SORRY MADAM (68)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
SEHEMU YA SITINI NA NANE
ILIPOISHIA...
Sote tukajikuta tulicheka, kwa maana sikutarajia kuwa hawa jamaa muda huu nitakuwa ninacheka nao kwa furaha kiasi hiki
“Hapana jamani, ubabe nimeacha siwezi kumpiga mume wangu, mwenyeni ninampenda kama nini?”
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Ahaaa Dorecy leo unapenda, kwa maana ninakumbuka afande Nyendeza alikutongozaga kipindi tupo porini, acha umporomoshee mangumi”
“Hahaaaa, yule alikuwa mwehu, Eti ananitongoza huku ananilazimisha kuninyonya denda hapo hapo, kwa nini nisimpige mangumi”
“Ahahaa, jamaa tulikuwa naye hapa Chumbageni, ila alihamishwa mwaka jana kapelekwa Handeni huko”
“Dooo, muache akakutane na watoto wa kizigua wamroge hadi akome”
“Haaaha, na ule weusi lazima wamtengenezee carolaiti ya tura”
Sote tukajikuta tukicheka kwa furaha kwani, mazungumzo ya hawa jamaa yamenifanya nijihisi mchangamfu gafla
“Unajua yule ndio chanzo cha mimi kupelekwa JWTZ?”
“Weee”
“Mama vile, si alikuwa anajiona mbabe.Sasa nilivyo mpiga ile siku ticha akaniita ofisini kwake na kunihoji hoji maswali, akaniambia tangu aanze kufundisha haijawahi kutokea afande wa kike kumpiga afande wa kiume”
“Ila alikupa kabahati”
“Kiupande mmoja ninamshukuru, kwa maana alinisaidia sana”
“Sisi bwana, bado tunakula ngwamba na wananchi, nakuona wewe upo kitengo kikubwa, hadi munatembelea na V8?”
“Dulla hembu acha utani?”
“Kweli Dore unadhani ni utani? Sisi tumesha telekezwa, tunakazi ya kutembelea vidifender hivi vilivyo choka, kila siku vinakazi ya kushinda gereji”
“Ahaaaa Dulla wewe ropoka usikiwe, utahamishiwa kitivo huko ukale makabichi”
Sote tukabaki tukiwa tunachekea kwa sauti ya juu hadi baadhi ya askari walio karibu nasi wakawa na kazi yakutushangaa
“Kwenye ukweli, inatubidi tuzungumze”
“Ni kweli, ila mmmmmm”
“Jamani, naona tukikaa sana hapa, hamuta enda lindo sisi ngoja tusepe”
“Kwani, munakwenda wapi muda huu?”
“Tunataka twende pande, jeshini”
“Mbona usiku, chukueni hoteli mulale, asubuhi na mapema mudimke”
“Etii?”
“Hakuna cha etiii, njia hiyo usiku sasa hivi sio nzuri”
“Kuna majambazi?”
“Mara mia kungekuwa na majambazi”
“Ila?”
“Kuna vituko vya ajabu, unaweza kukuta watu wanakatiza barabarani wakiwa na kanzu huku wanakwenda kuzika, ukisema uwapige risasi, kesho unakufa”
“Mmmmm”
Ilinibidi nigune
“Kaka Eddy wala usigune, hii ndio Tanga bwana, ukicheza vibaya wala humalizi siku”
“Sasa hapa ni wapi kwenye Hotel nzuri?”
Dorecy aliuliza
“Zipo nyingi, ni pesa yako tuu”
“Maeneo gani zipo?”
“Chuda si unapapata?”
“Ndio?”
“Sasa, ule mtaa ukikosa sehemu ya kulala ujue unabahati mbaya”
“Sawa jamani, ngoja tuondoke, nikisema tuendelee hapa tutakesha”
“Umeona eheee”
“Nishidaaa”
“Jamani, tutaendelea kuwasiliana”
“Tunawasiliana vipi wakati hatuna hata namba za simu ulizo tuachia”
“Simu sina”
“Haaaa, unaishije bila simu?”
“Nitachukua kesho”
“Sikia chukua simu yangu, mukifika sehemu mutakapo pata chumba utatujulisha, si unajua wewe sasa hivi ni mtu mkubwa kwetu, shemeji samahani bwana kwa kuipendekaza kumkabithi simu bibie, usije ukanihisi vibaya”
“Hamna shida, ndugu zangu pia mutakuwa mumetusaidia sana”
“Ndio maana nimekukubali shem wangu, ingekuwa jinga lengine hapa lingevuta mdomo kama yule bibi tuliye mkamata jana ameanguka na ungo wao wakichawi”
“Eheee, hayo mengine tena, mumeanza kukamata hadi wachawi?”
