SORRY MADAM (117)
JINA: SORRY MADAM Mwandishi: Eddazaria G Msulwa SEHEMU YA MIA MOJA HAPA ILIPOISHIA... " Mungu wangu " Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka. NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU SASA ENDELEA... "Kumi na tano" Nikashika nyaya moja nyekundu na kuikata, chakushangaza, bomu likaendelea kurudisha sekunde zake nyuma. "Nane" Nikazidi kuchanganyikiwa, na kukata wanya mweusi, hali ikawa ni ile ile. "Tano" Mikono yote, ikazidi kutetemeka hadi nikaangusha kikatia kucha, nikakiokota kwa haraka, hata kukaa mkononi vizuri, nkawa ninashindwa kukishika. "Tatu" Nikamuona muhudumu, akipiga ishara ya msalaba akiashiria mwisho wetu ndio unakaribia, nikashika waya wa rangi ya kijani, sekunde ikawa imebaki moja, nami nikawa nimeukata. Sekunde hiyo ikasimama hapo hapo na bomu kuzima. Nikashusha pumzi nyingi, huku mwili wangu wote ukiwa umesha vuja jasho lakutosha had…