ROHO MKONONI (7) JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Baada ya kuikamilisha akarejea nayo ofisini kwa mkuu wake na kumkabidhi... Inspekta wa jeshi la polisi John Butu anapokea barua ya kuamishwa kazi,jambo hilo anapingana nalo na kuamua kuandika barua ya kuacha kazi kabisa je unadhani nini kitaendelea?! KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SASA ENDELEA... Tayari akili yake ilishagubikwa na ukungu wa kukurupuka, Akupenda hata kuchukua wasaa angalau dakika moja na ushee aidha kutafakari kile akifanyacho. Tabia hii kila mara ndo ilo mfanya ajutie kile aamuacho kwanzia kumuua yule mwandishi,kumuua huyu alo mjua kama mr x na pia kuandika barua ya kuacha kazi,akaikabidhi kwa bosi wake,akuishia hapo akapiga saluti muinuko,na kutoa kofia yake ya polisi akaiweka mezani,palepale akageuka na kuuendea mlango,hata mkuu wake alipo muita akuangaika kugeuka,alisha amua,na Butu kawaida…