Dorecy aliuliza
“Ohoo, shosti huu mji bwana ahaaa, Juzi kati maeneo ya mwakizaro huko, tulipewa taarifa kuna bibi ameanguka na ungo, acha wananchi wamabamize mawe.Sasa sisi tukaitwa kumchukua, mwanagu kabibi kaze japo kamepigwa ila hakajafa, sasa huo mdomo alivyo uvuta mbele kama anapiga busu la karne”
Jamaa alizungumza na kuzidi kutufanya tucheke kwani alitoa mfano wa jinsi bibi huyo alivyo uvuta mdomo wake mbele
“John unafanana naye”
“Dullah hembu acha ujinga bwana”
“Hahaaa, jamani ngoja tuondoke”
“Sasa utaondokaje pasipo mimi kukuambia namba gani unipigie”
“Haya mwaya, niambie”
John akachukua simu aliyo mpa Dorecy, na kuandika namba na kumuonyesha Dorecy
“Haaaaa....!!”
Dorecy alihamaki
“Nini?”
“Mbona mba mbaya hivi, kama amba za majeneza”
“Ahaaa Dore sasa hizo dharau”
“Ahaaa kwa hiyo John na wewe unanunaga?”
“Hapanaaa”
“Unazani atanuna, anaogopa ukamfanaya kama shosti yake Nyandeza”
“Jamani, hembu achani utoto, hapa mume wangu ana njaa ngoja twende sehemu tukale kwanza kisha nitawapigia simu sehemu muje tunywe kidogo”
“Mambo si ndio hayo”
“Nyooo, John ndio maana pesa yako ya marupurupu unaimalizia kwenye pombe”
“Ahaaa nina shida gani, sina mke wala mtoto, acha niuponde ujana”
“John hadi sasa hivi huna mtoto!?”
“Wewe unaye?”
Dorecy akizungumza
“Ahaaa haya bwana, kwa herini”
“Sawa, bro Eddy mkumbushe bwana huyo kuja kunywa kidogo, si unajua tena katikati ya mwenzi huu, hali mbayaa”
“Powa kaka zangu, tupo pamoja”
Niliwajibu, Dorecy akafunga mlango wa gari na kuanza kuondoka taratibu,
“Tunaelekea wapi?”
“Kuna, hiteli hapo mbele inaitwa Nyinda Anex ngoja nikacheki kama tutapata chumba”
“Powa, hivi wale rafiki zako wanafanya kazi kweli?”
“Ahaaa, wale ni pumba, ningesema nikae nao pale.Tungekesha”
Tukafika kwenye hoteli aliyo niambia, Dorecy akashuka kwenye gari na kuniomba nimsubiri.Nikageuka siti ya nyuma na kukikuta kibegi changu cha madini, nikakifungua ndani na kukuta kikiwa kama kilivyo, hakuna kitu hata kimoja kilicho pungua.Dorecy akarudi na kuingia ndani ya gari
“Vipi umepata?”
“Vyumba vimejaa”
“Ahaa, mkosi huo”
“Ngoja twende, hapo mbele kuna Hotel ya ghorofa tuliipita”
“Powa, alafu bastola zangu zipo wapi?”
“Fungua hapo, pembeni utaziona”
Dorecy akanielekeza, nikafungua sehemu ya pembeni yangu kwenye siti na kuzikuta zote mbili, nikazichukua na kuzichomeka kwenye viatu, Tukafika kwenye Hotel moja inayo itwa Mtendele.Kama kawaida Dorecy akashuka na kuniacha kwenye gari, akaingia na baada ya dadika tano akarudi akiwa ameshika funguo ya chumba mkononi
“Nimepata”
Nikashuka ndani ya gari huko nikiwa nimeshika kibegi changu chenye madini, na sote tukaingia kwenye hoteli, hiyo iliyo tengenezwa vizuri kwa kwenda juu.Tukapandisha ghorofa ya tatu kilipo chumba chetu,
“Eddy, hivi hicho kibegi kina nini?”
“Nitakuambia, ila kikubwa kwanza, tuzungumze vitu vya maana”
“Hata kuoga hatuogi?”
“Tutaoga, kikubwa tuzugumze ni jinsi gani tutampata mzee Godwin?”
“Eddy, mzee Godwin anamtandao mkubwa sana, tena sana.Sio mtu wa kumuendea kichwa kichwa, wewe mwenyewe unaona jinsi alivyo kutia nguvuni, laiti ingekuwa sio mimi, sijui ungekuwa wapi hadi sasa hivi.”
“Sawa, ila kuna vitu ambavyo nahitaki kuvifahamu kupitia wewe”
“Uliza”
“Hivi ni watu gani ambao, mzee Godwin anashuhulika nao?”
