SEHEMU YA TISINI NA TATU
ILIPOISHIA...
“Ahaaa”
“Tena yule John, ana roho nzuri sana. Haswa yule mke wake.”
“Chanzo cha baba, kua rafiki na yule John. Walitoa Hotel yao sisi kuishi tangu tunakuja hadi tulipo pewa nyumba, tuliyo andaliwa. Kwani balozi aliye pita kabla ya baba, alifariki kwa ajali ya ndege.”
NIPE SAPOTI KWA KUTAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWANGU
SASA ENDELEA...
“Kwa hiyo vitu vyake havikuamishwa, kwenye ñyumba tunayo ishi, sasa hivi. Ikatulazimu kuishi Hotelini, John akajitolea hoteli yake tuishi bure kwa kipindi chote”
“Ahaaa”
“Hata ile Hotel tunayo kaa sasa hivi ni ya John na mke wake”
“Kweli?”
“Ndio”
“Kumbe nimatajiri dana ehee?”
“Ndio nimatajiri sana, ila nasikia kwamba utajiri wao ni wakuridhi, kutoka kwa baba yake Victoria, ambaye kwa sasa ni marehemu”
Nikastuka, huku nikimtazama Bruno, akili yangu ikaenda moja kwa moja katika tukio walilo lifanya John na Victoria kutaka kumuua baba yangu.
“Huyo baba yake, Victoria anaitwa nani?”
“Kwakeli simfahamu, ila nilisikia kwamba baba yake alijinyonga, chumbani kwake. Inasadikika alikuwa na ugonjwa wa kichaa”
Nikahisi mwili wangu, ukisisimka, kwani John amechukua, kila kitu kwenye maisha yangu. Kuanzia mali za baba yangu. Hadi familia yañgu.
Muda wa kuruhusiwa, ukawadia. Daktari akaniomba azungumze na mimi. Tukaingia ofisini kwake na kukaa kwenye viti vilivyomo humu ndani.
“Tumekufanyia uchunguzi wa kina, tukakukuta na matatizo mawili kwenye mwili wako. Endapo hayata fanyiwa uharaja wa matibabu, unaweza kupelekea kifo chako. Bwana Eddy.”
Daktari alizungumza huku akinitazama machoni mwangu. Wasiwasi haukuacha kunitawala usoni nwangu.
“Ninaumwa na nini Daktari?”
“Tatizo la kwanza, ni hasira iliyo pitiliza kiwango. Ambayo ikikupanda sana, inapelekea mfumo wako wa mapigo ya moyo kukuenda kasi sana. Moyo unapeleka kasi damu kwenye mishipa mbali mbali mwilini mwako. Na ndipo kuna baadhi ya damu, zinatoka puani mwako.”
“Ukishindwa kujizuia hasira yako, itapelekea mishipa ya damu kupasuka, hapo utakua ni mwisho wako wa kuishi duniani”
“Tatizo la pili, tumegundua kwamba, unayemelewa na ungonjwa wa Saratani, ya damu.”
Nikahisi mwili mzima ukifa ganzi, kwani sikifikiria kama nitaumwa nà ugonjwa wa Canser, tena ya damu
“Ila usiwe na wasi, nimezungumza na muheshimiwa, utakwenda kufanyiwa matibabu Marekani. Na saratani itakwenda kupona, kwani ndio ipo kwenye hatua za mwanzoni mwanzoni.”
Daktari akanikabidhi dawa, za kunywa pale nitakapo jihisi vibaya.
“Siwezi kufa hadi nirudishe, kila kitu alicho kichukua John kutoka mikononi mwangu.”
Nilizungumza kimoyo moyo huku, nikitoka chumba cha daktari, nikajumuika na balozi, pamoja na wanae kurudi hotelini.
***
Siku mbili, zikapita na hali yangu ikazidi kuimarika. Kila asubuhi nikawa na jukumu la kufanya mazoezi, ili kuuimarisha mwili wangu. Nikiwa nimevalia nguo za mazoezi, raba pamoja na earphone, nikibrudika kwa mziki, kupitia Ipad aliyo nipa Casey, jana usiku. Nikaendelea kukimbia barabanani, huku saa yangu ya mkononi, ikinionyesha ni saa kumi na moja alfajiri.
Katika barabara ninayo kumbia, hakuna wa watu wengi, zaidi ya mtu mmoja mmoja, ninao kutana nao wakifanya mazoezi kama mimi ya kukimbia.
Nikamkuta dada mmoja aliye vali, suti ya kijivu, Akionekana kuchanganyikiwa, kwani gari lake analo liendesha, limepata pacha tairi la mbele.
“Samahani kaka”
Aliniita baada ya kumpita kidogo, nikavua earphone zangu, na kugeuka kumsikiliza ahahitaji kuzungumza na mimi kitu gani.
“Ndio”
“Nakuomba, unisaidie kubadilisha tairi la hili gari.”
Nikamtazama juu hadi chini, pasipo kumjibu chochote. Nilipo ridhika na udadisi wangu, nikamsogelea.
“Kwani ilikuaje?”
“Nimekuta tu tairi, likiisha upepo”
“Toa hilo jengine”
Akazunguka nyuma ya gari lake kwa haraka, akatoa tairi pamoja navifaa vingine vya kusaidia kubadilishia tairi la gari. Nikaanza kazi ya kulifungua tairi lenye pancha, huku yeye akiwa na kazi ya kunibadilisha kila spana nitakayo muomba anipatie.
Haikuchukua muda sana, nikamaliza kumfungia tairi lake jipya.
“Asante sana”
“Usijali”
Akafungua mlango wa upande wa dereva, na kutafuta kitu. Kutokana sikuhitaji kulipwa, nikaanza kuondoka babla sijapiga hatua hata sita nikasikia akiniita.
“Kaka subiri uchukue zawadi yako”
Nikageuka, sikuamini macho yangu kwani, nikakutana na bastola aliyo ishika huyu dada, akinielekezea mimi
“Tulia hivyo hivyo, ukijaribu kupiga hatua nitakufumua ubongo wako.”
Alizungumza huku akiwa ameishika, bastola yake kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine akiwa na simu.
“Ninaye hapa”
Alizungumza kupitia, simu yake. Wala sikujua à nazungumza na nani. Mbaya zaidi siwezi fanya chochote kutokana hii barabara imenyooka sana, na haina sehemu ya kujificha. Gari nne nyeusi, zenye muundo wa gari kama zinazo bebea pesa za mabenki, zikafunga breki katika eneo tulilopo. Wakashuka watu walio valia ñguo nyeusi, makofia meusi yaliyo waficha sura zao, na kubakishs macho yao tu. Kila mmoja mkononi mwake ameshika bundiki, na wote wakanizungu huku wakinitazama kwa umakini.
Mmmoja wao akatoa amri ya mimi kuiamsha mikono yangu juu, nikatii pasipo kubishana. Akatoa amri nyingine ya mimi kulala chini, hapo ndipo nilipo anza kuleta ubishi, kwani siwezi kukamatika kirahisi.
Kitendo cha mimi kusogeza mguu nyuma, nikastukia kitu chenye ncha kali kikinichoma mgongoni, kwa haraka nikaupeleka mkono wangu nyuma, kwa ajili ya kukichomoa. Nikakuta ni sindano
yenye dawa, iliyo anza kuvinyong’onyeza viungo vyangu vya mwili. Taratibunikajikuta nikianza kuishiwa na nguvu. Nikaanguka chini, kila nilipo jaribu kunyanyua hata mkono sikuweza, nikajikuta nikiwatazama watu hao walio nikaribia na kuninyanyua. Nikastukia kitu kizito kikinipiga, kichwani, giza kali likanitawala machoni mwangu.
********
“Eddy…. Eddy”
Nisauti nyororo, iliyo anza kuisikia taratibu, ikipenya masikioni mwangu. Taratibu nikayafungua macho yangi, nikakutana na sura ya kike, huku kichwa chache kikiwa kimejaa nywele nyingi nyeusi na zilizo ndefu sana.
Macho yake makubwa kiasi, na yadura kiasi, yaliendelea kunitazama huku akiwa ameniimamia, kutoka katika kitanda nilicho kilala.
“Karibu tena duniani” Alizungumza huku akiwa ametabasamu.
“Duniani?”
“Ndio duniani”
“Kwani nilikua, sipo duniani?”
Hakuzungumza chochote zaidi ya kusimama, pembeni ya kitanda nilicho lala.
“Kwa jina ninaitwa dokta, Agines, nimtaalamu katika maswala ya saikolojia”
“Ngoja, hapa ni wapi?”
“Upo Washinton DC, Marekani”
“Ahaaaa?”
“Usishangae, ninaimani kwamna unatambua, nitukio gani ulilo lifanya kwa ajili ya hii nchi, nasi tumeamua kukuweka karibu nasi na kukusaidia kwa kila jambo”
Akafungua pazia, kubwa lililopo kwenye moja ya ukuta, hapa ndipo nilipo anza kuona majengo makubwa yaliyopo katika mji huu, ambapo ndipo yalipo makao makuu ya serikali ya nchi ya Marekani.
“Tutahakikisha tunakufanyia kila unacho kihitaji”
Akaniandalia chakula, akaniomba nile.
“Ukimaliza kula, kuna watu nitahitaji uonane nao”
“Wakina nani?”
“Utawaona tuu”
Nikamaliza kula, akanionyesha bafuni, nikaoga na kurudi kitandani, huku nikiwa nimejifunga taulo.
“Unaweza kuvaa”
“Mbele yako?”
“Kwani kuna tatizo lolote, tambua kwamba mimi nitakuwa pamoja nawe kwakipindi cha siku tisini”
“Za nini?”
“Eddy vaa bwana, watu hao wanakusubiri.”
Nikamtazama kwa muda, nikavua taulo, nikachukua nguo moja baada ya nyingine alizo zipanga kwenye kitanda.
