ROHO MKONONI (10) JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Baada ya Butu kutoka tu kichaa yule wa kike alimsindikiza kwa macho baada ya kupotelea mtaa wa pili,akawasiliana na Isack,kisha akanyanyuka,akabeba pochi lake moja chafu na kuelekea kunapo geti,tena alificha uso wake kwa mikono kusudi kamera za pale getini zisinase sura yake. KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SASA ENDELEA... Alipofika getini akaingiza moja ya funguo alizokuwa nazo,akafungua na kuzama ndani,alitembea haraka haraka juu ya tails zilizopo chini mpaka katika mlango wa nyumba ya ndani,akaingiza pia funguo,akafungua,ile kuingia akakutana na sebule nzuri,akaifata korido,chumba cha kwanza akasimama akashika kitasa akakizungusha kikamtwii,akazama ndani! Hiki ndicho kilikuwa chumba cha Butu cha kulalia macho ya kichaa yule yakadondokea katika kabati,kwa hatua za taratibu akalifata,alipolifikia akatia fun…