“Ahaaa, ni wazito serikalini, ukumbuke kwamba yule ni mtu mkubwa sana kwenye hii nchi, pili utambue ni mkuu wa jeshi, yaani akitoka raisi katika mamlaka ya jeshi anafwata yeye, so huyo sio mtu wa kusema unamuendea kichwa kichwa.Nilazima tuwe na mipango ambayo itatufanya tuweze kumpata mama kwanza, kisha hao wengine watafwata”
Nikashusha pumzi zangu huku ninamtizama Dorecy kwa umakini machoni
“Eddy, lengo la mimi kukuleta huku ni wewe kwanza ukapate kwanza mazoezi ya kijeshi, japo wewe mwenyewe unajiona umekamilika ila bado, tena sana”
Dorecy alizungumza huku akinitazama machoni
“Kwani kupambana na mtu kuna ulazimu wa mazozi ya kijeshi?”
“Ingekuwa sio hivyo basi hata wauza mitumba wangeenda kupigana vitani”
Jibu la Dorecy likabaki likinipa msongamano wa mawazo
“Ila huoni kama baba atajua?”
“Baba gani?”
“Mzee Godwin”
“Ahaaa, huko ninapo kupeleka mimi, atakaye jua ni mimi na huyo ndugu yangu ninaye mfwata huko”
Dorecy alizungumza kwa kujiamini sana
“Sawa nimeku.....”
Nikastukia Dorecy akinivuta kwa nguvu na kuninyanyua kwenye sofa nililo kaa, nikastukia akinitandika kichwa cha uso kilicho niyumbisha huku nikiona giza kwenye macho yangu, zikiambatana na nanenane
“Ahaaa”
Niliropoka, ila nikastukia akinitandika ngumi mbili za kifua zilizo niangusha chini, nikachomoa bastola ya kwanza kwenye kiatu hata kabla sijaishika vizuri nikashtukia teke likitua kweny mkono wangu na kuiangushia mbali bastola, nikachomoa ya pili, hali ikawa kama hiyo hiyo ya kupigwa teke la mkono
“Unanipigia nini, sasa”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, nikajaribu kunyanyuka, ila nikaikuta miguu yangu ikipigwa na mguu mmoja wa Dorecy, nikajikuta nikirudi chini tena.Kwa jicho langu moja nilamchunguza Dorecy jinsi alivyo simama huku mikono yake akiwa ameikunja ngumi
Nikasimama kwa haraka, Dorecy akarusha ngumi, niliyo bahatika kuiona na kuikwepa.Kitendo cha mimi kuikwepa ngumi, nikastukia kigoti cha Dorecy kikitua kifuani mwangu na kujikuta nikinyanyuka kwenda juu mithili ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme, nikastukia ngumi moja kali ikitua kwenye komo langu na kunisabanisha kunirudisha kwenye kochi huku macho yangu nikiwa nimeyafumba baada ya kuiona ngumi nyingine ikinijia kwenye uso, nikaisikilizia ila haikufika kwa wakati muafaka ikanibidi kufumbua macho na kujikuta nimetazamana jicho moja la bastola aliyo ishika Dorecy, huku ikiwa imesimama sentimita chache kutoka yalipo macho yangu
“Sali sala yako ya mwisho?”
Dorecy alizungumza huku sura yake ikiwa imejaa jasho jingi, na mikonjo iliyonifanya niamini huu ni mwisho wa maisha yangu mimi Eddy Godwin
“Dorecy umechanganyikiwa?”
Nilimuuliza Dorecy anayeonekana kumaanisha kile kitu anacho kizungumza, hakunijibu kitu cha aina yoyote zaidi ya kuendelea kunielekezea bastola yake kwenye sura yangu
“Eddy usimuamini kila unaye muona utaumia sawa?”
Dorecy alizungumza na gafla nikastukia akinipiga na kitako cha bastola kwenye kichwa changu, giza lililo andamana na maruwe ruwe kitanitawala taratibu katika macho changu na kwa mbali nikausikia mlango ukifunguliwa, baada ya muda kidogo sikujua ni kitu gani kinacho endelea
***
Nikahisi nikiguswa mgongoni, taratibu nikayafumbua macho yangu na kukutana na viatu vya mwanaume vikiwa vimesimama kando yangu, nikakinyanyua kichwa changu taratibu huku nikiwa ninamaumivu makali, nikakutana na sura ya mwanaume ambaye amevalia sare za wahudumu wa hoteli hii
“Kaka, habari yako”
Jamaa alinisalimia, huku akinitazama usoni mwangu.Sikumjibu cha kwanza kutazama ni kuangalia sehemu nilipo weka begi langu lenye madini ndani, sikuliona na kujikuta nikikurupuka na kusimama, nikaingia bafuni na kukuta kweupe hakuna mtu
“Kaka vipi?”
“Ku..kunaa dada hiv...i mrefu ume...muona wapi?”
“Yule uliye ingia naye jana usiku?”
“Jana, usiku? Eheee huyo huyo”
Niliungumza huku nikipiga hatua kuelekea kwenye dirisha, nikatamani kuanguka chini na kupoteza fahamu, kwani mwanga mkali wa jua nilio ukuta nje ya dirisha umenichanganya kiasi kwamba nimekosa la kuzungumza
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni