MAHABA NIUE (24)

Zephiline F Ezekiel
MAHABA NIUE (24)
JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... "Haya bwana poa poa ukimaliza kupika niambie" Ramsey alitabasamu kidogo kutokana na uwongo ule wa Esta Foleni zilianza kutembea na Ramsey kuanza kucheza na usukani, "nani ulikua una mpigia simu:?" KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... Alihoji Josephine. "AAh anti yangu, sitaki ajue nipo huku town," "sawa, nataka umuache huyu rafiki yako kwake alafu mimi nawewe tuongozane kwangu" "yaani niende kwako"? "yes, kwangu, kwani kuna ubaya"? "ila nita rudi sitolala" "no problem" Ramsey alitikia huku akizidisha mwendo kasi akiwa makini sana juu ya usukani ule huku akimuwaza ESta na moyo kumuuma sana kwanini alimdanganya, ila nafsi nyingine ina mfariji na kusema pia ngoma droo namimi mbona nina mademu wengine, licha ya nafsi ya pili kumfariji ila moyo uliendelea kumuuma sana. baada ya kufika magomeni mapipa ana mshusha Prosper…