“Umependeza sana”
“Asante”
“Upo tayari”
“Ndio”
Tukatoka ndani ya chumba, hichi kilicho tengenezwa kwa mfumo wa wakisasa, tukaingia ndani ya lifti na kushuka chini, hapa ndipo nilipo gundua ghorofa tuliyokuwa ni ya hamsini kutoka chini.
Tukafika chini, kabisa tukaongozana hadi nje ya ghorofa hili, tukakuta gari karibia sita zenye muundo mmoja wa milango sita zikitusubiri sisi.
Tukaingia kwenye moja ya gari, na gari zote zikaondoka.
“Tunapo kwenda ni wapi?”
“Ahaaa utapaona usiwe na wasiwasi”
Akanipa glasi iliyo jaa whyne
“Ninaamini unatunia hiki kinywaji?”
“Ndio”
Nikaendelea kutazama jinsi mji huu ulivyo jengeka, kwa majengo marefu. Tukafika kwenye mojo ya geti kubwa, gari zote zikaingia kwa pamoja.
Tukashuka mimi na Agie, tukapokelewa na mdada mmoja aliye valia suti nyeusi. Akatupeleka kwenye moja ya meli, iliyo simama pembezoni mwa bahari
“Ni nani huyo tunakwenda kuonana naye?”
“Eddy mbona una haraka, utamuona tu”
Tukaingia ndani kabisa ya meli hii ya kifahari, kila niliye mtazama alionekana kutabasamu. Wengine wakadiriki kunisalimia, kwafuraha.
“Tuingue humu chumbani”
Tukaingia kwenye moja ya chumba kilicho humu ndani ya meli hii. Tukakuta baadi ya watu wanao onekana ni wanamitindo.
Wakanichukua vipimo vya mwili wangu, wakaanza kunishonea nguo ya mtindo nilio uchangua kati ya mitindo mingi, waliyo nionyesha.
“Agie mbona, mimi sielewi?”
“Huelewi nini Eddy?”
“Mambo yote haya, munanifanyia kwa maana ipi?”
“Eddy kama nilivyo kuambia, inatupasa kulufanyia kitu kama kukulipa fadhila ya uliyo fanya kwa raia wa Marekani”
“Hata kama, ila bado haijaniingia akilini!”
“Kwa nini?”
“Ni watu wangapi, walikufa kwa ajili ya wamarekani muliwafanyia hivi?”
“Ndio ila kila mmoja ana bahati na nafasi yake kwenye maisha. Kwahiyo nafasi yako no hii”
Ndani ya lisaa, nguo niliyo hitaji kushonewa ikawa imekamilika, wakanipa niijaribu, kutokana na uzoefu wao, hawakukosea kitu hata kimoja.
“Ni muda wakutoka kwenda kukutana na watu nilio, kuahidi utaonana nao”
Nikashusha pumzi huku nikimtazama Agie, ambaye naye, alibadilisha nguo alizo kuja nazo na kuvalia gauni, refu jekundu.
Tukatoka tukiwa tumeshikana mikono, sauti yakiume, kupitia kipaza sauti nikaisikia ililitaja jina langu, ukumbi wote ukafura kelele za makofi. Watu walizidi kushangilia huku wakianza kuimba wimbo wa Happy birtday, wakiashiria ni siku yà ngu ya kuzaliwa.
Agie akanipeleka hadi mbele ya ukumvi kwenye sehemu iliyo nyanyuka kidogo. Kwa matatizo yalivyo nizonga, hata siku yangu ya kuzaliwa sikuikumbuka.
Ukimya ukatawala ndani ya ukumbi, huku watu wakinisubiri nizungumze kitu chochote.
“Kipindi, nilipo kuzaa, nilitambua kwamba ipo siku utakuja kua mtu muhimu kati ya watu wengi ulimwenguni humu”
Sauti ya mama, ilinistua, kupitia vipaza sauti vilivyomo humu ndani, nikatazama pande zote za ukumvi ila sikumuona mama.
“Usipate shida ya kunitafuta, nipo hapa mwanangu”
Nikamuona mama, akisimama katikati ya watu huku mkononi mwake akiwa ameshika kipaza sauti.
“Leo maombi yà ngu, Mungu ameyasikia. Nilikutafuta kwa miaka mingi mwanangu. Hadi leo nimekuona”
Mama alizungumza huku akipiga hatua akija mbele nilipo, mashafu ya mama yakaanza kujaa machozi, yanayo mtiririka kutoka machoni mwake.
“Umekua mwanangu, hadi leo unatimiza miaka ishirini na tato, kweli umekua mwanangu”
Nikashikwa na kigugumizi hata sikuweza kuzungumza, mama akanikaribia na kunitazama usoni mwangu, nami nikashindwa kuyazuia machozi yangu.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE NAOMBA TAZAMA VIDEO HII NDIO MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA YA KUKUSOGEZEA SIMULIZI
KWA USHAURI NA MAONI ANDIKA HAPA:
Inbox: Messanger
Email: ZephilineEzekiel@Gmail.Com