe"
"Mazungumzo gani?"
Nikasimama na kuzifungua video nilizo ziona zikihusiana na mauaji ya Victoria aliyo yaganya John. Pamoja na video ya ngono ya Sheila. Pretty hakuonekana kustuka, alicho kifanya ni kuja nilipo simama, kisha akazima computer.
"Video ya kwanza, niliiba kwenye laptop ya John, nikiwa ninatafuta namba za akaunti zake za benki"
"Video ya pili niliipata kwenye mtandao mmoja wa siri sana. Wanao ingia matajiri watupu ndipo nilipo iona hiyo video"
Maelezo ya Pretty yalijitosheleza vizuri hadi kuyaelewa.
"Umechukua hatua gani juu ya hizu video?"
"Sijafanya lolote kutokana sijui lakufanya juu ya hizo video"
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni